MASWALI
- Lazima
Wewe ni Mwenyekiti wa Tume ya kupigana na ufisadi nchini. Umealikwa kuhutubia magavana kuhusu athari za ufisadi huku ukipendekeza hatua za kukabiliana na jinamizi hili. Andika hotuba utakayoiwasilisha. - Mitandao ya kijamii ina madhara mengi kuliko faida. Jadili.
- Andika kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Achezeaye tope humrukia.
- Andika insha itakayoanza kwa maneno yafuatayo:
Mara nilisikia ukemi mkali kutoka nje. Majibwa yalibweka kwa mfululizo kana kwamba yanasemezana…

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
- Hii ni insha ya hotuba. Muundo ufuatao uzingatiwe.
- Kichwa/Mada/Anwani ya hotuba km. Hotuba kuhusu Athari za ufisadi na jinsi ya kukabiliana nao. (Anwani iandikwe kwa herufi kubwa na kisha ipigiwe mstari.
- Utangulizi
- Itifaki izingatiwe katika kuwatambua watu muhimu waliopo.
- Mhutubi ajitambulishe kwa hadhira yake na lengo la hotuba yake.
- Pawe na maamkizi.
- Alama za mtajo zaweza kutumiwa mwanzoni mwa hotuba na mwisho mwa hotuba ama zisitumiwe.
- Mwili
- Hii ni sehemu ya maudhui/hoja.
- Athari za ufisadi zitajwe na kufafanuliwa ipasavyo na kisha mapendekezo yatolewe.
- Hitimisho
- Mhutubi atoe shukrani kwa hadhira yake kwa kutenga muda wao ili kumsikiza.
- Atilie mkazo kiini cha hotuba yake.
Athari za ufisadi - Ukosefu wa dawa hospitalini.
- Ujenzi duni wa barabara nchini.
- Kuongezeka kwa ajali barabarani.
- Watu kupewa ajira ambazo hawajasomea na kusababisha huduma mbovu.
- Mijengo kuporomoka na kusababisha mauti na hasara .
- Nchi kufifia kiuchumi.
- Taifa kuwa na sifa hasi ughaibuni.
- Pengo kati ya matajiri na maskini kupanuka zaidi.
- Nchi kunyimwa msaada na mataifa/mashirika ya ufadhili (kadiria hoja za mtahiniwa
Mapendekezo - Kupiga kalamu mafisadi.
- Kufungwa gerezani.
- Faini kubwa kwa mafisadi.
- Kutowaruhusu mafisadi kuwania kiti chochote cha uongozi.
- Mali iliyopatikana kifisadi itwaliwe na serikali.
- Umma kuhamasishwa athari za ufisadi kupitia vyombo vya habari.
- Somo kuhusu maadili lifunzwe katika shule za msingi, upili na hata vyuo vikuu. (kadiria hoja za mtahiniwa.
- Swali la mjadala/mdahalo.
- Mtahiniwa aunge mkono mada kwa kutoa hoja nyingi zinazoonyesha madhara ya mitandao kisha atoe hoja chache za faida.
- Mtahiniwa apinge mada kwa kutoa kutoa hoja nyingi za faida na chache za hasara.
- Mtahiniwa atakayezungumzia upande mmoja tu k.m. Faida na akose kutoa hasara, asipite C+ 10.
Hasara za mitandao - Inaendeleza utapeli k.m Umeshinda katika mchezo wa bahati nasibu na kumbe ni ulaghai.
- Inaendeleza wizi wa mitihani ya kitaifa nchini.
- Imezorotesha utamaduni wa kiafrika k.m mavazi.
- Unaendeleza uozo k.m. ponografia.
- Matendo ya kihalifu hupangwa kupitia mitandao hii.
- Watu hupoteza fedha zao zilizo katika akaunti zao kupitia mitandao hii. (kadiria hoja za mtahiniwa.)
Faida za mitandao - Imerahishisha mawasiliano.
- Imenawirisha biashara.
- Ulipaji nauli umerahisishwa.
- Nafasi za ajira zimebuniwa.
- Imeendeleza utafiti wa kimasomo na kisayansi.
- Upashaji wa habari umerahisishwa.
- Mambo muhimu huhifadhiwa kwa mitandao hii.
- Wanaosaka ajira hujuzwa sehemu zilizo na nafasi za kazi.
(kadiria hoja za mtahiniwa).
- Swali la methali
- Achezeaye tope humrukia.
- Maana: Mtu anayechezea tope huishia kuchafuliwa nalo.
- Matumizi: Methali hii huwakanya watu dhidi ya kuandamana au kuhusiana na watu wenye sifa mbaya. Anayehusiana na mtu mbaya huishia kuambukizwa ubaya huo.
- Mtahiniwa atunge kisa kinachodhihirisha matumizi haya.
- Insha ya mdokezo.
- Mtahiniwa aonyeshe mtu/watu waliokuwa taabani nje na hatua aliyoichukua kuwanusuru.
- Mtahiniwa azingatie nafsi ya kwanza umoja.
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kakamega Evaluation Mock Exams 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates