Kiswahili Paper 2 Questions - ACK Diocese Mumias Joint Evaluation Mock 2022

Share via Whatsapp

Maswali

MAAGIZO:

  • Jibu maswali yote.

 

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    SOMA KIFUNGU KIFUATACHO KISHA UJIBU MASWALI YANAYOFUATIA

    Nchi yetu imeraukia mawio ya machafuzi ya kisiasa baada ya shughuli za uchaguzi zilizogonga Mwamba mkuu. Hili lilijiri baada ya Tume ya uchaguzi kukosa kuendeleza uchanguzi kwa njia inayostahili. Jambo hili lilizaa msukosuko wa kisiasa usiomithilishwa katika historia ya taifa letu.

    Hivi sasa wakenya waishi kwenye kambi za watu wasio na makazi. Hiki ni kinaya kikuu kwani matukio haya yamezuka baada ya miongo minne ya uhuru. Vilio vya wakenya vimeshamiri na kupaaza sauti vikalalamikia Kukosa makazi , lishe nadoa kusambaratika. . Ndoa zimevunjika baada ya wenyeji kuwatimua ‘ wageni na damu kumwagika.

    Kenya imekuwa miongoni mwa mataifa yanayowapa faraja wakimbizi kutoka nchi jirani Zinazokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita katika Somalia vimesababishwa na koo mbalimbali zinazopigania uongozi hali ambayo imekwamisha shughuli zote za kiuchumi.

    Hali ya sasa ya Kenya imechochewa na msururu wa sababu; ukabila na tamaa ya uongozi zilionekana Wazi katika miundo ya vyama vikuu vya kisiasa na katika kampeni zao. Wakenya walipiga kura kwa misingi ya kikabila kilaupande ukitazamia mtu wao kushinda uchaguzi huo.

    Kwa upande mwingine, viongozi hao kutokana na tamaa ya uongozi walikuwa wameamua kushinda uchaguzi huo kwa vyovyote vile. Leo munavuna matunda ya siasa za ukabila na tamaa ya mamlaka.

    Maelfu ya wakenya ni wakimbizi nchini na katika nchi jirani ya Uganda. Wakenya hao wanahitaji msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kimsingi. Serikalina shirikala msalaba mwekundu zimefanya juhudi kuwasaidia wahasirikwa lakini kuna tetesi kwamba ubaguzi umejipenyeza katika ugawaji wa msaada huo.

    Waliopewa jukumu la kugawa msaada huo ni sharti waelewe kuwa waathiriwa ni wakenya wenzao na hawafai kubaguliwa kwa misingi ya makabila yao. Matukio kama haya hayastahili asilani katika taifa hili.

    Twahitaji zao aali la viongozi wasiojitwika ubabe bali wawe watumishi wa wananchi wanaostahili kutupilia mbali tamaa za kujlimbikiza mali na kung’ang’ania uongozi. Pia katiba inafaa irekebishwe. wakenya wanastahili kuelimishwa kuhusu unduguna utaifa. Fauka ya haya ,masuala yanayohusiana na hatimiliki na ardhi yanafaa kutandarukiwa kwa dhati.
    1. Taja madhara manne ya ukabila al 4
    2. shughuli za ugawaji wa misaada zimekumbwa na changamoto gani ? (al. 2)
    3. Eleza tofauti ya chanzo cha vita nchini Somalia na Kenya (al. 2)
    4. Mwandishi anatoa mapendekezo gani ya kutatua tatizo hili la ukabila. (al.3)
    5. Eleza kinaya cha Maisha ya wakenya kwa sasa (al.2).
    6. Eleza maana ya maneno haya yalivyotumika katika kifungu cha ufahamu (al.2)
      1. Mawio
      2. Tandarukiwa kwa dhati.
  2. UFUPISHO
    Soma Makala haya kishaujibu maswali yanayofuata

    Tangu asili – na jadi nasikitika kusema kuwa tumekuwa tukiwakandamiza mabanati wetu na kuwateka bakunja ilhali wameonyesha kuwa mikono miepesi. Siku mojanilikuwa nikitembea na babu yangu mkongwe tulipoliona tapo lawanawake kwambali. ‘’ Funika kombe mwanaharamu apite! Akaninong’onezea, wanahusudu uwezo tu. ‘’Kwa uchungu watu wa fikiria sikuelewa yakini nilichotazamialakini hii leo nang’amua. Basi imenibidi kutupilia mbali dhana hiyo hafidhina kwani aisifuye mvua aghalabu imemnyea.

    Jina nzuri hung’aa gizani na bila shaka majina ya wanawake wetu yameremeta kama nyota. kwanza, wamejitolea mhanga katika Nyanja za masomo. Si haba ambao wamehitimu kutoka vyuo vikuu vya humu nchini na vile vile vya ughaibuni na kujipa shahada kadha wa kadha. Wamepata ujuzi wa kutotsha katika maswala tatizo kama vile udaktari na uanasheria. Hivi ni kumaanisha kuwa tuna madakitari shupavu, basi tuwape nafasi tusiendelee kuwa nyuma mithili ya koti katika kipengele hiki muhimu cha maisha.Ni wanawake ndio lakini mgalla muue na haki umpe!

    Vile vile wanawake wenu wamejitokeza kifua mbele katika hatamu za uongozi. Mifano mwafaka ni Katika serikali yetu, ambapo mawaziri ni wanawake Nani asiyewafahamu, Cecily Kariuki, Racheal Omamo na Amina Mohamed? Wote wanafanya bidii za mchwa kustawi Maisha ya wananchi. gekuwa ida na inadi kama tungewanyima viongozi hawa nafasi hizo na bila shaka jambo hili lingeathiri sana ujenzi wa taifa kwani ndio nguzo ya kila kitu.

    Kwa upande mwingine wanawake ni walezi waliomakinika. Kama tujuavyo udongo hupatilizwa ungali maji na usipoziba ufa huna budi kujenga ukuta. Nani ndio wamepokezwa jukumu mahiri la malezi? Nina zetu hujitolea kwa hali na mali kuwakuza watoto kwa tajriba zinazofaa na kuwafunza maisha ndiposa wasifunzwe na ulimwengu. Aliyemakinika atakubaliana nami kuwa malezi si jambo la kufanyiwa mzaha katika harakati za ujenzi wa taifa. Na huu wajibu wote ni wa mwanamke.

    Siwezi kuwasahau wanawake wanamuziki. Sote twaelewa kuwa kwa uchumi kama wetu,. Kutegemea kazi ya kuajiriwa ni kutaka muhali,chambilicho wahenga mchagua jembe si mukulima. Nashukuru wanadada wetu kwa kutia bidii katika uwanja wa mziki badala ya kuwa viruka njia. Kupitia kwa sauti nyororo kama kinanda wameweza kuwavutia hata watalii kuitembelea nchi yetuna kutuachia pesa za kigeni. Nawahimiza wengi kama iwezekanavyo wajaribu bahati yao… jambo hili linajuza sana katika ujenzi wa taifa imara.

    Katika kitengo cha spoti, wanawake wamejizatiti vilivyo na kutokea watanashati kwelikweli. Wamezika katika kaburi la sahau kuwa mchezo ni utawala wa wanaume. Kwa mfano katika michezo Ya Olimpiki au jumuiya ya madola timu zetu za wanawake zimefanya vyema na kurudi nyumbani na nishani chungu nzima. Kwa wale wasiohusika katika michezo ningewasihi wajikakamue kisabuni basi wasiwaonee kijicho wenzao, kwani nyota ya mwenzio usilalie mlango wazi. Iwapo tutazingatia ufanisi katika michezo, taifa hili halina budi kuendeleza uchumi wake.

    Kwa kukunja jamvi, ningetaka kusisitiza kuwa hata igawa jitihada haziondoikudura, wanawake wetu wamefanya bidii za kutosha na inafaa wapewa nafasi sawa na wanaume katika ujenzi wa taifa. Ningewahimiza wanaume wasiwe na kinyongo dhidi ya wamawake bali chanda chema huvishwa pete. Huu ndio wito wangu na kama tujuavyo kuro hasemi uongo na mbiu ya mgambo ikilia haikosi ina jambo.

    MASWALI
    1. Fafanua dhima ya mwanamke kulingana na makala haya ( maneno 70 – 80) (al. 6)
      1. Matayarisho
      2. Nakala safi
    2. Bila kubadilisha maana fupisha aya ya pili naya tatu (maneno 50 – 55) ( al.7)
      1. Matayarisho
      2. Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Andika meneno yanayoafiki maelezo haya: al 2
      1. Nazali ya midomoni, kipasuo sighuna cha midomoni, kiyeyusho, irabu ya chini kati
      2. Kipua ghuna cha kaakaa laini, irrabu ya chini kati, kimadende ghuna cha ufizi, irabu ya chini kati
    2. Ainisha mofimu kwa kurejelea majukumu ya kisarufi katika neno hili (al.3)
      |Alijipelekea
    3. Tunga sentensi ya swali ukitumia kiwakilishi nafsi ambata nafsi ya pili wingi (al.2)
    4. Kwa kutolea .mifano, andika miundo miwili ya ngeli ya LI-YA (al.2)
    5. Andika sentensi ifuatayo kwa udogo wingi. (al.2)
      Mtoto mkaidi aliiba kitabu cha mwenzake.
    6. Tunga sentensi ukitumia nomino dhahania katika wakati ujao hali ya kuendelea. (al. 2)
    7. Andika katika usemi halisi mtindo wa kitamthilia. (al. 4)
      Khaemba Ouma alitaka kujua ni kwa nini Wandera Otieno alipenda Hisabati, Wandera Otieno akamweleza alipenda Hisabati kwa kuwa babake alikuwa mwalimu wa somo hilo.
    8. Unda nomino tatu kutokana na kitenzi safari (al.3)
    9. Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya daka na taka (al.2)
    10. Tunga sentensi mbili tofauti kuonyesha matumizi ya alama za mtajo. (al.2)
    11. Yakinisha katika umoja
      Msipofanya bidii hamtapita mtihani. (al.1)
    12. Tunga sentensi ukitumia ka kuonyesha mfulilizo wa matukio ya wakati uliopita (al.2)
    13. Unda sentensi changamano kutokana na tungo zifuatazo: (al.2)
      Mtoto alikuja nyumbani jana
      Mtoto ndiye huyu
    14. Jibu swali kulingana na agizo.
      Halima alimbebea mwalimu mzigo Kwa gari. (Anza kwa yambwa tendewa) (al. 2)
    15. Changanua sentensi ifuatayo kwa kilelezo cha visanduku. (al. 5)
      Kile kizuri kilikuwa kikitumika na baba yule
    16. Tunatumia shabaha tunapofurahishwa na jambo …………………………tunapokula kiapo na yarabi ………………………………. (al.2)
    17. Andika maana ya maneno yafuatayo: (al.2)
      1. Kula kalenda
      2. kula njaro
  4. ISIMUJAMII. (al.10)
    Janga tandavu la korona limeathiri maisha ya kila mtu duniani.Umepewa nafasi kama muuguzi kuzungumza na wanafunzi kuhusu suala hili.Andika sifa za lugha utakayotumia katika hotuba yako.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions - ACK Diocese Mumias Joint Evaluation Mock 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?