Maswali
Maagizo
- Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
- Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
- Kila insha isipungue maneno 400.
- Kila insha ina alama 20.
- Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
- Insha zote sharti ziandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
- Kurasa zote zimepigwa chapa.
- Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa kuchunguza athari za mikopo ya kifedha inayochukuliwa na serekali kutoka mataifa ya kigeni. Andika kumbukumbu za uchunguzi huo. Alama 20
- Andika insha kuhusu umuhimu wa hazina ya ustawishaji wa maeneo bunge. Alama 20
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo : alama 20
Pang’okapo jino pana pengo - Tunga kisa kitakachomalizika kwa
...... milio ya manusura wenzangu ilihanikiza ukumbi wa shule na kuyaziba masikio ya waombolezaji. Alama 20
Mwongozo wa Kusahihisha
- Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa kuchunguza athari za mikopo ya kifedha inayochukuliwa na serekali kutoka mataifa ya kigeni. Andika kumbukumbu za uchunguzi huo. Alama 20
- Inasababisha uoga mionkgoniu mwa wananchi kuwa watakuwa watumwa wa mataifa na mashirika haya.
- Mikopo huja na masharti ambayo yanaumiza kwa vile hayafaidi taifa letu. Kwa mfano kuwaajiri wafanyakazi kutoka nje kama China.
- Huenda mikopo hii ikailemea taifa letu.
- Biashara zetu na mataifa haya zitaathirika – zikakosa faida. Kwa vile mataifa haya , huenda yakawa yananunua bidhaa zetu kwa bei watakayo – hivyo sisi ndio tutawahitaji zaidi
- Kutawaliwa na mataifa au mashirika ya kifedha. Kwa mfano, masharti tutakayowekewakama kupunguzaidadi ya wafanyakazi wa serekali ilhali idadi ya watu inaendelea kuongezeka.
- Kuingilia uhuru wetu wa kibiashara pale ambapo wananchi wa mataifa hayo na mashirika yao ya kifedha wataanza kufanya biashara zinazotakikana kufanywa na wenyeji.
- Asilimia kubwa ya mapato yetu itagharamia ulipaji wa mikopo na kutuacha tukiwa wategemezi wa mashirika na mataifa hayo.
- Inachangia ukoloni mambo leo
- Inaleta utegemezi mkubwa wa taifa.
- Kupandisha gharama ya maisha kwa wananchi
- Kudunisha dhamana ya shilingi
- Uhamiaji wa wasomi na wawekezaji katika nchi zingine zilizo na sera nzuri za kibiashara na utendakazi
- Kuanguka kwa mashirika ya kibinafsi na ya kiserikali kutikana na bidhaa zinazotoka nje ya nchi kwa bei nafuu
- Andika insha kuhusu umuhimu wa hazina ya ustawishaji wa maeneo bunge. Alama 20
- Hazina hii inatumika kuimarisha na kustawisha miradi na miundo msingi katika nchi nzima - mathalani maji ya mabomba
- Kustawisha elimu – inatumika kulipia karok w awatoto mayatima na kuwasaidia wanafunzi hawa kuhitimisha masomo yao
- Wazazi wamepungukiwa na mzigo wa ujenzi wa shule. Wanaweza kushughhulikia watoto wao ipasavyo katika mahitaji mengine kama malazi na makazi.
- Uchukuzi kulahisishwa kwa vile barabara zimeboreshwa hivyo kupunguza hasara kutokana na barabara mbovu
- Kuleta maendeleo kwa wanajamii- kama vile kufadhili mradi wa kusabazwa kwa umeme
- Kuanzisha nafasi za kazi hasa katika sekta ya juakali
- Kuinua na kuboresha kiwango cha maisha ya wananchi kwa kuwaletea huduma karibu na wanakoishi kama vile ofisi za chifu
- Imeimarisha afya kwa kujenga vituo vipya vya afya kote nchini.
- Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo : alama 20
Pang’okapo jino pana pengo.
Methali hii ilenge kisa kitakachoonyesha umuhimu wa:- Mzazi baada ya kuondoka mfano kufa
- Umuhimu wa serikali iliyojishughulisha na wananchi inapoondoka na nyingine kuchaguliwa isiyoshughulika
- Kupoteza kazi na baadaye kuteseka
- Kupatwa na ajali napengine kupoteza kiungo cha mwili kama vile uwezo wakutembea
- Tunga kisa kitakachomalizika kwa
..... milio ya manusura wenzangu ilihanikiza ukumbi wa shule na kuyaziba masikio ya waombolezaji. Alama 20
Kisa hiki kifanyike katika mazingira ya shuleni- Visa vinaweza kutokana na :
- Kisa cha moto uliotokea bwenini na kuwaumiza wanafunzi
- Kisa cha mjengo ulioporomokla shuleni
- Kisa cha shambulizi la kigaidi lililotokea shuleni
- Choo ambacho kilichozama wanafunzi wakiwa ndani.
- Tukio la ambukizo la ugonjwa hatari wa Korona uliosambaa na kuwaumiza wengi
Join our whatsapp group for latest updates
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mathioya Mock Exams 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students