Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Londiani Joint Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Jibu maswali manne pekee.
  2. Swali la kwanza ni la lazima.
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki, yaani: Tamthilia, Riwaya, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.
  4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  6. Karatasi hii ina kurasa 5 zilizopigwa chapa.
  7. Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.
  8. Majibu yote sharti yaandikwe kwenye karatasi za majibu ulizopewa.

MASWALI

  1. SEHEMU YA A: USHAIRI
    SWALI LA LAZIMA.
    1. Mbiu naipulizia, kwa wa hapa na wa ng’ambo,
      Kwani ngoja ‘mesikia, inaumiza matumbo,
      Kwa upole sitafyoa, hata kama kwa kimombo,
      Yafaa jihadharia, maisha yas,ende kambo;
    2. Maisha yas’ende kombo, kututoa yetu ari,
      Zingatia haya mambo, wetu walezi mukiri,
      Kuwa wana kwa viambo, huwa Baraka na kheri
      Watunzeni na maumbo, msijezusha hatari
    3. Msijezusha hatari, na nyingi hizi zahana,
      Wazazi haya si siri, mawi mnayoandama
      Twaeleza kwa uzuri, matendoyo yatuuma.
      Watoto tunayo mori, ni lini mtajakoma?
    4. Ni nani mtajakoma, na pombe ziso halali?
      Sio baba sio mama, mbona ny’hamtujali
      Mwafa ja nzi twasema, mwatuacha bila hali
      Hangaiko acha nyuma, kwani hamuoni hili?
    5. Kwani hamuoni hili, kila mwapigana
      Nyumbanizo hatulali, jehanamu tumeona
      Mwatusumbua akili, twaumia tena sana
      Achene na ukatili, kwani upendo hamna,
    6. Kwani upendo hamna, Kama mbwa mwatuchapa
      Mwatuchoma sisi wana, mioyetu yatupapa
      Pa kujificha hatuna, tumebaki tukitapa
      Maisha hamu hayana, timevunjwa na mifupa.
    7. Tumevunjwa na mifupa, hata leo uke wetu,
      Mwatubaka na kuapa, kutung’ata nyi’ majitu,
      Maisha hatujakopa, fahamu mkosa utu,
      Hayo makeke na pupa, mtakoma utukutu,
    8. Mtakoma utukutu, na kutumia mikiki,
      Na tabia zenye kutu, tumechoka nayo chuki,
      Hatutakubali katu, kutendewa yenya siki,
      Serikali fanya kitu, kwani nasi tuna haki.

Maswali

  1. Eleza dhamira ya mtunzi wa shairi hili (alama 2)
  2. Fafanua tamathali nne za usemi zilizotumiwa katika shairi hili. (alama 4)
  3. Taja nafsi neni katika shairi hili. (alama 1)
  4. Eleza bahari nne zinazowakilishwa katika shairi hili. (alama 4)
  5. Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (alama 4)
  6. Eleza maudhui matatu yanayojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
  7. Huku ukitoa mfano taja uhuru mmoja wa mshairi ambao umetumiwa katika shairi hili. (alama 2)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA:
KIGOGO-PAULINE KEA

Jibu swali la 2 au 3
2. “Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko.”

  1. Weka maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili (alama 2)
  3. Kando na kufungiwa soko, Wanasagamoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka. (alama 14)

3. .Utawala mbaya ni tatizo sugu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika. Jadili, kwa kurejelea matukio ishirini katika tamthilia ya Kigogo. (alama 20)
SEHEMU YA C: RIWAYA:
CHOZI LA HERI-ASSUMPTA K MATEI
Jibu swali la 4 au 5
4. “ Umu hawa ni marafiki wangu wa chanda na pete. Ni watu wakarimu na wenye imani’

  1. Eleza muktadha wa dondo hili. (alama 3)
  2. Taja mbinu ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 1)
  3. Fafanua umuhimu wa Umu. (alama 6)
  4. Huku ukirejelea riwaya nzima chambua maudhui ya ukarimu. (alama 10)

5. Riwaya ya Chozi la Heri ni ya Utamaushi jadili kauli hii (alama 20)
SEHEMU YA D: HADITHI FUPI:
TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

Jibu swali la 6 au 7

6. “hebu sikiza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Tambua mbinu tatu za lugha zilizotumika katika dondoo hili na umuhimu wake (alama 6)
  3. Onyesha jinsi dhana ya nzi kufia kidondani inabainika hadithini (alama 4)
  4. Hali ya kutowajibika inajitokeza vipi katika hadithi? (alama 6)

7. Huku ukirejelea diwani ya Tumbo lisiloshiba fafanua matatizo yanayokumba vijana katika jamii (alama 20)
SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
8. Soma hadithi hii kisha ujibu maswali
Ilikuwa alfajiri yenye baridi. Umande ulitapakaa kote. Ukungu ulitanda hivi kwamba hungeweza kumuona mtu alikuwa hatua chache mbele yako.Ndovu alipoamka, alikuta fisi mlangoni pake. Fisi alikuwa amemlimia ndovu shamba lake, lakini alikuwa hajalipwa ujira wake.
Kila alipomwendea ndovu kwa ajili ya malipo yake, fisi alitiliwa huku na kutolewa kule.”Leo ni leo”,fisi alimwambia ndovu.”Nimevumilia vya kutosha. Kila siku ninapokuja kuchukua pesa zangu, hukosi hadithi mpya ya kunisimulia. Leo sitoki hapa bila pesa zangu!”
Fisi alipomaliza kumwaga joto lake, ndovu alimwambia: “Sikiliza fisi. Mimi nimeheshimika kote kijijini. Naona haja yako ni kunivunjia heshima –mbele ya familia yangu na wanakijiji kwa jumla. Sikulipi pesa zako, mpaka ujifunze kuwaheshimu wazee. Nakuamuru uondoke hapa mara moja, kabla sijakasirika! Nataka uende popote, unapofikiria kwamba unaweza kupata msaada. Ukienda kwa chifu, usisahau kwamba tunakunywa na yeye. Ukienda polisi, mkuu wa kituo amejaa tele mfukoni mwangu. Ukienda mahakamani, hakimu tulisoma darasa moja. Popote uendapo, hakuna yeyote atakayekusikiliza”
“Zaidi ya hayo, hakuna yeyote atakayekuamini.Mimi naitwa Bwana pesa.Kwangu umeota mpesapesa na kustawi. Nani ataamini kwamba naweza kushindwa kulipa vijisenti vichache ninavyodaiwa na fisi?”
Fisi alisikiliza kwa makini majitapo ya ndovu. Aliamua kumpasulia ndovu mbarika: “Bwana ndovu najua kuwa wewe una nguvu na uwezo mkubwa wa kifedha.Lakini hayo yote mimi hayanihusu ni yako na familia yako. Sitakuruhusu unidhulumu kilicho haki yangu. Usiutumie uwezo uliopewa na Muumba kuwaonea na kuwanyanyasa maskini wasio mbele wala nyuma” alimaliza usemi wake na kuondoka huku machozi yakimdondoka.
Fisi alipofika nyumbani, aliwasimulia fisi wanyonge wenzake yaliyomsibu.Fisi walikusanyika na kulizingira boma la ndovu huku wakisema: “Tunataka haki itekelezwe! Dhuluma lazima ikome! Unyanyasaji lazima ukome!” Ndovu aliposikia kelele langoni mwake, alipiga simu kwenye kituo cha polisi.
Mara, kikosi cha polisi wa kupambana na ghasi kiliwasili. Fisi walipigwa mijeledi na kuezekwa marungu. Waliojifanya mabingwa walipigwa risasi. Fisi waliosalia walikimbilia makwao, huku wakichechemea kwa maumivu. Mpaka wa leo fisi wangali wanatembea kwa kuchechemea.
Maswali

  1. Usimulizi huu ni wa aina gani? Toa sababu. (alama 4)
  2. Eleza mtindo wa lugha uliotumika katika hadithi hii. (alama 4)
  3. Eleza sifa za ndovu katika hadith hii. (alama 5)
  4. Fafanua jinsi kisa hiki kinavyo dhihirisha methali: ‘Mwenye nguvu mpishe’ (alama 4)
  5. Je, hadithi zina umuhimu gani katika jamii? (alama 3)

MWONGOZO

  1.                  
    1. Mwandishi anadhamiria kutuonyesha jinsi watoto wanadhulumiwa na
    2. kunyimwa haki na wazazi/watu waume
      zozote 2 x 1 = 2
  2. Tamathali nne za usemi
    1. Tashibihi – mwafa ja nzi, kama mbwa
    2. Methali – ngoja , mesikia, inaumiza matumbo
    3.  Msemo – kupuliza mbiu – kutangaza
    4. Jazanda – jehanamu tumeona
      Za kwanza 4 x 1 = 4
  3. Nafsineni ni mtoto 1 x 1 = 1
  4. Bahari
    1. Tarbia – mishoro 4 katika kila ubeti
    2. Pindu – utao wa mstari wa mwisho kuanza ubeti
    3. Ukaraguni - hakuna urariwa vina
    4. Manthawi – kila mshororo una vipandi viwili
    5. Sabilia – halina kibwagizo lina kimalizio
      Za kwanza 4 x 1 = 4
  5. Ubeti wa 4 kwa lugha nathari
    • Wanauliza ni lini wataacha kunywa pombe haramu
    • Wazazi wote baba na mama wanakunywa bila kuwajali
    • Wanakufa kama nzi nuia kuwaachia matatizo
    • Kwa nini hawaoni/hawatambui ukweli huu
      4 x 1 = 4
  6. Maudhui
    • Watoto ni Baraka katika jamii
    • Watoto wanaumia kwa matendo maovu
    • Madhara ya wazazi kunywa pombe
    • Watoto kupigwa vibaya na wazazi wao
    • Anakashifu ubakaji unaotekelezwa kwa watoto wa kike ya kwanza 3 x 1 = 3
  7. Uhuru wa kishairi
    • Inkisari – mesikia –nimesikia.
    • Kufinyanga sarufi – jehanamu tumeona- tumeona jehanamu
    • Ritifaa – nyi – nyinyi Za kwanza 1 x 2 = 2 Kutaja 1, Mfano 1

TAMTHILIA- KIGOGO
2.

  1.                                        
    1. Mnenaji ni Ngurumo
    2. Mnenewa ni Sudi
    3. Mahali ni Mangweni kwa Mamapima.
    4. Sudi alikuwa amemwuliza swali kuhusu watu waliokuwa sokoni iwapo wamehamia kwa Mamapima. (al 4 x 1 = al 4)
  2. Kinaya- Watu wamekuja kuuguza majeraha ilhali wengine wanakufa na kupofuka kwa pombe.
    Swala balagha- Ulitaka wahamie wapi siku kama hizi?
    Kutaja: - 1
    Mfano: - 1 (1 x 2 = al 2)
  3.                
    1. Majoka anawaua wapinzani wake kisiasa ili kuzuia upinzani: Jabali.
    2. Majoka analifunga soko la Chapakazi na kuwafanya watu wateseke: Ashua, Sudi
    3. Sumu ya nyoka inayotengenezwa na kampuni ya Majoka inapenya shuleni, wanafunzi wanaitumia na hivyo kuwafanya makabeji.
    4. Majoka anamfungia Ashua gerezani ili kumlazimisha Sudi kumchongea kinyago cha Ngao.
    5. Majoka anaagiza Ngurumo kuuliwa ili asitoboe siri ya njama yake ya kutaka kumwangamiza Tunu.
    6. Majoka anawapa watu kibali kukata miti, jambo linaloacha ardhi kuwa jangwa hivyo mazao kupungua: Hashima anasema alivuna kichele tu.
    7. Majoka analifunga soko la Chapakazi kama njama ya kumnasa Ashua ili kutimiza ashiki zake za kimapenzi.
    8. Uongozi wa Majoka unasambaza vijikaratasi kuwachochea watu kuhama Sagamoyo. Jambo ambalo linawatia watu hofu: Siti
    9. Majoka anawapa polisi kibali cha kuwashambulia waandamanaji, jambo linalopelekea vijana tano kuuliwa.
    10. Majoka anampa kibali Asiya kutengeneza pombe haramu, watu wengi wanaaga na wengine kuwa vipofu.
    11. Majoka anamfuta Kingi kazi baada ya kukaidi amri yake ya kuwafyatulia watu risasi.
    12. Majoka, Chopi na Ngurumo wanapanga njama ya kumwangamiza Tunu. Tunu anavunjwa mundu wa mguu.
    13. Majoka anaamrisha vituo vya kutangaza habari kufungwa ili kubakie tu na kimoja.
    14. Majoka anamtumia Husda ujumbe mfupi afike ofisini mwake ili kuchongea ugomvi kati ya Husda na Ashua. Jambo linalopelekea Ashua kupigwa na kupata majeraha.
    15. Majoka anaamrisha wafadhili wa upinzani kuhama kutoka jimbo la Sagamoyo.
    16. Majoka anawaongezea mishahara walimu na madaktari na pia kuongeza kodi maradufu. Jambo linalofanya bei ya vyakula kupanda.
    17. Majoka anakopa pesa kutoka mataifa ya Magharibi kufadhili miradi duni ya kuchonga vinyago. Mikopo hii ingelipwa na vizazi kwa miaka mia moja.
    18. Majoka anaagiza watu kusherehekea uhuru wa jimbo la Sagamoyo kwa mwezi mmoja. Jambo hili lingeathiri uchumi wa Sagamoyo.
    19. Kandarasi zinapeanwa kwa njia ya ufisadi. Asiya licha ya kuoleka na Boza anashiriki mapenzi na Ngurumo ili apewe kandarasi ya kuoka keki.
    20. Majoka anamlazimisha Tunu kuoleka na Ngao Junior ili kudhoofisha upinzani.
    21. Ardhi ya soko la Chapakazi inagawa na Majoka pamoja na washiriki wake wa karibu kama vile Kenga, jambo ambalo linawaathiri wachuuzi kiuchumi.
    22. Uongozi umesalia katika familia moja ya Majoka tangu uhuru ulipopatikana, jambo ambalo linaathiri upinzani: Jabali anauliwa; Tunu anaumizwa mguu. (za kwanza 14 x 1 = al 14)

3. Utawala mbaya ni tatizo sugu linalozikumba nchi nyingi za kiafrika.

  1. Uongozi umesalia katika familia moja ya kina Majoka tangu uhuru ulipopatikana.
  2. Badala ya kupiga vita pombe haramu, serikali inatoa kibali cha kuuza pombe hiyo kinyume na sheria.
  3. Badala ya kulinda usalama, polisi wanatumiwa kuwatawanya na kuwapiga watu wanaoandamana kwa amani.
  4. Viongozi wa upinzani ambao wanapinga utawala wa kiimla wa Majoka wanauawa k.v Jabali.
  5. Majoka ana unafiki kwani anasema wasiruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kikoloni kuwarejesha katika utumwa. Yeye anatenda mambo yayo hayo anayoyakashifu.
  6. Watawaliwa wanapumbazwa kwa nyimbo na matangazo kwenye vyombo vya habari. Wimbo wa kizalendo unatumiwa kumsifu Ngao, kiongozi wa Sagamoyo.
  7. Viongozi k.v Majoka wanapanga kuongeza misharara ya walimu na wanguzi kisha wapandishe kodi.
  8. Viongozi kutumia propaganda. Wanatumia vyombo vya Dola k.v tevevisheni na askari kama njia ya kuoneza propaganda zao.
  9. Utawala unajaribu kutumia hila kuwatenganisha Tunu na Sudi ili kudhoofisha upinzani. Majoka anapendekeza Tunu aolewe na Ngao Junior.
  10. Mojaka anapanga njama ya kumuua Ngurumo kisha anapendekeza chatu mmoja atolewe kafara ili watu wasitilie maanani kifo chake.
  11. Serikali inakopa pesa nyingi kugharamia miradi duni ya kuchonga vinyago.
  12. Ardhi ya sokoni inagawiwa washiriki wa karibu wa Majoka k.v Kenga.
  13. Serikali inashiriki katika biashara ya kukata na kuuza miti badala ya kutunza mazingira.
  14. Badala ya kuchimba mabwawa ya maji itakayowanufaisha wananchi wote, viongozi wanajichimbia visima katika maboma yao.
  15. Viongozi wanatumia vyeo vyao kuwashinikiza watu kutekeleza matakwa yao. Majoka anapanga njama ya kumtia Ashua mbaroni ili amshinikize Sudi kumchongea kinyago.
  16. Majoka anaagiza watu kusherehekea uhuru wa jimbo lao kwa mwezi mmoja.
  17. Soko la Chapakazi linanuka uvundo wa maji chafu kwenye mitaro licha ya wananchi kulipa kodi.
  18. Kandarasi zinapoanwa kwa njia ya ufisadi.
    Ngurumo mshiriki wa karibu wa Majoka anakula uroda na Asiya na kumpendekeza apewe kandarasi ya kuoka keki.
  19. Majoka and Majoka Company inatengeneza dawa za kulevya na kuharibu vijana akiwemo Ngao Junior.
  20. Majoka and Majoka Academy inawaharibu wanafunzi na kuishia kuwa makabeji kwa kutumia dawa za kulevya.
  21. Majoka anakopa pesa kutoka mataifa ya magharibi kufadhili miradi duni ya kuchonga vinyago.
  22. Mama pima anapika pombe haramu kwa kibali cha Majoka ilhali ni kinyume na katiba.
  23. Majoka anaagiza televisheni ya wazalendo ifungwe ibaki tu yake ya sauti ya mashujaa.
  24. Majoka anatumia ushirikina katika uongozi wake. Nembo ya chama chake ni swira / nyoka.
    (za kwanza 20 x 1 = al 20)

RIWAYA- CHOZI LA HERI
4

  1. mnenaji :mawazo ya Umu ya maneno ya mwalimu Dhahabu
    Mahali: shuleni Tangamano
    Sababu: Mwangeka na Apondi walikuwa wamekuja kumpanga Umu. (Alama 1X3)
  2. msemo- chanda na pete
  3. Umuhimu wa Umu
    1. Ni kielelezo cha vijana wasiokufa moyo maishani hata wanapokumbwa na shida tele
    2. Anaendeleza maudhui ya uwajibikaji anapowalea wadogo wake sophie na Ridhaa wazazi wake wanaposafiri
    3. Ananendelelza maudhui yautu anapompa ndugu yake chakula chake
    4. Anajenga sifa za Mwangeka na apondi kama wakarimu
    5. Anajenga sifa za sophie kama mwenye hasira anapokuwa dawa yake ya hasira zake za kivolkani
  4. Ni tendo la kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali bila masharti
    • Ridhaa anatumia uwezo wake kuwavutia wanakijiji maji ya mabomba ili yawapunguizie makali ya ukosefu wa maji uk 11
    • Shirika la makazi bora linajitolea kuwajengea wakimbizi wa msitu wa mamba makazi ma kuwapa vyakula na maji uk 11
    • Ridhaa aliwasaidia watu mbalimbali kutokana na matatizo mengi waliyokuwa wakiyashuhudia uk 35
    • Mashirika yasiyo ya kiserikali yanawatuma wawakilishi wao ili kuwapa ushauri na nasaha waathiriwa wa makabiliano yaliyowaishia kulowea msitumi uk 36
    • Julida anamkaribisha umu kwa furaha na kumhakikishia kwamba atakuwa salama hadi wakati atakapokabidhiwa kwa idara ya watoto uk 189
    • Marafiki wapya wa umu shuleni wanamhimiza kwa ukarimu avumilie maisha ya shule mpya, kwani siku moja atayazoea uk 91
    • Mtawa pacha anawonyesha zohali ukarimu kwa kumuokoa kutoka njia ya uharibifu uk 99
    • Mwalimu mkuu Bi Tamasha wa shule ya msingi wa kilimo anasikiliza kwa makini na ukarimu mkuu masaibu ya chandachema na hatimaye kumsaidia uk 105
    • Chandachema anaokolewa na shirika la hakikisho la haki na utulivu uk 107
    • Mwangeka na apondi wanakuwa wakarimu kwa watu wenye mahitaji mbalimbali uk 116
    • Apondi na mwangeka wanakubali kumchukua umu kama mtoto wao wakiwa radhi kumtunza uk 117
    • Neema na mwangemi wanakuwa wakarimu wanapokubali kumchukua mwaliko kama mtoto wao wa kupanga. (alama 1x10)

5. utamaushi ; ni ile hali ya kukata tamaa kwa jambo Fulani maishani. Wahusika mbalimbali waliweza kukata tamaa kwa njia moja aua nyingine;

  • Pete anakata tamaa maishani baada ya kupata watotto watatu akiwa chini ya miaka shirini na moja jambo linalomfanya kutaka kujiua
  • Ridhaa mkewe na familia yake ilipoangamia kwa moto alikata tamaa ya mapenzi katika maisha yake
  • Zohali licha ya kuzaliwa katika familia ya tabaka la juu anakata tamaa katika maisha na kuingia mtaani kutumia gundi na wenzake
  • Mwangemi na Neema wanakata tamaa ya kupata mtoto na kuamua kupanga Mwaliko
  • Shamsi anakata tamaa ya kupata kazi na kudhamini pombe licha ya kuwa wa kwanza kuingia chuo kikuu kutoka eneo lao’
  • Naomi anakata tamaa kuishi na Lunga na kuamua kwenda kutafuta kazi mjini
  • Naomi anakata tamaa kuishi mjini na kurudi msitu wa samba ila anakuta Lunga aliaga na watoto wakaondoka
  • Umu anakata tamaa ya kupata nduguye hasa baada ya kugundua kuwa hapati usaidizi katika kituo cha polisi
  • Mwanaheri anakata tamaa baada ya kifo cha mamake Subira
  • Subira anakata tamaa ya kuishi kwa Kaizari kutokana na chuki ya mamamkwe kwa kiini kuwa hawakuwa wametoka katika jamii moja
  • Lunga anakata tamaa ya maisha baada ya kuachishwa kazi, kunyakuliwa kwa mazao yake na kuachwa na mkewe jambo linalosababisha kufa kwake
  • Chandachema anakata tamaa baada ya nyanya yake kufariki na kunyanyaswa na jirani yake satua. (Alama 1x10)

HADITHI FUPI
Tumbo lisiloshiba na Hadithi zingine
6. “Hebu sikiliza jo! Pana hasara gani nzi kufia kidondani?”

  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 4)
    Kauli ni ya Otii
    Msemewa ni rafiki yake
    Rafiki yake alikuwa akimtahadharisha dhidi ya wasichana warembo anapotambua ana uhusiano na Rehema.
    Otii anasema maneno haya ili kujitetea na kuuhalalisha uhusiano wake na Rehema
  2. Tambua mbinu tatu za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili na umuhimu wake (alama 6)
    1. Nidaa - “Sikiliza jo!” Otii anadhihirisha hisa zake za hasira anapokosolewa na rafiki yake.
    2. Balagha – “Pana hasara gani nzi kufia kidondani. Otii anadhihirisha hisia kuwa tayari anaelewa anachokifanya na rafikiye hana haja ya kuingilia lisilomhusu.
    3. Methali - methali nzi kufa juu ya kidonda si hasara imedokezwa. Methali hii inatumika kuonyesha kuwa anaelewa hasara zinazoweza kutokana na mahusiano yake na vimanzi.
      Pia inadhihirisha mapuuza ya Otii (3 x 2 = 6)
  3. Dhana ya nzi kufia kidondani inavyobainika katika hadithi (alama 4)
    1. Otii anaugua maradhi ya ukimwi na kuishia kujutia kitendo chake
    2. Rehema anaangamia kwa ukimwi katika harakati za kujitafutia raha
    3. Otii anaishia kuvunjika muundi wake akiwa katika raha za kucheza kandanda.
    4. Otii anakonda kama ng’onda na kubakia mwembamba kama sindano
      (4 x 1 = 4)
  4. Jinsi hali ya kutowajibika inavyojitokeza katika hadithi (alama 6)
    • Hospitali zinashindwa kuwajibikia hali ya wagonjwa.
      Otii anarejeshwa nyumbani
    • Vyombo vya habari vinashindwa kuwajibikia hali ya Otii hasa baada ya kuvunjika muundi. Wanamfuata Otii anapokuwa na afya na umaarufu.
    • Serikali inamtelekeza Otii baada ya kuvunjika muundi.
    • Otii anakosa kuwajibikia maisha hata baada ya kuonywa na rafiki yake.
    • Rehema anakosa kuwajibikia ujana wake. Anaendeleza maradhi ya ukimwi
    • Wanachama wa chama cha nyumbani wanapuuza agizo la Otii la kuzikwa Mombasa badala ya nyumbani Sidindi.
    • Klabu ya Bandari FC haikumjali mchezaji wao hodari Otii baada ya kuvunjika muundi.
      ( 6 x 1 = 6)

MATATIZO YA VIJANA
7. Umaskini. Hadithi ya ‘Mapenzi ya kifaurongo’ Dennis Machora anakunywa uji bila sukari

  • Hana pesa/maskini
  • Ni zikeni papa hapa Otii anaishi kwenye kibanda kilichotalizwa kwa udongo na kuezekwa kwa makuti
  • Dawa za kulevya. Hadithi ‘Mkubwa’ vijana wanakufa kwa sababu ya kutumia dawa za kulevya.
  • Kubakwa ‘mame Bakali’ Sara anabakwa akitoka kuhudhuria masomo ya ziada usiku.
  • Kuavya mimba ‘Shogake dada ana ndevu’ SAfia anaavya mimba, inayosababisha kifo chake.
  • Kuvunjika kwa Uchumba ‘Mapenzi ya kifaurongo Peninah anavunja uchumba wake na Dennis Machora kwa sababu ya Dennis kuwa maskini.
  • Ukosefu wa ajira ‘Mapenzi ya Kifaurongo’ Dennis amekamilisha masom ya chuo kikuu lakini ametafuta ajira kwa miaka mitatu bila mafanikio.
  • Magonjwa – Nizikeni papa hapa’ Otii anaambukizwa virusi vya ukimwi Rehema Wanjiru
  • Tamaa ya Mapenzi “Nizikeni papa hapa” Otii ana tamaa ya mapenzi.
  • Mimba za mapema ‘hadithi ya Mame Bakari’
  • Mhusika Sarah
  • ‘Shogake dada ana ndevu’ Safia.
  • Malezi duni- Mashaka alikosa mapenzi ya wazazi wake
    Elimu duni- Mashaka hakupata masomo ya kiwango cha kumpa kazi. (Zozote 10x2) MTAHINI AKADIRIE MAJIBU MENGINE YA MWANAFUNZI.

8. FASIHI SIMULIZI
8. -Hurafa (alama 1)

Ameshirikisha wanyama kama wahusika (alama 1)
0. Usuli

  1. Unaeleza chanzo cha fisi kuchechemea (alama 1)
    1. Methali - Leo ni leo
      1. Semi
        1. Kumpasulia mbarika
        2. Kuvunjia heshima
        3. Wasio na mbele wala nyuma
        4. Amejaa tele mfukoni.
          Kutaja 1 Mfano 1 Zozote 2 x 2 = 4
    2.                                      
      1. Mwenye majitapo
      2. Mwenye nguvu
      3. Mwenye uwezo mkubwa
      4. Mdhalimu
      5. Mnyanyasaji
      6. Mjeuri Zozote 5 x 1 = 5
    3.                                
      • Ndovu ni mwenye nguvu
      • Anamdhulumu fisi kwa kutomlipa pesa baada ya kufanya kazi shambani.
      • Fisi hana nguvu / mnyonge
      • Fisi wanapoamua kuitisha haki wanapigwa mijeledi na waliosalia kuchechemea kwao.
        Hoja 4 x 1 = 4
    4. Kuelimisha
    5. Kuburudisha
    6. Kuendeleza maadili zozote 3 x 1 = 3
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Londiani Joint Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?