Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mokasa II Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

  1. Lazima
    Visa vya ukiukaji wa kanuni za shule vimekithiri katika Shule ya Tangamano. Wewe kama mwalimu mkuu wa shule hii, waandikie wanafunzi memo kuhusu suala hili huku ukipendekeza hatua zitakazochukuliwa.
  2. Asasi mbalimbali katika jamii zafaa kushughulikia kuwepo kwa mshikamano wa kitaifa. Fafanua
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali:
    Atafutaye hachoki na akichoka keshapata
  4. Tunga kisa kitakachokamilika kwa maneno yafuatayo:
    … kwa kweli, kulizukamseto wa mawazo baada ya tukio hilo.

Mwongozo Wa Usahihishaji

  1.  Huu ni utungo amilifu (memo). Vipengee viwili vikuu vishughulikiwe; muundo /sura na maudhui.
    1. Muundo
      1. Anwani ya shule /mahali
      2. Nembo ihusishe neno MEMO/ARIFA chini ya anwani
      3. Mtajo :
        1. Kutoka kwa : Mwalimu mkuu
        2. Kuenda kwa: Wanafunzi
        3. Tarehe :
        4.  Kuhusu : Mada.
      4. Hitimisho:
        1. Sahihi
        2. Jina
        3. Cheo.

          Sura ya memo ibainike waziwazi. Mtahiniwa aondolewe alama (4s) sura baada ya kutuzwa iwapo amekosa vipengee muhimu vya (iii) na (iv).
          Akikosa vipengee vichache vya sura, lichukuliwe kuwa kosa la mtindo.
    2. Maudhui
      • Maudhui yajitokeze kuwili; visa na mapendekezo/hatua.
      • Mtahiniwa atakayehulutisha hatua atakuwa amepungukiwa kimaudhui.

        MIFANO
        1. Visa vya wizi shuleni > kulipia mara dufu.
        2. Kupigana shuleni > kurejeshwa nyumbani
        3. Sare zisizo rasmi > kuchukuliwa au hata kuchomwa.
        4. Kurejelea mlo kabla ya wengine > kusafisha bwalo /vyombo siku nzima. Kuzungumza kwa lugha isiyo rasmi > kushinikizwa kuzungumza lugha hiyo gwarideni.
        5. Matumizi ya mihadarati > kupelekwa kwenye vituo vya kurekebishia.
        6. Kutumia vijia mbadala shuleni > kuziba mianya yote yenye vijia hivyo.
        7. Utupaji ovyo wa taka > kuondoa mabiwi yote ya taka shuleni.
        8. Kuchelewa kufika darasani > kupiga magoti darasani kipindi kipindi kizima.
        9. Kukosa kufanya kazi darasani /shuleni > kupewa kazi mara dufu.
      • TANBIHI
        1. Haya ni mapendekezo tu au hatua za kuchukuliwa.
        2. Kadiria mapendekezo ya mtahiniwa mradi tu yamo katika mawanda ya shule.
        3. Mtahiniwa sharti ataje adhabu inayopendekezwa wala sio kusema tu ; ataadhibiwa vikali.
      • UTUZAJI
        • Mtahiniwa ajadili angaa hoja sita na kutoa mapendekezo
        • Atakayezua visa bila mapendekezo atakuwa amejibu swali nusu. Asipite alama 10/20 C+
  2. Swali la mjadala
    • Hili ni swali la ufafanuzi. Mtahiniwa afafanue hoja zake akirejelea namna asasi mbalimbali za jamii zinafaa kushughulikia mshikamano wa kitaifa.
    • Mtahiniwa atoe mapendekezo – yale asasi zafaa kufanya.
    • Mtahiniwa atakayezungumzia yaliyofanywa atakuwa amepotoka kimaudhui.
    • Baadhi ya hoja ni kama zifuatazo:
      1. Wanasiasa wanafaa wahubiri umoja na wala si kuwachochea wananchi.
      2. Taasisi za elimu ziweze kuchangia umoja wa kitaifa kwa kuwaalika wanafunzi kutoka sehemu zote za nchi kujiunga na kidato cha kwanza.
      3. Taasisi za elimu pia zifunze umoja miongoni mwa wanafunzi bila kujali tabaka, kabila na wala rangi ya mhusika. Hal hii itachangia kuendeleza mshikamano kitaifa.
      4. Asasi za kidini zihubiri wananchi kuishi pamoja bila ya kubaguana. Ujumbe wa dini kuu nchini ni wa kutobaguana.
      5. Serikali ihakikishe kuwa kipengee cha katiba kinachomkubalia yeyote kuishi na kufanya biashara au kazi popote nchini kimezingatiwa.
      6. Nafasi za kazi katika kila taasisi iwe ya umma au ya kibinafsi zigawanywe kwa usawa bila kuzingatia kabila, eneo analotoka mtu au dini yake.
      7. Serikali kuu au zile za kaunti - Ugavi wa raslimali za nchi uwe wa usawa bila kubagua eneo lolote la nchi./kaunti.
      8. Ndoa mseto ziungwe mkono kwani ni njia mojawapo ya kuziunganisha jamii kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
      9. Aila zihimize watoto kutangamana wao kwa wao bila kubaguana kwa namna yoyote ile.
      10. Wananchi waweze kuzuru sehemu mbalimbali za nchi ili kuweza kufahamiana na watu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
      11. Katika biashara, masoko yanayowajumuisha wafanya biashara kutoka sehemu mbalimbali za nchi yahimizwe. Kufanya biashara pamoja kutachangia utangamano kwa kiwango kikubwa.

        Atakayezua na kueleza hoja sita atakuwa amejibu swali
  3. Swali la tatu
    1. Hii ni insha ya methali (Atafutaye hachoki na akichoka keshapata)
      • Hili ni swali la methali
      • Mtahiniwa asimulie kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali hii
      • Mtahiniwa anaweza kumulika hali zifuatazo:
        1. Mtoto ambaye anatoka katika familia ya kichochole anakosa karo lakini kwa bahati nzuri akampata mfadhili anayempa ruzuku ya kimasomo. Anajibidiisha kimasomo na anafaulu kujiunga na chuo kikuu.
        2. Mtoto ambaye anapoteza wazazi wake analazimika kukatiza masomo yake kwa ukosefu wa karo.Baada ya muda mrefu wa kukaa nyumbani, anapata mhisani aliyejitolea kulipia karo yake baada ya masaibu yake kuangaziwa katika vyombo vya habari. Anasoma kwa kujituma na hatimaye anafaulu
        3. Mtu aliyekuwa na maono ya kuwa pengine daktari,mwalimu au rubani anajikakamua kimasomo na kufaulu kusomea taaluma aliyokuwa akiitamani.
        4. Mfanyakazi fulani ambaye alitaka naisesheni kazini.Alifanya kazi yake kwa juhudi kuu na hatimaye akafaulu kupandishwa cheo pengine kuwa meneja kurugenzi, mkurugenzi au msimamizi wa masuala ya wafanyakazi.
        5. Mkulima ambaye alijituma katika shughuli za kilimo. Licha ya vizingiti vingi alivyokumbana navyo ikiwemo ukosefu wa pembejeo na hata halianga isiyotabirika, hatimaye jitihadi zake zilizaa matunda.
        6. Kijana kutoka familia iliyolemazwa na ukata anadhamiria kuoa kutoka katika familia fulani lakini posa yake inakataliwa. Anajikakamua kwa kufanya vibarua vya hapa na pale na kutunduiza fedha kiasi cha haja. Anapoleta posa mara ya pili inakubaliwa na hivyo anapata barafu ya moyo wake.

          TANBIHI
          • Sharti kisa cha mtahiniwa kionyeshe hali zote mbili: yaani mhusika ambaye alikuwa katika hali fulani ya uhitaji na namna alivyofanya bidii ili kujiopoa kutokana na hali hii tete.
            Au
            Mhusika aliyewania kitu fulani maishani na mbinu alizotumia kuafikia tamanio lake
            Atakayekosa kushughulikia pande zote mbili za methali atakuwa amepotoka – atuzwe D- 03/20
  4. Swali 4
    • Tunga kisa kitakachokamilika kwa maneno yafuatayo:
      ... kwa kweli, kulizuka mseto wa mawazo baada ya tukio hilo.
    • Hii ni insha ya mdokezo inayomhitaji mtahiniwa kuyasanisi mawazo yake na kubuni hadithi inayoafikiana na mwisho huu.
    • Mtahiniwa atunge kisa kitakachoonyesha hali zifuatazo:
      1. Kisa chenye tukio na ambacho mwishowe kilimwacha mtahiniwa katika hali tatanishi kimawazo.
      2. Kisa chenye tukio na ambacho mwishowe kilizua hali tatanishi ya kimawazo.
    • Mwanafunzi lazima akamilishe kwa maneno yayo hayo atakayepachika tu maneno hayo na atakayekosa kukamilisha kwa maneno hayo atuzwe 03/20
    • Kisa kiegemee upande mmoja (tukio zuri au tukio baya)
    • Kuonekane mseto/mchanganyiko wa mawazo kinzani.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mokasa II Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?