Kiswahili Paper 2 Questions - Maranda Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Jibu maswali yote.
  2. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

MASWALI

  1. UFAHAMU: ( Alama 15)
    Soma maigizo yafuatayo kisha ujibu maswali.
    (Asubuhi. Kijiji kimetulia. Nje ya nyumba ya Mzee Kasi.)
    Mzee Kasi: (Kwa hasira) Siwezi kukubali kuona mambo kama haya yakitendeka hapa kwangu nyumbani. Mimi leo nimekuwa mtu wa kuchezewa? Sasa nitakuwa mtu wa kupigiwa mfano mbaya. Haiwezekani! Atakiona leo. (Anaita) Mama Subira! Niletee bakora yangu.
    Mama: (Akileta bakora. Ana mshangao mkubwa) Ni adui yupi aliyetuvamia jamani? Mama wee!
    Mzee Kasi: (Bado amelemewa na hasira) Leta haraka! Maswali mengi ni ya nini? (Anaipokea) Sasa kwaheri. Tena ya kuonana. Ninaweza kuja nikiwa hai, kuletwa kwa machela au kurudi jina tu.
    Mama: (Anashtushwa na usemi huo) Unamaanisha nini mume wangu?
    Mzee Kasi: Ni hivyo hivyo ulivyosikia. Naenda kupambana. Mzee Fosi hawezi kuibarizi roho yake huku mimi kaniachia saratani ya moyo. Binti yangu wamemfikisha kilele hiki? Tangu juzi anatapika tu. Hakosi ni huyu Jodari. Kila mara wanafuatana njia moja kwenda shuleni.
    Mama: Si mpaka tufanye uchunguzi. Huwezi kuchukua hatua yoyote kabla ya kupata uhakika. Yaweza kuwa Jodari hana makosa.
    Mzee Kasi: Acha kumtetea. Niache nikamtie adabu. (Anaondoka.)
    Mama: Ningoje tuandamane.
    Mzee Kasi: Kaa papo hapo. Yale unayotaka kwenda kuyashuhudia huko utayasikia redioni kesho. (Mama anabaki. Hana la kufanya.)
    (Nyumbani kwa Mzee Fosi. Asubuhi iyo hiyo. Mama Jodari anaosha vyombo. Pana mbuzi amefungwa karibu na njia)
    Mzee Kasi: (Anamtandika bakora yule mbuzi) Ondoka njiani! Huna adabu kama hawa wanaokufuga.
    Ma Jodari: (Kwa mshangao) Haya! Kuna nini? Mbona unatujia na vituko leo? Mbuzi amekutenda nini jamani?
    Mzee Kasi: Wewe wajua vituko? Bado hujaona vituko. Yu wapi mumeo? Mtoe hapa tupambane.
    Ma Jodari: Kwani jamani una nini leo? Hebu tulia unieleze.
    Mzee Kasi: Nani atulie? Mnataka kunitia aibu kijiji kizima. Sina pahali pa kuficha uso wangu.
    Ma Jodari: Aibu gani Mzee Kasi?
    Mzee Kasi: Msinizungushe hapa. Yaani yote haya yanayoendelea hamyaoni? Kweli kigumba ni kwa nguruwe...
    Mzee Fosi: Nakusalimia Bwana Kasi. (Mzee Kasi haitikii.)
    Mzee Kasi: Sitaki salamu zako. Nenda kasalimie kombamwiko chooni.
    Mzee Fosi: Ee! Leo una nini? Pepo gani kakupanda bwana we?
    Mzee Kasi: Pepo wa kucharaza bakora.
    Mzee Fosi: Acha mzaha. Hebu tuliza moyo na tuzungumze yaliyokuleta hapa.
    Mzee Kasi: Nikueleze nini na unayajua yote. Kwani Jodari si mwanao?
    Mzee Fosi: Ni mwanangu. Ala! Ana nini?
    Mzee Kasi: Imekuwa hujui? Utajuaje na si wewe uliyeharibikiwa?
    (Jodari anaingia. Mzee Kasi anamkodolea macho kwa hasira. Anamrukia na kumchapa bakora. Wanashikana miereka. Wanaangushana chini, wanaviringishana)
    Ma Jodari: Majirani njooni! Watauana!
    Mzee Kasi: Utakiona cha mtema kuni leo. Utalipa deni la utovu wa adabu. (Anamkaba koo)
    (Wazazi wa Jodari wanawatenganisha, majirani wanaingia)
    Mzee Kasi: Niacheni nimtie adabu.
    Jirani: Msalie mtume! Hebu tulia tuyatatue haya mambo kwa upole.
    (Mzee wa Kijiji anaingia)
    Mzee Kijiji: Hebu kila mtu atulie
    Amani itufikie
    Mambo mema yatujie
    Mabaya yatuondokee.
    Tuzungumze tuelewane
    Nasaha zetu zifane
    Maovu tukanyane
    Tukae tupendane.
    Watu wote: (Wanaitikia) Amina.
    Mzee Kijiji: Tutulieni sote. Bila kupoteza wakati wowote, nataka Mzee Fosi atusimulie chanzo cha zogo na zahama hii.
    Mzee Fosi: Wazee wenzangu, mimi sina mengi ya kueleza ila nina masikitiko na mshangao tu kwa yaliyotokea. Hakuna siku tumekosana kabisa. Ajabu ni hii leo aliponiraukia kwa hasira na hatimaye kumcharaza kijana wangu bakora bila sababu yoyote. Ni hayo tu.
    Mzee Kasi: (Anasimama na kuotesha bakora) Wewe Fosi tuheshimiane. Yaani unadhani mimi ni...
    Mzee Kijiji: (Anamkatiza) Tulia usituletee fujo hapa. Haya tuambie nawe.
    Mzee Kasi: Huyu Fosi hana adabu. Inaonekana wazi kuwa ameshindwa kabisa kuiongoza jamaa yake. Hajamfunza maadili huyu Jodari. (Anamuotesha bakora) Je, ni haki kijana wa Mzee Fosi kumringa binti yangu? (Watu wanatazamana kwa mshangao) Hii ni haki kweli? Huu ndio ... ndio ujirani mnaoutaka kijijini hapa? Haya ni makosa na sitamsamehe. Nataka anilipe ng’ombe arubaini, mbuzi ishirini, mchele na ...
    Mzee Kijiji: Hebu komea papo hapo. Wewe una ushahidi gani kuwa bintiyo ni mjamzito?
    Mzee Kasi: Huniamini? Kila mtu anawaona wakienda shule pamoja. Sasa tangu juzi Subira anatapika tu, mwili ni moto na kazi yake kulala tu.
    (Watu wanacheka)
    Mzee Kijiji: Tusipoteze wakati bure. Hili jambo lazima lithibitishwe. Mzee Kaja, andamana na wazazi wa Jodari na wa Subira pamoja na Subira mwenyewe mpaka hospitalini. Huko akapimwe kuhakikisha kama ni mjamzito. Kesho tukutane hapa tena kujua la uhakika.
    (Watu wanakubaliana hivyo. Wanafumukana. Siku ya pili. Watu wamekutanika. Ripoti ya daktari inasomwa. Inaeleza kuwa Subira ana homa ya malaria)
    Mzee Kijiji: Natumai sote tumeisikia ripoti ya daktari. Sasa wazee wenzangu mna nasaha gani?
    Mtu 1: Mimi naonelea kuwa Mzee Kasi amlipe Jodari kwa kosa la kumtandika bakora na pia kuzusha rabsha katika boma la Mzee Fosi.
    Kijana: Mtambua ndwele ndiye mganga. Tuongoze wewe.
    Mtu 11: Apelekwe polisi. Kwanza acha niende nikawaarifu. (Anatoka mbio)
    MTU 111: Ile mali aliokuwa akidai alipwe, sasa ailipe yeye. Lililompata peku na ungo pia.
    Mzee Kasi: Mimi silipi chochote. Na liwe liwalo.
    Mtu 1: Anajibu kwa ujeuri! Acheni tumtie adabu. (Anamzaba kofi. Mzee Kasi anaona vimulimuli na kuramba sakafu. Umati wa wanakijiji unamsogelea. Wako tayari kumpiga.)
    Mtu 11: Atiwe adabu. Mchezea tope humrukia.
    Mzee Kasi: (Akiwa na wasiwasi mkubwa.) Ndugu zangu. Nawaomba msamaha. Tafadhali ... ngojeni kwanza. Nisameheni. Mwana akinyea kiweo hakikatwi... tafadhali ndugu.
    Mzee Kijiji: Msichukue sheria mikononi. Rudini nyuma. Mwacheni. Amekiri makosa yake.
    (Watu wanazidi kumfuata Mzee Kasi. Anajaribu kusema. Sauti imemezwa na kelele. Mtu mmoja anainua gongo)
    Mtu 11: Polisi hao! (Gari la polisi linaingia. Wanashuka upesiupesi. Watu wanashtuka. Kila mtu anaangusha alichokibeba. Wanatawanyika isipokuwa wazee watano wa kijiji na Mzee Kasi)
    1. Kwa mifano minne, thibitisha kuwa jina Mzee Kasi linamwafiki. (alama 4)
    2. Onyesha mikakati minne ya kusuluhisha migogoro kwa mujibu wa maigizo. (alama 4)
    3. Andika mafunzo yanayojitokeza katika mchezo huu. (alama 3)
    4. Fafanua uhusiano uliokuwepo kati ya familia za Mzee Kasi na Mzee Fosi. (alama 2)
    5. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika kifunguni. (alama 2)
      1. Kuibarizi........................................................................................
      2. kuramba sakafu............................................................................
  2. UFUPISHO (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
    Sisi vijana wa Kenya inatuwajibikia kufanya kazi kwa bidii, na kwa dhati ya moyo wetu tuweze kupata ufanisi, na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke “ ajizi ni nyumba ya njaa” kwa hivyo hatufai kulaza damu tukiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga. Lazima tufanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na ya watu wazima, kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa lenye watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kuweza kutekeleza mipango mbali mbali ya maendeleo. Tupende, tusipende lazima tuzidishe mazao ya mashambani, kwani kila kukicha idadi ya watu nchini inaongezeka. Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya hayo pia lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni Wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wa biashara. Wengi ni wale wenye mawazo ya kwamba lazima kila mmoja aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya mwananchi wa Kenya badala ya kuwaachia ambao hawahusiki.
    Mafunzo tunayoyapata majumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya Mwanakenya kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayotupumbaza na kutufanya tusione mbele, sisi vijana tukiwa viongozi wa siku zijazo tuwe kielelezo chema kwa wengine. Watu lazima washirikiane na kufikiria kwamba wao ni wamoja, “utengano ni uvundo”. Lugha ya taifa ndicho chombo cha pekee ambacho kitatuunganisha na kuweza kutuwasilishia mapendekezo, mawaidha na hisia zetu. Kukosa ndiko kibinadamu, wakati tunapokosea lazima tukubali tumekosea na kufanya masahihisho mara moja, kwani “usipoziba ufa utajenga ukuta”. Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu na wenzetu. Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi yetu tukiwa wazalendo halisi. Sisi tukiwa vijana sharti tujishughulishe na kuangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashutumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Utamaduni wa asili unakariri sana kuwa tuwe na nidhamu ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeleo, amani na upendo. Lazima tuwe na bidii na ushirikiano mwema, kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo. Tukiwa na viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo basi tutabaki nyuma kama mkia siku zote. Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo atokao ama kwa utajiri wake. Kwa hivyo basi, tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na nasaba kubwa ya utajiri.
    1. Fupisha aya ya kwanza ( maneno 60 - 70) (alama 7 na 1 ya mtiririko)
      Matayarisho
      ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
      Jibu
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
    2. Eleza mambo muhimu anayoibua mwandishi katika aya ya pili. (maneno 80 - 90) (alama 8 na 1 ya mtiririko)
      Matayarisho
      ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
      Jibu
      ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….
  3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
    1. Andika maneno yenye miundo ifuatayo: (alama 2)
      1. Irabu ya juu nyuma, kipasuo ghuna cha kaakaa laini, kiyeyusho cha midomo, irabu ya mbele wastani ...........................................................................................................................................
      2. Kikoromeo, sauti ya kati mviringo, kikwamizo hafifu cha mdomo-meno, irabu ya nyuma juu..............
    2. Taja sifa mbili za mzizi wa neno. (alama 2)
    3. Taja kiwakilishi ngeli cha nomino ‘kucha’ (alama 1)
    4. Bainisha mofimu za neno: walioonana (alama 3)
    5. Unda kitenzi kutokana na nomino ‘zawadi’ (alama 1)
    6. Akifisha sentensi ifuatayo. (alama 2)
      rununu simu zitazimwa wakati wa uchaguzi mkuu
    7. Nyambua kitenzi vaa katika kauli ya kutendwa. (alama 1)
    8. Ainisha sentensi ifuatayo kimajukumu / kiuamilifu. (alama 1)
      Nunua matunda mawili mawili .................................................
    9. Tambua aina za vielezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mara kwa mara apatapo pesa huzuru ng’ambo kujivinjari.
    10. Toa maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Mama aliwaendea watoto wale.
    11. Tunga sentensi kudhihirisha wakati uliopita hali timilifu. (alama 2)
    12. Vishazi tegemezi vina uamilifu gani? Taja hoja mbili na utungie sentensi. (alama 2)
    13. Ni hisia ipi inayodhihirika katika matumizi haya ya kihisishi. (alama 1)
      Maskini! Alinyimwa msaada na serikali…………………………………
    14. Tambua chagizo na aina za yambwa katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
      Mchezaji maarufu aliyepeperushiwa bendera ya taifa amewasili kwa ndege.
    15. Changanua sentensi kwa kielelezo cha mstari. (alama 2)
      Hayo yao yalikuwa yameiva shambani.
    16. Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kinyume. (alama 2)
      Nyanya aliomboleza baada ya janga hilo.
    17. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. (alama 2)
      KN (V + N) + KT (T + RH) ......................................
    18. Andika katika udogo. (alama 2)
      Nyoka yule mrefu alipigwa kwa kijiti.
    19. Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya susu na zuzu. (alama 2)
    20. Ukitoa mfano, andika matumizi mawili ya kiambishi “u” (alama 2)
    21. Jino linapong’oka huacha pengo, hali jeraha linapopona huacha............................................. (alama 1)
    22. Thurea ni kwa nyota ................................................... ni kwa nyuki. (alama 1)
    23. Andika kisawe cha: pata jiko. .......................................................................... (alama 1)
  4. ISIMU JAMII (Alama 10)
    Tumia kauli ifuatayo kujibu maswali
    1. Mwenda zake alikuwa mja mwenye upendo kwa watu na mcha Mungu…sote tunajua ni kudura... makiwa
      1. Tambua sajili rejelewa. (alama 1)
      2. Eleza sifa tano za sajili hiyo. (alama 5)
    2. Eleza majukumu manne ya Kiswahili kama lugha ya kimataifa. (alama 4)

 

  1.              
    • Sisi vijana wa Kenya inatuwajibikia tujibidiishe kazini ili tufanikiwe na kuinua nchi yetu.
    • haifai kulaza damu tukiwa matatizo yametuzonga.
    • Lazima tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima, kilimo, uchumi na amani.
    • bila elimu itakuwa vigumu kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo.
    • lazima tuzidishe mazao ya mashambani kwani idadi ya watu inaongezeka.
    • Lazima tujishughulishe na biashara.
    • Yatupasa kuleta uchumi mikononi mwa wakenya badala ya kuwaachia wasiohusika. (alama 7)
  2.            
    1. Mafunzo tunayoyapata majumbani, shuleni na katika jamii lazima yatutambulishe na mbinu za kupitia.
    2. Elimu tambuzi inapaswa imfanye mwanakenya kujua wajibu wake.
    3. Elimu pumbao inatufanya tusione mbele.
    4. Vijana wanapaswa kuwa kielezo chema kwa wengine

5.     

  1. Lazima watu washirikiane na kuwa na umoja.
  2. Lugha ya taifa ndicho chombo kinachotuunganisha
  3.  Tunapokosea, tukubali na kufanya masahihisho
  4.  Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi kama wazalendo.
  5. Tujishughulishe na kuyangalia matatizo ya nchi na kuyatatua.
  6. Tuwe na nidhamu
  7. Nidhamu huleta maisha bora, maendeleo, amani na upendo.
  8. Tuchague viongozi wenye mioyo ya maendeleo.
  9. Wananchi wengi huchagua viongozi kwa kufuata ukoo ama utajiri wake.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions - Maranda Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?