Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Maranda Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  1. Jibu maswali manne pekee.
  2. Swali la kwanza ni la lazima.
  3. Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki Riwaya, Tamthilia, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi.
  4. Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  5. Maswali yote ni sharti yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

MASWALI

SEHEMU A: USHAIRI.

  1. Lazima
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Haihitaji makini, kwa mwenye macho mazima
    Utaona walakini, mradi ukitazama
    Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
    Yafanana na sodoma, miji yetu kwa yakini

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
    Wanatafuna maini, vijana na kina mama,
    Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema,
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema
    Baba na binti ndani, wanacheza lelemama
    Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
    Wameikataa dini, toka tumboni mwa mama
    Wadai Wataliani, watajirisha mapema
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Wadai Wataliani, watajirisha mapema
    Hivyo mambo ya kigeni, yametunukiwa dhima
    Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama,
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
    Watu hawana Imani, umezidi uhasama,
    Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
    Wamekeuka yamini, kati yao na Rahima
    Wamemuasi Manani, na kusahau kiyama
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini
    Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
    Wamemuasi manani, na kusahau kiyama,
    Ya Illahi tuauni, tuwe watu maamuma
    Tukue katika dini, siku zetu za uzima
    Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

    Maswali

    1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
    2. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo. (alama 3)
      1. Idadi ya mishororo
      2. Mpangilio wa maneno
      3. Vina
    3. Ni ujumbe upi unaojitokeza katika shairi hili. (alama 5)
    4. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo katika shairi hili. (alama 3)
      1. Tashbihi
      2. Taswira
      3. Tasfida
    5. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
    6. Bainisha nafsinenewa katika shairi hili. (alama 2)
    7. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari. (alama 4)

SEHEMU B: RIWAYA
A.Matei: Chozi la Heri.
Jibu swali la 2 au la 3

2. “Alikuwa wapi siku kiduka changu ambacho mimi na aila yangu tumekitegemea kwa miaka kumi kilipoporwa na kugeuzwa majivu?”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Tathmini umuhimu nne wa msemaji katika kuijenga riwaya hii. (alama 4)
  3. Jadili umuhimu wa mandhari katika kujenga riwaya ya Chozi la Heri kwa kurejelea Msitu wa Mamba. (alama 12)

3.

  1. “Nina wazazi wawili, ila hawa ni wazazi tu, hawajadiriki kuwa walezi wangu, wala jina ‘mlezi’ haliwaafiki.”
    Onyesha jinsi kauli iliyopigwa mstari inavyowaafiki baadhi ya wazazi katika Jumuiya ya Wahafidhina ukirejelea riwaya Chozi la Heri. (alama 12)
  2. “Tumeendelea kuwakweza akina dada huku tukididimiza nguzo ya jamii yetu.”
    Kwa hoja nane, onyesha jinsi ambavyo nguzo ya jamii inadidimizwa kwa mujibu wa riwaya Chozi la Heri. (alama 8)

SEHEMU C: TAMTHILIA
Pauline Kea: Kigogo
Jibu swali la 4 au la 5
4. “Dudu liuuu...ma...malo halipewi chanda, Tunu si wa hulka yako. Wachezea moto, ukiungua lilia mvunguni usichekwe.”

  1. Tambua toni inayojitokeza katika dondoo hili. (alama 2)
  2. Kwa kutolea mifano, onyesha aina nne za taswira zinazojitokeza katika dondoo. (alama 4)
  3. Jadili mbinu-ishi zinazoibuliwa na msemewa katika tamthilia Kigogo. (alama 7)
  4. Jadili umuhimu wa mazungumzo kati ya Ashua na Majoka katika kujenga tamthilia Kigogo. (alama 7)

5. “…mbio za sakafuni zimefika ukingoni. Ikiwa umekataa kushindwa, mimi nimekubali.”

  1. Kwa kurejelea hoja kumi na mbili, thibitisha namna kauli iliyopigwa mstari inavyotimia ukirejelea wahusika mbalimbali kwenye tamthilia Kigogo. (alama 12)
  2. Fafanua mchango wa msemaji wa maneno haya katika kufanikisha ploti kwenye tamthilia Kigogo. (alama 8)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
Alifa Chokocho na Dumu Kayanda (wah): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 6 au la 7
. Salma Omar Hamad: Shibe Inatumaliza
6. “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza.”
“Lakini kula kunatumaliza vipi?

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 5)
  2. Changanua vipengele vya kimtindo katika dondoo. (alama 5)
  3. Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari ukirejelea hadithi Shibe Inatumaliza. (alama 10)

Alifa Chokocho: Tulipokutana Tena
7. 

  1. “Nitakuacha kwa marafiki zetu, na nitakuacha huko kwa muda. Ni watu wazuri sana marafiki hao.”
    Kauli hii ni kinaya. Thibitisha kwa hoja kumi ukirejelea hadithi Tulipokutana Tena. (alama 10)
    Eunice Kimaliro: Mtihani wa Maisha
  2. “Ana faida gani huyo? Ameniletea hasara tu. Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni.”
    1. Bainisha mbinu nne za lugha zinazojitokeza katika dondoo. (alama 4)
    2. Mrejelewa ni mtamauka. Thibitisha kwa hoja sita ukirejelea hadithi Mtihani wa Maisha. (alama 6)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
8. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.
Ewe Mainga wa Ndumi
Siwe uloambia akina mama
Siku tulopiga foleni
Chakula cha msaada kupata
Turudishe vifaranga kwenye miji
Wageuke vijusi tena
Njaa isiwaangamize?
Siwe ulopita
Matusi ukitema
Chumvi na sukarikuturushia ja samadi?
Uhitaji wetu ukatutuma
Kuokota vihela uloturushia
Ukatununua,kura ukapata?
Sasa miaka mitano imetimia
Waja tulaghai tena
Mainga wa Ndumi huna lolote safari hii
Ubunge umekudondoka ukitazama

Maswali

  1. Huu ni wimbo wa aina gani? (alama 2)
  2. Taja shughuli mojamoja ya kijamii na kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utungo huu. (alama 2 )
  3. Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani, eleza mambo sita ambayo utazingatia katika uwasilishaji wako. (alama 6)
  4. Jadili jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)
  5. Maandishi ni mojawepo ya vifaa vya kukusanya na kuhifadhi fasihi simulizi. Tathmini udhaifu wa kutumia kifaa hiki. (alama 5)                 

MWONGOZO

SEHEMU A: USHAIRI.
1. Lazima

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Haihitaji makini, kwa mwenye macho mazima
Utaona walakini, mradi ukitazama
Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
Yafanana na sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wanazini hadharani, wana kwa watu wazima
Wanatafuna maini, vijana na kina mama,
Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema,
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Hawana haya nyusoni, wameharamisha wema
Baba na binti ndani, wanacheza lelemama
Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Marijali wa mbioni, kujipagaza umama
Wameikataa dini, toka tumboni mwa mama
Wadai Wataliani, watajirisha mapema
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wadai Wataliani, watajirisha mapema
Hivyo mambo ya kigeni, yametunukiwa dhima
Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama,
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Uwaonapo fuoni, nusu uchi wa mnyama
Watu hawana Imani, umezidi uhasama,
Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Na viongozi wa dini, kuabudu darahima
Wamekeuka yamini, kati yao na Rahima
Wamemuasi Manani, na kusahau kiyama
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini
Miji yetu kwa yakini, kidogo kama Sodoma!
Wamemuasi manani, na kusahau kiyama,
Ya Illahi tuauni, tuwe watu maamuma
Tukue katika dini, siku zetu za uzima
Yafanana na Sodoma, miji yetu kwa yakini

Maswali

  1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka.    (alama 1)
    • Sodoma!
  2. Bainisha bahari ya shairi hili ukijikita katika ruwaza zifuatazo.    (alama 3)
    1. Idadi ya mishororo
      • Takhmisa/utano 
    2. Mpangilio wa maneno
      • Kikwamba – neon Miji wetu imetumika kuanza kila mshororo
      • Mkufu/upindu/unyoka/ukufu - neno miji yetu kwa yakini imetumika kutamatisha mshororo wa mwisho na kuanza mshororo wa kwanza kwenye kila ubeti.
    3. Vina
      • Mtiririko – vina vyake vya ukwapi na utao vinatiririka
  3. Ni ujumbe upi unaojitokeza katika shairi hili.  (alama 5)
    • Watu kuzini hadharani
    • Watu wameharamisha kutenda mema
    • Watu wamekataa dini
    • Kuna baadhi ya watu wanataka kujitajirisha mapema
    • Watu kuonea fahari vitu vya kigeni
    • Watu pia wmeasi mungu
    • Mshairi anahimiza watu wakue katika dini
  4. Bainisha mbinu zifuatazo za kimtindo katika shairi hili.    (alama 3)
    • Tashbihi mfano kidogo kama Sodoma
    • Taswira mfano uwaonapo fuoni,nusu uchi mnyama
    • Tasfida mfano wanatafuna maini
  5. Eleza toni ya shairi hili.    (alama 2)
    • Kukashifu/kusuta/kushauri.
  6. Bainisha nafsinenewa katika shairi hili.    (alama 2)
    • wanajamii
  7. Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.      (alama 4)
    • Hakika miji yetu imekuwa sodoma,watu hawana haya kwani nwametupilia mbali maadili,baba na binti zao hushiriki mapenzi,wasichana wadogo kwa waja wazito.miji yetu inafanana na Sodoma                                                                               

SEHEMU B: RIWAYA

A.Matei: Chozi la Heri.

2. “Alikuwa wapi siku kiduka changu ambacho mimi na aila yangu tumekitegemea kwa miaka kumi kilipoporwa na kugeuzwa majivu?”

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.    (alama 4)
    • Msemaji ni Kaumu, Msemewa ni Askari, Mandhari ni Msitu wa Mamba. Hii ni baada ya askari huyo kuwasihi wakimbizi kuwa watulivu wanapogawiwa chakula na makanisa na masikiti.
  2. Tathmini umuhimu nne wa msemaji katika kuijenga riwaya hii.    (alama 4)
    • Maudhui ya uwajibikaji:Askari kutoajibika wakati kiduka chake kiliporwa.
    • Uporaji wa mali ya umma,Kiduka chake kiliporwa na kugeuzwa majivu.
    • Mapuuza,Askari kuwatazama kama wehu walipokuwa wakililia usaidizi.
    • Ukimbizi;mzee Kaumu ni mmoja wa wakimbizi
    • Utegemezi/umaskini;wanategemea chakula cha msaada unaotolewa.
    • Umuhimu wa Amani nchini;sasa hivi ndio anaona thamani ya utulivu nchini.
    • Mabadiliko
    • Kupitia kwake, athari za vita miongoni mwa Wahafidhina inabainika.
    • Anatumiwa kujenga sifa za Wahafidhina kama Mhusika aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitman’ za uhuni.
    • Ametumiwa kuonyesha nafasi za asasi za utawala katika kutekeleza majukumu yao.
  3. Jadili umuhimu wa mandhari katika kujenga riwaya ya Chozi la Heri kwa kurejelea Msitu wa Mamba.  (alama 12)
    • Kuonyesha dhiki za kisaikolojia inayopata wakimbizi.mfano Kaizari na aila yake.
    • Kuonyesha suala la ubakaji. Mfano Mwanaheri na Lime
    • Kuonyesha shida ya njaa na kupigania chakula. Kuna milolongo mirefu ya chakula.Ridhaa anatafuna mzizi mwitu
    • Kuonyesha mabadiliko,Mwekevu kupewa nafasi ya kuongoza.
    • Kuonyesha suala la ukimbizi;Misafara ya wahafidhina waliohama bila kujua waendako.
    • Kuonyesha vita baada ya uchaguzi;mizoga ya watu,magofu ya majumba nk.
    • Kuonyesha suala la ulawiti wa wanaume na hakuna anayewatetea.
    • Kuonyesha uporaji wa mali ya umma.mfano magari kuchomwa,maduka ya wahindi kuporwa.
    • Kuonyesha unafiki;katika upigaji kura kwa wasiojua kusoma.
    • kuopnyesha ahadi hewa walizopea vijana
    • kuonyesha utabaka,msitu wa mamba ulikuwa na usawa wa watu.Daktari Ridhaa,Kaizari,Selume
    • Kuonyesha usaliti na ubinafsi wa viongozi;viongozi wenyewe baada ya kupiga kura walikalia majumbani mwao.
    • Kuonyesha tanzia.mamia za roho zisizo na hatia zilisalimu amri chini ya pambaja za risasi.
    • Kuonyesha suala la ufisadi;viongozi mfano kugawia kila mtu shilingi mia mia.
    • Kuonyesha ukoloni mamboleo;
    • Kuonyesha athari ya ukabila.Tulia kuwasihi Kaizari watoke kama bado wanataka kuishi.
    • Kuonyesha mchango wa mashirika mbalimbali. 

3.

  1. Nina wazazi wawili, ila hawa ni wazazi tu, hawajadiriki kuwa walezi wangu, wala jina ‘mlezi’ haliwaafiki.”
    Onyesha jinsi kauli iliyopigwa mstari inavyowaafiki baadhi ya wazazi katika Jumuiya ya Wahafidhina ukirejelea riwaya Chozi la Heri. (alama 12) 
    • Naomi anawahini wanawe malezi kwa kumtoroka Lunga kwa sababu ya umaskini.Umu,Dick na Mwaliko wanaishia kulelewa na kijakazi sauna.
    • Baba Kairu anamtelekeza Kairu kwa kumwacha kulelewa katika maisha ya umaskini kwa sababu mamake hakujiweza kiuchumi.
    • Wazazi wa Zohali wanamdhalilisha na kumsimanga Zohali baada ya kupachikwa mimba na kufukuzwa shuleni badala ya kumsaidia kukabili hali yake mpya.
    • Fumba anamtelekeza mwanawe Chandachema kwa nyanyake bila kumpa pesa za matunzo yake.
    • Baba Kipanga anamkana Kipanga kuwa mwanawe wa kuzaa,hali inayomsababisha kutoroka nyumbani na kuanza kunywa kangara.
    • Baba Pete anamkataa Pete kuwa mwanawe akidai kwamaba hawafanani.Pete anaishia kulelewa na nyanyake katika hali ya kimaskini.
    • Mama Pete anamtelekeza Pete kwa nyanyaake bila kumnunulia mahitaji kama sodo.Inabidi Pete kutumia tambara la blanketi.
    • Subira anawakosesha Lime na Mwanaheri malezi kwa kumtoroka Kaizari kutokana na dhuluma za mavyaa ake.
    • Baadhi ya wanawake kutupa watoto kwenye biwi la takataka.
    • Maya anambaka Sauna na kumringa mimba.
    • Mama Sauna anamomonyoa maadili ya Sauna kwa kumsaidia kuavyaa mimba.
    • Mama mwangemi na mama Mwangeka kuwanyima Mwangemi na Mwangeka chakula baada ya kuiga babu yao.
    • Fungo anamfurusha Pete na mwanawe bila kuwazia hatima ya mtoto huyo.
    • Ami za Lucia wanaendeleza ubaguzi wa kijinsia kwa kupinga masomo ya Lucia na Akello kwa kuwa ni wasichana.
    • Satua anamdhulumu Chandachema kwa kuwa anajua hana walezi.
    • Tenge anafanya ukahaba machoni pa wanawe hivyo kuwaachia dhiki za kisaikolojia.
      (Mtahiniwa aonyeshe jinsi wazazi wanavyokosa kuwajibika katika kuwalea wanao hivyo kuwaasababishia kutaabika.)
  2.  “Tumeendelea kuwakweza akina dada huku tukididimiza nguzo ya jamii yetu.”
    Kwa hoja nane, onyesha jinsi ambavyo nguzo ya jamii inadidimizwa kwa mujibu wa riwaya Chozi la Heri. (alama 8)
    • Buda anashiriki katika ulanguzi wa mihadarati kwa kutumia watu kama Dick na kuwahonga polisi.
    • Mhusika aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitman’ anatamauka baada ya kusaliotiwa na viongozi na kusiriki uhuni pamja na mauaji.
    • Ridhaa anabaguliwa na wanafunzi wenzake wanapomwita mwizi wa kalamu na mfuata mvua.
    • Shamsi anageuka na kuambulia ulev ili kukumbana na utamaushi uliomkumba.
    • Lunga anageukia ukataji miti ili kukumbana na kupoteza kwake ajira.
    • Mwanaharakati Teteti anaendelea propaganda dhidi yake dhidi ya wanawake na kuonyesha jinsi wanawake walivyowakandamiza wanaume katika enzi za kiistiimari.
    • Hazina anasawiriwa kama ombaomba anayeshiriki katika uvutaji gundi kabla ya serikali kumwokoa na kumsomesha.
    • Dick anatumiwa na Mzee Buda kulangua mihadarati.
    • Kipanga, baada ya kutengwa na wazaziwe, anazamia unywaji pombe haramu.
    • Bwana Maya anamnajisi mwanawe Sauna.
    • Bwana Mwanzi anakataa kukubali kushindwa licha ya Bi. Mwekevu kushindwa waziwazi.
    • Makaa anachomeka anapojaribu kuwasaidia waliokuwa wakichomeka baada ya kujaribu kuchota mafuta kwenye lori.
    • Wanawe Kaizari wananajisiwa mbele yake, jambo linalomwacha akiuguza majeraha ya moyo.
    • Tenge anashiriki ufuska kila mara Bi. Kimai anapoondoka.
    • Mze Kedi anashiriki katika kuteketeza familia ya Ridhaa, anachoma jamaa za Ridhaa hadi wanageuka majivu.
    • Mabavu ananyakua shamba la kina Shamsi na kuwatumikisha kwenye shamba lao.
    • Kimbaumbau anatisha kumdhulumu Naomi kimapenzi na hata kumtesa baada ya kumwajiri, jambo linalomfanya kuacha kazi.
    • Babu Mwimo Msubili ana mtazamo hasi kuhusu wanawake na kuchukulia kuwa kukutana nao asubuhi ni balaa.
    • Wajombaze Pete wanashiriki katika kumwoza licha ya pingamizi kutoka kwa nyanyake.
    • Babake Kairu anambagua na kumtenga Kairu kwa vile ni motto aliyezaliwa nje ya ndoa.
    • Babake zohali anamtumikisha na kumfanyisha kazi nyingi baada ya kuambulia ujauzito.
    • Bwana fumba anajihusisha katika uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wake Rehema na hata kumpa mimba.
    • Ami zake Luca wanapinga ndoa kati ya ukoo wa anyamvua na Waombwe licha ya kutohusika katika kumlea na kumsomesha.

SEHEMU C: TAMTHILIA
Pauline Kea: Kigogo

4. “Dudu liuuu...ma...malo halipewi chanda, Tunu si wa hulka yako. Wachezea moto, ukiungua lilia mvunguni usichekwe.”

  1. Tambua toni inayojitokeza katika dondoo hili.  (alama 2)
    • Kukejeli/kudhihaki/kutania - Dudu liuuu...ma...malo halipewi chanda, Tunu si wa hulka yako
    • Kuonya/kunasihi/kukanya - Wachezea moto, ukiungua lilia mvunguni usichekwe
  2. Kwa kutolea mifano, onyesha aina nne za taswira zinazojitokeza katika dondoo.   (alama 4)
    • Taswira oni – Dudu liuuu...ma...malo, lilia mvunguni usichekwe.
    • Taswira hisi- Dudu liuuu...ma...malo
    • Taswira muonjo - Dudu liuuu...ma...malo
    • Taswira mguso - Dudu liuuu...ma...malo
  3. Jadili mbinu-ishi zinazoibuliwa na msemewa katika tamthilia Kigogo. (alama 7)
  4. Jadili umuhimu wa mazungumzo kati ya Ashua na Majoka katika kujenga tamthilia Kigogo.
    • Kufufua matukio ya awali;Majoka aliwahi kumchumbia Ashua akakataa.
    • Kusisitiza umuhimu wa kuaminiana na kujiheshimu katika ndoa;Ashua anasisitiza kuwa ameolewa.
    • Kuonyesha jinsi viongozi wanavyotumia vibaya ofisi zao
    • Kuonyesha jinsinbaadhi ya viongozi hawajathamini ndoa za wananchi;Majoka hajali kuvunjika kwa ndoa ya Ashua.
    • Kuonyesha athari za ukosefu wa chakula kwa watoto
    • Kuonyesha kuzinduka kwa wanawake katika kutetea haki zao
    • Kuonyesha ubinafsi wa viongozi.
    • Kuonyeha baadhi ya miradi duni ambazo viongozi wanashughulikia.
    • kujenga sifa za wahusika;mfano kupitia mazungumzo haya tunatambua ufuska wa Majoka kuonyesha usaliti wa viongozi
    • kuonyesha ukatili wa viongozi;ashua anakamatwa ilhali ananyonyesha
    • kuonyesha unafiki;majoka anamwambia Ashua kuwa haja zangu ni haja zako
    • kuonyesha umaskini;Ashua kugeuka omba omba kwa kukosa chakula
    • Kuonyesha maudhui ya ajira; Ashua ana shahada ya ualimu ila hana kazi.
    • kuonyesha maudhui ya elimu;Ashua amehitimu
    • Kuonyesha jinsi wanawake wanavyonyanyaswa.

5. “…mbio za sakafuni zimefika ukingoni. Ikiwa umekataa kushindwa, mimi nimekubali.”

  1. Kwa kurejelea hoja kumi na mbili, thibitisha namna kauli iliyopigwa mstari inavyotimia ukirejelea wahusika mbalimbali kwenye tamthilia Kigogo.  (alama 12)
    • Kenga anakubali kushindwa na kuungana na Wanasagamoyo dhidi ya Majoka.
    • Asiya, baada ya kugeukwa na walevi, anamwomba Tunu msamaha na kuungana na Wanasagamoyo.
    • Walevi wanachoshwa na Asiya, wanamgeukia na kumwaga pombe yake.
    • Ashua anakubali kuungana na Tunu na Sudi kupigania ukombozi wa Sagamoyo.
    • Ngurumo ananyongwa na chatu na hatimaye kuuawa anapotoka Mangweni.
    • Ngao Junior anakufa kutokana na athari ya sumu ya nyoka.
    • Babake Tunu anakufa kwa njia ya kutatanisha katika kampuni ya Majoka and Majoka.
    • Kingi anamgeuka Majoka na kuwaunga mkono Wanasagamoyo kwa kukaidi amri yake ya kuwapiga Wanasagamoyo risasi.
    • Majoka anageukwa na Wanasagamoyo na kubaki peke yake/Babu anamsuta mpaka anaingiwa na majuto.
    • Jabali anauawa na chama chake cha Mwenge kupotelea mbali.
    • Kombe na Boza wanatupiwa vijikaratasi wahame Sagamoyo si kwao licha ya kumwuunga mkono Majoka.
    • Inabainika hatimaye kuwa Ngurumo alishiriki uroda na Asiya ili kupewa kandarasi ya kuoka keki.
    • Vijana watano wanauawa atika Majoka and Majoka Company.
    • Chopi anapangiwa safari baada ya kumsaidia Majoka kuwakandamiza Wanasagamoyo.
    • Wafadhili wanapanga kufurushwa ili wasifadhili juhudi za kina Tunu za kuwapigania haki.
    • Wanafunzi wa Majoka and Majoka Academy wanadungana sumu ya nyoka na kuwa makabeji, hawafuzu hatimaye.
    • Wanasagamoyo wanachoshwa na Majoka, wanasusia mkutano wake na hatimaye kumfurusha.
  2. Fafanua mchango wa msemaji wa maneno haya katika kufanikisha ploti kwenye tamthilia (alama 8)
    • Kupitia kwake tunaelezwa kuhusu usuli wa Ngurumo kumvunja Tunu mguu.
    • Anajenga mgogoro kati ya wanamabadiliko n wanaotaka hali ibakie hivyo.Kenga anasemakuwa amekubali kushindwa.
    • Anatumiwa kujenga mgogoro wa kijinsia unaotumiwa kufanya kampeni dhidi ya utawala wa tunu.
    • Kupitia kwake, nafahamu chanzo cha kifo cha jabali.
    • Ushari wake mbaya unamfanya Majoka kufanya maamuzi mabaya kwa mambo mengi hivyo kupelekea kung’olewa kwake madarakani.
    • Kuonyesha mustakabali wa sagamoyo.Anaomba msamaha.
    • Baadhi ya matukio katika maisha ya wahusika yanaangaziwanaye moja kwa moja.Anaenda katika karakana ya Sudi.
    • Matendo yake yanampa msomaji mwao kuhusu aliyepanga na kumwuua Ngao Junior hasa baada ya kutatizika Majoka anapomtangaza Ngao Junior kama mrithi wake.
    • Kupitia kwake tunafafanuliwa kuhusu ila na hila za majoka.
    • Matukio katika ofisi ya Majoka yanatusaidia kujua kuwa ndiye aliyepanga njama ya kumfunga Ashua Jela.
    • Kuonyesha hatima ya mgogoro kati ya viongozi na wanyonge.Kuwa amekubali kushindwa.

SEHEMU D: HADITHI FUPI
Alifa Chokocho na Dumu Kayanda (wah): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Salma Omar Hamad: Shibe Inatumaliza

6. “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza.”
 “Lakini kula kunatumaliza vipi?

  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.    (alama 5)
    • Haya ni mazungumzo kati ya sasa na Mbura. Kauli ya kwanza ni ya Sasa. Kauli ya pili ni ya Mbura. Wakiwa nyumbani kwa mzee Mambo walikohudhuria sherehe. Wanazungumzia kula na madhara yake.
  2. Changanua vipengele vya kimtindo katika dondoo.   (alama 5)
    • Takriri – kula kunatumaliza
    • Jazada – kula, kula kunatumaliza
    • Swali balagha – kula kunatumaliza vipi?
    • Taswira – kula kunatumaliza.
    • Uhuishi – kula kunatumaliza
    • Chuku – kula kunatumaliza
    • Kinaya – kula kunatumaliza
    • Ukwelikinzani – kula kunatumaliza
    • Dayolojia
    • Usambamba – kula kunatumaliza
  3. Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari ukirejelea hadithi Shibe Inatumaliza (alama 10)
    • Viongozi wa mataifa yanayoendelea kutowajibika katika kazi zao-wanakubali bidhaa duni kurundikwa nchini mwao (mchele wa basmati)
    • DJ anafungua duka la dawa zilizotolewa katika bohari ya serikali
    • Serikali kwalipa watu ambao hawafnyi kazi mshahara hivyo kudhhofisha uchumi wa nchi/wanaolipwa wanafanya kazi yaukwe tu.
    • Wafanyikazi wakubwa serikalini kama Mzee mambo hawalipwi mishahara, wanajichotea na kujinyakulia.
    • Dini inatumiwa kama kigezo cha kuhalalisha Mola kumpa amtakaye.
    • kituo cha televisheni kutumika kupeperusha matangazo ya sherehe ya kwa mzee Mambo ambayo haina umuhimu wowote.
    • Mzee mambo anafisidi serikali kwa kutumia magari ya serikali kusomba maji na jamaa zake.
    • DJ anapata huduma za kimsingi kama vile maji,matibabu huku wananchi wakibaki maskini
    • sasa na mbura kula tena na tena bila kushiba
    • DJ kulipwa mabilioni ya pesa na serikali ilhali sherehe ilikuwa ya kibinafsi
    • badala ya sasa na Mbura kuwa kazini,wanaibia serikali muda ya kufanya kazi.
    • Wimbo unaochezwa kwenye sherehe ni ‘Sijali Lawama’ hivyo inatumiw kuhalalisha ufujaji wa fedha za serikali.
    • Watu wanakula na kupiga foleni tena na tena kwa Mzee mambo.
    • Watu wanapigana kutokana na kula.
    • Magonjwa kama obesiti na presha yanawapata watu kutokana na kula.
    • Kula kunawasababishia watu wengi vifo.
    • Watu kama Mbura wanajimaliza kisiasa wanapopyora na kusuta wafadhili wao wakishashiba.

Alifa Chokocho: Tulipokutana Tena
7.    

  1. “Nitakuacha kwa marafiki zetu, na nitakuacha huko kwa muda. Ni watu wazuri sana marafiki hao.”
    Kauli hii ni kinaya. Thibitisha kwa hoja kumi ukirejelea hadithi Tulipokutana Tena.    (alama 10) 
    • Sinai anamlazimisha Bogoa kufanya kazi nyingi bila hiari yake, kazi zisizo kikomo.
    • Bogoa analazimishwa na Bi. Sinai kuamka alfajiri na kuchoma
    • Bogoa analazimishwa kuyauza yale maandazi shuleni na Sinai.
    • Bogoa anabaguliwa na watoto wenzake pale shuleni na kuonwa kama mtoro ambaye hataki kusoma, kauli ambayo iliungwa mkono na wazazi wa watoto wale.
    • Bogoa ananyimwa uhuru wa kucheza na watoto wenzake, hasa watoto wa Sinai.
    • Kila mara Bogoa anapochelewa kurudi nyumbani, alipigwa
    • Wazaziwe Bogoa walipokuja kumtembelea, alinyimwa fursa ya kutangamana nao ili kuwafafanulia kadhia alizokuwa
    • Bogoa alilazimishwa kula makombo/makoko baada ya kila mtu
    • Bogoa alilazimishwa kula wa mwisho wakati ambapo kila mtu pale nyumbani kwa Sinai alikuwa ameshiba.
    • Bogoa alilazimika kula kwenye sufuria na vyungu wakati ambapo kila mtu alikula kwenye
    • Sinai alimtisha Bogoa kuwa angemkata ulimi endapo angesema chochote kuhusu maisha yao ya ndani.
    • Bogoa aliposinzia na maandazi yakachomeka, alichomwa kijinga cha moto viganjani, jambo lililomsababisha
      Zozote 10×1=10
  2. Eunice Kimaliro: Mtihani wa Maisha
     “Ana faida gani huyo? Ameniletea hasara tu. Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni.”
    1. Bainisha mbinu nne za lugha zinazojitokeza katika dondoo. (alama 4)
      • Swali balagha – Ana faida gani huyo?
      • Koja – Ana faida gani huyo/ Ameniletea hasara tu
      • Chuku – nilitoa tu maradhi tumboni
      • Isitiari - nilitoa tu maradhi tumboni
      • Jazanda – maradhi
      • Kinaya - Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni.
      • Ukwelikinzani - Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni.
      • Litifati - Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni.
      • Tanakuzi - Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni.
      • Taswira - Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni/ Ameniletea hasara tu
      • Kejeli/dhihaka - Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni
      • Uhuishi - Sikuzaa mwana, nilitoa tu maradhi tumboni
    2. Mrejelewa ni mtamauka. Thibitisha kwa hoja sita ukirejelea hadithi Mtihani wa Maisha. (alama 6)
      • Anakiosa kujitayarisha ipasavyo kwa mtihani wa mwisho uliokuwa wa kuamua hatima yake maishani.
      • Anajitia ujasiri bandia kwa kukariri dhana potovu.
      • Ni mtvu wa nidhamu shuleni kwani wenzake walimwita ‘rasta’
      • Anawadanganya wazaziwe kuhusu matokeo (kwamba hakupewa kwa kuwa alikuwa na salio la karo)
      • Ana mtazamo hasi kuhusu shule na kuiona kama jela
      • Anapyora na kumtukana mwalimu mkuu katika mawazo yake. Anamwita hambe na hata kusema anaitaji upasuaji wa ubongo.
      • Anajiingiza katika mapenzio ya kiholela na Nina anapokuwa shuleni.
      • Anawaonea wivu waliofanikiwa maishani.
      • Anataka kujiua kwa kutumbukia bwawani anapofeli.
      • Amejaa mawazo ya namna babake atakavyomtelekeza na kumtenga baada ya kfeli.
      • Anaamua kujificha msalani wenzake wnapomwuuliza kuhusu matokeo yake.
      • Anajaribu kujitupa tena bwawani hata baada ya kuokolewa.
      • Anaingiwa na aibu anapomwona Nina pale kwenye umati.
      • Anatupiwa matokeo yake sakafuni na mwalimu mkuu.
      • Ana imani kuwa mwalimu mkuu hakuwahi kumwamini kuwa angepita mtihani.

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI
8. Soma utungo ufuatao kisha ujibu maswali yanayofuata.

Ewe Mainga wa Ndumi
Siwe uloambia akina mama
Siku tulopiga foleni
Chakula cha msaada kupata
Turudishe vifaranga kwenye miji
Wageuke vijusi tena
Njaa isiwaangamize?
Siwe ulopita
Matusi ukitema
Chumvi na sukarikuturushia ja samadi?
Uhitaji wetu ukatutuma
Kuokota vihela uloturushia
Ukatununua,kura ukapata?
Sasa miaka mitano imetimia
Waja tulaghai tena
Mainga wa Ndumi huna lolote safari hii
Ubunge umekudondoka ukitazama

Maswali             

  1. Huu ni wimbo wa aina gani? (alama 2)
    • siasa mfano umetaja kura na ubunge
  2. Taja shughuli mojamoja ya kijamii na kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utungo huu  (alama 2 )
    • shughuli ya kijamii –siasa mfara kura, ubunge
    • Shughuli ya kiuchumii –biashara
  3. Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani, eleza mambo sita ambayo utazingatia katika uwasilishaji wako.  (alama 6)
    • Kuigiza baadhi ya matukio
    • Kushiriki kuimba wimbo huo
    • Kutoa mifano ya baadhi ya wahusika
    • Kuuliza maswali balagha
    • Kubadilisha toni/kiimbo
    • Matumizi ya viziadalugha/sehemu za mwili.
    • Kutumia mtuo wa kidrama kuongeza taharuki au kusisitiza ujumbe.
    • Kuwa mchangamfu na mcheshi.
    • Kuwa na ujuzi na ufasaha wa lugha ili kuwasilisha mawazo kwa njia mwafaka.
  4. Jadili jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi.    (alama 5)
    • Kupitia tamasha za muziki mfano wanafunzi hukariri
    • Kupitia sherehe za harusi,mazishi ambayo ni mifano ya mivigha
    • Utegaji na uteguaji wa vitendawili kupitia runinga
    • Michezo ya kuigiza katika runinga
    • Tamasha za drama huendeleza utanzu wa maigizo
    • Sarakasi zinazofanywa na wasanii huhifadhi kipera cha vichekesho
    • Utambaji wa hadithi bado hufanyika
  5. Maandishi ni mojawapo ya vifaa vya kukusanya na kuhifadhi fasihi simulizi. Tathmini udhaifu wa kutumia kifaa hiki.    (alama 5)
    • Mambo kama vile kiimbo,toni ,hisia na mapigo ya muziki huweza kupotea,
    • Kwa vile maandishi si hai,hayawezi kutenda wala kusema
    • Kuandika fasihi simulizi hufanya kukosa ile taathira asilia
    • Kuiandika fasihi simulizi huidhibiti na kupunguza hadhira yake na kuathiri vibaya usambazaji wake.
    • Baadhi ya watafiti huenda wakaandika yale ambayo wanahitaji kwa wakati mahuhususi na kupunguza mengine.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Maranda Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?