Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Alliance Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. Umetangazwa kuwa mwanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa. Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Tangamano amekualika katika shule hii yake kuwahutubia wanafunzi kuhusu kilichochangia ufanisi wako. Andika hotuba utakayowatolea walimu, wazazi na wanafunzi wa shule hiyo.
  2. Wewe ni mwandishi wa habari. Umepata nafasi ya kumhoji waziri wa utalii kuhusu faida na hasara za utalii nchini. Andika mahojiano hayo.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Umetangazwa kuwa mwanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Tangamano amekualika katika shule hii yake kuwahutubia wanafunzi kuhusu kilichochangia ufanisi wako. Andika hotuba utakayowatolea walimu wazazi na wanafunzi wa shule hiyo. Kichwa lazima kiandikwe kwa herufi kubwa, kitaje neno hotuba, kipigiwe mstari mmoja akisitoneshwe hapo mwisho. - 4 mks
    Muundo uwe na mambo matano:
    Alama ya kunukuu isitumiwe-2mks
    Nafsi ya kwanza itumiwe-akitumia ya tatu asipite 04/20
    Awatambue waliohudhuria kulingana na vyeo kuanzia cheo cha juu. Akikosa asipite 08/20
    Maudhui yawe manane. Yakipungua manane asizidi 10/20
    Aya ya mwisho awashukuru waliohudhuria. Akikosa asizidi 12/20
    Baadhi ya hoja 
    1. Nilisoma kwa bidii
    2. Nilifanya mitihani ya mara kwa mara 
    3. Nilidurusu katika makundi 
    4. Niliwahusisha walimu mara kwa mara
    5. Nilikarilisha silabasi kwa wakati 
    6. Nilikuwa na utulivu shuleni 
    7. Nilizingatia nidhamu 
    8. Nilikuwa na vitabu vya kutosha 
    9. Nilipata msaada mzuri wa wazazi (kadiria hoja za mtahiniwa)
      Mtahiniwa akiwa hana lugha na hana maudhui kiwango chake ni 01-05
      Mtahiniwa akiwa hana lugha japo ana maudhui kiwango chake ni 06-10
      Mtahiniwa akiwa ana lugha na ana maudhui kiwango chake ni 11-15
      Mtahiniwa akiwa ana lugha, maudhui pamoja na umbuji na ustadi wa hali ya juu wa mapambo ya lugha na ubunifu, kiwango chake ni 16-20
  2. Wewe ni mwandishi wa habari. Umepata nafasi ya kumhoji waziri wa utalii kuhusu faida na hasara za utalii nchini. Andika mahojiano hayo. Kichwa lazima kiandikwe kwa herufi kubwa, kitaje neno mahojiano, kipigiwe mstari mmoja akisitoneshwe hapo mwisho. - 4 mks Mtindo wa kitamthilia utumiwe. Mhusika mmoja aulize maswali na wa pili atupe majibu ya maswali hayo kiaya. Wote wakichangia huo ni upungufu wa kimtindo. Usimwadhibu mradi kuna alama
    Baadhi ya maudhui
    Faida
    Fedha za kigeni aseme umuhimu wa fedha hizo.
    Asiposema asipite 10/20
    Ajira na umuhimu wake
    Barabara kuimarishwa
    Hoteli kuboreshwa
    Usalama kuimarika
    Uhusiano mwema baina ya mataifa
    Hasara
    Tamaduni potuvu
    Vijana kuacha shule
    Ulanguzi wa dawa. Kila hasara iishie kwa suluhu,
    1. Maudhui
      1. Mtahiniwa aandike maudhui manane na zaidi 
      2. Aanze na maudliui mazito mazito 
      3. Maudhui yaandikwe kiaya 
      4. Aya iwe ya mraba / wina 
      5. Aya zisipungue kumi 
      6. Mstari mmoja urukwe kabla ya kuanza aya nyingine 
      7. Kila aya iwe na maudhui moja, 
      8. Maudhui yajadiliwe kwa kina 
      9. Maadili na urasmi wa lugha vizingatiwe na kudumishwa.
      10. Maudhui yajitokeze wazi hasa katika sentensi ya kwanzakwenye kila aya 
      11. Vidokezo viorodheshwe katika sehemu yenye maswali. 
      12. Aya iwe kati ya mistari 5-7, au maneno 40-50
      13. Katika swali linalohitaji suluhisho, suluhisho hilo lijitokezekatika kila sentensi ya mwisho kwenye kila aya. Iwapomaudhui ni manane basi suluhu pia ni nane.
      14. Uhalisia uzingatiwe hasa katika insha 1 na 2 
      15. Katika swali lililo na sehemu mbili, faida na hasara, zote ziangaziwe na msimamo kutolewa katika aya ya mwisho.(6.2 au 5.3) kwa kuegemea hoja nyingi, si 4,4 au 7,1 au 8,0
    2. Mtindo
      • Mtahiniwa afahamu sura ya insha zote za kiuamilifu. Lazima afahamu umbo la kila aina ya insha.
      • Azingatie urefu zaidi ya kurasa 4 au maneno 400
      • Azingatie nyakati kulingana na aina ya insha.
      • Azingatie nafsi/ajihusishe kulingana na aina ya insha. 
      • Unadhifu wa insha uzingatiwe. Kazi safi humpendezamtahini. Kazi chafu humkwaza na kumtamausha mtahini. 
      • Asikatekate silabi kiholela, kwa mfano, katika, badala yakati-ka. Konsonanti na irabu zisitenganishwe. 
      • Aonyeshe nambari ya insha anayojibu kikamilifu.
      • Aandike herufi vizuri bila kuzishikanisha na kwa utaratibu 
      • Atoneshe herufi i naj vizuri 
      • Asitenganishe maneno visivyo, k.m aliye kuja badala ya aliyekuja, nime kuadhibu badala ya nimekuadhibu
      • Akumbuke kuwa palipo na 'o rejeshi kwenye kitenzi, nenohilo na moja si mawili. Kwa hivyo asitenganishe. Kwamfano, lililopotea wala si lililo potea
      • Asiunganishe maneno visivyo, kwa mfano kwa sababu badala ya kwa sababu
      • Mtahiniwa asidondosha herufi katika neno, kwa mfano aandike kibia badala ya kimbia, 
      • Mtahiniwa acpuke kupachika ama kuongeza herufi katika neno. Kwa mfano aandike mu kutano badala ya kuandika mkutano. 
      • Kubadilisha herufi za neno pia ni kosa. Kwa mfano aandikeneno sigilisa badala ya sikiliza, 
      • Matumizi ya tarakimu yawe nadra. Atumie mneno badala ya tarakimu kwa wingi. 
      • Vifupisho viepukwe-k.mkv.m.f.n.k. 
      • Mtiririko na mshikamano wa mawazo kiaya na katika inshanzima uonekane. 
      • Hati nzuri na inayosomeka kwa urahisi itumiwe. 
      • Wino wa samawati utumiwe.
      • Sentensi komavu na zenye mnato zitumiwe kwa wingi.
      • Insha zote sharti ziwe na kichwa
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Alliance Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?