Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kijiset Revision Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

  • Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  • Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

 

  1. Wewe kama mwanahabari umetembelea afisi ya gavana wa gatuzi lako.Andika dayolojia iliyojiri baina yako na gavana kuhusu namna ugatuzi umechangia maendeleo katika jamii.
  2. Suala la ubaguzi wa jinsia limekithiri sana katika jamii. Jadili.
  3. Tunga kisa kitakachoafiki maana ya methali:
    Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamano.
  4. Andika kisa kitakachomalizika kwa maneno yafuatayo:
    …sasa ninaelewa maneno yake kuhusu kufanya maamuzi ya busara.Sasa nimepata baraka za wazazi na ridhaa ya kuishi pamoja.

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. Wewe kama mwanahabari umetembelea afisi ya gavana wa gatuzi lako.Andika dayolojia iliyojiri baina yako na gavana kuhusu namna ugatuzi umechangia maendeleo katika jamii.
    • Swali la kwanza. vigezo
      • Hii ni insha ya kiuamilifu.
      • Zingatia sura ya dayolojia, achukue mtindo wa tamthilia.
    • Baadhi ya hoja zinazotarajiwa
      • Nafasi za kazi zimebuniwa
      • Huduma za serikali zimeletwa karibu na wananchi
      • Ushindani chanya baina ya kaunti/maeneo mbalimbali
      • Ushirikiano wa kibiashara baina ya kaunti mbalimbali.
      • Wananchi wanahusishwa vilivyo katika kufanya maamuzi muhimu.
      • Imeokoa wakati wa kushughulikia maswala fulani kwani hakuna kutafuta huduma mbali.
      • Wananchi wamepata fursa ya kuendeleza kaunti zao kama inavyofaa kutegemea mahitaji yao.
      • Miundo misingi imeboreshwa
      • Usalama umeboreshwa
      • Huduma nyingi za kijamii na za kimsingi zimeletwa karibu na wanajamii
      • Nafasi katika taasisi za elimu ya juu zimeweza kunufaisha wenyeji kinyume na ilivyokuwa hapo awali.
  2. Suala la ubaguzi wa kijinsia limekithiri sana katika jamii.Jadili.
    • Hili ni swala la mjadala.
    • Mtahiniwa aunge mkono na aonyeshe jinsi suala la ubaguzi wa jinsia limekithiri katika jamii.
    • Ubaguzi wa kijinsia ujitokeze kwa jinsia zote.

      Wanawake wanavyobaguliwa kijinsia.
      1. Kutorithi mali
      2. Wajane kunyang’anywa mali
      3. Kutoelimishwa
      4. Kunyimwa ajira kwa kupendelea wanaume
      5. Kunyimwa haki ya kusema
      6. Kudhibitiwa na waume wao

        Wanaume wanavyobaguliwa
        1. Kutelekezwa
        2. Kutengewa kazi za sulubu
        3. Mashirika mengi ni ya kutetea haki za wanawake.
        4. Serikali kupigia upato elimu ya mtoto wa kike.
        5. Haki za wanaume zimepuuzwa kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na za wanawake.
        6. Kutopewa nafasi sawa za ajira na jinsia ile nyingine.
  3. Tunga kisa kitakachoeleza ukweli wa methali; mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.
    • Kisa kibainishe maana ifuatayo.
    • Anayeenda nyuma na mbele ya jahazi huishia katikati ya chombo hicho.
    • Mhusika aliyepuuza jambo fulani,analirudia jambo hilo mwishowe.

      Tanbihi
      1. Kwa vyovyote vile pande zote mbili za methali sharti zijitokeze.
      2. Mtahiniwa akizingatia upande mmoja, amepungukiwa kimaudhui.
      3. Mtahiniwa akiandika anwani lakini kisa kisioane na maana ya methali atakuwa amepotoka kimaudhui- Apewe D 03.
      4. Atakayeandika methali tofauti na aliyopewa na kujibu atakuwa amejitungia swali na kulijibu apewe BK 01
      5. Aandike kisa kimoja.
  4. Hii ni insha ya mdokezo.
    1. Lazima mwanafunzi ahitimishe kwa maneno aliyopewa.
    2. Akiacha neno ama kuongezea atakuwa amejitungia swali.
    3. Mtahiniwa ajihusishe na kisa (nafsiya kwanza)
    4. Mtahiniwa amhusishe aliyempa wosia.
    5. Ruwaza ya kisa idhihirike hivi kwamba mhusika alikuwa amepotoka na kuvuruga uhusiano na wazazi wake lakini akapata mawaidha/mwelekeo/wosia kutoka kwa mhusika mwingine na uhusiano mwema ukarejeshwa kati yake na wazai wake.
  5. Baadhiya visa ni kama;
    1. Mhusika anayetoroka nyumbani kwa kukosana na wazazi, apewe ushauri kisha aamue kurudi kuomba msamaha na kuendeleza maisha pamoja na wazazi.
    2. Mhusika anayetamauka kimasomo kwa sababu fulani.Jambo hili livuruge uhusiano na wazazi wake.apewe ushauri na mwalimu au mwanafunzi mwenzake asome afaulu na kufurahisha wazazi wake.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Kijiset Revision Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?