Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Kijiset Revision Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

 • Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 • Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
 • Jibu maswali manne pekee.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Maswali hayo mengine yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki: yaani; Riwaya, Tamthilia,Hadithi fupi na Fasihi simulizi.Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
 • Majibu yote sharti yaandikwe kwenye nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.

SEHEMU A: USHAIRI

 1. SWALI LA LAZIMA
  Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

  1. Wenye vyao watubana, twaumia maskini,
   La kufanyiza hatuna, hali zetu taabani,
   Kwa sasa kilo ya dona, bei mia ishirini,
   Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  2. Washindana matajiri, kwa bei siyo utani,
   Na pigo kwa mafakiri, tunao hali ya chini,
   Wazeni kutafakari, wanyonge tu madhilani,
   Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  3. Limekuwa kubwa zogo, hakwendeki madukani,
   Fungu moja la muhogo, sasa shilingi miteni,
   Huo mkubwa mzigo, waelemea vichwani,
   Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  4. Si hichi wala si kile, hakuna cha afueni,
   Bei imekuwa ndwele, wenye macho lioneni,
   Ukiutaka mchele, pesa jaza mfukoni,
   Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  5. Waliko hao samaki, huko ndiko uchawini,
   Wachuuzi hawacheki, zimewatoka huzuni,
   Vibuwa havishikiki, kimoja kwa hamsini,
   Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  6. Maisha yetu viumbe, yamekuwa hilakini,
   Wenye vyao kila pembe, wametukaa shingoni,
   Nyama ya mbuzi na ng’ombe, sasa hali maskini,
   Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

  7. Maji yamezidi unga, kwa lodi wa darajani,
   Kajitolea muhanga, kwa bei hawezekani,
   Mvao wake wa kanga, ni shilingi elifeni,
   Wakubwa tuteteeni, wenye vyao watubana.

   Maswali
   1. Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (alama 1)
   2. Jadili dhamira ya nafsi neni. (alama 2)
   3. Tambua toni ya shairi hili. (alama 1)
   4. Andika ubeti wa sita kwa lugha tutumbi. (alama 4)
   5. Onyesha vile kibali cha utunzi wa mshairi kilivyotumiwa kukidhi mahitaji ya kiarudhi. (alama 2)
   6. Taja na ueleze bahari mbili za ushairi ukizingatia. (alama 4)
    1. Ubeti
    2. Vina
   7. Tambua aina tatu za taswira ukirejelea shairi hili. (alama 3)
   8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika kwenye shairi. (alama 3)
    1. Dona
    2. Zogo
    3. Waelemea

SEHEMU YA B: RIWAYA
Assumpta K. Matei: Chozi la Heri
Jibuswali la 2 au la 3

 1. “…poa sana sistee,wewe ni mnoma.siku moja nitakuhelp hata mimi…”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza sifa mbili za mnenaji zinazojitokeza kwenye kauli hii. (alama 4)
  3. Taja na ufafanue maudhui yoyote mawili yanayotokana na matini haya. (alama 4)
  4. Je, ahadi aliyoitoa mnenaji ilikuja kutimia? Eleza kwa kina. (alama 8)
   AU
 2. Ukirejelea riwaya nzima ya Chozi la heri:
  1.  Fafanua umuhimu wa elimu katika jamii. (alama 10)
  2.  Jadili jinsi mwamndishi alivyoshughulikia maudhui ya ufadhili. (alama 10)

SEHEMU YA C: TAMTHILIA
Paulina Kea: Kigogo
Jibuswali la 4 au la 5

 1.      
  1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

   Utaindoa karaha
   Usiwe kama juha
   Kujipa bure usheha
   Kutembea kwa madaha
   Eti wenenda kwa staha
   Ndani kwa ndani kuhaha
   Domo mbele kama mbweha
   Dume acha mzaha
   Shika yako silaha
   Kujipa mwenyewe raha
   Iwe yako shabahaaa
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   2. Taja mtindo huu wa uandishi. (alama 1)
   3. Bainisha tamathali moja ya usemi inavyojitokeza katika dondoo hili. (alama 1)
   4. Fafanua majukumu ya nafsineni katika tamthilia ya kigogo. (alama 4)

  2. Kwa kurejelea wahusika mbalimbali katika tamthilia ya kigogo,eleza jinsi mwandishi alivyotumia nyimbo kuendeleza maudhui. (alama 10)
   AU
 2.  
  1. Utawala wa Sagamoyo unatumia mbinu nyingi kubakia mamlakani.Fafanua mbinu zozote kumi. (alama 10)
  2. Mwanamke ni nguzo imara katika ujenzi wa jamii.Eleza kauli hii ukirejelea tamthilia ya Kigogo. (alama 10)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI
Jibuswali la 6 au la 7
A.Chokocho na D. Kayanda: TumboLisiloshiba na HadithiNyingine

 1. “Halikuwa jambo la kawaida maana maji yalikuwa hayapatikani karibu pale kijijini petu.Sharti mtu aende masafa marefu kuyatafuta.Na sabuni? Sabani ilikuwa kitu cha anasa kwa familia yetu.Wazazi wangu hawakuwa na uwezo wa kununua sabuni.Labda mara moja moja siku za sikukuu..’
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza majukumu manne ya takriri katika dondoo hili. (alama 4)
  3. Kwa kurejela hadithi tulipokutana tena,jadili jinsi haki za watoto zinavyokiukwa.(alama 12)
   AU
 2. “ Wahusika katika hadithi Shibe inatumaliza wametumia uhuru wao vibaya’’ Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano. (alama 20)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

 1. Malaika,
  Nakupenda malaika x 2
  Ningekuoa malaika…
  Ningekuoa dada…
  Nashindwa na mali sina wee…
  Ningekuoa malaika x 2
  Pesa, zasumbua roho yangu x2
  Nami nifanyeje,kijana mwenzio
  Nashindwa na mali sina wee…
  Ningekuoa malaika x 2

  Maswali.
  1. Tambua utungo huu. (al.2)
  2. Toa sababu za jibu lako hapo juu. (al.2)
  3. Taja shughuli ya kijamii na shughuli ya kiuchumi kwenye kipera hiki. (al.2)
  4. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa kwenye utungo huu. (al.2)
  5. Jadili vipi mwasilishaji wa kipera hiki anaweza kuboresha wasilisho lake. (al.6)
  6. Ni matatizo yapi yanayoweza kumkumba mkusanyaji wa kipera hiki nyanjani. (al.6)

Mwongozo wa Kusahihisha

 1. MAJIBU YA USHAIRI
  1. Wenye vyao wanatubana. al.1
  2. Dhamira ya nafsi neni nio kuangazia gharama ya juu ya maisha al.2
  3. malalamishi al.1
  4. Maisha ya viumbe yamefika mwisho na walionavyo wanaendelea kuwanyanyasa.Maskini hamudu bei ya nyama ya mbuzi wala ng’ombe.Wakubwa tuokoeni kwa dhiki tulizonazo.
  5.    
   1. Mazida – neno hilakini limetumika kuleta utoshelezi a mizani.
   2. Ukale ndwele limetumika kuleta urari wa vina al.2
  6.  
   1. Ubeti-mathnawi,lina vipande viwili katika kila ubeti.
   2. Ukara kwa sababu vina vya nje havibadiliki kutoka ubeti wa kwanza hai wa mwisho ilhali vile vya ndani vinabadilika.
  7.  
   1. Taswira oni-wenye macho lioneni
   2. Taswira mwendo-hakwendeki madukani
   3. Taswira hisi-zimewatoka huzuni
  8.  
   1. Dona-unga wa mahindi yasiyikobolewa
   2. zogo-hali ya kukosa utulivu
   3. Waelemea-uzito zaidi upand mmoja
 2. MAJIBU YA CHOZI LA HERI
  1.    
   1. Maneno ya Hazina.
   2. Akimwambia umulkheri.
   3. Walikuwa barabarani wakati Hazina alikuwa ombaomba.
   4. Anamshukuru Umulkheri kwa sababu amemfaa kwa uhitaji wake anapompa shilingi mia mbili.
    (1x4)
  2. Mnenaji ni Hazina.
   1. Mwenye shukrani-alimshukuru Umulheri kwa kumuauni wakati huo kwa vile sio wengi hufanya hivyo.
   2. Mwenye matumaini-anatumaini kuwa hali yake ingeimarika.Anatumaini kuwa siku moja angekutana naye na pia akapata fursa ya kumsaidia.
    (2x2)=4
  3.  
   1. Umaskini-Hazina ni ombaomba aliye barabarani kwa sababu ya ulitima uliomzingira.
   2. Ukarimu-Umulkheri alimsaidia Hazina ambaye anaahidi kumsaidia siku moja pia.
    (2x2 = 4)
  4.  
   1. Hali yake Hazina inaimarika wakati anapochukuliwa na serikali na kupelekwa shuleni.Amejifunza upishi na anafanya kazi kwenye hoteli.
   2. Umulheri anapofika mjini anakutana na Haina ambaye anamfaa,anampa chakula
   3. Hazina anamwongoza Umulkheri na kumpeleka kwenye makao na kumjulisha kwa Bi.Julida msimamizi wa makao hayo.
   4. Kupitia juhudi za Julida Umulkheri alijiunga na shule ya upili ya Tangamano na kuendelea na masomo yake tena.
    Zozte 10x1
 3.  
  1. Umuhimu wa Elimu (al.10)
   1. Chombo cha kueneza amani na upendo
    mamake Ridhaa anamtuliza baada ya kusimangwa na wanafunzi wenzake shuleni na kumshauri kuwa ni vyema kujifunza kuishi na wenzake bila kujali tofauti za ukoo na nasaba.
   2. Nyenzo ya kumfikisha binadamu kwenye kilele cha ufanisi
    Mwangeka, Ridhaa,Mwangemi,Lunga wanafanikiwa maishani kutokana na elimu.
   3. Nyenzo ya kuzindua jamii.
    Shuleni Tila wanafunzwa kuhusu mabadiliko,uwajibikakji wa mtu usipimwe kutokana na jinsia.
    Mwekevu anachaguliwa kama kiongozi baada ya jamii kuzinduliwa.
   4. Nyenzo ya kutoa maarifa ya kuendeleza jamii
    Lunga anatumia elimu katika kilimo kuwaelimisha raia kuhusu mbinu bora za kilimo.
   5. Nyenzo ya kuleta mabadiliko
    Mwanaheri anajiunga na shule ya Tangamano kw lengo la kuandama elimu ili aweze kuleta mabadiliko katika jamii.
   6. Nyenzo ya kuwaokoa vijana kutokana na uovu.
    Hazina anaokolewa kutokana na kinamasi cha uvutaji gundi na matumizi ya mihadarati anapopelekwa shuleni katika mradi wa serikali.
   7. Njia ya kukabiliana na changamoto za maisha
    Hazina anapata kazi katika hoteli,wengiwao(watoto wa mtaani) ni maseremala,waashi na mafundi wa juakali baada ya kuelimishwa.
   8. Nyenzo ya kuondoa mwemeo wa mawazo/huzuni
    Wasichana katika shule ya Tangamano wanatumia fursa hiyo kusimulia juu ya maisha yao na kuliwazana.
    Walimu pia wanawaliwaza wanafunzi wao na kuwapa matumaini.mf Mtawa Pacha anamliwaza Zohali.
   9. Chanzo cha kuboresha miundomsingi katika jamii
    Ridhaa anajenga kituo cha afya cha Mwanzo Mpya.
    Serikali inajenga makao ya watoto pmoja na shule ili kufadhili elimu.
   10. Kigezo cha kupima uwajibikaji
    Neema anakiokota kitoto barabaranui kwani alielewa haki za watoto.
    Mwangeka anamshauri Dick kuacha ulanguzi wa dawa za kulevya na pia ankubali uamuzi wa Apondi kumlea Umu.
    Mwekevu anaikwamua jamii kwa miradi ya maji kinyume na wagombea wenza.

    Zozote 10x1
  2.  
   1. Shirika la Makao bora lilijitolea kuwajengea wakimbizi nyumba bora.
   2. Misikiti na makanisa yalikusanya magunia ya vyakula kuwalisha wakimbizi.
   3. Serikali inajenga makao ya watotowa mtani n kufadhili elimu yao.
   4. Serikali inazindua hazina ya kufadhili masomo ya watoto(idara ya watoto)
   5. Kituo cha wakfu wa Mama Paulina kinawafadhili watoto wa mataani kama Zohali.
   6. Familia ya Bw Tenge inamfadhili Chandachema kwa kukubali kuishi naye anapopata nafasi katika shule ya msingi ya kilimo
   7. Shirika la kidini la Hakikisho la haki na utulivu lilimpeleka Chandachema katika makao ya jeshi la wajane
   8. Ridhaa anawasomesha wapwaze Mzee Kedi.
    Zozote 5x2
 4. MAJIBU YA TAMTHILIA YA KIGOGO
  1.        
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (al.4)
    1. Huu ni wimbo wa Asiya.
    2. Anawaimbia Sudi na Tunu.
    3. Anawaimbia wakiwa mangweni.
    4. Tunu na Sudi wamnawaalika waliokuwa mangweni kuhudhuria mkutano utakaofanyika mbele ya lango kuu la soko ya Chapakazi siku ya maadhimisho ya uhuru ili kushinikiza kufunguliwa kwa soko .
     4x1
   2. Mtindo wa uandishi
    Wimbo 1x1
   3. Tamathali ya usemi
    Tashbihi mf:usiwe kama juha 1x1
   4.    Majukumu ya mhusika
    • Ametumiwa kufanikisha maudhui ya ulevi na athari zake-unywaji wa pombe haramu umewafanya watu kuwa vipofu.
    • Ametumiwa kuonyesha udhalimu wa viongozi kwani anapewa kibali kuuza pombe haramu na Majoka.
    • Anachimuza changamoto zinzokumba ndoa kama ukware.
  2. Jinsi mwandishi alivyofanikiwa kutumia nyimbo kuendeleza maudhui
   • Wimbo wa uzalendo-wimbo unaoimbwa katika kituo cha habari cha uzalendo.wimbo unosifu sagamoyo na kiongiozi wake.
   • Wimbo wa Hashima-wimbo unaoashiria kuwa mambo hubadilika,Kila siku wasema heri yalipita jana.
   • Wimbo wa Ngurumo-anaimba wimbo wa kumsuta Tunu kwa kuwa yeye ni mwanamke anapaswa kuoleka.
   • Wimbo wa umati-wanaimba wimbo katika lango la soko la Chapakazi.Yote yawezekana bila majokax2
   • Wimbo wa Ashua –anaimba kuwa soko lafunguliwa bila Chopi kumaanisha kuw vikaragosi hawana nguvu dhidi ya mapinduzi.
    Zozote 5x2
 5.  
  1. Mbinu za utawala
   • Propaganda-majoka kueneza habari za uongo kumhusu Tunu
   • Vitisho-vitisho kwa wanasagamoyo kama vile Tunu na Sudi
   • Mauaji-anapanga mauaji ya jbali katika ajali ya barabarani
   • Matumizi ya vyombo vya dola-askari wanaamrishwa kuwapiga riasi waandamanaji.
   • Vifungo gerezani-ashua anatiwa gerezani kumuogopesha sudi
   • Tenga –tawala –majoka anajaribu kuwatenganisha Sudi na Tunu
   • Wizi wa kura-Majoka mnadai kuwa hata Tunu angepewa kura zote bado angemshinda
   • Kufukarisha raia-soko lfungwa na hapo ndipo watu walikopata riziki
   • Hongo-Majoka najaribu kumhonga Tunu kwa kutaka kumoza Ngao Junior
   • Kujaza raia hofu
    Zozote 10x1
  2.       
   • Mtetezin wa haki-Tunu anapigania haki za wnasagamoyo
   • Mwenye maadili-Ashua analinda ndoa yake kwa kukataa kushiriki mapenzi na Majoka.
   • Mwenye bidii-Ashua anachmia familia yake kwa kuchuuza maembe.
   • Jasiri-Tunu anamkabili majika na kumueleza maovu yake bila uoga.
   • Menye mapenzi-Ashua anampeda Sudi na wanawe.
   • Mwenye msimamo dhabiti-Ashua anakataa katakata kushiriki uhusiano na majoka.
   • Mwenye hekima-Tunu alitambua ujanja wa majoka wa kutaka kumtenganisha na Sudi
   • Mpenda mabadiliko-Asiya anabadilika na kuacha kuuza pombe
   • Mwenye shukrani-Tunu anamshukuru Siti kwa kumtembelea.
   • Mwenye utu-Tunu anawahurumia wanawe Sudi na kumwomba siti awapeleke kwa mama yake Bi Hashina
    Zozote 10x1
 6. Ulisahau kwamba siku za mwizi ni arobaini?
  1. Fafanua muktadha wa dondoo hili. (al.4)
   • Haya ni maneno ya Bogoa
   • Anamwambia msimulizi na Kazu
   • Wako katika club Pogopogo
   • Bogoa na msimulizibwanakutuna baada ya miaka 41 baada ya kutoroka kwasababu ya kuwa mtumwa wa nyumbani kwa Bi.Sinai. (4 x 1 = 4)
  2. Majukumu mawili ya takriri
   • Imetumika kuchimuza hali ya umaskini kwani hata sabuni hangeweza kununua
   • Imetumika kuendeleza maudhui ya umaskini
   • Imetrumika kusisitiza wa.mfano kutokuwa na uwezo wa kununua sabuni isipokuwa siku ya sikukuu.
   • Imetumika kuendeleza tamathali nyingine tamathali nyingine zasemi mfano chuku.
    Zozote 4x4
  3. Jinsi haki za watoto zinavyokiukwa
   • Kutengwa na familia-Bogoa al;ikuwa na umri wa miaka mitano na hakuwa na baba,mama
   • Kuamrishwa kufanya vitu bila hiari ya Bogoa
   • Bogoa atwishwa mambo yote ya nyumbani alikuwa motto mdogo
   • Watoto maskini hawapaswi kusoma shuleni
   • Bogoa hakuwa na uhuru wa kucheza na watoto wa Bi. Sinai
   • Kutishiwa maisha- Bi. Sinai alimtishia Bogoa kuwa angemkata ulimi
   • Kuadhibiwa kwa kuchomwa-Bi Sinai alimchoma Bogoa vidole
   • Kutoambiwa ukweli-Bogoa anawalaumu wazazi wke kwa kumdanganya
    Zozote 6x2
 7.  
  • Mzee Mago anatumia uhuru wa cheo chake serikalini vibaya kwa kupokea mishahara kutoka wizara mbalimbali ilhali hafanyikazi yoyote.
  • Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao vibaya kwa kupanga na kupangilia wapi kwa kudoea badala ya kushiriki katika shughuli ya ujenzi wa jamii.
  • Wananchi w ataifa la mee Mago wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuzingatia kwenda kazini bila kujali kama wanafanya kazi yoyote.Muhimu si kwenda kazini ila kufanya kazi.
  • Mzee Mago anatumia uhuru wake vibaya kwa kutumia mali na wakati wa taifa kuandaa sherehe zisizo na msingi wowote.mf kuingizwa kwa motto wake nasari
  • Mago anatumia magari ya serikali kuhudumu katika sherehe yake
  • Wanahabari wanatumia vyombo vya habari vibaya kwa kupeperusha sherehe ya kibinafsi moja kwa moja badala ya kumulika mambo yanayoathiri taifa.
  • Sasa na Mbura wanatumia uhuru wa wao wa kula kila kitu.Hili linawaweka katika htari ya kupatwa na maradhi.
  • Dj na wenye nafasi katiak serikali wanatumia uhuru wao kupokea mabilioni ya pesa za serikali kutumbuiza katika sherhe ya mtu binafsi.
  • Dj na wenzake wanatumia uhuru wao kupata huduma za msaji,umeme,matibabu miongoni mwa huduma nyingine bila malipo huku wananchi wakilazimika kulipia huduma hizi kwa dhiki na ufukara.
 8. MAJIBU YA FASIHI SIMULIZI 
  1.  Wimbo auwimbo wa mapenzi. 1x2
  2.    
   • Matumizi ya lugha mkato na kuvuta kwa mfano…
   • Urudiaji wa vipande;ningekuwa malaika
   • Uwepo wa beti
   • Kuna kiitiko
    2x1=2
  3.  
   1. Shughuli ya kijamii-kuoa/ndoa 1x1
   2. Shughuli ya kiuchumi-ulipaji mahari 1x1
  4.  
   • Nafsi neni; Kijana anayaetaka kuoa 1x1
   • Nafsi nenewa: Msichana anayechumbiwa 1x1
  5.  
   • Kupandisha na kushusha sauti
   • Matumizi ya viziada lugha
   • Uwe mfaraguzi
    Kubalisha kiimbo na toni kulingana na hali
    Awe jasiriili aweze kuimba bila aibu.
    Zozote 3x2
  6.  
   • Gharama ghali za utafiti mf;kununua vifaa kama tepurekoda
   • Kupotea au kufisidiwa vifaa vya kuhifadhia data.
   • Ukosefun wa wakati wa kutosha wa kufanyia utafiti
   • Vikwazo kutoka kwa watawala-kunyimwa nafasi
   • Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi
   • Mtatizo ya kibinafsimf;kushindwa kudhibiti wahojiwa.
   • Ukosefu wausalama mf; kuvamiwa
    (zozte 3x2)

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Kijiset Revision Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?