Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bondo Joint Mocks Exams 2022

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  •  Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ni alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  • Karatasi hii ina kurasa 10 zilizopigwa chapa.
  • Watahiniwa ni lazima wahakikishe kwamba kurasa zote za karatasi hii zimepigwa chapa sawasawa na kuwa maswali yote yamo.

 

  1.  Lazima
    Umeteuliwa kama mwenyekiti wa tume inayoshughulikia mambo yanayochangia visa vya wanajamii kuwa na msongo wa mawazo. Umewaalika wanatume wengine wawili ili kujadili chanzo cha swala hili. Andika mazungumzo baina yenu.
  2. Jadili namna mshikamano baina ya walimu na wanafunzi shuleni unavyoweza kuboreshwa.
  3. Andika kisa kinachounga mkono methali;
    Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu.
  4. Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno haya;
    Sauti za watu, wengine wakinishangilia na wengine wakinikashifu, zilichanganyika hewani na kuwa kelele zisizoeleweka…

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. Swali la lazima
    Umeteuliwa kama mwenyekiti wa tume inayoshughulikia mambo yanayochangia visa vya wanajamii na msongo wa mawazo. Umewaalika wanatume wengine wawili ili kujadili chanzo cha swala hili. Andika mazungumzo baina yenu.
    Insha hii ina sehemu mbili kuu:
    1. Mtindo
    2. Maudhui

      1. Mtindo
        • Hii ni insha ya mazungumzo
        • Sura ya mazungumzo izingatiliwe kama ifuatavyo;

          1. Anwani
            • Ionyeshe wahusika wa mazungumzo
            • Ionyeshe kiini cha mazungumzo

              MFANO: MAZUNGUMZO BAINA YA WANATUME YA KUSHUGHULIKIA VISA
              VYA WANAJAMII KUKUMBWA NA MSONGO WA MAWAZO.
          2. Utangulizi
            • Uwatambulishe wanatumbe.
            • Utambulishe mahali pa mazungumzo.
            • Unaweza kutambulisha kiini cha mazungumzo.
          3. Mwili
            • Utachukwa mtindo wa tamthilia ambapo jina la mzungumzaji litakuwa kushoto, maelezo yatakuwa kwenye mabano kisha maneno ya wazungumzaji yatakuwa kulia. Mfano, kuwe na salamu
              MWENYEKITI: (Hamjambo wenzangu! Ninasimama na kuwasalimu).Karibuni kwenye
              ofisi hii.
          4. Hitimisho. Wazungumzaji watoe shukurani na maagano.
            TANBIHI: Asiyezingatia sura ya mazungumzo aondolewe alama 4 za sura (- 4 s)
      2. Maudhui
        CHANZO CHA MSONGO WA MAWAZO KWA WANAJAMII
        1. Majukumu yanayopita kiasi.
        2. Masaibu ya walio karibu
        3. Matukio ya kushitua
        4. Kukosa njia za kujikimu.
        5. Kutengwa/ kudharauliwa
        6. Kuporwa
        7. Kuachwa na mpendwa/ wapendwa .
        8. Mazingira ya hatari.
        9. Magonjwa yasiyotibika.
        10. Kujitenga/ kukosa kujihusisha na wengine
        11. Matarajio yanayopita kiasi.
        12. Migogoro katika jamii.
        13. Dawa za kulevya.
        14. Kufeli/ kugundua habari za kusikitisha kuhusu mtu/ jambo fulani.
        15. Ukosefu wa mazoezi na lishe bora.
  2. SWALI LA PILI
    Jadili namna mshikamano baina ya walimu na wanafunzi shuleni unavyoweza kuboreshwa.
    Mtahiniwa aeleze kwa undani jinsi mshikamano baina ya walimu na wanafunzi unavyoweza kuboreshwa. Baadhi ya hoja ni kama vile;
    1. Ushauri kuhusu umuhimu wa mshikamano.
    2. Kutumia njia mwafaka za kukosoana
    3. Heshima
    4. Wanafunzi kuhakikisha wanafanya kazi wanayopewa.
    5. Kufuata sheria na taratibu zilizowekwa
    6. Mafunzo bora
    7. Kuwa na njia za kuwashughulikia wanafunzi wenye changamoto mbalimbali.
    8. Kuimarisha michezo.
    9. Kuimarisha vyama vya kielimu, muziki, uigizaji n.k
    10. Mikutano ya mara kwa mara ili kuwapa wahusika nafasi ya kujieleza.
    11. Kushughulikia maslahi ya wanafunzi / walimu katika nyanja mabalimbali.
    12. Kuwepo kwa usawa na haki.
    13. Kuwa na ufahamu wa changamoto wanazopitia wahusika.
  3. SWALI LA TATU
    • Andika kisa kinachounga mkono methali;
      Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu.
    • Hii ni insha ya methali.
      Mtahiniwa atunge kisa kinachoonyesha maana ya methali hii.
      Maana: Anayeambiwa mawaidha/ maneno (hasa maonyo) huharibikiwa na mambo.
      Insha ina pande mbili;
      1. Kuambiwa na kukataa kitu.
      2. Kupata hasara / madhara

    • MIKONDO
      1. Mwanafunzi anayekatazwa na walimu dhidi ya kutotilia maanani masomo. Anapuuza na mwishowe kuanguka mtihani.
      2. Msafiri aonywe dhidi ya kutumia njia fulani, apuuze kisha apate ajali au afike kuchelewa au atatizike.
      3. Mfanyabiashara anayeonywa dhidi ya kuwekeza katika biashara fulani, apuuze kisha apate hasara.
        Kisa kikadiriwe vilivyo.
        Anayeegemea upande mmoja asipate alama 10

        SWALI LA NNE
  4. Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno haya;
    Sauti za watu, wengine wakinishangilia na wengine wakinikashifu, zilichanganyika hewani na kuwa kelele zisizoeleweka…
    • Msimulizi yuko katika hali mbili: kushangiliwa na kukashifiwa. Hivyo kuna wanaoona aliyofanya/ anayofanya / anayotaka kufanya ni mazuri / ya kufurahisha kuna wengine waonao ni mabaya/ ya kuudhi.
      Pia, msimulizi anaweza kuwa anataka kufanya jambo; wapo wanaomuunga mkono na wengine wanampinga.

      MFANO
      1. Msimulizi anataka kuokoa mtu aliyeanguka majini na anaelekea kuzama. Anashangiliwa kwa kuokoa maisha. Anakashifiwa kwa kuwa anayeokolewa ni jambazi / mkosa maadili. Asimulie kinachotokea baadaye.
      2. Msimulizi anazua rabsha na polisi kwa kuvamiwa kwa kosa asilolitenda. Anasifiwa kwa kujitetea. Anakashifiwa kwa kukosa heshima.
        Kwa vyovyote vile, hali hizi mbili zijitokeze / zidokozewe.
      3. Anayeshughulikia kushangiliwa tu au kukashifiwa tu atuzwe kulingana na mwongozo wa kudumu.

        MWONGOZO WA KUDUMU
        KIWANGO CHA D KWA JUMLA (ALAMA 01-04)
        1. Insha haieleweki kwa vyovyote vile. Uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba MTIHANI lazima afikirie kile mtahiniwa anachojaribu kuwasilisha.
        2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
        3. Lugha ya mtahiniwa wa kiwango hikini hafifu mno, mondo ya sentensi ni mibovu kissing kwamba insha inakosa muwala na mshikamano. Uakifishaji ni mbaya mno na insha ina makosa mengi ya sarufi na hijab.
        4. Mtahiniwa anayejitungia swali na kulijibu huwa katika kiwango hiki.
        5. Insha ya refund wa robot tatu ikadiriwe hapa.

NGAZI MBALIMBALI ZA D

  • D- ( D ya chini) alama 01- 02
    1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile.
    2. Mtahiniwa amejitungia swali tofauti na kulijibu.
    3. Mtahiniwa anaandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya ndimi.
    4. Mtahiniwa ananakili swali au maswali na kuyarudiarudia.
    5. Mtahiniwa ananakili swali

  • D wastani (alama 03)
    1. Insha inakosa mtiririko wa mawazo
    2. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
    3. Mtahiniwa anatumia lugha halafu mno.
    4. Insha ina makosa mengi ya kila aina.

  • D+ (D ya juu alama 04-05)
    1. Insha ya aina hii huwa na makosa mengi lakini unaeza kutambua like ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.
    2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu. Mada haikukuzwa ipasavyo.
    3. Mtahiniwa hana uhakika na matumizi ya lugha.
    4. Mtahiniwa hujirudiarudia.
    5. Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa.(swali la kwanza)

  • KIWANGO CHA C KWA JUMLA (alama 6- 10)
    1. Mtahiniwa anajaribu kuishughulikia mada japo hakuikuza na kuiendeleza vilivyo.
    2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia hafifu/hana ubunifu wa kutoa.
    3. Mtahiniwa anaakifisha sentensi vibaya.
    4. Mtiririko wa mawazo unaanza kujitokeza japo kwa njia hafifu.
    5. Insha ina makosa mengi ya sarufi, hijai na msamiati.
    6. Insha yenye urefu wa nusu ikadiriwe hapa

NGAZI MBALMBALI ZA C

  • C- ( C ya chini alama06- 07)
    1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake.
    2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo.
    3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, hijai na msamiati na insha yake haieleweki kwa urahisi.
  • C ya wastani (alana 08)
    1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
    2. Dhana tofautitofauti hazijitokezi wazi.
    3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha
    4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa.
    5. Amejaribu kushughulikia mada aliyopewa.
    6. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi, hijai na msamiati lakini bado insha inaeleweka.
  • C+ (C ya juu alama 09-10)
    1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini kwa njia isiyo na mvuto.
    2. Dhana mbalimbali zinajitokeza kwa njia hafifu.
    3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha uanaofaa.
    4. Misemo na methali imetumika kwa njia hafifu.
    5. Ana shida ya uakifishaji.
    6. Kuna makosa ya sarufi, hijai na msamiati yanayoathiri mtiririko wa mawazo.

KIWANGO CHA B KWA JUMLA (alama 11-15)

  • Katika KIWANGO hiki mtahiniwa anaonyesha hali ya kuimudu lugha.
  • Mtahiniwa anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi vizuri.
  • Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha.
  • Mada imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.
  • Insha ya urefu wa robo tatu ikadiriwe katika kiwango hiki.

NGAZI MBALMBALI ZA B

  • B-(B ya chini maki 11-12)
    1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri kwa kuwasilisha hoja mbalimbali akizingatia mada.
    2. Mtahiniwa ana mtiririko mzuri wa mawazo.
    3. Mtahiniwa anatumia mifano michache ya msamiati.
    4. Makosa yanadhihirika/kiasi
  • B ya wastani (alana 13)
    1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
    2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika akizingatia mada.
    3. Mtahiniwa anateua na kutumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
    4. Sarufi yake ni mzuri.
    5. Makosa ni michache.
  • B+ (B ya juu alama 14-15)
    1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika waziwazi akizingatia mada.
    2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
    3. Mtahiniwa ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia
    4. Sarufi yake ni nzuri.
    5. Uakifishaji wa sentensi zake ni mzuri.
    6. Makosa ni machache ya hapa na pale.

KIWANGO CHA A KWA JUMLA (Alama 16-20)

  • Mtahiniwa ana ubunifu wa mawazo (yenye uhalisia) yanadhihirika na kutiririka akizingatia mada.
  • Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato.
  • Ana uwezo wa kutumia tamathali za usemi ili kutoa hisia zake/ mawazo yake kwa njia bora na kwa urahisi.
  • Umbuji wake anadhihirisha ukomavu na ukakamavu wake kimawazo.
  • Insha katika kiwango hiki ina urefu kamili na hoja tano au zaidi.

NGAZI MBALMBALI ZA A

  • A- (A ya chini alama 16-17 )
    1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
    2. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika na anazingatia mada.
    3. Ana mtiririko na muumano mzuri wa mawazo.
    4. Msamiati wake ni mzuri/mwafaka na unavutia.
    5.  Sarufi yake ni nzuri.
    6. Anatumia miundo ya sentensi kiufundi.
    7. Makosa ni machache yasiyokusudiwa.
  • A ya wastani (alama 18)
    1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada.
    2. Anajieleza kikamilifu kutumia lugha yenye mnato.
    3. Anatoa hoja zilizokomaa.
    4. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi.
    5. Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi.
    6. Makosa ni nadra kupatikana
  • A+(A ya juu alama 19-20)
    1. Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughulikiwa vilivyo.
    2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato zaidi.
    3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi.
    4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unaovutia zaidi.
    5. Sarufi yake ni nzuri zaidi.
    6. Anatumia miundo tofautitofauti ya sentensi kiufundi zaidi.
    7. Makosa yake hayazidi matano kwa ujumla.
  • ALAMA ZA USAHIHISHAJI
    = Huonyesha kosa la sarufi . Hutiwa chini ya neno lenye kosa
    _ Huonyesha kosa la hijai. Hutiwa chini ya neno lenye kosa.
    ✓ Huonyeshwa pambizoni mahali hoja inakamilikia
    ✓ Huonyeshwa juu ya msamiati bora
    × Huonyeshwa juu ya msamiati usiofaa
  • UKADIRIAJI WA UREFU
    Hadi maneno 174 ni insha robo.
    Maneno 175 hadi 274 ni insha nusu.
    Maneno 275 hadi 374 ni insha robo tatu.
    Maneno 375 na zaidi ni insha kamili.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Bondo Joint Mocks Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?