Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mangu High School Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. Wewe ni mtangazaji wa kituo cha habari cha Ukweli. Umetembelewa na mwenyekiti wa kikundi cha watetezi wa haki za wanawake jimboni kuzungumzia namna wanawake walivyotelekezwa katika jamii ya leo. Andika mahojiano kuhusiana na swala hili.
  2. Unywanji wa pombe haramu una madhara mengi. Fafanua
  3. Andika kisa kinachoafiki methali; Mgaagaa na upwa hali wali kavu.
  4. Andika insha itakayomalizia kwa maneno yafuatayo;
    ..... Hapo ndipo iliponibainikia kuwa nilikuwa nikiogelea baharini pekee kinyume na wenzangu wote.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Wewe ni mtangazaji wa kituo cha habari cha Ukweli. Umetembelewa na mwenyekiti wa kikundi cha watetezi wa haki za wanawake jimboni kuzungumzia namna wanawake walivyotelekezwa katika jamii ya leo. Andika mahojiano kuhusiana na swala hili.
    • Hii ni insha ya mahojiano
    • Insha iwe na anwani / kichwa
    • Huwa na wahusika wawili
    • Maudhui hutokana na maswali na majibu ya washiriki
    • Mhoji ni mtangazaji
    • Mhojiwa ni mwenyekiti wa kikundi cha watetezi wa haki za wanawake
    • Sura ya mahojiano izingatiwe (mtindo wa tamthilia) maswali na majibu
    • Majina mhojiwa na mhoji au vyeo vyao viandikwe upande wa kushoto wa karatasi
    • Asiponzingatia sura ya mahojiano atolewe alama
    • Mwanafunzi ajihusishe kama mhusika. Asipojihusisha aondolewe alama mbili.
      Baadhi ya hoja
      ✓ Mtoto msichana kunyimwa elimu katika baadhi ya jamii.
      ✓ Mtoto msichana kukosa mahitaji ya kimsingi kama vile sodo.
      ✓ Ugavi wa raslimali, majukumu na hata mali kumpendelea mwanaume.
      ✓ Viongozi vijijini kama vile wazee wa vijiji na viongozi wa mabaraza tofauti ni wanaume.
      ✓ Uongozi wa makanisa na huduma za kidini kutengewa wanaume kwa misingi kuwa wahubiri na mitume wote walikuwa wanaume.
      ✓ Wanawake kutotengewa thuluthi tatu ya nyadhifa zote katika magatuzi na serikali kuu kama ilivyopendekezwa katika katiba.
      ✓ Idadi kubwa ya wenyekiti wa kamati mbalimbali za bunge la kitaifa na seneti ni wanaume.
      ✓ Katika sekta ya elimu walimu wengi wakuu ni wanaume hata katika shule za wasichana pekee.
  2. Unywanji wa pombe haramu una madhara mengi. Fafanua
    Madhara ya unywaji wa pombe haramu.
    ✓ Maradhi tofauti hasa ya maini
    ✓ Kupofuka
    ✓ Kufilisika - pesa zote hutumika kwa ulevi ✓ Kusambaratika kwa ndoa
    ✓ Vifo
    ✓ Uhalifu wengi hushiriki uhalifu kama wizi ili waweze kujipatia pesa za kununua pombe haramu.
    ✓ Kutamauka - wengi wanakosa nafasi za kazi kwa sababu ni walevi. ✓ Kudorora kwa uchumi wa nchi kwa vile vijana hawafanyi kazi
    ✓ Kutelekeza majukumu ya unyumba
    ✓ Huleta migogoro katika familia
  3. Methali - Mgaa na upa hali wali mkavu
    ✓ Kisa kionyeshe hali ambapo mhusika au wahusika wanahangaika / wanafanya juhudi za hapa na pale na mwishowe wanzoa matunda.
    ✓ Ufanisi uonekane kutokana na juhudi za mhusika
    "Tanbihi
    Kisa kionyeshe pande mbili za methali: Kujibidiisha hapa na pale na kule kufanikiwa.
  4. Andika insha itakayomalizia kwa maneno yafuatayo;
    ....Hapo ndipo iliponibainikia kuwa nilikuwa nikiogelea baharini pekee kinyume na wenzangu wote.
    • Msimulizi ujipate katika hali ambapo yuko kivyake. Kwa mfano amepotoka na baadaye anagundua wenzake hawajapotoka au anafanya bidii peke yake na wengine wanalaza damu.
    • Au anaunga au kupinga jambo Fulani pekee na alidhani wako pamoja na wenzake.
      Tanbihi
      Mtahiniwa atumie nafsi ya kwanza.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mangu High School Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?