Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mangu High School Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. SEHEMU YA A: SWALI LA LAZIMA
    USHAIRI
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
    Aldli zangu
    Zasimama ufuoni
    Macho yake
    Yakikagua bahari.
    Papa, mkali kama mauti
    Anahangaisha samaki
    Kwa ndaro na maringo
    Daima akijigamba
    Kwamba baharini
    Haupo uwezo unaomtisha
    Wala tisho linalomweza.
    Wakati anaendelea kutiririka
    Huku miongoni mwa samaki
    Wingu zito la huzuni
    Likizidi usani.
    Kama kwa sumaku
    Samaki wanavutwa pamoja
    Na nyuma ya ngao ya umoja
    Wanaenda mwendo wa mbele
    Waktimba nyimbo zenye cheche.
    Kwa hasira zenye moto
    Papa anaongeza ukali,
    Bali umati wa samaki
    Haulegei muumano
    Wala mwendo wa mbele
    Kupungua kasi.
    Mashambulizi makali.
    Bwaal Mashambulizi
    Kutoka pande milioni
    Dhidi ya papa muuaji.
    Sasa baharini
    Nyimbo za ufanisi
    Zinapaa angani
    Kama moshi wa ubani,
    Na kubusu masikio
    Kama muziki wa nyonga.
    1. Maudhui ya shairi hill yamegawanywa katika sehemu tatu. Zifafanue. (al. 3)
    2. Mbinu ya jazanda imetumika sana katika shairi hill. Thibitisha kwa kutoa mifano mitano. (al. 5)
    3. Onyesha mitindo mingine minne ambayo imejitokeza katika shairi hili. (al. 4)
    4. Tambua nafsi neni katika shairi hili. (al. 1)
    5. Jadili umuhimu wa aina mbili za urudiaji. (al. 2)
    6. Eleza umuhimu wa nidaa kama ambavyo imetumika katika shalri hili. (al. 2)
    7. Shairi hili linathibitisha toni kadhaa. Jadili ukweli huu kwa kutoa mifano mitatu. (al. 3)
      SEHEMU YA B:KIGOGO - PAULINE KEYA
      Jibu swali la 2 au 3
  2. Wewe ni msichana mdogo hata ubwabwa wa shingo haujakutoka ila tu umenaswa katika utandu wa kasumba na flasafa za ukoloni mambo leo.
    1. Yape maneno haya muktadha wake. (al.4)
    2. Bainisha mbinu mbili za kimtindo ambazo zimetumika katika dondoo hili. (al. 2)
    3. Kwa kumrejelea msemewa wa maneno haya; onyesha kinyume cha maneno yaliyopigiwa mstari. (al. 12)
  3.    
    1. Badala ya viongozi wa Sagamoyo kuwasaidia wananchi kupiga hatua kimaendeleo wanazibomoa juhudi zao. Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (al. 10)
    2. Kufungwa kwa soko la Chapakazi kunawaathiri Wanasagamoyo vibaya. Thibitisha kauli hii kwa kutoa mifano kumi. (al. 10)
      SEHEMU YA C: CHOZI LA HERI-ASSUMPTA MATEI
      Jibu swali la 4 au 5
  4. Wananchi katika riwaya hii wanasaidiana na kuinuana katika maisha. Jadili kweli wa kauli hii kwa kutoa mifano ishirini, (al. 20)
  5. Soma kifungu hiki na kisha ujibu maswali
    "Ni kweli asemavyo Tila," Ridhaa anayarudia maneno haya akilini, "mustakabali wa ukuaji wetu kiuchumi uligonga mwamba wakati sheria ya mkoloni ilipompa Mzungu kibali cha kumiliki mashamba katika sehemu zilizotoa mazao mengi. Ukengeushi wa ardhi ukatiliwa muhuri, umilikaji wa ardhi na Waafrika katika sehemu hizi ukapigwa marufuku; si mashamba ya chai, si ya kahawa... yote yakapata wenyeji wageni... dau la Mwafrika Ilkagonga jaball. Waafrika, akiwemo baba, Mzee Msubili, walilazimika kuwa, ama vibarua katika mashamba yaliyokuwa yao, au maskwota ambao maisha yao yalitegemea utashi wa Mzungu. Waafrika waliobahatika kuwa na makao yao binafsi walipata sehemu ambazo hazingeweza kutoa mazao yenyewe; na bila shaka hali yao iliweza kutabirika; kuvyazwa kwa tabaka la wakulima wadogowadogo, maskini, wasio na ardhi. Nadhani unaweza kukisia hali ilivyokuwa kwa familia nyingi za Kiafrika. Kama vile Mzee Msubili alivyokuwa akisema, jamii yetu iligeuka kuwa hazina kuu ya wafanyakazi ambamo Wazungu wangeamua kuchukua vibarua kupalilia mazao yao. Vijulanga vilinyakuliwa kwa lazima kutoka kwenye susu zao, hata vifua havijapanuka, vinapelekwa katika maeneo mbalimbali nchini kufanya kazi."
    “Hadi sasa hali hii haijabadilika, nakubaliana na Tila," Ridhaa alijiambia. "Ama hii ndiyo ile wanayoiita, Historical Injustice?" Ridhaa alimuuliza Tila mawazoni.
    1. Changanua mitindo katika kifungu hiki. (al. 10)
    2. Kwa kutoa mifano kumi, tafanua zaidi maswala haya ambayo Ridhaa anayarejea kama historical injustice. (al 10)
  6. SEHEMU YA D: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE
    Jadili maudhui ya uwajibikaji kama ambavyo yamejitokeza katika hadithi ya Mwalimu Mstaafu. (al. 20)
  7. Soma kifungu hiki na ujibu maswali
    Maisha yangu hayakuwa maisha kitu tangia udogo wangu. Si maisha si wazimu! Mamangu Biti Kidebe naye alihitaji kulelewa. Daima alilalamika, "Miguu hii mie nitaingia nayo kaburini! Enh, miguu isiyosikia dawa, miguu gani hiyo?" Kilichobaki ikawa ni kuleana. Alinilea nami nikamlea.
    Nilipokaramka nikaanza kujituma huku na huko. Nilijitahidi kutafuta vijikazi nilivyoviweza. Pengine nilichuma karafuu kwa kazi ya kibarua. Pengine nilimwangulia mtu nazi. Pengine nilienda pwani kurambaza au kuokota kombe na chanje. Pengine nilimsaidia mtu kijikazi chake mkono: kufyeka majani usoni pa nyumba yake, kuyachanja kuni magogo yake na hata kufua na kupiga pasi nguo zake. Kuna siku nilizochuma mabungo au zambarau au chocha au hata fuu kuuza. Nilichoambulia nilikipeleka nyumbani kitusaidic - mimi na mamangu. Hivyo hivyo, zikawa siku zinakwenda na umri unapungua.
    Kwa upande wake mamangu alikuwa na mengi ya kufanya. Alijaribu kila alichoweza ili tupone. Akapika na kupakua tulichobahatisha. Maji yalipozidi unga alivikopoa viakiba vyake. Labda kweli: Jungu kuu halikosi ukoko. Lakini nilitambua pia maana ya akiba haiozi! Tulikuwa na vishamba tulivyopewa kulima. Viwili vya mpunga. Kimoja tulilima msimu wa mwaka, na kingine, msimu wa vuli. Kipande cha tatu tulilima mihogo na migomba miwili mitatu, japo migomba ya bokoboko, maana tangu hapo bokoboko si ndizi. Ingawa kuna wakataao kauli hiyo kwa kuiimbia nyimbo juu:
    Pamoja na yote lakini mamangu hakuacha kunitia skuli. Zama za elimu bure hizo. Kwa taabu na mashaka nikamaliza chumba cha nane. Kumaliza tu na mama akaenda jongomeo!
    Bokoboko ni ndizi,
    Hasa likipata mpisi,
    Na mpisi n'babu 'Amisi.
    1. Changanua mitindo katika kifungu hiki.(al. 10)
    2. Jadili maudhui ya umaskini kama ambavyo yamejitokeza.(al. 10)
  8. SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI
    Umeanguka mwamba Jabali tuloegemea Lilotupa kimbilio Mahasidi kutishia Mti mkuu umegwa Wana wa ndege wawapi? Bila shaka hangaiko 'Metukumba makinda Angalikuwa pamwe nasi Maulana Mungu wetu Swali hilo tungemuuliza Mbona kaacha mauko Ngome yetu kuvamia? Ela mwenyewe Mwenza Ajua hatima yetu Lilobaki kumwamini Riziki kutuangushia
    1. Taja na ufananue muktadha ambao utungu huu unwaweza kutolewa. (al. 2)
    2. Taja sifa za ushairi simulizi ambazo zinazojitokeza katika utongo huu. (al. 5) 
    3. Onyesha mitindo ambayo imetumika katika kifungu hiki. (al. 6)
    4. Umeamua kufanya utafiti wa kipera hiki kwa kushiriki.
      1. Taja na ufafanue hasara zake.(al. 4)
      2. Taja na ufafanue faida zake.(al. 3)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1.    
    1.    
      1. unyanyasaji wa raia/utawala mbaya.
      2. Juhudi za ukombozi/wananchi kudai uhuru
      3. Matunda/manufaa ya juhudi zao/malipo/utulivu na amani
    2.    
      1. Bahari- nchi
      2. mapapa- viongozi/wenye nguvu
      3. Samaki - raia/watu wa kawaida/wananchi
      4. Wingu nzito la huzuni - athari za uongozi mbaya
      5. Macho ya nafsini -  Ukaguzi wakel
      6. Samaki kuvutwa pamoja - ushinkiano wa wananchi 
      7. Ngao ya umoja - umoja wa wananchi
    3.  
      1. Tashbihi - Kama kwa samaki mkali
      2. Uhuishi - Akili kusimama
      3. chuku - tishio linalomweza
      4. Nidaa - Ewaa! Mashambulizi
      5. Taswira - mguso - Kubusu masikio
    4. Mzalendo/mwanaharakati/mwananchi wa taifa husika/ambaye amechora dhuluma za viongozi
    5. Umuhimu wa aina za unidiaji
      1. Takuiri ya maana - ndano, maringo kujigamba
        umuhimu - kusisitiza kuhusu maringo na kutojali kwa viongozi
      2. Neno - Samaki, papa
      3. Kiambishi/Sauti - wa - wanavutwa
        wanaenda
        umuhimu - kufanya shairi limbike/mahadhi/Ridhimu .
    6. Matumizi ya nidaa
      1. kusisitiza mashambulizil
      2. Kuonyesha mshangao - Ewaa!
    7. Hasira - kwa hasira zenye moto/nyimbo cheche
      1. Maringo.majigambo
      2. utulivu
      3. Huzuni - wingu nzito la huzuni.
  2. Kigogo
    1.    
      1. maneno ya Majoka.
      2. kwa Tunu
      3. Ofisini mwa Majoka.
      4. Ni baada ya Tunu kumhoji Majuka Kuhusu vijana watano waliouwawa
    2. Msemo - ubwabwa wa shingo (Hajakomaa)
      1. Taswira (mguso) naswa katika utando Wa Kasumba na falsafa za ukoloni mamboleo.
      2. Utohozi - faisafa
    3. Kukomaa kwa Tunu.
      Wakati Asiya anamwomba msamaha anamsamehe.
      1. Anajua umuhimu wa usalama - anapomwona Kenga akihutubia wahuni chini ya mbuyu anahofia usalama wa wananchi na kuwataka Kombe Bora na sudi waende Wasiklia
      2. Anakataa ujenzi wa hoteli ya kibinafsi. Kwenye uwanja wa soko. Andenda kwa Ofisi ya Majoka na kumwambia kuwa hatajenga hoteli ya kibinafsi hapo.
      3. Anawahimiza raia kususia mkutano wa majoka ili kumshinikiza kulifungua soko
      4. Anakashifu upikaji wa pombe haramu anamwambia Asiya kuwa imewauwa watu wengi
      5. Amewahi kuwa kiongozi wa wanafunzi 
      6. Anawahimiza wanasagamoyo kutowachagua viongozi wanaowatusi
  3.    
    1.    
      1. Ulevi unaongezeka-Ngurumo anasema Kuwa mauzo ya pombe yalikuwa yameongezeka.
      2. Raia wanakataa kuhudhuria sherehe za majoka
      3. Uchumi wa jimbo unapungua wachuuzi hawalipi ushuru tena
      4. Majoka anaondolewa mamlakani-soko ni miongoni mwa Sababu
      5. Tunu anavamiwa na kupigwa kwa sababu anatetea kafunguliwa kwa soko
      6. Sudi Kombe na Bora wanahamisha Karakana yao na kuipeleka nyumbani. kwa sudi
      7. Vibanda vilivyokuwa karibu na soko vinabomolewa ili Majoka apate nafasi ya kujenga hoteli
      8. Njaa - Pili na Pendo wanalala njaa kwa sababu Sudi hana namna
      9. Kutishiwa kufungwa kwa Runinga ya mzalondo - Hii ni kwa sababu runinga. hii inapeperusha maandamano,
      10. Majoka anasema kuwa wafadhili wa Tunu wakunje jamri
      11. Maandamano - Raia wanaandamana ili kumhimiza majoka afungue soko
      12. Mauaji - vijana 5 wanaangamia warati wa maandamano haya
      13. Kisasi - majoka ana kisasi dhidi ya Tunu Kwa sababu ya kuongoza maandamano dhidi ya kunywa kwa soko na Majoka.
      14. Utegemezi - Ashua anaenda kwa Majoka, kuomba msaada wa chakula
      15. Kunyatuliwa mamlakani - sababu moja wapo inayowafanya raia kumchagua kwa sababu ya kufunga soko
      16. Kupanda kwa bei ya chakula
      17. Wafadhili wa Tunu wanafunishwa na Majoka
    2. Athari za kufungwa kwa soko
      1. Kukosa mahali pa kuuzia bidhaa - Sudi Bora na Kombe, wanakosa mahali pa kuuzia bidhaa zao.
      2. Njaa- watoto wake Sudi wanakosa chakula.
      3. Kuna mgogoro unaozuka kati ya Ashua na Sudi
      4. Migomo inaongezeka mfano mgomo Kwenye Kiwanda cha Majoka and Majoka.
      5. Umaarufu wa Tunu unazidi 60%
      6. Wachuuzi wengine wanakimbilia ulevini
      7. Bei ya chakula inapandishwa mara dufu
      8. Majoka anapata nafasi ya kulipiza kisasi
      9. Ardhi ya Soko inanyakuliwa na Majoka ili ajenge hoteli ya kibinafsi
      10. Majoka anawapa marafika zake ardhi
      11. Vijana watano wanauwawa kwenye maandamano
      12. Tunu anavamiwa na kujeruhiwa ili aache kuongoza maandamano
      13. Ashua anaenda kukopa kutoka kwa Majoka ambaye anachukua fursa hiyo na kulipiza kisasi
      14. Majoka anatishia kuwafunza wafadhili wa Tunu na kufunga kituo cha Runinga cha Mzalendo.
      15. Wananchi wanasusia sherehe za Uhuru ambazo zimeandaliwa na Majoka na Kuhudhuria mkutano wa Tunu kwenye Lango kuu.
      16. Kodi ya wachuuzi inakosa.
  4.      
    1. Ridhaa anawalipia wapwazo Kodi kavo.
    2. Anawajengea maskini hospitali
    3. Wakimbizi kwenye msitu wa mamba wanawapa chakula wale ambao hawakuwa nacho. (nafaka)
    4. Mothers union, Ewa, Guild Ansaa - wanawa pelekea wakimbizi chakula
    5. Anampanga umu - Anamsaidia Dick alipotaka kunzisha biashara
    6. Anampa babake hifadhi baada ya kurudi kutoka mashariki ya kati
    7. Umu - angempa nduguye chakula alipokuwa mdogo
    8. Lunga - anawatetea wananchi ili wasiuziwe mahindi haramu
    9. Tenge - anampa makao Chanda Chema
    10. Dhahabu - anamsaidia umu kupata udhamini wazazi
    11. Bi Tamasha anamsaidia Chanda chema kupangwa na familia ya Tenge
    12. Mwangemi na neema - Kumpanga mwaliko na kumpa malezi mazu
    13. Raia wanaojaribu kumwokoa Lemi na kumtopeleka hospitali
    14. Dick - anawaajiri vijana wenzake 
    15. Hazina - Kumsaidia umu kupata makao Kumnunulia cjhakula
    16. Pacha - Kuwasaidia watoto mayatima. Kupata makao, malezi chakula mapenzi na elimu. Ikuwahifadhi waliotoroka kwao
    17. Kaizani - wakiwa ukimbizini aliwasaidia wakimbizi na wazo la long drops hivyo kupunguza magonjwa 
    18. Aliyekuwa wazi - anasaidia kupanga water hivyo kuepusha sintofahamu
    19. Selume + Meko - Licha ya kuwapa wagonjwa matibabu wanawapa ushani pia. Wengi wamefaidi.
    20. Mzee Maarifa- anafanya juhudi za kukomesha tohara/mila na tamaduni zilizopitwa na wakati
    21. Tetei - Anawatetea. Anawatetea watoto wa kiume dhidi ya unyanyasaji
    22. Neema - anakiokota kiokota kitoto riziki Immaculata na kukisaidia kupata makao
    23. Kairo, chandachema, zohali na Lemi wanampa mawaidha umu na kumsaidia kuutua mzigo mzito wa mawazo
    24. Mkewe kuwa alimpa Jairo zawadi
  5.      
    1. Changanua mitindo katika kifungu hiki
      1. Nafsia - Ridhaa anayasema maneno haya akilini
      2. Ritifati - anayanidia maneno ya Tila kama ambavyo Tila aliyasema mmustakabali wa ukuaji wetu
      3. Nahau - gongwa mwamba kutofanikiwa
      4. Uhuishi - sheria kumpa micoloni kibali cha kumiliki mashamba/ Tia muhuni pigwa marufuku
      5. Tabaini si mashamba ya chai, Si ya Kahawa
      6. Methali - dau la mwafrika likagonga jabali
      7. Kinaya - Kuwa maskwota katika mashamba yaliyokuwa yao
      8. Tashbhi - Kama vile Mzee Msubili alivyokuwa akisema jamii yetu iligeuka kuwa hazina kuu ya wafanyikazi
      9. Chuku-  vijulanga vilinyakuliwa kwa lazima kutoka kwenye susu zao hata vifuo havijapanuka
      10. Jaranda - vijulanga, kusisitiza kuwa waligumikishwa wakiwa wadogo
      11. Usimulizi - Ridhaa anaamulia mazungumzo kati yake na Tila
      12. Mbinu rejeshi - Kisa chenyewe kilitendeka zamani
      13. Tanakuzi - wenyeji wageni
      14. Mdokezo wa methali - Dau la mwafrika likagonga Jabali
      15. Kuchanganya nyakati - wakati uliopita na wakati ullopo
      16. Dimi - Historical injustice
    2. Historical injustice
      1. Wazungu walipoingia Afrika walichukua mashamba ya waafrika na  kufanya yao
      2. Waliwachukua waafrika na kuwatumikia katika mashamba yao
      3. Waliwalipa waafrika mshahara
      4. Walipeleka mazao ng'ambo badala ya kuyatamishia hapa.
      5. Waliwatenga waafrika - Nyumba zao zilikuwa mbali na zile za waafrika
      6. Waliwakataza waafrika kupanda mimea ya kisasa - kahawa, majani
      7. Waliendelea kumiliki ardhi baada ya uhuru
      8. Walichukua ardhi ambazo zina hutuba na kuwaachia waafrika ardhi ambazo hazina mafao.
      9. Waliwanyima waafrika matibabu
      10. Wanapochimba maadini yetu, wanayapeleka kwao. Sisi hatufaidi kwayo.
      11. Mamake Kaizani anambagua subira Kwa misingi ya kikabila
      12. Mwimo hakutaka kuwaona wanawake asubuhi. Aliamini kuwa wangemletea nuksi.
      13. Wazungu wanaomiliki mashamba makubwa
      14. Kuna watoto wavulana ambao wanalawitiwa na hawana wa kuwatetea.
  6.  
    1. Uwajibikaji
      1. Wazazi na wanafunzi wanafika shuleni kumzawidi mwalimu Mosi kwa sababu ya kazi nzuri
      2. Mwalimu Mosi anawasuta wanafunzi wake kwa kuendeleza ubaguzi
      3. Mwalimu mosi anawaomba watu kumpigia Jairo makofi
      4. Mwanafunzi mmoja wa zamani anajitolea kumpelekea a Mwalimu Mosi vitu kwa gari lake
      5. Sera anamsihi mwalimu Mosi aikubalie fimilia ya Jairo ikae pale kwake
      6. Mwailmu Mstaafu Mosi anaipa famila ya Jairo nyumba
      7. Mkewe Mosi anamwambia mwalimu mstaafu amchuke kama mkewe lakini mwalimu mstaafu anakataa
      8. Mkewe Jairo na mkewe Mosi wanafanya kazi kwa ushirika
      9. Mosi anampeleka bintiye Jairo mjini akanunue vitabu vya hesabu.
      10. Mosi na mkewe wanampeleka bintye Jairo kwa shule ya bweni
      11. Jairo anapotaka Kujitasha majini, kijiji kizima kinamzuia asifanye hivyo
      12. Mosi alipokuwa mwalimu aliwashauri wanafunzi wake dhidi ya ulevi
    2. Kutowajibika
      1. Jairo hakuzingatia masomo alipokuwa shuleni hata baada ya kushauriwa na kuhimizwa na Mwalimu Mosi 
      2. Anumtishia maisha mwalimu Mosi eti kwa kukioa Kitoto chake.
      3. Pia anaitoa familia yake kama zawadi
      4. Anaitelekeza familia yake kwa mwalimu mstaafu - hakufika huko kwa siku ayami
      5. Bi Sera anampendekeza mumewe amchukue mkewe Jiaro kama mkewe
      6. Watu wanamjaza Jairo maneno ya uongo na kumafanya ashikwe na hasira
      7. Jairo anataka kumuua mwalimu Mosi eti kwa kukica kitoto chake anenda kwake na panga kukitenganisha kichwa chake na kiwiliwili chake
      8. Pia anapopata kuwa ule ulikuwa uvumi tu anataka kujitosa majini afe
      9. Mwalimu Mstaafu Mosi hakumwambia
  7.    
    1.    
      1. Tabaini - Si maisha si wazimu!
      2. Nidaa - si maisha si wazimu!
      3. Kinaya - mama mari kunhitaji malezi
      4. Balagha... miguu gani hiyo
      5. Ritifah - Kunukuu maneno kama yalivyosemwa na mtu mwingine
      6. Kuchanganya nafsi - nasfi ya kwanza na nafsi 3
      7. Takuiri- Pengine/hivyo hivyo
      8. Usambamba - Pengine nilichuma
        Pengine nilienda
        Pengine nilimsaidia
      9. Ulinganishi - Juhudi za mashaka
        Kila mtu anajitahidi ili wapate riziki
      10. Jazanda - kupona - kupata chakula 
      11. Tanakuzi Pika Pakua
      12. Methali - jungu kuu halikosi ukoko 
        Akiba haiozi
      13. Nyimbo - wimbo wa bokoboko
    2. Umaskini Katika Ndoto ya Mashaka.
      1. Mashaka anajitahidi kutafuta vijikazi ili kujilisha na kumlisha Biti Kidebe.
      2. Mashaka pia anasema kuwa kazi wanazofanya ni za kijungu jiko
      3. Makao ya maska. maska ni duni - Kibanda kimeshikana na choo
      4. Hana kitanda wala godoro.
      5. Ndoa ya Mashaka inavunjika kwa sababu ya umaskini
      6. Mzee Rubaya anapomaliza kuwaoza mashaka na wanali anaondoka kwa sababu ya aibu
      7. Kwenye ndoto yake mashaka maskini wanaandamana kwa sababu wamechoka umasiani Baadaye mambo yanakuwa mazuri
      8. Mashaka anashindwa kuikimu familia yake mkewe
      9. Wanawe wa kiume wa Mashaka wanalala jikoni kwa chakupewa kwa sababu nyumba yako ni ndogo.
  8.    
    1. Muktadha wa mazishi - Mwamba umeauguka, miti mkuu umegwa 
      Ataje na atoe mfano
    2. Mishororo
      1. Uborongaji - ngome yetu kuvamia
      2. Inkisan - wawapi - wako wapi?/Lililotupa/Pamwe/pamoja.
      3. Ritifaa - 'metukumba
      4. Lugha ya mafumbo- makinda
        miti
        Jabdli.
    3.    
      1. Jazanda - makinda watoto
        -mti- mzazi
        Jabelli- mzazi (mwamba.)
        mti kugwa-mzazi kufa..
      2. Balagha - wana wa ndege wa wapi?
      3. Mdokezo wa methali - mti mkuu umegwa
      4. Udondoshaji + Ritifaa - metukumba.
      5. Taswira - Jabali tuliloegemea/ mti mkuu umegwa.
      6. Mishata - Mbona kuacha mauko
        jabali tuliloegemea.
      7. Hasara za kushiriki
    4.    
      1. Mbinu hii huchukua muda mrefu kuliko kuuliza maswatle.
      2. Huenda mshiriki akatekwa na yaliyomo na kusahau kurekodi
      3. Ugeni wa mtafiti huweza kuzua wasiwasi miongoni mwa wenyeji wakakosa kutenda kama kawaida.
      4. Uchanganuzi wa data inayokusanywa hivi huwa mgumu na ni rahisi kwa mtafiti kuacha maswala muhimu.
      5. Ni njia ghali ya kutafiti - lazima mtafiti asafiri nyanjani,
      6. Vifaa atakavyotumia pia hughanmu pesa mingi mfano Kanda za video
      7. Falda zake
      8. Mtafiti huja karibu sana na jamii na hupata habari za moja kwa moja tena za kuaminika
      9. Ni njia bora zaidi kutumia kwa watu ambao hawajui kusoma wala kuandikwa
      10. Ni rahisi kwa mtafiti kuuliza maswali kuhusu kipera kilichowasilisha
      11. Ni rahisi kunasa anayosikiliza au kutazama hivyo. Kuhifadhi kumbo, toni na ishara
      12. Mtafiti hupata hisia halisi ya yanayowasilishwa kwa vile anakabiliana ana kwa ana na watendaji
      13. Hukuza utangamano kati ya mtafiti na wanajamii - hivyo kupata habari za cutegemeka.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mangu High School Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?