Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2023

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia
  • Kila insha isipungue maneno 400
  • Kila insha ina alama 20
  1. LAZIMA
    Wewe ndiwe mhariri wa jarida la MSINGI IMARA litakalochapishwa shuleni mwishoni mwa mwaka. Andika tahariri juu ya vyanzo vya mikasa ya moto katika shule za sekondari, kisha upendekeze hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuzuia visa hivyo. (alama 20)
  2. Wananchi ndio wa kulaumiwa kwa sababu ya kudorora kwa usalama nchini Kenya. Jadili. (alama 20)
  3. Andika kisa kitakachoafiki maana ya methali: Kidole kimoja hakivunji chawa. (alama 20)
  4. Andika insha itakayokamilika kwa maneno yafuatayo:
    ….tangu siku hiyo nikaamini kuwa kila jinsia ina umuhimu wake. (alama 20)

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SWALI LA KWANZA

Hii ni insha ya tahariri

  1. Muundo/sura
    • Jina la jarida na tarehe
    • Iwe na kichwa
    • Iwe na utangulizi
    • Mwili(sehemu ya maudhui)-maelezo kiaya Hitimisho-jina la mhariri na cheo chake
  2. Maudhui
    • Vyanzo vya mikasa ya moto shuleni
      1. Hitilafu ya nguvu za umeme
      2. Kutowajibika/utepetevu katika utendakazi wa wapishi jikoni.
      3. Majirani au wahusika kutoka nje kufuatia uhusiano mbovu kati yao na shule.
      4. Uchochezi kutoka kwa wafanyakazi wa shule.
      5. Utunzi au matumizi mabaya ya kemikali katika maabara.
        Mikasa hii pia husababishwa na wanafunzi wenyewe kwa sababu kama zifuatazo:
        1. Utumizi wa dawa za kulevya unaoathiri wanafunzi hata wakashiriki jambo hili.
        2. Miigo ya wanafunzi wanaotekeleza uovu huu kutoka shule nyingine/jirani. Hofu ya mitihani
        3. Malezi duni
        4. Njia moja ya kushinikiza usimamizi ili matakwa/haki zao zizingatiwe/zisikilizwe k.v chakula bora, burudani, likizo, n,k.
        5. Athari za mitandao ya kijamii na kuwa na shauku ya kuifanyia majaribio
          Hatua za kuzuia
          1. Uchunguzi wa nyaya za umeme mara kwa mara na kurekebisha hitilafu.
          2. Kutengeneza ua dhabiti
          3. Kuwa na vizima moto katika majengo tofautitofauti ya shule
          4. Shule ziajiri walinzi wa kutosha
          5. Kuweka kamera za CCTV sehemu mbalimbali za shule
          6. Kuhimiza wapishi wawajike ipasavyo
          7. Kuimarisha kitengo cha ushauri-nasaha shuleni
          8. Kuimarisha mikakati ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya. Wahudumu wa maabara wawe makini.

SWALI LA PILI

Kuunga mkono

  1. Chuki/uhasama baina ya makabila (vita vya kikabila).
  2. Uundaji wa vikundi haramu vya vijana
  3. Tamaduni duni/zilizopitwa na wakati k.v kuibiana Mifugo
  4. Mitazamo hasi ya wananchi kuhusu maafisa wa usalama Umiliki wa silaha hatari na baadhi ya wananchi
  5. Wananchi kukataa kufichua wahalifu miongoni mwao
  6. Maandamano ya wananchi yanayovuka mipaka na kuvuruga usalama (viii) Wananchi fukara kuingilia uhalifu kwa madai ya kujitafutia riziki.

Kupinga

  1. Magaidi kutoka nchi za kigeni wanaotatiza usalama nchini.
  2. Uhaba wa vifaa vya kuendeleza na kuimarisha usalama
  3. Idadi ndogo ya maafisa wa usalama
  4. Uhaba wa fedha za kuendeleza uimarishaji wa usalama
  5. Kiwango cha chini cha mafunzo kwa walinda usalama Ukosefu wa ajira kwa Vijana

SWALI LA TATU

  • Hili ni swali la methali. Sehemu mbili za methali zijitokeze. Si lazima afafanue maana na matumizi ya methali.
  • Maana ya methali idhihirike katika kisa cha mtahiniwa
  • Kisa kiibue umuhimu wa ushirikiano katika jamii
  • Mtahiniwa pia anaweza kutunga kisa cha kudhihirisha athari ya kutoshirikiana katika jamii.
    Mifano ya visa:
    1. Mwanafunzi mwerevu masomoni lakini aliye na ubinafsi na hapendi kushirikiana na wengine. Mwishowe katika mtihani wa kitaifa wengi wampiku.
    2. Mmoja katika familia asipende kushirikiana na wengine kwa sababu ya uwezo aliyo nao kama vile wa kifedha. Akumbwe na shida fulani,atafute ushirika wa wenzake lakini ambulie patupu.
    3. Kiongozi wa nchi Fulani,asiyethamini viongozi majirani akumbwe na janga Fulani kama vile tetemeko la ardhi kisha jirani wajitokeze kumpa misaada halafu ajifunze kuhusu umuhimu wa ushirikiano.
      Tanbihi: mwalimu akadirie visa vya wanafunzi ipasavyo.

SWALI LA NNE

  • Huu ni mdokezo wa kuhitimisha. Mwanafunzi aitimishe insha yake kwa maneno hayo.
  • Atunge kisa cha kudhiirisha ubaguzi wa kijinsia lakini mwisho athari zake ziwe wazi.
  • Kisa pia kinaweza kuwa cha mhusika wa jinsia fulani, ambayo hudharauliwa,kuwa na mchango chanya katika jamii.
  • Kinaweza kuwa mhusika kushiriki shughuli ambayo hapo awali ilitengewa tu jinsia fulani,lakini akanawiri.
    Mifano ya visa.
    1. Mwanamke ajitose katika uga wa siasa,akumbane na vizingiti mbalimbali hasa vya ubaguzi halafu aibuke mshindi. Kisha awe kiongozi bora Zaidi kuliko watangulizi wake wa kiume.
    2. Familia ijaliwe watoto wa kike pekee,idharauliwe lakini baadaye wasichana hao wahitimu
      masomoni,kitalanta na kutokea kuwa watu wa kutegemewa mno katika familia na jamii kijumla ikilinganishwa na familia zilizo na watoto wa kiume.
    3. Mhusika wa kiume ametelekezwa kwa ajili ya kumuinua mtoto wa kike. Mwishowe mhusika huyo wa kiume aondokee kuwa wa msaada mkubwa kwa familia au jamii iliyopendelea jinsia ya kike.
    4. Mwanamke kama kocha wa wachezaji wa kiume kuwakifisha viwango vya juu Zaidi kwa mfano katika kandanda. N.k
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Samia Joint Mock Examination 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?