Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Cekana Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  •  Andika insha mbili
  • Swali la kwanza ni la LAZIMA
  • Kila insha isipungue maneno 400
  • Chagua insha nyingine moja kutoka kwa hizo tatu zilizosalia
  • Kila insha iandikwe kwa lugha ya Kiswahili
  • Karatasi hii ina kurasa 12,mtahiniwa ahakikishe kuwa maswali yote yamo na yamepigwa chapa


MASWALI

  1. LAZIMA
    Wewe ni katibu wa jopokazi lililoteuliwa kuchunguza vyanzo vya ongezeko la umaskini nchini. Andika ripoti ya uchunguzi huo huku ukitoa mapedekezo (alama20)
  2. Unywaji wa pombe haramu umekithiri miongoni mwa vijana shuleni. Wewe kama kiranja wa ushauri nasaha, waandikie ilani kuhusu madhara ya pombe haramu (alama20)
  3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali; Achanikaye kwenye mpini hafi njaa (alama20)
  4. Tunga kisa kitakachoanza kwa maneno yafuatayo;
    Majeruhi walifikishwa hospitalini mmoja baada ya mwingine wakiwa katika hali mahututi. Sauti nzito ya daktari mkuu ilihanikiza hewani baada ya ………………… (alama20)


MWONGOZO 

  1.  Hii ni ripoti
    Yafuatayo yazingatiwe:
    1.  Muundo
      Sura ya ripoti idhihirike.
      1. Kichwa - kionyeshe kiini cha uchunguzi
      2. Utangulizi
        •  Mtahiniwa ataje jopokazi: Wanachama walioteuliwa, aliyeteua jopokazi.
        • Hadidu za rejea (Masharti na mipaka ya utekelezaji wa kazi iliyopangiwa jopokazi)
        • Sampuli lengwa - Habari zilizokusanywa.
        • Njia za ukusanyaji - Hojaji, Mahojiano, Majadiliano kwenye vikundi
      3. Mwili - Hoja zijadiliwe humu, vichwa vidogo vitumiwe
        • Vyanzo/visababishi
        • Mapendekezo
        • Hitimisho
        • Kimalizo(sahihi, jina, tarehe)
    2. MAUDHUI
      Baadhi ya hoja ni:
      • Majanga - Kama magonjwa, Mafuriko n.k ambayo huharibu mali na kusababisha umaskini
      • Bei duni ya bidhaa katika masoko - wakulima wanakosa motisha
      • Uzembe na utegemezi wa wananchi - Wanakosa kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali.
      • Mabadiliko ya hali ya hewa yasiyoweza kubashiliwa - Kuwa na vipindi virefu vya jua/ukame
      • Mtazamo hasi wa vijana kuhusu kazi - wanataka kazi za ofisi na hivyo kudharau baadhi ya kazi
      • Kuongezeka kwa idadi ya watu nchini.
      • Ufisadi katika nchi za kiafrika - rasilimali ambazo zingewafaidi watu huporwa na kunufaisha vigogo wachache
      • Utawala mbaya unaosababisha vita na chuki
      • Kuporomoka kwa uchumi wa nchi, hivyo mapato ya kitaifa yanadidimia.
      • Kusambaa kwa magonjwa yasiyo na tiba mfano; Ukimwi na Saratani hivyo kuathiri jamii kwa kiwango kikubwa.
      • Ukosefu wa elimu mwafaka ambayo haiwawezeshi wanafunzi kumiliki stadi za kuweza kujitegemea na kushiriki katika shughuli za kuzalisha mali.
      • Madeni mengi kutoka mataifa ya kigeni
      • Ukosefu wa nyenzo muhimu k.v mtaji za kuzalisha mali.
      • Vijana kukataa masomo
        Mtahiniwa atoe angaa mapendekezo mawili
      • Kuimarisha na kupanua kilimo kwa kuyalima mashamba zaidi
      • Kuongeza nafasi za elimu ya juu ili watu wapate ujuzi utakaowafaa kuzimbua riziki.
      • Kupunguza mikopo kutoka ughaibuni
      • Kuhamasisha wanacnhi kuhusu umuhimu wa kufanya kazi kwa kujitegemea
      • Kuwaelimisha wanajamii kuhusu namna na umuhimu wa kupanga kazi
      • Serikali kukomesha ufisadi nchini
      • Kuimarisha bei ya bidhaa za mashambani katika masoko nchini
      • Kuweka mtaala wa elimu unaooana na mahitaji /gharama ya maisha
      • Kuhamasisha vijana kutotegemea kazi za kiofisi pekee bali waanzishe miradi midogo midogo ya kibiashara.
        Tan:
        1. Sharti muundo wa ripoti ujitokeze
        2. Mtahiniwa atakayepotoka kisura kabisa aadhibiwe alama nne(4s)
        3. Atakayepungukiwa na sehemu mojawapo ya ripoti, achukuliwe kwamba amepungukiwa kimtindo.
        4. Sharti mtahiniwa ajadili vyanzo vya ongezeko la umaskini nchini.
  2. Hii ni ilani
    Yafuatayo yazingatiwe:
    1. Muundo
      1. Kichwa
        Kibainishe yafuatayo:
        • Jina la idara ya ushauri nasaha /anayetoa ilani
        • Inatoka wapi na walengwa ni kina nani
        • Mada - Sharti itaje ilani na inahusu nini
      2. Utangulizi
        Maelezo mafupi kuhusu kinachozungumziwa
      3. Mwili
        Hoja/maudhui yajadiliwe hapa
      4. Hitimisho
        Mtahiniwa aonyeshe hatari ya kukaidi tahadhari iliyotolewa
        Sahihi
        Jina
        Cheo
    2. Maudhui
      Baadhi ya maudhui ni;
      1. Kudhoofisha afya ya watumiaji kwa watumiaji k.v figo na maini
      2. Husababisha mafarakano miongoni na wanafunzi na walimu
      3. Huathiri uwezo wa ubongo wa kuweza kuamua kwa urahisi
      4. Kutumwa nyumbani kwa wanaotumia pombe hii na hivyo kukatiza elimu
      5. Kusababisha ufujaji wa pesa miongoni mwa wanafunzi
      6. Kusababisha vifo miongoni mwa wanafunzi
      7. ukosefu wa maadili miongoni mwa vijana mfano wizi ili kupata pesa za kununua pombe
      8. Kusababisha utengano wa mahusiano baina ya wazazi na wanafunzi, walimu na wanafunzi.
      9. Husababisha ajali barabarani (Shule za kutwa)
      10. Hufanya mtumiaji awe mlegevu kimasomo
        Tan:
        1. Sharti muundo wa ilani ujitokeze
        2. Atakayepungukiwa na sehemu mojawapo ya ilani achukuliwe kwamba amepungukiwa kimuundo.
        3. Sharti mtahiniwa ajadili madhara yanayotokana na unywaji wa pombe haramu miongoni mwa vijana shuleni
  3. Hii ni insha ya methali
    Kisa kidhihirishe maana ya ifuatayo:
    Mtu anayetaabika kwa kazi sana mwishowe hufanikiwa katika shughuli ile
    Baadhi ya hali ambazo zinaweza kujitokeza ni:
    1. Mtahiniwa anaweza kutumia mpini kufanya kazi ngumu ya ukulima, mwishowe afanikiwe kwa kupata mazao mengi
    2. Mhusika awe katika hali ngumu ya maisha, ateseke katika mazingira hayo na mwishowe afanikiwe
      mfano: hali ngumu ya;
      1. kimapenzi/ndoa
      2. kibiashara
      3. kielimu
      4. kikazi
      5. kidini n.k
        Tanbihi:
        1. Pande zote za methali sharti zionekane
        2. Atakayeshughulikia kijisehemu kimoja asipite kiwango cha C+ (alama 10)
        3. Mtahiniwa anaweza akatumia nafsi ya kwanza au mbinu rejeshi
        4. Lazima mtahiniwa aonyeshe hali ngumu iliyomkabili mhusika, jinsi alivyoteseka na alivyofanikiwa baadaye
  4. Hii ni insha ya kibinulizi
    Mtahiniwa aandike insha inayoanza kwa maneno aliyopewa
    Kisa kinaweza kudhihirisha hali zifuatazo:
    1. Mmoja wa majeruhi aweza kuwa jamaa wa karibu wa daktari mkuu
    2. Hali mbaya ya majeruhi ilimfanya daktari mkuu atoe sauti mzito
    3. Idadi kubwa ya majeruhi waliofikishwa hospitalini ilimshtua daktari aliyetaka kuondoka hospitalini
      Tan:
      1. Mtahiniwa ajikite katika mazingira ya hospitalini
      2. Sharti mtahiniwa asimulie kiini cha sauti nzito ya daktari mkuu kusikika na kuhanikiza hewani
      3. Mtahiniwa anaweza kutumia nafsi ya kwanza pale ambapo yeye ni miongoni mwa waathiriwa au mtazamaji
      4. Mbinu rejeshi inaweza pia kutumika

USAHIHISHAJI NA UTUNZAJI
Mtahini aisome insha ya mwanafunzi kwa kuzingatia;

  1. Maudhui
  2. Msamiati
  3. Sarufi
  4. Hijai/tahajia
  5. Muundo
    • sura
    • Mpangilio wa aya
    • Mtindo – upekee wa matumizi ya lugha
    • Urefu
      Maneno chini ya 174 – 05 +
      Maneno chini ya 174 – 274 (Nusu) – 10 C+
      Maneno chini ya 275 – 374 (Robo tatu) – 15 B+
      Maneno chini ya 375 – 400 (Kamili) – 20 A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Cekana Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?