KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 MOKASA PRE MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp
Download PDF for future reference

SEHEMU A: TAMTHILIA
Kea: Kigogo

 1. Lazima
  Chombo chenye rubani imara huhimili vishindo na hasira ya mawimbi makali.
  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake.                         (alama 4)
  2. Tambua na ufafanue fani iliyotumika katika dondoo hili.             (alama 2)
  3. Onyesha jinsi msemewa alivyofeli kuhimili ‘vishindo na hasira ya mawimbi makali’ katika tamthilia hii.    (alama 4)
  4. Eleza kwa tafsili mambo yoyote kumi yanayokwaza usawa katika jamii ya Kigogo.           (alama 10)

SEHEMU B:   USHAIRI
Jibu swali la 2 au la 3

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
  Ewe hisia!
  Umeniamshia ndoto niloisahau zamani
  nyimbo ya kale
  na mdundo usonivutia
  ila hayawani na mwangu rohoni.
  Tulia sasa tulia
  Hebu tulia ewe hisia ulo mtimani
  Nataka katu kusisimka
  kwa sauti yako laini
  Kwani njia zetu ni
  daima hazioani
  Umesubutu vipi kuniita
  kutoka mwako ngomeni
  ulimosahauliwa tangu zamani
  Basi yawache maombolezi yako yaso maoni,
  yawateke hao mashujaa wa kale
  wafu walo kaburini.
  Hebu tulia, usiniingilie
  Usinihangaishe!
  Kukuandama katu haimkini
  Kwani hata sasa…kwa kukuwaza tu dakika hini
  naona majuto ya mbali moyoni          
  kama kwamba nimegawa wangu wakati
  na wazimu, majinuni.
  Basi nenda zako hisia…shuu…hebu tokomea.

  Maswali
  1. Huu ni utungo wa aina gani?                                                                      (alama 2)
  2. Huku ukitoa mifano, fafanua sifa zinazoufanya utungo huu kuwa shairi (alama 5)
  3. Mistari mishata ni nini? Toa mifano kwenye shairi hili.                            (alama 4)
  4. Fafanua tamathali za kifasihi katika shairi hili.                                         (alama 3)
  5. Eleza mbinu tatu alizotumia mtunzi kutosheleza kaida za kishairi.                       (alama 6)
 1. Soma shairi lifwatalo kisha uyajibu maswali yanayoliandama:
  Naandika yangu haya, kwa uwezo wa Wadudi,
  Kanipa njema afiya, kumsifu sina budi,
  Nifundishie insiya, hino methali ya jadi,
  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo
  Ago mchama huuya, mbele mambo yakizidi,
  Hurudi pakawa kaya, kupapenda hana budi,
  Kwingi angawayawaya, ago shuruti arudi,
  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.
  Kule kwetu Mwarakaya, kijiji chetu cha jadi,
  Yalidhihirika haya, bwana mmmoja mkaidi,
  Aloalikwa ulaya, kadhani ‘mepata sudi,
  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo,
  Alidhani hatauya, ‘endapo nchi baidi,
  Na kusema bila haya, kwa inda na ukaidi,
  Kwamba akenda ulaya, harudi kwenya samadi,
  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.
  Aliranda akitaya, kwa mbwembwe na zake tadi,
  Nguo moto kazitiya, nyumbaye akainadi,
  Kasema vyote ‘ishiya; kurudi sina ahadi
  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.
  Matusi aliyamwaya, mengi yasiyo idadi,
  Mkewe kamwita yaya, na kudharau abidi,
  Kanena ‘mekata waya’, ng’ambo nenda kufaidi,
  Mchama ago hayeli, huenda akauya papo,
  Ng’ambo alielekeya, kwa vishindo kama radi,
  Kumbe aliyemwendeya, kabambwa kwa ufisadi,
  Vya watu amebugiya, rushwa na kuhepa kodi,
  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo.
  Kombo yakamwendeya, mambo mno yakazidi,
  Akabakia kuliya, nyumbani ataka rudi,
  Nyumba ipi ‘taingiya’, hana tena tabaradi,
  Mchama ago hanyeli, huenda akauya papo

  Maswali
  1. Kwa kutolea ushahidi ufaao shairini, jadili kifupi maswala matatu makuu ambayo mtunzi ameyashughulikia.                                                   (alama 6)
  2. “Mtunzi huyu ni bingwa wa kutumia lugha kupitisha ujumbe.” Tetea.                     (alama 4)
  3. Fasiri ujumbe wa mtunzi katika ubeti wa sita. (alama 4
  4. Nafsi nenewa katika shairi hili ni nani? (alama 2)
  5. Zaidi ya tarbia, ungelipangaje tena shairi hili?                                                       (alama 2)
  6. Fafanua msamiati ufwatao kama ulivyotumika shairini:                                     (alama 2)
   1. Baidi
   2. ‘mekata waya’

    SEHEMU C: HADITHI FUPI
    Jibu swali la 4 au la 5

 2. Chokocho na D. Kayanda: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
  “Madhila ya mtoto mvulana katika karne ya ishirini na moja ni mengi.” Tetea kauli hii kwa hoja ishirini ukirejelea hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo, Masharti ya Kisasa na Ndoto ya Mashaka.                     (alama 20)   
 1. Salma Omar: Shibe Inatumaliza
  1. “ Sijali lawama mnonilaumu”
   1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   2. DJ na wenzake wanaonekana kufurahia maudhui ya wimbo huu. Thibitisha. (alama 6)
  2.  Alifa Chokocho: Shogake Dada ana Ndevu
   “…tumshukuru kwa jinsi alivyomwongoza na kumwelekeza kwenye njia iliyonyooka”      Ukirejelea wasifu wa Safia, tetea na upinge kauli hii.                             (alama 10)

SEHEMU D: FASIHI SIMULIZI

 1. “Magwiji wa uwanda mpana wa tamaduni za Kiafrika: wazee walioila chumvi wakabobea katika falsafa za turathi zetu, maghuluma wenye misuli tinginya na vifua vya mfumbata vinavyostahimili hujuma za kila nui na malaika wa kike uliosheheni mizinga na chemichemi ya urembo, nawasabahi. Wa zamani waliamba kuwa mwacha mila ni mtuma. Turathi zetu ni uhai. Turathi zetu ni msingi wa ubinadamu wetu. Turathi zetu zinabeba mustakabali wetu. Tuzienzi kama tuenzivyo asali.”

  Maswali
  1.  
   1. Tambua kipera cha utanzu wa mazungumzo kinachohusishwa na kifungu hiki. (alama 1)
   2. Thibitisha jibu lako katika (i) kwa mifano yoyote mitatu.                            (alama 3)
  2. Iwapo umehudhuria utendaji wa kipera hiki nyanjani eleza sifa tano za mtendaji utakazoziona zisizojitokeza kwenye kifungu.          (alama 5)        
  3. Taja na kueleza miktadha minne ambamo kipera hiki kinaweza kutumiwa katika jamii ya kisasa.           (alama 4)
  4. Andika sifa zozote nne za jamii ya nafsi neni katika utungo huu.                      (alama 4 )
  5. Eleza njia tatu za ukusanyaji wa data unazoweza kutumia kukusanya data kuhusu kipera hiki.                                                                                                                   (alama 3)

SEHEMU YA E: RIWAYA

Matei: Chozi la Heri
Jibu swali la 7 au la 8

 1. “Nitapigana kwa jino na ukucha kuulinda utu wangu.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                                    (alama 4)
  2. Eleza umuhimu wa msemaji wa dondoo hili.                                                (alama 4)
  3. Kwa kutolea mifano riwayani, thibitisha namna binadamu alivyopungukiwa na utu. (alama 12)
 1. Mwanamke ametwezwa katika kiwango sawa na namna alivyotukuzwa. Thibitisha ukweli wa madai haya kwa kurejelea riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)

Download KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 MOKASA PRE MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-


Read 12306 times Last modified on Saturday, 18 April 2020 14:35

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.

Print PDF for future reference Join our whatsapp group for latest updates