KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 JOINT PRE MOCK EXAMINATION NAMBALE

Share via Whatsapp

MASWALI
LAZIMA

  1. Wewe kama rais umekerwa na kukithiri kwa ufisadi katika wizara mbalimbali. Andikia arifa mawaziri wako ukiwaeleza madhara ya ufisadi na hatua utakazochukua ikiwa hawatakomesha ufisadi katika wizara zao. (alama 20)
  1. Dhuluma katika asasi ya ndoa haiathiri tu wanajamii husika nyumbani bali elimu ya watoto wao pia. Fafanua.       (alama 20)
  1. Andika kisa kinachoafiki methali:…. Usishindwe kupika ukasingizia jiko la moshi. (alama 20)
  1. Andika insha itakayokamilika kwa maneno yafuatayo:
    ……….Ni jicho gani lisilolengwalengwa na chozi la mshangao na huzuni kwa kushuhudia unyama wa aina hii. Wanadamu wamesahau kuwa mtu ni utu.            (alama 20)


MARKING SCHEME

SWALI LA 1.
Hii ni insha ya arifa/barua memo. Insha hii izingatie yafuatayo:

  1. Iwe na mada/ anwani ya neo Arifa/ Memo juu ya karatasi.
  2. Chini ya anwani iandikwe idara/ sekta ambamo arifa inatokea. Mfano: IKULU YA RAIS.
  3. Ifuatwe na tarehe ya kuandikwa.
  4. Nambari ya rejea ijitokeze chini ya tarehe. Mfano RAS /12/2019K
  5. Idhihirishe arifa inatoka kwa nani. Mfano: KUTOKA KWA: AFISI YA RAIS
  6. Idhihirishe arifa inaelekea kwa nani. Mfano: KUELEKEA KWA: MAWAZIRI WOTE
  7. Hitimisho iwe na sahihi, jina na cheo cha mwandishi.

Baadhi ya hoja za kujibia swali.
Madhara ya ufisadi

  1. Kudorora kwa uchumi.
  2. Utengano miongoni mwa viongozi.
  3. Utepetevu wa maendeleo.
  4. Ukosefu wa ajira kwa sababu ya mapendeleo katika ajira.
  5. Kukwama kwa baadhi ya miradi kutokana na kufujwa kwa fedha.
  6. Hupanua pengo kati ya matajiri na maskini.
  7. Umaskini hukithiri.
  8. Wafisadi kufutwa kazi/kupoteza ajira.
  9. Hushusha hadhi ya mtu husika na taifa kwa jumla.
  10. Huzuia wawekezaji kuwekeza katika miradi ya maendeleo.
  11. Hutamausha wananchi.
  12. Huzua uhasama baina ya viongozi na wanaoongozwa.
  13. Huchochea hisia za kikabila.
  14. Huweza kusababisha migomo katika sekta mbalimbali.
  15. Huipa taifa gharama ya kulipa deni nyingi za kigeni.
  16. Walipa ushuru huumia zaidi kwa kuwekewa mzigo wa kulipa fedha zilizofujwa na wafisadi.
    Tathmini majibu mengineyo.

Hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wafisadi.

  1. Kuachiswa kazi.
  2. Kushtakiwa kortini.
  3. Kushushwa madaraka.
  4. Kuamrishwa kurejesha mali waliyofuja.

Swali la 2.
Athari za dhuluma katika asasi ya ndoa.
Katika jamii husika

  1. Huweza kusababisha mauti/kifo/mauaji miongoni mwa wanandoa.
  2. Baadhi ya vita vya ndoa husababisha ulemavu wa viungo vya mwili kutokana kujeruhiwa katika vita.
  3. Huzalisha talaka.
  4. Uharibifu wa mali na pia stakabadhi za elimu kama vile vyeti vya kufuzu katika vyuo mbalimbali. Hasira huchangia wanandoa kuteketeza stakabadhi hivi eti kama njia ya kumwadhibu mwenziwe.
  5. Wahusika huathirika kisaikolojia. Hupata msongo wa mawazo na mafadhaiko mengi.
  6. Malezi ya watoto huathirika hivi kwamba watoto hutelekezwa kutokana na ugomvi mwingi na vita vya wazazi.
    (Tathmini hoja nyinginezo za mtahiniwa. Zozote 4 katika sehemu hii zafaa.)

    Athari kwa elimu ya watoto
  1. Watoto husheheneza utovu mwingi wa nidhamu kutokana na malezi mabaya nyumbani. Hili huchangia matokeo hasi masomoni.
  2. Watoto hulala sana nyakati za masomo shuleni. Hili hutokana kwa mfano na kutolala nyumbani kwa sababu ya vita vya wazazi usiku kucha.
  3. Watoto hukosa muda wa kudurusu na kufanya kazi ya shule wakiwa katika mazingira ya nyumbani.
  4. Watoto wengi huathiriwa na ukosefu wa karo kwa sababu wazazi hawana wasaa wa kupangia elimu ya watoto wao.
  5. Kutelekeza watoto huathri masomo ya watoto kwa kukosa ushauri nasaha wa wazazi.
  6. Watoto kugeuka dhulumati shuleni na kuishia kuadhibiwa mara kwa mara huathiri masomo yao.
    (Tathmini hoja nyinginezo za mtahiniwa. Zozote 3, zafaa)

Swali la 3.
Methali: usishindwe kupika ukasingizia jiko la moshi.

Maana yake: Mtu akishindwa na kupika hutafuta kisingizio na kusema eti jiko lina moshi.             
Matumizi: Hutumiwa kumzindua mtu anayeshindwa na kutenda jambo fulani akaanza kutafuta visingizio au vijisababu visivyofaa.
Tanbihi:Mtahiniwa aandike kisa kitakachodhihirisha maana ya mthali.
Methali huwa na sehemu mbili. Mtahiniwa lazima abainishe sehemu zote mbili za methali katika kisa chake. Vinginevyo, hatakuwa amejibu swali ipasavyo. Asituzwe zaidi ya alama 8 (C ya wastani).
Akipotoka kwa maana ya methali, hatakuwa amelijibu swali. Atuzwe Bk 02/20.

Swali la 4:
Mdokezo:
….Ni jicho gani lisilolengwalengwa na chozi la mshangao na huzuni kwa kushuhudia unyama wa aina hii. Wanadamu wamesahau kuwa mtu ni utu.    (alama 20)

Kisa kidhihirishe jinsi wanadamu wamekosa utu na kuishia kutenda unyama inayozua toni ya mshangao na huzuni. Kisa kidhihirishe ukweli wa methali kuwa mtu ni utu.
Sharti mtahiniwa amalizie insha yake kwa maneno aliyopewa. La sivyo atuzwe Bk 02/20.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 JOINT PRE MOCK EXAMINATION NAMBALE.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest