KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 NYANDARUA PRE MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

Maagizo.

  • Andika Insha mbili.Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobaki.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
  1. Umepata tangazo la nafasi ya kazi ya uhariri katika shirika la uchapishaji wa vitabu vya fasihi andishi kwenye gazeti la Taifa Leo. Andika barua ya kuomba nafasi hii na uambatanishe na wasifu kazi wako kwa maelezo zaidi.                                                  (Alama 20)
  2. Utelekezaji wa mtoto wa kiume nchini ni janga kuu. Jadili.              (Alama 20)
  1. Andika insha inayoafikiana na methali Baniani mbaya kiatu chake dawa.(Alama 20)
  1. Andika insha itakayomalizikia kwa;
    …walipofungua mlango huo hatimaye,wengi hawakuweza kuzuia hisia zao.Waliangua vilio kwa maafa waliyoyashuhudia.                         (Alama 20)


MARKING SCHEME

  1. Umepata tangazo la nafasi ya kazi ya uhariri katika shirika la uchapishaji wa vitabu vya fasihi andishi kwenye gazeti la Taifa Leo. Andika barua ya kuomba nafasi hii na uambatanishe na wasifu kazi wako kwa maelezo zaidi. (Alama 20)
    1. Muundo wa barua rasmi - yenye anwani 2
      1. Ina anwani ya kwanza: - Mwandishi - mtahiniwa abuni anwani yake – Iwe wima       (Alama1)
      2. Tarehe - Chini ya anuani ya kwanza                                                                           (Alama½)
      3. Anwani ya pili Mwandikiwa- mkurugenzi wa shirika la uchapishaji                             (Alama1)
      4. Maamkizi - Kwa Bwana/ Bibi,                                                                                    (Alama½)
      5. Mtajo / mada - KUH/MINT/ YAH: KUOMBA KAZI YA UHARIRI (Alama2)
      6. Mwili wa barua –
        1. Utangulizi _ Asili ya habari kuhusu nafasi ya kazi – tangazo
        2. Maelezo ya kibinafsi kwa kifupi.
        3. Ufaafu wake kwa hiyo nafasi                                                                           (Alama4)
        4. Maelekezo kwa wasifu kazi kwa maelezo zaidi.
      7. Hitimisho - Sahihi ya mwandishi , jina na cheo kama anacho.                                   (Alama1)
    2. Wasifu kazi/ Tawasifu kazi
      1. Habari za kibinafsi
        – Jina
        - Jinsia
        - Umri / Tarehe ya kuzaliwa
        - Ndoa – ameolewa au la /Hadhi       
        - Anwani - Barua pepe, meme/webu nambari ya simu.
        - Dini
        - lugha uzijuazo                                                                          (Alama2)    
      2. Elimu – Orodha ya shule – Aanze kwa kiwango cha juu zaidi na kumalizia shule ya msingi.
        Ataje hadhi na jina la taasisi, kipindi cha wakati, cheti alichohitimu.   (Alama2)
      3. Tajriba – Ujuzi wa kikazi/ maarifa. Ataje tajriba aliyonayo katika utendaji kazi anayoiomba.
        Ujuzi alionao uonyeshe shirika au kampuni alipofanya kazi.                    (Alama2)
      4. Ufanisi - Ataje na aeleze ufanisi wake.                                                                  (Alama1)
      5. Uraibu - Ataje mambo ambayo anapenda kufanya wakati wa ziada au anapokuwa hayumo
        kazini. K.m. kusoma, kusaidia jamii n.k.                                                 (Alama1)
      6. Wadhamini/ Warejelewa wa wili au zaidi.                                                              
        Habari zifuatazo kuhusu wadhamini zitolewe.
        - Wawe wawili au watatu.
        - Jina /majina
        - Vyeo/ Taaluma/ kazi
        - Anwani
        - Nambari ya simu
        - Kipepesi.                                                                                                            (alama2)
  1. Utelekezaji wa mtoto wa kiume nchini ni janga kuu. Jadili.

    Jinsi ametelekezwa
    Kukosa waelekezi
    Kuwachwa kujikidhi pekee.
    Kutopigiwa debe kama msichana.
    Kutwikwa majukumu angali mchanga.
    Kutoajariwa na mashirika ya ufadhili.
    Vyama vya kupigania mvulana kutowajibika.
    Kunyimwa nafasi ya masomo.
    Kukosa mashirika ya utafiti kuhusu wavuluna.

    Janga
    Anaacha masomo
    Anaingilia dawa za kulevya na anasa.
    Anaungana na vikundi vya ugaidi.
    Wanakosa hadhi ya mwanamume.
    Kuchangia kuporomoka kwa misingi ya kifamilia.
    Kukosa viongozi wa kesho.
    TANBIHI
    1. Lazima aonyeshe pande mbili, asipo atuzwe nusu ya alama.
    2. Kuwe na kichwa au mada.
    3. Atimize maneno kati 350 – 400
    4. Kadiria hoja nyinginezo.
  1. Andika insha inayoafikiana na methali Baniani mbaya kiatu chake dawa.

    Maana.
    kiatu cha baniani ni kitu au kundi la watu ambalo limechukiwa au kudharauliwa.
    Dawa: Kitu husika huenda kikawa ndicho jibu au jawabu au suluhisho kwa tatizo fulani maishani mwa mtu au katika jamii
    Mtahiniwa aandike kisa kuthibitisha matumizi haya ya methali
    Mtahiniwa anaweza kutumia methali nyingine zenye maana sawa kama;
    1. Matango na matikiti ndio maponya njaa
    2. Wembamba wa reli gari moshi hupita
    3. Nyumba nzuri si mlango fungua uingie Utuzaji
    4. Pande zote za methali zishughulikiwe.Anayeshughulikia upande moja asipite alama C 08/20
      Anayetaja tu upande wa pili bila maelezo kikamilifu achukuliwe kuwa amelenga lakini ana udhaifu wa maudhui
    5. Anayekosa kulenga katika kisa chake amepotoka kimaudhui alama D 03/20
  1. Andika insha itakayomalizikia kwa;
    …walipofungua mlango huo hatimaye,wengi hawakuweza kuzuia hisia zao.Waliangua vilio kwa maafa waliyoyashuhudia.

    Mtahiniwa ahitimishe insha yake kwa maneno aliyopewa
    Kisa chake kifungamane na mawazo ya kauli aliyopewa
    Kisa kilenga tukio lililozua taharuki miongoni mwa wahusika
    Tukio lenyewe lazima lidhihirishe maafa /maangamizi
    Lazima litokee kwenye sehemu iliyozingirwa kama vile ndani ya nyumba,katika gari n.k
    Mtahiniwa atumie nafsi ya tatu hali ya wingi(warejelewa)
    Atumie wakati uliopita.
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI PAPER 1 - KCSE 2019 NYANDARUA PRE MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest