KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 NYANDARUA PRE MOCK EXAMINATION

Share via Whatsapp

SEHEMU YA A: RIWAYA
Assumpata K. Matei: Chozi la Heri
LAZIMA

 1. “Haiwezekani! Hili haliwekazi! Itakuwa kama kile kisa cha yule kiongozi wa kiimla wa kike”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili.                                                                                      (alama 4)
  2. Eleza kwa kifupi yaliyowapata wahafidhina baada ya usemi huu.                                  (alama.4)
  3. Riwaya ya chozi la heri inaonyesha maovu yanayotamalaki katika jamii.Thibitisha.    (alama 12) 

SEHEMU B: TAMTHILIA
Kigogo.Pauline Kea.
Jibu swali la 2 au la 3

 1. Tatizo la uongozi katika bara la Afrika ni kikwazo kikubwa cha maendeleo. Kwa kurejelea matukio kwenye tamthilia ya kigogo, jadili ukweli wa kauli hii       (alama 20)

  AU

 2.  “Mtalipa kila tone la damu mlilomwaga sagamoyo ;wewe na watu wako.”
  1. Eleza muktadha wa maneno haya                                                                              (alama 4)
  2. Eleza sifa za mzungumzaji                                                                                           (alama 4)
  3. Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa maisha ya anayezungumziwa yametawaliwa na dhuluma. (alama 12)                

SEHEMU YA C: HADITHI FUPI

 1. Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo, onyesha jinsi jamii imegawanyika kitabaka  kuegemea.
  1. Kielimu
  2. Kikazi
  3. Kiuchumi                                                                               (alama 20)                                                                                                                            

SEHEMU D:   SHAIRI
WASIA

 1. Huno wakati mufti, vijana nawausia
  Msije juta laiti, mkamba sikuwambia
  Si hayati si mamati, vijana hino dunia
  Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula
  Japo aula kushufu, na machoni vyavutia
  Dunia watu dhaifu, yaugua nasikia
  Vijana nawasarifu, falau mkisikia
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.
  Jepusheni na zinaa, mlale penye sheria
  Msije andama baa, makaa kujipalia
  Jepusheni na zinaa, madhara kukadiria
  Uonapo yyang’aria, tahadhari vitakula.
  Ngawa waone wazuri, nadhifu kukuvalia
  Wajimwaie uturi, na mapoda kumichia
  Si mlango nyumba nzuri, ngia ndani shuhudia
  Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.
  Wawapi leo madume, anasa walopapia?
  Wamepita ja umeme, leo yao sitoria
  Shime enyi wana shime, bora kumcha Jalia
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula
  Nambie faida gani, nambie ipi fidia
  Upatayo hatimani, waja wakikufukua
  Ila kufa kama nyani, kasoro yako mkia
  Uonapo vyang`aria, tahadhari vitakula.
  Vyatiririka tariri, vina vyanikubalia
  Alo bora mshairi, pa tamu humalizia
  Nahitimisha shairi, dua ninawapigia
  Uonapo vyang’aria , tahadhari vitakula.
  Ewe Mola mtukuka, si shaka wanisikia
  Wakingie wanarika, na anasa za dunia
  Amina wangu Rabuka, dua yangu naishia
  Uonapo vyang’aria, tahadhari vitakula.

  MASWALI:
  1. Ni ujumbe gani wanaopewa vijana kupitia shairi?.   (alama 4)
  2. Bainisha tamathali mbili za usemi katika shairi hili.    (alama 2)
  3. Eleza bahari ya shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo.   (alama 2)
   1. idadi ya vipande katika mshororo
   2. mpangilio wa vina katika beti.    
  4. Eleza mbinu zozote mbili za kishairi zilizotumika katika shairi hili.   (alama 2)
  5. Andika ubeti wa pili kwa lugha nathari (alama 4)
  6. Eleza toni ya shairi hili.   (alama 1)
  7. Tambua:                     (alama 2)
   1. Nafsi neni
   2. Nafsi nenewa
  8. Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo iliyotumika katika ubeti wa tano. (alama 2)
  9. Eleza maana ya msamiati: ‘aula’   (alama 1)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1. Eleza maana ya miviga. (alama.2)
  2. Eleza sifa tano za miviga. (alama.5)
  3. Miviga ina udhaifu gani. (alama.3)
  4. Fafanua umuhimu wa ngomezi katika jamii. (alama.6)
  5. Eleza vizingiti viwili vinavyokumba ngomezi. (alama.4) 


MARKING SCHEME

LAZIMA

 1.  
  1. -Maneno ya Tetei, Mwanaharakati
   -Anawaambia wananchi/wapiga kula.
   - Baada ya mwekevu kutawazwa/ Kiogozi mwanamuke
   - Watu walishukuwa silaha kupigania uhuru wao.           
  2. - Watu walishukuwa silaha kupigania uhuru wao.
   -Mlio ya buduki ilisikika.
   -Vilio vilijaa hewani.
   -Vyombo vya dola vilitumwa kudumisha amani.
   -Msafara ya watu ilionekana ikimaha kwao.
   -Mazao yalichomwa mashambani
   -Majumba yalichomwa
   -Watu waliuliwa.
   Zozote nne (1 x4)
  3. - Nyumba ya Ridhaa inateketezwa
   • Luga anafutwa kazi bila sababu.
   • Mwanaheri kunajisiwa
   • Fumba kuringa mwanafunzi wake mamba
   • Familia ya ridha kuteketezwa majirani.
   • Pete kuozwa
   • Subira kubaguliwa Kwa sababu za kiukoo.
   • Naomi kuwatelekeza wanawe.
   • Uharibifu wa mazingira – serikali inakata miji.
   • Chandachema chema anadhumiwa kimapenzi na mwalimu wake fumba.
   • Shamba lao shamusi linanyakuliwa.
   • Pete anakeketwa.
   • Ndoa za mapema/pete
   • Uuzaji wa pombe haramu
   • Ulaguzi wa madawa ya kulevya
   • Ulaguzi wa watoto.
    TANBIHI Kadiliria jawabu la mwanafunzi zozote kumi na mbili. (12x1) 
 1. KIGOGO
  Ufisadi
  - Wafanyabiashara wanalazimishwa kutoa hongo kombe anasema lazima tutie tonge kinywanina tuwape wenye nchi kitu kidogo
  - Mapendeleo ya kinasaba
  - Majoka anamteua Kenga binamuye kuwa mshauri wake mkuu (maneno ya sudi uk 9)
  - Majoka anapanga kumtambulisha Ngao Junior kama mrithi wake (uk 36)
  - Usaliti/ukiukaji wa majukumu
  - Watawala wanasaliti wapiga kura kuwa kutotokeleza majukumu yao. Soko linanuka uvundo kutokana na maji machafu ya taka. Wanachojua viongozi ni kukusanya kodi (uk2) hawatekelezi majukumu yao ya kusafisha soko
  - Udhalimu/ukatili
  - Viongozi kutumia vitisho na kuwanyang’anya wafanyabiashara kilicho chao (sudi anasema katika uk 3)
  - Vijana watano waliokuwa wakifanya maandamano wanauawa na wachuuzi sokoni wanaumia uk 16
  - Chuki za kikabila
  - Vijikaratasi vinaenezwa kuwatia woga watu kutoka kabila Fulani. Wanaambiwa kuhama (uk.51-52) Unafiki
  - Majoka anasema kuwa wanasagamoyo wasiruhusu watu wachache waliojazwa kasumba za kiloloni kuwarejesha katika utumwa. Pia anadai kuwa hatuwezi kukubali kutawaliwa tena yeye anatenda mambo yayo hayo anaokashifu.
  - Ubadhirifu
  - Serikali inakopa pesa nyingi na kuziweka katika miradi isiyofaa (pesa inakopeshwa na kutumiwa katika mradi wa kuchonga kinyago cha hayati Marala Bin Ngao
  - Unyakuzi wa ardhi ya umma
  - Ardhi ya soko inanyakuliwa na majoka anajenga hoteli ya kifahari katika ardhi hiyo na kuwagawia wendani wake kama vile kenga baadhi ya sehemu ya ardhi hiyo
  - Matumizi mabaya ya mamlaka Kenga anamshauri majoka kutumia uwezo wake kuharamisha maandamano na kuwaamuru maafisa wa polisi watumie nguvu zaidi kuwatawanya waandamanaji (uku 34)
  - Dawa za kulevya na pombe haramu Tunu anasema kuwa juzi walizika watu waliokufa kutokana na pombe haramu. Wengine wamegeuka kuwa vipofu (ku 63
  - Umaskini umekidhiri katika jamii hii wafanyabiashara katika soko la sagamoyo ni watu wenye elimu na talanta kochokocho kama vile Sudi. Wangali wanaishi katika umaskini licha ya bidii zao. Boza anasema kijirununu cha pesa nene.. maskini akipata (uk 7
  - Vijana wanatumiwa kumvamia Tunu na wapinzani wengineo (zozote (alama 20)
  - Tamaa, Majoka ana tamaa ya mali ya umma kwa sababu analifunga soko la chapakazi ili ajenge hoteli ya kifahari. Vilevile yuko na tama ya wake za wengine m.f Ashua
  - Uozo, Mamapima anapewa kibali na serikali ya majoka kuwauzia watu pombe haramu inayowaua na kuwafanya vipofu. Vilevile majoka yuko na kampuni kubwa ya uzalishaji sumu ya nyoka barani (dawa za kulevya) ambayo inauzwa katika shule ya majoka na majoka academy
  - Ubarakala: Kuna vibaraka ambao wanamshauri Majoka isivyofaa m.f. Kenga anamshauri Majoka kulipiza kisasi kwa Ashua.
  - Tenga Utawala: Majoka anawatenga wasiomuunga mkono k.v. Tunu na Sudi na kuwaleta karibu wanaoukubali ungozo wake m.f. ni mama pima na Ngurumo na pia Kenga.
  - Matumizi ya vyombo vya dola: Polisi wanatumika kuwatawanya wananchi kutumia vitoza machozi. Hali hii inwafanya wanasagamoyo kufa na wengine kuwa walemavu.
  - Kuotkuwa na uhuru wa vyombo vya habari: Majoka anasema Sagamoyo kitabaki kituo kimoja tu Sauti ya Mashujaa.
  - Hali ngumu ya maisha: Wananchi wanoishi katika mazingira machafu, Kombe anasema wamegeuza soko kuwa uwanja wa kemikali na taka. Wanasagamoyo wengine hawana hata chakula.
  - Ukosefu wa uwajibikaji: mama pima anawauzia watu pombe haramu licha ya kuwa ni kinyume cha sheria. Pombe hiyo inawaua watu na kuwapofusha vilevile mama pima anamgawia Ngurumo uroda ili amsaidie kupata kandarasi ya kuoka keki ya uhuru.
  (1 x 20 =20) 
 1. KIGOGO
  1. -maneno ya Tunu
   -anamwabia majoka
   -ofisini mwa majoka
   -Ashu alikuwa gerezani
  2. Sifa za Tunu
   - Mwanamapiduzi
   - Msomi
   - Mtetezi wa haki
   - Jazili
   - Mzalendo
   -Mwajibikaji
   - Mzindushi
   -Mwenye mhawalaka mwema
  3. Thibitisha kwa kutoa mifano kuwa Maisha ya Majoka yametawaliwa na dhuluma.
   • Dhuluma ni kitendo cha kumnyima mtu haki au stahiki yake; ni uonevu, ni tendo lisilo la haki. Majoka alidhihirisha dhuluma maishani mwake binafsi na katika uongozi mwake.
   • Serikali yake hutoza wanabiashara kodi lakini wanafanyia kazi katika mazingira machafu. Uvundo umekithiri. Sudi anasema. “Ni jukumu lao kuhakikisha soko ni safi si kukusanya kodi pekee….. (uk 3).
   • Bali na kulipa kodi isiowaletea huduma yoyote wafanyakazi wa soko wanalalamika kuwa wanadaiwa pesa zaidi. Kombe asema kuwa ni lazima wpate chakula na pia wawape wenye nchi kitu kidogo.
   • Shua asema mahali wanapofanya kazi wanadaiwa kitu kikubwa au kitu chote.
   • Utawala wake unawanahangaisha wafanyakazi, hawafanyi kazi kwa amani Ashua asema “…na kuhangaishwa na wenye nguvu ndiyo hewa tunayopopumua…” (uk2). Sudi anathibitisha hilo anapolalamika kwamba, “si haki kuchukua kilicho chetu na kututishatisha”(uk3).
   • Anadhulumu raia kwa kutumia raslimali za Sagomoyo kujinufaisha pamoja na wachache, wanaomunguka. Wao ndio hula ile keki kubwa, huku raia wakitaabika. Sudi anamwambia Boza, “Hapo basi – kijikeki. Kwa nini wewe upate kidogo? Sagamoyo ni kwenu, shrehe ni zenu.. na keki kubwa ni ya kina nani”(uk 14)
   • Ni dhuluma pia kwa serikali ya majoka kufunga soko la Chapakazi mahali ambapo watu wengi hufanya biashara ili kupata chakula chao cha kila siku.
   • Katika kiwanda chake wafanya kazi wanapujwa. Soko la Chapalazi lilipofungwa bei ya chakula kwenye kioski cha kampuni ya Majoka and Majoka ikapanda maradufu. Wafanyakazi hawawezi kugharimia chakula. Hii ni dhuluma dhidi ya wafanyakazi. Majoka kuendelea kujitajirisha huku wafanyakazi wake wakiumia (uk 17)
   • Maandamano yanayokumba jimbo la Sogamoyo si walimu, si wauguzi, si wafanyakazi wa kampuni, si wafanyakazi wa soko ni ithibati tosha kuwa watu wanadhulumiwa.
   • Ni dhuluma pia kuwaua watu.
   • Alimuua Jabali kuwa mshindani katika siasa.
   • Wale vijana watano wa Majoka and Majoka Company waliuawa wakidai haki yao kwenye maandamano.
   • Tunu alikuwa auawe kwa kukashifu vitendo vyake vya kidhalimu.
   • Kingi alionywa kuwa angevunjwavunjwa na chatu kwa kukaidi amri ya Majoka ya kuwapiga watu risasi.
   • Majoka anawaua hata washirika wake wa karibu akihofia kuwa wangetoa siri zake. Kwa mfano Ngurumo aliuawa ilhali alikuwa mfuasi wake sugu. Chopi alipangiwa kuuawa pia kwa kijua ‘mengi’. Hii ni dhuluma iliozidi. Majoka anasema anaona ziwa kubwa ajabu lililofurika damu… kuna kilio cha ndani kwa ndani na machozi mengi humo yasiyoonekana… (uk 73) na kwamba mikono yake ilikuwa imefungwa nanga humo damuni. (uk 73).
   • Serikali yake imewahini wananchi raha, wanaishi kwa hofu. Heshima anakiri kwamba yeye na Tunu wake wanaishi kwa hofu nyingi. Wanaogopa kwamba wanaweza kuvamiwa wakati wowote hasa akitilia maanani kuwa mwanawe nusura auawe. Tunu anapopiga nduru kwa kuota mamake anafikiri wameshambuliwa.
   • Isitoshe serikali ya Majoka inawahangaisha watu kuwatupia vijikaratasi vya kuwashurutisha wahame Sagamoyo si kwao. Siti anasema, “Jana walitutupia vijikraratasi… Tuhame Sagamoyo si kwetu” (Uk 52-53).
   • Anaamuru polisi kusambaratisha kikatili maandamano raia ambao hawakuwa na hatia. Walikuwa wakidai haki yao tu.
   • Anwawadhulumu raia waliochagua kwa kutowapa huduma muhimu kama vile hospitali, barabara, maji safi, vyoo, nguvu za umeme, elimu na hata ajira kwa vijana waliokamilisha masomo. Viogozi wasiowajibika hawatilii maanani mahitaji ya umma. 
 1. HADITHI FUPI.
  Kwa kurejelea hadithi ya mapenzi ya kifaurongo onyesha jinsi jamii imegawika kitabaka kuegemea
  • Uchumi
  • Kazi
  • Elimu
  • Tabaka ni kundi la watu katika jamii linalojitofautisha na kundi jingine kwa misingi ya kiuchumi, kielimu, kikazi n.k. katika hadithi hii matabaka haya yamedhihirika.
   1. Kiuchumi, kuna tabaka la juu matajiri na la chini la maskini. Watu wenye fedha nyingi wanaweza kununua magari makubwa ya kibinafsi, kujenga majumba ya ghorofa, kununua matatu na mabasi.
    • Matajiri wanaweza kuwapeleka watoto wao shule za mikoa na kitaifa maana wanau wezo wa kulipa karo ya huko.
    • Watoto wa matajiri wakifuzu kwenda chuo kikuu wanahahikisha wanaishi maisha ya kifahari. Mavazi yao ya kutoka nchi za nje wamenunuliwa simu za bei ghali, vipakatalishi na Ipad
    • Wazazi hawa ni msaada kwa watoto wao, wanawapa pesa za kutosha za matumizi chembilecho Penina, babake humtumia elfu tano kila wiki.
    • Watoto wa matajiri hawasumbuki hata baada ya kufuzu vyuoni na kukosa kazi. Penina analipiwa kodi na wazazi wake na nyumbani mwake mna runinga na kochi. Bila shaka amenunuliwa na wazazi wake.
    • Utajiri wa wazazi ndio unawafanya baadhi ya wanafunzi wa chuo cha kivukoni kutokuwa makini sana. Masomo yakiwa magumu, wengine wanahiari kuyaacha. Wanajua wanaweza ungana na wazazi wao katika biashara zinazowaletea mapato makubwa, kwa mfano magari ya uchukuzi na nyumba za kupanga.
    • Shakila anatafutiwa kazi na mamake kwa sababu ana cheo kikubwa kazini mwake. Ni mkurugenzi mkuu.
    • Tabaka la maskini linawakilishwa na Dennis na wazazi wake. Dennis mara nyingi anabaki kutamani/kumezea mate magari makubwa yanayoendeshwa na wenye pesa.
    • Dennis anakiri kuwa “kwetu tunapigania mikono ielekee vinywani.” (uk 20) Haya ndio maisha amezoea”Dennis, hata chuoni anakosa chakula, anakosa pesa za kununua na anakosa kwa kukopa,asema, pesa zangu zimekwisha na sina kwingine ninakoweza kukopa kwa”(uk 18.)
    • Maisha ya watu maskini ni ya hadhi ya chini; ya kunywa uji mweupe bila sukri, mavazi ya bei ya chini yakilinganishwa nay a matajiri ambayo ni ya kutoka nchi za nje.
    • Chumba cha Dennis kinaonyesha anatoka katika tabaka la chini. Hakina vitu vya thamani. Kuna kijiredio ambacho kinaimba kwa sauti ya chini, shuka za kitandani ni kuu kuu zimechanikachanika n.k. hakika kuna utengano wa wazi kati ya maskini na matajiri.
    • Watoto kutoka jamii maskini wanasomea shule za hadhi ya chini, shule za vijijini. Watoto kama vile Dennis huishi wakiwazia umaskini wao katika jamii uliowakossha nafasi ya kusomaa katika shule za kifahari.
    • Tabaka la maskini hufikiri kuwa elimu ni njia moja ya kuwanasua kutoka umaskini. Dennis anasoma kwa bidii ili awe daktari, mhadhiri, mtangazaji au mwandishi msifika.
    • Anatamani kuwa ataweza kununua gari kubwa na hata kuwasaidia wazazi wake. Anawaza moyoni hivi, “Maskini nitawalipaje wazazi wangu wema wlionitendea? Nani atawafidia nguvu na jasho lao…uk 25. Kwa hivyo ni jambo la kutamausha mno Dennis anaposaka kazi kwingi na anakosa. Miaka mitatu baada ya kufuzu chuoni na bado alikuwa akifanya ‘tarmacking’ yaani kutafuta kazi.
    • Watoto kutoka jamii maskini hawapati msaada wa kupata ajira kutoka wazazi. Maasa wazazi hawajulikani na hawana uwezo. Hii ndio sababu Shakila anapata kazi katika kampuni ambamo mamake anafanya kazi naye Dennis anakosa.
 1. LAZIMA: SHAIRI
  1.  
   1. Kujitahadhari na vyote vinavyong`ara sababu zitawadhuru
   2. Kujiepusha na zinaa
   3. Wasiandame baa.
   4. Wasifikirie wanaovalia kinadhifu na kujipondoa ndio wazuri na kuwaandama.
   5. Wasiandame/ wasipapie anasa
   6. Kumcha Jalia
   7. Kuvumilia na kujikaza Zozote 4 x 1 = 4
  2.  
   1. Tabaini – si hayati si mamati ub 1
   2. Msemo - makaa kujipalia ub 2
    kaza kamba.
   3. Methali - si mlamgo nyumba nzuri…ub 4
   4. Tashbihi- wamepita ja umeme ub 5
    kufa kama nyani       ub 6 Zozote   2 x 1 = 2
  3.  
   1. Mathnawi – migao miwili kila mshororo.
   2. Ukara – vina vya ndani vinatofautiana lakini vya nje vinafanana kila ubeti.
    ( 2 x 1= 2)
  4.  
   1. Tabdila          - huno             - huo   ubeti 1
   2. Inkisari – mkamba - mkaamba ubeti 1
    juta – kujuta  ubeti 1
    alo – aliye       ubeti 8
    ngia – ingia ndani
   3. utohozi - sitoria ub 5
   4. Lahaja -hino – hiyo ubeti 1
   5. kuborogha sarufi – makaa kujipalia
    Madhara kukadiria zozote 2 x 1= 2
  5.  
   1. Ingawa vitu vitaonekana bora na kuvutia machoni.
   2. Dunia ina udhaifu na maovu mengi.
   3. Vijana ninawasarifu / nawasihi iwapo mtanisikia.
   4. Tahadhari na vyote vinavyong`ara kwani vinaweza kukudhuru.   4 x 1= 4
  6. Toni ya ushairi- mshairi anawashauri vijana dhidi ya kutotahadhari na ya dunia.   1x 1= alama 1
  7. Nafsi neni – mshauri/ mzazi/ mhenga     alama 1
   Nafsi pokezi – vijana                                     alama 1
  8.  
   1. Balagha – wawapi leo madume, anasa walopapia?
    Umuhimu – kuibua hisia za nafsi nenewa kuhusu kupapia anasa na raha.
   2. Bora/ zuri     (alama 2)

FASIHI SIMULIZI

 1.  
  1. Miviga ni sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii yoyote katika kipindi maalumu cha mwaka. (1x2=alama2)
  2. Sifa za miviga
   • Miviga huandamana na matendo Fulani k.m kucheza ngoma, kupioga magoti
   • Huongozwa na watu mahususi k.m kuna wanaongoza kafara
   • Huandamana na utoaji mawaidha/ulumbi
   • Maleba huvaliwa na wanaohusika
   • Hufanyiwa katika mazingira maalum
   • Huambatana /hufungamna na utamaduni wa jamii husika
   • Hufanya katika kipindi/wakati maalum
   • Huwa na kutolewa kafara
   • Sadaka hutolewa
   • Kuna kula viapo – wahusika huweka ahadi kutenda wema (zozote 5x1=alama5)
  3. Udhaifu
   • Husababisha kudorora kwa maendeleo
   • Huleta utengano kati ya jamii/majirani
   • Huasi mabadiliko ya kiwakati (nyingine zimepitwa na wakati)
   • Madhara yaweza kutokea hasa vifaa butu vinapotumika
   • Huleta utengano wa kijinsia, kumtukuza mwanaume na kudunisha mwanamke k.m jando na unyango (zozote 3x1=alama3)
  4. Umuhimu wa ngomezi
   • Ni njia ya kuwasiliana katika jamii husika
   • Hudumisha usiri wa jamii husika
   • Hutumiwa kutangaza matangazo muhimu kuhusu shughuli maalum
   • Huendeleza utamaduni wa jamii
   • Huisaidia jamii kuionea fahari historia yao
   • Hutahadharisha kuhusu matokeo ya dharura
   • Hudhihirisha ufundi wa kisanaa (kutumia zana Fulani za muziki)
   • Hutekeleza majukumu ya maandishi katika jamii zisizojua kuandika
   • Huburudisha (zozote 6x1 = alama 6)
  5. Vizingiti
   • Mwingiliano wa makabila tofauti hauruhusu tena matumizi ya ngomezi
   • Maendeleo ya teknolojia hayaruhusu ngomezi k.m barua, simu
   • Watu wamekuwa wabinmfsi – hawawezi kuitika ngoma ikipigwa
   • Ukosefu wa usalama – watu kushambiliwa wakiitikia wito wa ngomezi (zozote 2x1=alama 2)

Download KISWAHILI PAPER 3 - KCSE 2019 NYANDARUA PRE MOCK EXAMINATION.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest