Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Joint Pre-Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

INSTRUCTIONS TO CANDIDATES

 • Jibu maswali manne pekee.
 • Swali la kwanza ni la lazima.
 • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu zilizobaki ; yaani, Tamthilia, Hadithi Fupi, Riwaya na Ushairi.
 • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
 • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili

SEHEMU YA A : FASIHI SIMULIZI (ALAMA 20)

SWALI LA LAZIMA

 1.  
  1. Fafanua sifa za nyimbo za watoto. (alama 5)
  2. Eleza maana ya; (alama 5)
   1. Vitanza ndimi
   2. Tarihi
   3. Vivugo
   4. Matambiko
   5. Maapizo
  3. Jadili mifano mitano ya ngomezi za kisasa. (alama 5)
  4. Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)

SEHEMU YA B: TAMTHILIA (ALAMA 20)

 1. Wanaishia kuwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka.’
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza sifa za msemaji wa maneno haya. ( alama 4)
  3. Thibitisha jinsi mwandishi wa tamthilia alivyofaulu kutumia mtindo wa kinaya. (al 8)
  4. Eleza changamoto zinazoikumba elimu. (alama 4)
   AU
 2.  
  1. Tamthilia ya Kigogo ni taswira halisi ya matatizo yanayokumba mataifa mengi barani Afrika.Thibitisha. (alama 10)
  2. Huku ukitoa mifano, angazia nafasi chanya alizopewa mwanamke katika Tamthilia ya Kigogo. (alama 10)

SEHEMU C:HADITHI FUPI (ALAMA 20)
Alifa Chokocho (Tulipokutana Tena)

 1. “Ile haikuwa ziara ya muda mfupi … palikuwa jahanamu kwangu.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  2. Eleza sababu iliyomfanya mzungumzaji kuenda katika “ziara”. (alama 2)
  3. Kwa kutolea hoja zozote kumi na nne, fafanua vile mzungumzaji alipitia “jahanamu”. (alama 14)

SEHEMU YA D : USHAIRI (ALAMA 20)
Jibu swali la 5 au 6

 1. SIPENDI KUCHEKA

  Pana jambo nanatukiya, kwangu hilo ni muhali
  Kitenda naona haya, kujishusha yangu hali
  Sipendi unipe hidaya, sipendi kutenda hili
  Sipendi mimi kucheka

  Sipendi mimi kucheka , kuchekea mawa
  Sipendi ya dhihaka, kwangu nyemi hiwi
  Sipendi kwa hakika, mwovu kistawika
  Halafuye nikacheka!
  Maskini akiteswa
  Yatima akinyanyaswa
  Mnyonge naye akinyonywa

  Sipendi hata ikiwa
  Unazo nguvu najuwa
  Ni hili sitatekezwa

  Mbona lakini nicheke, kwayo furaha?
  Na wewe ukajiweke, uli na siha
  Na yatima pweke, wa anahaha?
  Amenyimwa haki yake, hanayo raha!
  Na moyo wangu ucheke, kwa ha! ha! ha!
  Kucheka kwa kuchewa mimi katu sitacheka.

  1. Hili ni shairi la aina gani? Thibitisha jibu lako kwa kutaja mifano miwili. (alama 3)
  2. Kwa nini mshairi hataki kucheka. (alama 3)
  3. Eleza umbo la ubeti wa tatu wa shairi hili. (alama 4)
  4. Tambua nafsineni katika shairi hili. (alama 2)
  5. Tambua toni ya shairi hili. (alama 1)
  6. Dhihirisha matumizi ya uhuru ufuatao katika shairi hili. (alama 2)
   1. Tabdila
   2. Kuboronga sarufi
  7. Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. ( alama 3)
  8. Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi hili. (alama 2)
   1. Hidaya
   2. Nyemi
 2. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  Naingia ukumbini, nyote kuwakariria,
  Ushairi niwapeni, hoja nitawaachia,
  Mnipe masikioni, shike nachoeleza,
  Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

  Naanza kwa uzalendo, nchi yetu tuipende
  Yadhihirishe matendo, nchi yetu tuipende,
  Wa kila mtu mwendo, usije kawa mpinde,
  Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

  Linda demokrasia, uongozi tushiriki,
  Haki kujielezea, wachotaka na hutaki,
  Changu naweza tetea, demokrasia haki,
  Taifa sio taifa,pasi kuwa maadili.

  Tuwe na uadilifu, twache tamaa na hongo,
  Tusiwe na udhaifu, wa kuwa watu waongo,
  Tukomeshe uhalifu, kisha tuache maringo,
  Taifa sio taifa, pasi kuwa na maadili,

  Ubinafsi si adili, ila ni kusaidia,
  Ukiwa nayo mali, asiye nacho patia,
  Kama mtu mswahili, ubinafsi mtu achia,
  Taifa sio taifa , pasi kuwa na maadili.

  Na inavyoelezea,katiba ni kielezi,
  Tutii kwa mazoea, hadi kijacho kizazi,
  Kwa hayo nitamwachia, hiyo ya ziada kazi,
  Taifa sio taifa, pasi kuwa maadili.

  1. Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na maadili. (alama 4)
  2. Eleza mtindo wowote ule uliotumika katika shairi hili. (alama 2)
  3. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (alama2)
   1. Mpangilio wa vina
   2. Vipande katika mshororo.
  4. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (alama 2)
  5. Eleza toni ya shairi hili. (Alama 2)
  6. Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa nne. (alama 4)
  7. Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. (alama 4)

SEHEMU YA E: RIWAYA: CHOZI LA HERI (alama 20)

 1. ‘Tawala Wahafidhina tawala, Mwanzi wetu tawala…. ‘
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili . (alama 4)
  2. Ni mbinu gani imetumika hapa. (alama 2)
  3. Eleza makosa saba ya maneno haya. (alama 14)
   AU
 2.  
  1. Jadili dhana ya Chozi katika riwaya ya Chozi laHeri. (alama 10)
  2. Riwaya ya Chozi la Heri imejaa aina mbalimbali za migogoro. Jadili. (alama 10)


MARKING SCHEME

 1.  
  1. Fafanua sifa za nyimbo za watoto. (alama 5)
   • Hujaa urudiaji
   • Huashiria kazi za jamii husika
   • Hutumia kiimbo cha juu
   • Huimbwa kwa toni ya furaha
   • Huambatanishwa na uchezaji wa viungo vya mwili.
   • Huhimiza tabia chanya
   • Hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine.
  2. Eleza maana ya; (alama 5)
   1. vitanza ndimi- ni kauli au sentensi zenye maneno ambayo yana mfuatano wa sauti zinazotatanisha kimatamshi.
   2. Tarihi- ni rekodi za matukio ya kihistoria ambayo hupangwa yakifuatana kiwakati na huwasilishwa kwa njia ya masimulizi bila ya kutolewa ufafanuzi.
   3. Vivugo- ni maigizo ya kujigamba ambayo yanaweza kuambatanishwa na ngoma na maleba.
   4. Matambiko- ni sadaka au ada inayotolewa kwa Mwenyezi Mungu, miungu, pepo au mizimu
   5. Maapizo- ni maombi maalum ya kumtaka Mwenyezi Mungu , miungu au mizimu ili kumwadhibu mhusika hasidi, mkinzani au mwovu. (5x1)
  3. Jadili mifano mitano ya ngomeziza kisasa. (alama 5)
   • Milio ya ambulensi
   • Toni katika rununu
   • Kengele shuleni
   • Toni katika saa
   • Kengele za milangoni (5x1)
  4. Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)
   • Vitendawili huwa na fomyula ya uwasilishaji ilhali methali haina fomyula mahususi.
   • Vitendawili huwa na fumbo ambalo lazima lifumbuliwe hapo hapo na hadhira ilhali methali fumbo halifumbuliwi papo hapo na huwasilishwa na mwenye kutumia methali.
   • Vitendawili ni maarufu kwa vijana ilhali methali huwa maarufu miongoni mwa wazee na watu wazima.
   • Vitendawili hutolewa kwenye kikao maalum ilhali methali si lazima zitengewe vikao maalum.
   • Vitendawili huwa na hadhira tendi ilhali methali huwa huwa na hadhira tuli.
   • Vitendawili huwasilishwa kwa majibizano ilhali methali huwasilishwa kwa kauli moja tu na msemaji. (5x1)
 2. ‘Wanaishia kuwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka.'
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   • Msemaji – Ashua
   • Msemewa – Majoka
   • Mahali - ofisini mwa Majoka
   • Sababu – majoka alipompendekezea akubali kufunza katika Majoka and Majoka Academy
  2. Eleza sifa za msemaji wa maneno haya. ( alama 4)
   • Ashua – ni jasiri. Anamkabili Majoka kwa kupaaza sauti ofisini mwake
   • Ni mnyenyekevu. Ananyenyekea mbele ya Majoka ofisini mwake na kumwomba msamaha
   • Ni mwenye heshima. Anakiri kwamba anamheshimu Majoka.
   • Ni mwaminifu. Anakataa kufanya mapenzi na Majoka kwa kuhofia talaka yake.
   • Ni msomi. Amesomea shahada ya ualimu.
   • Ni mwenye tamaa. Anamwambia Sudi kuwa amechoka kupendwa kimaskini, tama ya mali inamtawala.
   • Ni msaliti. Anasaliti ndoa yake kwa kuomba talaka.
   • Ni mwajibikaji. Amewajibika kwa kuwatafutia wanawe chakula.
   • Ni mzalendo. Anakataa kazi anayopewa na Majoka ya kufunza kwa sababu hakutaka kuendeleza ufisadi.
   • Ni mwenye msimamo dhabiti. Anakataa katakata kuhusiana kimapenzi na majoka
    (4x1)
  3. Thibitisha jinsi mwandishi wa tamthilia alivyofaulu kutumia mtindo wa kinaya. (al 8)
   • Watu wengi wantarajiwa kufika katika uwanja wa ikulu kusherehekea uhuru lakini ni kumi tu wanaofika.
   • Ni kinaya uvumi kuenea kuwa Sudi na Tunu ni wapenzi ilhali wao ni wanamapinduzi.
   • Ni kinaya polisi Sagamoyo kuwatawanya waandamanaji ilhali polisi wanapaswa kulinda na kutetea haki za wananchi.
   • Ni kinaya Ngurumo kudai kuwa tangu soko kufungwa, Sagamoyo ni pazuri zaidi mno na mauzo ni maradufu.
   • Ni kinaya wanasagamoyo kulipa kodi na kitu juu yake ilhali soko halisafishwi.
   • Ni kinaya Majoka kutangaza kufunga soko kwa mwezi mmoja ilhali ni mahali watu wanapata riziki.
   • Ni kinaya Majoka kumpa Asiya kibali cha kuuza pombe haramu ilhali ni kiongozi. Pombe hiyo inasababisha vifo na watu kuwa vipofu.
   • Ni kinaya Ashua kuomba Sudi talaka ilhali walikuwa mume na mke kwa madai kuwa amechoka kupendwa kimaskini.
   • Ni kinaya Kenga kumwacha Majoka ilhali ndiye aliyenufaika na uongozi wake.     (8x1)
  4. Eleza changamoto zinazoikumba elimu. (alama 4)
   • Ukosefu wa ajira kwa waliosoma, mfano Tunu na Ashua
   • Matumizi ya dawa za kulevya- wanafunzi katika shule ya Majoka wanadungana sumu ya nyoka.
   • Wivu- husda anamuonea kijicho Ashua kwa kuwa amesoma licha ya kuwa yeye ana kisomo cha msingi.
   • Ukiukaji wa haji- Tunu na Sudi wanapigania haki za wanafunzi wenzao chuoni
   • Mtazamo hasi kuhusu walimu- Ngurumo hakuwa na uhusiano mwema na mwalimu wake wa somo la Historia.
   • Migomo- walimu wanagoma kila wakati.
   • Mtazamo hasi kwa walioelimika- mfano Majoka na Kenga wanadharau shahada ya udaktari ya Tunu.
   • Wanafunzi kuishia kuwa ovyo- wanafunzi wa shule ya Majoka and Majoka Academy wanaishia kuwa makabeji kwa kudungana sumu ya nyoka.
   • Ufisadi. Majoka anamwambia Ashua kuwa angekuwa akifunza katika shule mojawapo ya kifahari.
    (4x1)
    AU
 3.  
  1. Tamthilia ya Kigogo ni taswira halisi ya matatizo yanayokumba mataifa mengi barani Afrika. Thibitisha. (alama 10)
   • mauaji ya kiholela-Jabali
   • vitisho kwa wananchi- Chopi
   • unyanyasaji wa wananchi kwa kutozwa kodi ya juu
   • unyakuzi wa ardhi ya umma – soko la Chapakazi
   • kukatiza juhudi za ukombozi-Tunu
   • kutiwa jela bila sababu- Ashua
   • uchafuzi wa mazingira-ukataji wa miti
   • uongozi wa kidikteta- Majoka
   • viongozi kuzawadi vikaragosi wanaounga uongozi wao mkono
   • ukosefu wa ajira kwa waliosoma- Ashua, Tunu
   • viongozi hawataki kutoka uongozini
   • kuendelezwa kwa biashara haramu- Asiya anauza pombe haramu
   • viongozi wanaendeleza ufisadi
   • viongozi kuomba ufadhili kutoka nchi za magharibu kufadhili miradi isiyofaa- uchongaji kinyago
    (zozote 10x1)
  2. Huku ukitoa mifano, angazia nafasi chanya alizopewa mwanamke katika Tamthilia ya Kigogo. (alama 10)
   • ni mkombozi- Tunu anatetea haki za wanyonge na hatimaye kuleta mageuzi.
   • Ni mtetezi wa haki- Ashua na Tunu wako katika mstari wa mbele kutetea kazi za wanyonge wanapoenda ofisini mwa Majoka.
   • Mwenye utu- Tunu anamshauri Siti awapeleke watoto wa Sudi kwao.
   • Ni jasiri- Ashua anamkosoa Majoka waziwazi bila uoga.
   • Ni msomi. Ashua ana shahada ya ualimu, Tunu ana shahada ya uanasheria.
   • Ni mwenye heshima- Siti anamsalimu mamake Tunu kwa heshima, Tunu anahutubia wanasagamoyo kwa heshima.
   • Ni mwadilifu- Ashua anakataa kumvunjia Sudi heshima licha ya shinikizo kutoka kwa Majoka.
   • Ni mtiifu- Siti anaposhauriwa awapeleke watoto wa Sudi kwa kina Tunu anafanya hivyo.
   • Ni mwenye msimamo thabiti- Tunu na Ashua wanakataa kushawishiwa na Majoka.
   • Ni mwenye bidii.- Ashua anatia bidii kazini ili amsaidie mumewe kukimu familia.
   • Ni mcha Mungu- Hashima anaamini kuwa Mungu alikuwa amekasirishwa na umwagikaji wa damu Sagamoyo.       (zozote 10x1)
 4. “Ile haikuwa ziara ya muda mfupi … palikuwa jahanamu kwangu.”
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
   Msemaji- Bogoa
   Msemewa-anawaambia rafiki zake kina Sebu.
   Mahali- wako katika club Pogopogo
   Sababu- Bogoa alisema maneno haya ili kuwaeleza mateso aliyoyapitia mikononi mwa mlezi wake Bi Sakina.
  2. Eleza sababu iliyomfanya mzungumzaji kuenda katika “ziara”. (alama 2)
   • Alilazimishwa na babake kuenda kuishi jijini kwa marafiki (Bi Sakina)zao ili kupunguza mzigo wa ulezi kwa kina Bogoa ambao walikuwa maskini.    (1x2)
  3. Kwa kutolea hoja zozote kumi na nne, fafanua vile mzungumzaji alipitia “jahanamu”. (alama 14)
   • Aliamrishwa kufanya kazi za nyumbani kama vile kummenyea Bi. Sinai vitunguu maji,mhogo, n.k licha ya kuwa mtoto mdogo.
   • Ilimbidi kuamka alfajiri na mapema kuchoma maandazi na kuyauza shuleni.
   • Bi Sinai aliwaambia watoto wake kuwa Bogoa alikuwa mtoro, hakutaka kwenda shuleni.
   • Bogoa hakuwa na uhuru wa kucheza na watoto wenzake.
   • Alipigwa vibaya na Bi. Sinai alipochelewa kurudi kutoka michezoni.
   • Alinyimwa fursa ya kusoma- alifundishwa tu na rafikiyeSebu kusoma a,be, che,de
   • Alitusiwa na Bi. Sinai
   • Wazazi wake wanapokuja kumuona, Bi Sinai hampi nafasi ya kuwa na wao pamoja.
   • Anakula makoko ya vyakula au makombo ya watu waliyoachabaada ya kushiba.
   • Anakula akiwa wa mwisho wakati kila mtu ashakula.
   • Anakula kwenye vyungu wakati kila mtu alikula vyunguni.
   • Anamwogopa Bi Sinai kwani kila siku alimtisha kumkata ulimi kama angesema chochote kuhusu maisha yake ya ndani.
   • Bi Sinai anamchoma kijinga cha moto viganjani anapochukuliwa na usingizi na kuyaacha maandazi yakiungua.     (zozote 14x1)
 5. SIPENDI KUCHEKA
  1. Hili ni shairi la aina gani? Thibitisha jibu lako kwa kutaja mifano miwili. (alama 3)
   Shairi huru
   • Hakuna urari wa vina
   • Vipande vinatofautiana
   • Idadi ya mishororo inatofautiana
   • Mizani haijitoshelezi.         Zozote 3x1
  2. Kwa nini mshairi hataki kucheka. (alama 3)
   • Atakuwa anajishusha hadhi
   • Hapendi kuchekea mabaya
   • Hapendi dhihaka
   • Hapendi kucheka mnyonge aliyenyimwa haki
   • Anaona haya kucheka         zozote 3x1
  3. Eleza umbo la ubeti wa tatu wa shairi hili. (alama 4)
   • Una mishororo sita
   • Mishororo mitano ya kwanza imegawika katika vipande viwili huku miwili ya mwisho ikigawika katika kipande kimoja
   • Haina urari wa vina
   • Vina vinatofautiana toka ubeti mmoja hadi mwingine. 4x1
  4. Tambua nafsineni katika shairi hili. (alama 1)
   • Mtetezi wa wanyonge
  5. Tambua toni ya shairi hili. (alama 1)
   • Toni ya huzuni/malalamiko/masikitiko
  6. Dhihirisha matumizi ya uhuru ufuatao katika shairi hili. (alama 2)
   1. Tabdila - najuwa badala ya najua
   2. Kuboronga sarufi- sipendi mimi kucheka- mimi sipendi kucheka
  7. Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4)
   • Mshairi anasema hapendi maskini akiteswa na mayatimakunyanyaswa naye mnyonge akinyonywa. Hata ikiwa anayewanyanyasa ana nguvu, anajua kuwa hili halitamtikisa
  8. Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika katika shairi hili. (alama 2)
   1. Hidaya- zawadi
   2. Nyemi – furaha
 6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
  1. Eleza mambo yoyote manne ambayo mshairi anashauri taifa lifanye ili kuwa na maadili. (alama 4)
   • Kuwa wazalendo/kuipenda nchi yao
   • Kuwa na umoja/ kuacha ukabila
   • Kuwa na mgao sawa wa raslimali
   • Kuacha tama
   • Kukomesha uhalifu
   • Kuacha maringo
   • Kutii katiba
   • Kuacha ubinafsi na kusaidiana.       Zozote 4x1
  2. Eleza mtindo wowote ule uliotumika katika shairi hili. (alama 2)
   • Msemo – nipe masikioni- nipe sikio
   • Jazanda / istiari- kawa upinde
   • Takriri – kawa mpinde
   • Tashbihi – kama mtu mswahili
   • Utohozi – demokrasia, bajeti.         Zozote 2x1
  3. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: (alama2)
   1. Mpangilio wa vina
    • Ukaraguni- vina vya kati na vya mwisho vinabadilika toka ubeti hadi mwingine
   2. Vipande katika mshororo.
    • Mathnawi- limegawika katika vipande viwili
  4. Bainisha nafsi neni katika shairi hili. (alama 2)
   • Mwananchi/raia/mzalendo/mkereketwa
  5. Eleza toni la shairi hili. (alama 2)
   • Kunasihi/kushawishi/kuhimiza
  6. Eleza umuhimu wa aina mbili za uhuru wa kishairi zilizotumiwa katika ubeti wa nne. (alama 4)
   • Kubananga/kuboronga sarufi -uongozi tushiriki
    Umuhimu- kuleta urari wa vina
   • Utohozi- demokrasia
    Umuhimu- kuleta urari wa vina
   • Inkisari - pasi badala ya pasipo
    Umuhimu- kuletya urari wa mizani

    2x2 =4
    Aina =1  
    Umuhimu =1
  7. Andika ubeti wa pili kwa lugha tutumbi. (alama 4)
   • Naanza kwa kueleza uzalendo kwamba tuipende nchi yetu. Matendo yetu yaonyeshe kuwa tunaipenda nchi yetu.Tabia ya kila mtu ionyeshe msimamo . Nchi haikamiliki bila ya kuwa na matendo mema. 4x1
 7. ‘Tawala Wahafidhina tawala, Mwanzi wetu tawala…. ‘
  1. Eleza muktadha wa dondoo hili . (alama 4)
   • Ni wimbo ambao Kaizari anaskia waandamanaji wakiimba kwenye runinga kusifu mpinzani wa Mwekuvu wa kiume.ujumbe unalenga raia wa Wahafidhina.
  2. Ni mbinu gani imetumika hapa. (alama 2)
   • Takriri – tawala , tawala
   • Wimbo- tawala wahafidhina tawala Mwanzi wetu 1x2
  3. Eleza matokeo saba ya maneno haya. (alama 14)
   • Raia kama Lime na Mwanaheri wanabakwa
   • Subira anakatwa kwa sime
   • Magari yanachomwa barabarani, nyumba za Ridhaa na Kaizari zinachomwa.
   • Vijana wanaoandamana barabarani wanapigwa risasi na polisi hadi kufa.
   • Ridhaa , Kaizari, Subira na wengine wanajipata katika kambi ya wakimbizi.
   • Uhasama unaingia kati ya koo zilizokuwa zimeishi kwa amani kwa muda mrefu.
   • Familia zinasambaratika; Ridhaa anatengana na mkewe na wanawe
   • Wakimbizi kama Ridhaa katika kambi wanataabika, wanakosa chakula, huduma za afya.     7x1
 8.  
  1. Jadili dhana ya Chozi katika riwaya ya Chozi laHeri. (alama 10)
   • umu analia sana anapowakumbuka nduguze Dick na Mwaliko
   • Umu anahuzunika kwa kukosa kwao nyumbani.
   • Watoto wa Lunga , Dick, Mwaliko na Umu wanalia machozi ya heri wanapopatana katika hoteli ya Majaliwa
   • Ridhaa analia baada ya familia yake na jumba lake la kifahari kuteketezwa.
   • Mwangeka analia kilio cha uchungu babake anapomweleza sababu ya kutozika mabaki ya familia yake.
   • Selume analia inapomlazimu kuondoka na kuacha mtoto na ndoa yake kwa sababu ya ukabila.
   • Subira alipokatwa kwa sime alilia kwa kite.
   • Subira anakilovya kifua chake kwa machozi kwa sababu ya mama mkwe anayemshtumu hali inayopelekea kumwacha mumewe na wanawe.
   • Ridhaa analia kwa kubaguliwa shuleni.
   • Ridhaa alilia machozi ya uchungu alipomweleza Mwangeka mkasa wa kuipoteza aila yake.
   • Kumbukizi za maongezi kati ya Terry na Ridhaa zinamfanya atokwe na machozi.
   • Mwangeka na Annatila wanalia walipokuwa wanaigiza kifo cha mdogo wao Dede.
   • Wenyeji walilia katika mazishi ya Dede.
   • Umu alipokutana na Hazina alilia machozi.
  2. Riwaya ya Chozi la Heri imejaa aina mbalimbali za migogoro. Jadili. (alama 10)
   • Mgogoro wa kikabila- Subira anafukuzwa na mamamkwe kwa sababu ya kutoka kwa jamii tofauti,,, Ridhaa aliitwa mfuata mvua na kutengwa na wenzake shuleni
   • Mgogoro wa kikoloni- mkoloni anapuuza sera za mwafrika za umiliki wa ardhi na kumchukua kama mfanyikazi wake.
   • Mgogoro wa kiimani- Lily anakinzana na wazo la Mwangeka kuwa askari
   • Mgogoro wa kisiasa- kuna mgogoro kati ya wafuasi wa Mwekevu na mpinzani wake mwanamme.
   • Mgogoro waardhi- jamii iliyoselelea katika msitu wa mamba inaondolewa na serikali bila ya kufidiwa.
   • Mgogoro wa kiutawala- vijana wanaamua kutotoka kwa njia jambo linalosababisha wao kupigwa risasi na kujifia
   • Mgogoro wa kitabaka- matajiri wanapewa mikopo ya elimu iliyotengewa watoto wa kimaskini.
   • Mgogoro wa kisaikolojia- darasani Umu anaonekana akiwa mwingi wa mawazo mengi. Mwanaheri anasema anashindwa kumsikiliza mwalimu ju wa msongo wa mawazo.
   • Mgogoro wa nafsi- pete ana mgogoro na nafsi yake jambo linalomfanya kutumia dawa ya panya.
   • Mgogoro wa kiuchumi- Dick anakataa kazi ya ulanguzi wa dawa za kulevya ila anashindwa atapata vipi chakula asipokubali kazi hii
   • Mgogoro wa matibabu- selume analalamika jinsi viongozi katika hospitali za umma wananyakua dawa na kuacha hospitali bila dawa.                    (zozote 10x1)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Joint Pre-Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest