Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Pre Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KARATASI YA 1
(Insha) 

MAAGIZO:

 • Andika insha mbili. Swali la kwanza ni la lazima
 • Kisha chagua insha moja nyingine kutoka kwa hizo tatu zilizobakia
 • Kila insha isipungue maneno 400
 • Kila insha ina alama 20
 1. Wewe kama mwandishi wa habari wa shirika fulani la utangazaji nchini, andika mahojiano yako na waziri wa Usalama wa ndani kuhusu utovu wa usalama nchini
 2. Ungekuwa Rais wa Kenya, fafanua njia utakazotumia kustawisha uchumi uliosambaratika.
 3. Vita vya panzi furaha ya kunguru.
 4. Andika insha utakayokamilishia kwa maneno haya
  ………………..Ijapokukuwa moyoni nilimhurumia sana mwandani wangu Sudi, niliona kuwa alistahili yaliyompata. Jinsi alivyoadhibiwa, sidhani kama atarudia tendo hilo.

MAAKIZO

Mwongozo wa kusahihishia

Mwongozo rasmi wa kusahihishia insha

Tazama

Karatasi hii imedhamiria kutahini uwczo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe sahihi, wenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asili, ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo

Mtahini Iazima aisome insha yote ili aweze kuikadiria akizingatia viwango mbalimbali vilivyopendekezwa, yaani A, B, C, ama D kutegemea na mahali popote pale pafaapo, kuikaadiria insha yaa mtahiniwa.

Kiwango Cha D Maki 01-05

 1.  Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahiniwa lazima afikirie kile anachojaribu kwandika.
 2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutumia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
 3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makosa ya kila aina: kisarufi kimaendelezo mtindo mbovu n.k.

  Viwango tofauti vya D
  • D- (kiwango cha chini) Maki 01-02
   Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile. Kwa mfano, Kunakili swali au kujitungia swali tofauti na kulijibu. Hat a akitumia lugha mufti kiasi gani asitiliwe maanani.

  • D (Wastani) Maki 03
   Utiririko wa mawazo haupo na insha haieleweki, makosa ni mengi.

  • D+(Kiwango cha juu) Maki 04-05
   Ingawa insha ina lugha dhaifu ya Kiswahili na makosa mengi ya kila aina, unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha.

Kiwango cha C Maki 06-10
Kiwango hiki kina makosa yafuatayo:

 1. Mtahiniwa anaweza kuwasilisha mawazo yake lakini kwa kiwango kisichoeleweka kikamilifu.
 2. Hana uhakika wa matumizi ya lugha.
 3. Mada huwa haikukuzwa au kuendelezwa kikamilifu
 4. Mtahiniwa anaweza kupotoka hapa na pale.
 5. Kujirudiarudia ni dahiri.
 6. Mpangilio wake wa kazi ni hafifu na hauna mtiririko.
 7. Hana matumizi mazuri ya lugha.
 8. Mtahiniwa ana athari za lugha ya kwanza ambayo huonekana dhahiri, kama vile ‘papa’ badaala ya ‘baba’ ‘karamu’ badala ya ‘kalamu’ ‘tata’ badala ya ‘dada’ n.k

  Viwango vya C
  • C- (Kiwango cha chini) Maki 06-07
   • Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha mawazo yake.
   • Hana msamiati ufaao wala muundo wa sentensi ufaao.
   • Ana makosa mengi ya msamiati, hijai na matumizi mabaya ya sarufi.
  • C (Wastani) Maki 08
   • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwa njia hafifu.
   • Hufanya maakosa mengi ya sarufi.
   • Hana ubunifu wa kutosha.
   • Katika sentensi ndefu uakifishaji wake ni mbaya.
   • Ana makosa kadhaa ya hijai na msamiati.
  • C+ (kiwango cha juu) Maki 09 - 10
   • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwa njia isiyo na mvuto sana.
   • Dhana tofauti tofauti hazijitokezi kikamilifu.
   • Hutumia misemo, methali, tashbihi, tanakali za sauti n.k. kwa njia isiyofaa.
   • Mtiririko wa mawazo bado haujitokezi wazi.
   • Kuna makosa machache ya sarufi na hijai.

Kiwango cha B (maki 11-15)

 1. Katika kiwango hiki mtahiniwa anaonyesha kuimudu lugha vilivyo.
 2. Mtahiniwa hudhihirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kujieleza.
 3. Hutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi vizuri.
 4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha kama vile sentensi kuandikwa kwa njia tofauti na ikaleta maana sawa.
 5. Mada huwa imeelezwa na kuendelezwa kikamilifu.

  Viwango tofauti vya B
  • B-(kiwango cha chini) Maki 11-12
   • Mtahiniwa huwasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti.
   • Kuna utiririko mzuri wa mawazo.
   • Ana uwezo wa kutumia miundo tofauti ya sentensi.
   • Makosa machache yanaweza kuonekana hapa na pale.

  • B+(wastani) Maki 13
   • Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
   • Anawasilisha ujumbe wake wazi wazi kwa mawazo yanayodhihirika.
   • Matumizi ya lugha ya mnato huweza kudhihirika.
   • Anatumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
   • Matumizi ya tamathali za semi yanaanza kudhihirika.
   • Makosa ni machache ya hapa na pale.

  • B+ (kiwango cha juu) Maki 14-15
   • Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika.
   • Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa njia inayovutia na kwa urahisi.
   • Kuna makosa ya hapa na pale ambayo mtahiniwa hakudhamiria kuyafanya.
   • Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri.
   • Sarufi yake ni nzuri.
   • Uakifishaji wake ni mzuri.

Kiwango cha A Maki 16-20

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato. Ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka.
 2. Ana uwezo wa kutumia tamathali za lugha ili kutoa hisia zake kwa njia iliyo bora kwa urahisi.
 3. Umbuji wake hudhihirisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hali ya kumvutia msomaji wake.

  Viwango tofauti vya A
  • A- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 16 – 17
   • Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha. Ana utiririko mzuri wa mawazo kulingana na mada.
   • Huipamba lugha kwa kutumia tamathali za usemi.
   • Huzingatia matumizi mazuri ya msamiati na sarufi.
   • Makosa ya kawaida ya lugha ni machache

  • A (WASTANI) MAKI 18
   • Mawazo yanadhihirika zaidi.
   • Makosa ni machache mno.
   • Hutumia lugha ya mnato.
   • Hutumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia.
   • Sarufi yake ni nzuri.
   • Hutumia miundo tofauti ya sentensi kiufundi.
   • Hujieleza kikamilifu.

  • A+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 19-20
   • Mtahiniwa huwasilisha ujumbe kulingana na mada.
   • Hutiririsha mawazo yake vizuri zaidi.
   • Hujieleza kikamilifu bila shida.
   • Hutoa hoja zilizokomaa.
   • Makosa ni nadra.
   • Msamiati wake ni wa hali ya juu.

Makosa ya Hijai
Haya ni makosa ya maendelezo. Sahihisha huku ukionyesha yanapotokea mara ya kwanza tu.Makosa ya tahajia huwa katika:

 1. Kutenganisha maneno kama vile ‘aliye-kuwa’
 2. Kuunganisha maneno kama vile ‘kwasababu’
 3. Kukata silabi vibaya kama vile ‘ngan-o’
 4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno kama ‘mahari’ badala ya ‘mahali’
 5. Kuacha herufi katika neno kama aliekuja badala ya aliyekuja.
 6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama piya badala ya pia
 7. Kuacha alama inayotarajiwa kuwapo katika herufi.
 8. Kutoandika kistari cha kuunganisha neno ufikiapo pambizo au mwisho; au kuandika mahali si pake.
 9. Kukiandika kistari pahali pasipofaa.
 10. Kuandika maneno kwa ufupi mfano k.m. nk, v.v.

Mtindo
Mambo yatakayochunguzwa.

 1. Mpangilio wa kazi kiaya.
 2. Mtiririko wa mawazo.
 3. Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi.
 4. Namna anavyotumia methali, misemo, tamathali za usemi na mengineyo.
 5. Unadhifu wa kazi.
 6. Kuandika herufi vizuri k.m. Jj, Pp, Uu, n.k.
 7. Sura ya insha.

Msamiati
Jumla ya maneno yalivyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa.

Maudhui na msamiati
Baada ya kusoma mtungo utafikiria na kukadiria maudhui na msamiati uliomo kwa jumla.

Sarufi
Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanapotokea mara ya kwanza
Makosa ya sarufi huwa katika:

 1. Kuakifisha vibaya: mfano, vikomo, vituo, alama ya kuulizia n.k
 2. Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake
 3. Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakatii, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitenzi na majina.
 4. Kuacha au kuongeza neno katika sentensi kwa mfano kwa kwa
 5. Matumizi ya herufi kubwa.
  Tazama : matumizi ya herufi kubwa

Alama za Kutuza

= Makosa ya sarufi
- kosa la hijai
 msamiati
x msamiati mbaya
^ kuacha neno.

 1. Swali la lazima: Mahojiano.
  • Kuwe na mahojiano baina ya watu wawili.
  • Mwanafunzi ajihusishe kama mwanahabari.
  • Itifaki izingatiwe K.m. Mheshimiwa waziri n.k.
  • Pawe na msamiati unaohusiana na mada.
  • Insha ichukue muundo wa tamthilia.

   Adhabu
  • Asipokuwa na sura ya tamthilia – Ondoa alama (4 )

   Mifano ya utovu wa usalama
  • Wizi wa kimabavu.
  • Kuvamiwa na genge lililo mafichoni K.V. Mungiki, sabaot land defence (S.L.D.F) n.k.
  • Kuwepo na silaha hatari bila idhini.
  • Ulanguzi wa dawa za kulevya.
  • Migomo ya wanafunzi na wafanyakazi isababishayo uharibifu na mauji.
  • Vita katika nchi jirani k.v. Somalia na kuathiri usalama mipakani n.k.
  • Wanawake na watoto kubakwa.
  • Mauaji ya kiholela na majambazi barabarani na nyumbani.
  • Wanyama wa msituni kuvamia makazi ya watu na kuwaua k.v. Ndovu, Chui, Simba n.k.
  • Milipuko ya mabomu na kemikali nyingine kutokana na kutowajibika kwa vikosi vya usalama na ujinga wa wananchi.
  • Ajali barabarani kutokana na magari mabovu kwa sababu ya ufisadi wa polisi na ujinga wa wananchi.

 2. Maana ya Msamiati
  • Kustawisha – kuimarisha/kuinua/kuboresha/fanikisha/endeleza/fanya iwe na nguvu/madhubuti/imara
  • Uliosambaratika- ulioharibika/uko katika hali mbaya/si mzuri.

   Njia za kutumia
  • Kukomesha ufisadi
  • Ujenzi wa viwanda
  • Kuongeza nafasi za elimu
  • Kuimarisha usalama/ amani
  • Utafiti
  • Mikopo kutolewa kwa raia kwa riba ya chini
  • Kuhimiza watu kupenda na kuthamini bidhaa za humu nchini
  • Kuwajibika na kupiga vita uvivu na uzembe
  • Kuimarisha uchukuzi na mawasiliano
  • Kuleta usawa wa kisheria
  • Kuleta uhusiano mzuri kati ya Kenya na nchi zingine.

 3.  Insha ya Methali   
  1. Kueleza maana ya methali (si lazima)
  2. Sentensi ya ufafanuzi
  3. Toa kisa kinachoana na maana ya methali
  4. Toa 3.a) Kueleza maana ya methali (si lazima)
   kisa kimoja tu na kukiendeleza
  5. Sehemu mbili za methali zishughulikiwe
  6. Lugha fasaha itumike
  7. Mtiririko uwepo
  8. Kisa kionyeshe mtu wa tatu akifaidika kutokana na ugomvi wa watu wengine kwa mfano ndugu au marafiki wakigombana

 4. Andika insha utakayokamilishia maneno haya
  Ijapokukuwa moyoni nilimhurumia sana mwandani wangu Sudi, niliona kuwa alistahili yaliyompata. Jinsi alivyoadhibiwa, sidhani kama atarudia tendo hilo.
  Mwongozo
  • Mtahiniwa asimusulie kisa au aeleze kuhusu tendo baya/kosa alilofanya Sudi na adhabu kali aliyopata.
  • Adhihirishe mahali husika kama vile shule, Chuoni, Kazini, Kijijini au Mtaani walikoishi warejelewa.
  • Vile vile aonyeshe uhusiano wa karibu kati ya msimulizi na Sudi.
  • Msimulizi alifanya nini kumtahadharisha au kutaka kumwepesha mwandani wake Sudi kutoka tendo baya alilofanya?
  • Sudi alikaidi vipi ushauri wowote aliopewa?
  • Ni adhabu gani kali aliyopata-adhabu iliyomfanya mwenzake amhurumie?
  • Kisa chote kifungamane ipasavyo na mwisho uliotolewa na kiwahusishe kikamilifu msimulizi na mwenzake Sudi-mbali na wahusika wengine wanaofa.

   Tanbihi:
   Mtahiniwa asiongeze maneno baada ya mwisho wa kauli husika.

Namna Ya Kusahihisha

Alama za kutumia:

 • ∧ Neno achwa
 • = Kosa la kisarufi
 • ____ Kosa la hijai
 • ✓ Msamiati mwafaka
 • X Msamiati pungufu

Viwango vya Kutahini:

 • A na B
  • Makosa nadra / machache kabisa.
  • Mtahiniwa ameelewa swali na kuipamba lugha
 • C na D+ - Makosa yapo lakini anajaribu kujieleza.
  • Kazi ina mfululizo wastani.
 • D na D-
  • Mtahiniwa amepotoka na haeleweki kamwe.
  • Zingatia urefu,sarufi, msamiati na uelewa wa swali. 

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Pre Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest