Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Pavement Pre-Mock Exams 2021/2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote
  1. UFAHAMU: (alama 15)
    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali

    Mageuzi yanayotarajiwa katika idara ya polisi nchini yameanza kubisha hodi baada ya kuzinduliwa kwa mtaala mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi.

    Mtaala huo uliozinduliwa rasmi na Waziri wa Usalama wa ndani Prof. George Saitoti Jumatatu iliyopita, unalenga kuimarisha utendakazi katika kikosi ambacho kwa muda mrefu kimelaumiwa kwa kukolewa ufisadi na uvunjaji wa haki za kimsingi.

    Akihutubu katika hafla ya kuzindua mtaala huo iliyofanyika katika makao makuu ya shirika la ndege nchini mtaani Embakasi, Nairobi, Jumatatu iliyopita, Waziri Saitoti alisema, kuzinduliwa kwa mtaala huo kuliashiria mwanzo wa mageuzi makubwa yanayonuiwa kukipatia kikosi hicho sura mpya.

    “Nyakati zimebadilika na tutawapa maafisa wa polisi mafunzo mapya. Tunataka kuunda kikosi imara chenye nidhamu na kinachoheshimu haki za kibindamu. Tunataka kuwa na kikosi kinachoakisi sura ya karne hii na kinachoafikia hadhi ya kimataifa,” Waziri Saitoti alisema.

    Mtaala huo mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi ni matunda ya jopo lililoteuliwa na Rais mwaka wa 2003 kutathmini mageuzi katika kikosi hicho. Uliandaliwa na taasisi ya elimu nchini ikishirikiana na wanafunzi kutoka chuo cha mafunzo ya polisi cha Kiganjo kwa usaidizi wa wataalamu wa masuala ya usalama kutoka Uswizi.

    Chini ya mtaala huo, maafisa wa polisi watapokea mafunzo kwa kipindi cha kati ya miezi 15 na 21 kinyume cha awali ilipowachukua miezi 9 tu kukamilisha mafunzo.

    Aidha, alama za kujiunga na kikosi hicho zimeongezwa. Katika mtaala huo, wanaonuia kujiunga na idara ya polisi wa kawaida, kitengo cha G.S.U au polisi wa utawala ni lazima wawe wamepata alama ya C katika mtihani wa K.C.S.E na itawachukua miezi 15 kukamilisha mafunzo ikiwa ni pamoja na miezi 3 ya kujifahamisha na huduma ya kikosi.

    Hii ni tofauti na awali ambapo alama ya kujiunga na kikosi cha polisi ilikuwa ni D katika mtihani wa KCSE. Mtaala mpya unasema ni sharti asilimia 10 ya makurutu wawe na digrii kutoka chuo kikuu na watapokea mafunzo kwa miezi na kuhitimu cheo cha Naibu wa Inspekta wa Polisi.

    Kuanzia sasa, ni sharti usawa wa kijinsia uzingatiwe kikamilifu katika uajiri wa maafisa wa polisi. Wachanganuzi wa masuala ya usalama wanasema ukizingatiwa ipasavyo, mtaala huo utasaidia kuunda msingi dhabiti wa kikosi imara ambacho Wakenya wamekuwa wakihitaji.

    Maswali
    1. Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (alama 1)
    2. Mtaala mpya unalenga nini? (alama 4)
    3. Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (alama 2)
    4. Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (alama 3)
    5. Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (alama 2)
    6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (alama 3)
      1. Kubisha hodi
      2. Kukolewa
      3. Makurutu
  2. UFUPISHO (alama 15)
    Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata

    Mwezi jana serikali ya kitaifa na zile za kaunti ziliwasilisha makadirio yao ya bajeti, miezi miwili kabla ya mwaka wa kifedha kuisha kama zinavyohitajika na katiba. Serikali hizo zilieleza jinsi zinavyonuia kutumia mabilioni ya pesa kufadhili shughuli za mwaka ujao wa kifedha wa 2013/2014.

    Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta ilisema itatumia shilingi 1.6 trilioni kufadhili maendeleo na shughuli za sekta na idara zake tofauti. Makadirio haya yaliwasilishwa na kiongozi wa walio wengi bungeni, Bw. Aden Duale. Hata hivyo yalikosa kueleza jambo moja muhimu – jinsi kitita hicho kitakavyopatikana. Nasema hivi kwa sababu kuna habari ambazo zimenipa tumbojoto na wasiwasi mkubwa. Imebainika kuwa kufikia mwishoni mwa Machi mwaka huu, Kenya ilikuwa inadaiwa shilingi 1.8 trilioni na wafadhili wa humu nchini wa kigeni. Kama habari hizi hazijakushtua sitakulaumu kwa sababu huenda ukuwa hujui ukubwa wa kiasi cha fedha. Ili uweze kuelewa, nitazigawanya fedha hizi miongoni mwa Wakenya milioni 40 ili tujue kila mkenya anadaiwa kiasi gani. Kila Mkenya nchini, wakiwemo watoto na wazee wakongwe, anadaiwa shilingi 45,000! Hivyo basi ili deni hili liweze kulipwa, kila Mkenya atalazimika kutoa kiasi hicho cha fedha.

    Ni deni ambalo Rais Uhuru Kenyatta alirithi kitoka kwa mtangulizi wake, Rais Mwai Kibaki ambaye utawala wake ulivunja rekodi ya kukopa. Wahenga hawakukosea dawa ya deni ni kulipa. Deni hili linapaswa kimkosesha usingizi Rais Kenyatta ambaye anapaswa kutafuta njia za kulilipa bila kuathiri uchumi, maendeleo na utekelezaji wa ahadi nyingi alizowapatia Wakenya wakati wa kampeni.

    Hili halitafanyika kama Serikali itatenga fedha nyingi kuwalipa maafisa wake mishahara na marupurupu minono pamoja na kuwapa mabilioni ya pesa kununulia magari ya kifahari. Pengine Rais hajafahamiswa kuwa mwaka ujao wa kifedha serikali itajipata pabaya kwani Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA), haitaweza kukusanya kiwango kilichowekwa na serikali baada ya shughuli ya ukusanyaji ushuru kutatizwa na hofu iliyotanda wakati wa uchaguzi mkuu.

    KRA ilikuwa imekusanya shilingi 560 bilioni kufikia mwishoni mwa Machi ilhali ilikuwa imeagizwa kukusanya. Baada yake zimeomba serikali kuu ujaze pengo hilo au zipewe idhini ya kukopa.

    Rais Kenyatta hana budi kuchukua hatua za dharura kuhakikisha kuwa wakenya hawataendelea kuandamwa na madeni maishani mwao.
    (imenukuliwa kutoka Taifa Leo – Mei 9, 2013)
    1. Kwa maneno yasiyozidi 70, fupishsa aya za kwanza nne. (alama 9)
      Nakala ya matayarisho
      Nakala safi
    2. Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake. (maneno 40-50) (alama6)
      Nakala ya matayarisho
      Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Toa maelezo ya jinsi ambavyo hewa huzuiliwa wakati wa kutamka sauti inzi (alama 2)
      1. /P/
      2. /ch/
      3. /m/
      4. /r/
    2. Bainisha mofimu katika neno : Tuliyemcheza. (alama 3)
    3. Tunga sentensi moja yenye kitenzi kishirikishi kikamilifu na vitenzi sambamba (alama 3)
    4. Tumia neno msiri kama kielezi cha mfanano. (alama 1)
    5. Onyesha namna tatu za kutumia “na” katika sentensi moja, kisha neleze matumizi husika. (alama 4)
    6. Ziweke nomino hizi katika ngeli zake .
      1. Kiwavi-
      2. Vita-
    7. Tambua virai vilivyopigiwa mstari ni vya aina gani na uonyeshe miundo yake (alama 4)
      1. Ndege iliyotengenezwa jana itapelekwa Ulaya.
      2. Wenzetu walikuwa wakijinaki kabla ya dimba
    8. Eleza maana ya sentensi hizi kwa kuzingatia sehemu zilizopigiwa mstari (alama 2)
      1. Mgonjwa alinywesheka uji-
      2. Mvua ilimnyia jana-
    9. Tambua shamirisho na chagizo katika sentensi hii (alama 4)
      Juma alinjengea nyanya nyumba kwa mawe nzuri sana.
    10. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo bila kuambisha na ku (alama 2)
      1. Shika
      2. Shona
    11. Tumia njia ya matawi kuchangana sentensi ifuatayo (alama 4)
      Alipotuona alituangalia lakini sisi tulimuona
    12. Kamilisha kwa viingizi mwafaka
      1. Gari la Mwangeka lilisukumwa ------------------------ (alama.1)
      2. Jiwe lilianguka majini--------------------------- (alama.1)
    13. Tumia vitate vya baba, sara na toa katika sentensi tatu tofauti (alama 3)
    14. Yakinisha:- usipocheza vizuri hautachaguliwa (alama 2)
    15. Onyesha jinsi ya kutumia nukta pacha katika sentenzi (alama 1)
    16. Andika sentensi ifuatazo kwa lugha ya tafsida (alama 1)
      Mwanafunzi ameenda kwenye choo.
    17. Amrisha katika nafsi ya tatu wingi   (alama 1)
      Cheza   
  4. ISIMU JAMII (alama 10)
    Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.

    “Naona “Horsepower” mwenyewe ndiye atakayepiga, atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa……”
    1. Tambua sajili inayorejelewa (alama 2)
    2. Tambua sifa zinazobainisha sajili rejelewa (alama 8)


MARKING SCHEME

  1. UFAHAMU
    1. Ni dalili ipi inayoonyesha mwanzo wa mageuzi? (alama 1)
      • Kuzinduliwa kwa mtaala mpya wa kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi 1x1=1
    2. Mtaala mpya unalenga nini? (al.4)
      • Kuimarisha utendakazi katika kikosi ambacho kwa muda mrefu kimelaumiwa kwa kulowa ufisadi na uvunjaji wa haki za kimsingi
      • Unaashiria mwanzo wa mageuzi makubwa yanayonuiwa kukipatia kikosi hicho sura mpya
      • Kuwapa maafisa wa polisi mafunzo mapya
      • Kuunda kikosi imara chenye nidhamu na kinachoheshimu haki za kibinadamu 4x1 = 4
    3. Eleza lawama zinazoelekezewa kikosi cha polisi (alama 2)
      • Ukosefu wa nidhamu
      • Kutoheshimu haki za binadamu/kimsingi
      • Kukolea kwa ufisadi
    4. Kwa mujibu wa taarifa eleza mageuzi matatu yaliyofanywa katika kikosi cha polisi (al.3)
      • Maafisa wa polisi kupokea mafunzo kwa kipindi cha kati ya miezi 15 na 21 kinyume na awali ilipochukua miezi 9
      • Alama za kujiunga na kikosi hicho zimeongezewa kutoka D hadi C
      • Asilimia 10 ya makurutu wawe na digrii kutoka chuo kikuu ili kuhitimu naibu wa inspekta wa polisi
      • Usawa wa jinsia kuzingatiwa katika uajiri wa maafisa wa polisi 3x1 = 3
    5. Taja makundi mawili yaliyohusika katika kuandaa mtalaa mpya (alama2)
      • Jopo iliyoteuliwa na Rais mwaka wa 2003
      • Taasisi ya elimu
      • Wakufunzi kutokea chuo cha mafunzo cha Kiganjo
      • Wataalam wa maswala ya usalama kutoka Uswizi 2x1 =2
    6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika kifungu (alama 3)
      1. Kubisha hodi
        • Kuingia/kutukia
      2. Kukolewa
        • Kuendeleza/kushamirisha
      3. Makurutu
        • Wanafunzi wanaojiunga na kikosi cha polisi
  2. UFUPISHO
    1. Kwa maneno yasiyozidi 70, fupisha aya za kwanza nne. (alama 9)
      • Serikali kuwasilisha bajeti
      • Kueleza jinsi mabilioni yalivyotumiwa
      • Serikali ya Kenyatta kusema itatumia shilingi 1.6 trilioni kwa maendeleo.
      • Makadirio kuwasilishwa na kiongozi wa walio wengi bungeni
      • Kukosa kueleza jinsi ya kupata kitifa hicho
      • Habari hizi kunipa wasiwasi
      • Kenya kudaiwa shilingi 1.8 trilioni na wafadhili
      • Kutolaumu wale wasiolewa ukubwa wa deni hili
      • Kugawanya deni hili kwa Wakenya wote
      • Kila Mkenya kadaiwa shilingi 45,000
      • Kenyatta kurithi deni kutoka kwa Kibaki
      • Deni kumkosesha usingizi Rais
      • Kutafuta njia ya kulipa bila kuathiri uchumi
        9x1 = 9 alama
        Mtiririko alama 1
    2. Kwa nini serikali haitaweza kulipa madeni yake. (maneno 40-50) (al.6)
      • Serikali kutenga fedha nyingi kuwalipa wafanyikazi
      • KRA kutokusanya kiwango kinachohitajika
      • Ukusanyaji wa ushuru kutatizwa na hofu wakati wa uchaguzi
      • Serikali za kaunti kupendekeza kutumia mabilioni ambayo hawana
        4x1 = 4
        Mtiririko alama 1
  3. MATUMIZI YA LUGHA
    1. Toa maelezo ya jinsi ambavyo hewa huzuiliwa wakati wa kutamka sauti inzi (alama2)
      1. /P/ - hewa huzuiliwa kisha kuachiliwa ghafla kwa nguvu.
      2. /ch/ - hewa huzuiwa kisha nafasi ndogo kuachwa ili ipite ikiwa na mkwanzo.
      3. /m/ - hewa hupita kinywani na puani.
      4. /r/ - ulimi hugotagota ufizini (2x4)
    2. Bainisha mofimu katika neno : Tuliyemcheza. (alama 3)
      TU   -      LI       -    YE         -       M         - CHEZ  -       A
        ↓            ↓               ↓                   ↓               ↓               ↓
      Nafsi    Wakati     Kirejeshi     Mtendwa      Mzizi      Kimalizio
      Ngeli                                                                            tenda

      (1x3)
    3. Tunga sentensi moja yenye kitenzi kishirikishi kikamilifu na vitenzi sambamba (al.3)
      • Amekuwa uwajani alimochezea akisoma
      • Hajawa ibadani na tumeimba tukamsifu Mungu (1x3)
    4. Tumia neno msiri kama kielezi cha mfanano. (alama1)
      • Hufanya kazi yake kisiri(1x1)
    5. Onyesha namna tatu za kutumia “na” katika sentensi moja, kisha neleze matumizi husika. (alama4)
      • Baba na mama wanapigana kwani ana tabia ya kulewa
      • Baba na mama-kiunganishi.
      • Ana tabia-umilikaji.
      • Wanapigana-na-wakati uliopo
                             na-kutendana.
        (2x2)
    6. Ziweke nomino hizi katika ngeli zake .
      1. Kiwavi - A-WA
      2. VITA - VI-VI (2x1)
    7. Tambua virai vilivyopigiwa mstari ni vya aina gani na uonyeshe miundo yake (alama4)
      1. Ndege iliyotengenezwa jana itapelekwa Ulaya.
        • Kirai nomino- nomino+ kishazi tengemezi/kivumishi kirejeshi.
      2. Wenzetu walikuwa wakijinaki kabla ya dimba
        • Kirai kitenzi-kitenzi kisaidizi,kitenzi kikuu, kihusi shina nomino (2x2)
    8. Eleza maana ya sentensi hizi kwa kuzingatia sehemu zilizopigiwa mstari (alama2)
      1. Mgonjwa alinywesheka uji-tendesheka.
      2. Mvua ilimnyia jana-tendea (2x1)
    9. Tambua shanurisho na chagizo katika sentensi hii (alama4)
      Juma alinjengea nyanya nyumba kwa mawe nzuri sana.
      • Nyanya-kitondo
      • Nyumba kipozi
      • Mawe- kitumizi/ala
      • Vizuri sana –changizo (2x2)
    10. Unda nomino kutokana na vitenzi vifuatavyo bila kuambisha na ku (alama2)
      1. Shika  - Mashiko / shikio
      2. Shona - mshono/ushonaji (2x1)
    11. Tumia njia ya matawi kuchangana sentensi ifuatayo (alama4)
      Alipotuona alituangalia lakini sisi tulimuona
      kISWAHILI PP1 Ans3k PVPM 2122
    12. Kamilisha kwa viingizi mwafaka
      1. Gari la Mwangeka lilisukumwa ------------------------ (alama1)
        • Ngoko ngoko
      2. Jiwe lilianguka majini--------------------------- (alama1)
        • Chupwi
    13. Tumia vitate vya baba, sara na toa katika sentensi tatu tofauti (alama3)
      • Papa alivuliwa jana
      • Zara za uvuvi
      • Gari lilikuwa na doa
    14. Yakinisha:- usipocheza vizuri hautachaguliwa (alama2)
      • Ukicheza vizuri utachaguliwa (2x1)
    15. Onyesha jinsi ya kutumia nukta pacha katika sentenzi (alama1)
      • Kuh: Aletewa mgeni
      • Alifika saa 10:10 asubuhi.
    16. Andika sentensi zifuatazo kwa lugha ya tafsida (alama1)
      Mwanafunzi ameenda kwenye choo.
      • Msalani.
    17. Amrisha katika nafsi ya tatu wingi
      • Cheza-chezeni (alama1)
  4. ISIMU JAMII (alama 10)
    Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali.
    “Naona “Horsepower” mwenyewe ndiye atakayepiga, atakayecheza foul hiyo. Wachezaji wa……”
    1. Tambua sajili inayorejelewa (alama2)
      • Sajili ya michezo/kandanda/kambumbu
    2. Tambua sifa zinazobainisha sajili yenyewe (al.8)
      • Lugha changamfu/cheshi/porojo
      • Kupiga chuku/kutiwa chumvi
      • Lugha shawishi
      • Utohozi/mf. Foul, Horse power
      • Lugha mseto/kuchanganya ndimi/msimbo
      • Matumizi ya tamathali za usemi
      • Lugha nyepesi inayoeleweka
      • Kuhamisha ndimi
      • Huchanganywa na nyimbo
      • Matumizi ya msamiati teule wa kambukambu
      • Kauli/sentensi fupi fupi
      • Sentensi zisizokamilika
      • Uradidi/takriri/urudiaji
      • Matumizi ya lakabu
      • Sifa kemkem kwa wachezaji Zozote nane     1x8=8
        Adhabu
        Makosa ya sarufi ya kwanza manne yaondolewe alama 2 4x1/2 =2
        Makosa ya hijai hadi manne 4x1/2 =2
        Jumla alama 4
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Pavement Pre-Mock Exams 2021/2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest