Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Asumbi Girls Highschool Pre-Mock Exams May-June 2022

Share via Whatsapp
MAAGIZO: 
 • Andika insha mbili.
 • insha ya kwanza ni ya lazima
 • Chagua insha ya pili kutoka tatu zilizobakia.
 • Kila insha isipungue maneno 400.
 • Kila insha ina alama 20.
 • Kila insha iandikwe kwa lugha ya Kiswahili. 


MASWALI

 1. Lazima
  Wewe ni waziri wa usafiri nchini. Kumekuwepo na ajali nyingi za barabarani hivyo basi  umealikwa na kituo cha  runinga cha Mzalendo Kufafanua sababu za ajali hizi. Andika mahojiano yenu.
 2. Ujenzi wa reli za kisasa nchini una manufaa mengi kuliko madhara. Jadili. 
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo:
  Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
 4. Andika kisa kinachomalizika kwa maneno yafuatayo:
   Baba niliyemfahamu kwa picha pekee, hatimaye aliwasili nyumbani baada ya miaka ishirini. Nilimkumbatia huku machozi yakitudondoka sote.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Lazima
  • Wewe ni waziri wa usafiri nchini. Kumekuwepo na ajali nyingi za barabarani hivyo basi  umealikwa na kituo cha  runinga cha Mzalendo Kufafanua sababu za ajali hizi. Andika mahojiano yenu.
   • Hii ni insha ya kiuamilifu
   • Sura ya mahojiano izingatiwe.
  • Maudhui yagusie yafuatayo:
   • Uwepo wa magari mabovu 
   • Madereva kutokuwa waangalifu
   • Barabara mbovu
   • Madereva walevi barabarani
   • Undeshaji kasi wa magari
   • Hali mbaya ya hewa mfano uwepo wa ukungu
   • Askari wa trafiki kuchukua hongo ili wawaruhusu madereva kutozingatia sheria
  • Madereva kuendesha magari wakiwa wachoka
   • Mwanafunzi ashughulikie maudhui kikamilifu.
 2.                  
  • Ujenzi wa reli za kisasa nchini una manufaa mengi kuliko madhara. Jadili.
   • Hii ni insha ya mjadala. Swali linamlazimu mtahiniwa ashughulikie manufaa na hasara/madhara ya reli za kisasa. 
   • Mtahiniwa anaweza kuunga mkono au kupinga. 
   • Kuunga mkono: Mtahiniwa anayeunga mkono aeleze hoja nyingi za manufaa/faida na hoja chache za madhara/hasara. 
   • Kupiga:Mtahiniwa anayepinga aeleze hoja nyingi za madhara/hasara na hoja chache za manufaa/faida.
   • Mtahiniwa ashughulikie upande mmoja kwanza kisha ashughulikie upande wa pili.
  • Manufaa/faida ya reli za kisasa.
   • Kubuni nafasi za kazi kwa Wakenya
   • Wenye mashamba watalipwa kiasi kikubwa cha pesa kama fidia. 
   • Usafiri wa watu na usafirishaji wa bidhaa kuimarika. 
   • Kuimarika kwa viwanda kutokana na usafirishaji wa malighafi hadi viwandani na bidhaa za viwanda hadi sokoni. 
   • Barabara za lami zitadumu kwa muda mrefu kwani bidhaa nzito zitasafirishwa kwa reli hii badala ya barabara. 
   • Kufunguka kwa maeneo ya mashinani
   • Kuimarika kwa shughuli za uchimbaji madini. 
   • Kuimarika kwa teknolojia nchini.
  • Madhara/hasara za reli za kisasa.
   • Watu kupoteza mashamba
   • Uchafuzi wa mazingira na kuingiliwa kwa mbuga za wanyama. 
   • Serikali kutumia kiasi kikubwa cha pesa. 
   • Wanaoshiriki biashara ya kusafirisha mizigo kwa malori kupoteza kazi na biashara zao kuanguka. 
   • Mateknia kutoka mataifa ya nje kuleta tamaduni na mitindo ya kigeni nchini. 
   • Kuongeza kiasi cha deni la taifa
   • Ni fursa ya viongozi kushiriki ufisadi.
 3. Tunga kisa kitakacho dhihirisha maana ya methali ifuatayo:
  • Usitukane wakunga na uzazi ungalipo.
   • Hii ni insha ya methali. Mtahiniwa  aandike maana na matumizi ya methali hii. 
   • Mtahiniwa  anaweza  kueleza maana ya methali au asieleze. 
   • Maana ya methali hii ni kuwa: Usidharau mtu au kitu kilicho kufaa awali kwani huenda ukahitaji huduma au msaada wake baadaye.
  • Viza vinaweza kudhihirisha hali zifuatazo:
   1. Mhusika ambaye ameishi mahali kwa muda kisha anapoondoka/anapofanikiwa anapadharau. 
   2. Mwajiriwa ambaye amefanya kazi katika kampuni fulani kwa muda, kisha anapopataka mkwingine anajiuzulu kwa dharau. Baadaye patokee jambo linalomhitaji kupata barua kutoka kwa wakuu wa kampuni hiyo, ahasirike kwa kuona aibu kuomba barua.
   3. Baada ya kukamilisha masomo, wanafunzi awadharau walimu, wafanya kazi wa shule au wanafunzi wenzake kisha aaibike anaporudi kuchukua matokeo yake.
  • Taribihi: Hali ya  kudharau na kuathirikaidhihirike waziwazi.
 4. Andika kisa kinacho malizika kwa maneno ya fuatayo:
  … Baba niliyemfahamu kwa picha pekee, hatimaye aliwasili nyumbani baada ya miaka ishirini. Nilimkumbatia huku machozi yakitudondoka sote.
  • Hii ni insha ya mdokezo. Kisa cha mtahiniwa kiafikiane na ujumbe wa mdokezo. 
  • Kisa kionyeshe hali ambapo baba yake msimulizi ameishi mbali naye na sababu za hali hiyo. 
  • Aeleze ilikuwaje baba akarejea nyumbani.
  • Mtahiniwa anaweza kueleza maisha yake yalivyokuwa wakati babake alipokuwa mbali naye. 
  • Aeleze hali iliyopelekea  baba kurudi nyumbani.

Taribihi: Hali ya kuwa mbali isitazamwe tu keneo/kijiografia. 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Asumbi Girls Highschool Pre-Mock Exams May-June 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest