Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Momaliche Joint Pre Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)
    Soma kifungu kifuatacho halafu ujibu maswali yanayofuata.
    Ikolojia ni elimu ya kisayansi inayohusu uhusiano wa kimazingira kati ya vitu vyenye uhai (mimea na wanyama) na visivyo kuwa na uhai(hali ya hewa udongo) Elimu ya ikolojia ipo katika mfumo wa elimu ya mazingira). Mfumo huu umegawanyika katika sehemu mbili: mfumo wa mazingira ya nchi kavu, na mfumo wa mazingira ya majini (bahari, maziwa, mito na madibwi).
    Viumbe wamejirekebisha kulingana na mazingira yao. Kwa mfano samaki wanamata mvua yenye uwezo na kusharabu hewa ndani ya maji. Ng’ombe wana mapafu ya kuvuta hewa katika nchi kavu. Sehemu za mvua ya kawaida zina majani manene ili yaweze kuhifadhi maji nyakati za shida. Mimea, wanyama, odongo na viathiri vingine vya hali ya hewa vinahusiana sana kimazingira. Mimea huota kutegemea hali ya nchi, umbo au sura ya ardhi na aina ya udongo.
    Hali ya nchini wastani na hali ya joto ridi, wastani wa mvua, unyevunyevu hewani, upepo, msukumo na mwanga wa muda wa miaka thelathini. Dunia imegawanyika katika kanda mbalimbali. Kila kanda ina mimea na wanyamawa aina yake kutegemea hali ya nchi. Ukanda wa istiwaiu na joto, mvua na unyevunyevu mwingi. Miti ya ukanda huu hufanya misitu minene, yenye miti mirefu. Miti hii ni mirefu kwa sababu ya msongamano unaofanya miti igombanie mwanga wa jua kwa kurefuka. Katika misitu hii, ipo mimea ya kangaga inayotambaa na kukwea miti mingine. Katika ukandawa Savanna, hali ya joto na mvua si kubwa kama katika ukanda wa istiwai. Kwa sababu hii, sehemu nyingi ni vichaka na nyika zenye uwezo wa kuota nyasi zisizohitaji mvua.
    Upepo una faida na hasara katika mazingira. Upepo husaidia kusukuma mawingu yaletayo mvua. Upepo unapozidi hudhuru mimea na wanyama kwasababu hukausha mali ardhini, huvunja na kuharibu mimea, huleta vifo kwa wanyama na pengine kuharibu mazingira ya watu. Mimea katika mazingira hutegemea sana nuru ya jua ili kutengeneza chakula chake kiasi cha mwanga upatikanao mahali Fulani huadhiri mimea na wanyama wapatikanao katika mazingira yale.
    Maswali
    1. Pendekeza anwani kwa taarifa uliyosoma. (alama 1)
    2. Eleza maana ya ikolojia. (alama 2)
    3. Kwa nini wanyama huwa na sifa mbalimbali za kimaumbile? (alama 2)
    4. Ni kwa vipi ukanda wa istiwai unatofautiana na ukanda wa Savanna? (alama 3)
    5. Ni kwa namna gani upepo unaweza kuwa na athari mbaya kwa mazingira? (alama 4)
    6. Eleza maana ya msamiati huu kama ulivyo tumika katika kifungu(alama 3)
      1. Mata mvua
      2. Kusharabu hewa
      3. Istiwai
  2. Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali (alama 15)
    Chondepulika nikueleze ni juu ya maendeleo ya visiwa vya kwetu. Katika kisiwa cha migingo watu wanaishi pamoja katika vijiji. Walianzisha vijiji hivi kwa ajili ya kuondoa dhuluma na dhikiya mambo mengi ya lazima kwa maisha bora na ustawi. Wanaishi kwa jasho lao. Ushirikiano ndio ngao ya msingi wa maendeleo. Watu wote wa kila janibu na katika vitongoji vya kisiwa kizimani kama ndugu. Wote wanaishi kwa umoja. Ubaguzi umekwisha zikwa katika kaburi la sahau. Wote wanapenda kazi zao za uvuvi. Hakuna anayepigazo hali. Ni aibu kwa kila mwanakijiji kulaza damu. Shibe ndiyongaoyao. Kila mmoja anapigana kwa jino na ukucha kujaribu kuondoa hali ya unyonge, ufukara, ukosefu na hasa kuleta haraka iwezekanavyo hali ya maendeleo na ustawi kwa ashabu na kisiwa cha migingo.
    Viongozi na hata wazee wa vijiji hawaingilii sana vijiji hivi hata ikiwa kuna tatizo kubwa. Hata hivyo viongozi wa serikali wanaangalia kama watu wote wanapata chakula bora na hasa watoto, kunywa maji safi ili kuepukana na magonjwa, kutoa huduma kwa akina mama, watoto na kuchukua hatua kadhaa za kuendeleza afya ya watu kwa jumla. Watu wa msalaba mwekundu husaidia mambo kadha na mabwana afya hushughulikia kuzuia magonjwa ya kuambukiza kwa njia ya kuchanja kama vile ndui, kipindipindu na kadhalika.
    Watawala wa migingo wanatilia mkazo kwa watu wazima kuimarisha uvuvi ambao ndio utiwa mgongo wa kisiwa hiki ili kuinua hali ya uvivu, uchumi na maendeleo ya kisiwa kwa jumla.
    Maswali
    1. Fupisha aya ya kwanza kwa maneno 50. (alama 6, 1 utiririko)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Bila kupoteza maana asilia, andika mambo yote muhimu kutoka aya mbiliza mwisho.(maneno 60) (alama 7, utiririko 1)
      Matayarisho
      Jibu
  3. MATUMIZI YA LUGHA. (ALAMA 40)
    1. Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuiliwa taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja. (alama 2)
    2. Fafanua maana ya shadda. (alama 2)
    3. Bainisha shamirisho kipozina kitondo katika sentesi hii
      Babu ametengeneze wakitikizuri na mjukuu wake. (alama 2)
    4. Fafanua tofauti iliyopo kati ya kishazi na kirai. (alama 2)
    5. Huku ukitolea mifano mwafaka, fafanua majukumu yoyote manne ya viambishi awali. (alama 2)
    6. Unda nomino dhahania kutokana na kitenzi-abudu. (alama 1)
    7. Kanusha sentensi ifuatayo. (alama 2)
      Ukion avyaelea vimeundwa
    8. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizo kwenye mabano. (alama 2)
      1. Cha (kutendwa)
      2. Kosa (kutendesha)
    9. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi –ji- (alama 2)
    10. Tambua miundo yoyote mitatu ya nomino za ngeli ya LI-YA. (alama 3)
    11. Tunga sentensi ukitumia(alama 2)
      1. Kihusishi cha ulinganisho
      2. Kihisishi cha hasira
    12. Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya matawi. (alama 4)
      Alifikakisha akaondoka
    13. Andika sentensi hii katika hali ya kuamrisha wingi. (alama 2)
      Ondoka hapa.
    14. Andika sentensi hii kwa hali ya udogo wingi. (alama 2)
      Mtoto amefunga mlango wa nyumba yao.
    15. Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu(alama 2)
      Tamimaha kutuzwa siku hiyo.
    16. Andika kinyume. (alama 2)
      Sufuria iliyo injikwa mekoni ni chafu.
    17. Andika katika usemi halisi. (alama 3)
      Mwalimualinifokeanitokehapomaramoja.
    18. Kaaina maana ya keti. Andika maana zingine mbili. (alama 2)
  4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Nini maana ya dhana ya usanifishaji wa lugha? (alama 2)
    2. Nchi za Afrika mashariki ziliunda kamati ya lugha ilikusafirisha na kukuza Kiswahili, eleza malengo manne makuu na mafanikio yake katika usanifishaji. (alama 8)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. UFAHAMU
    1. Ikolojia
    2. Elimu ya kisayansi inayohusu uhusiano wa kimazingira kati ya vitu vyenye uhai na visivyo kuwa na uhai.
    3. Hujirekebisha kulingana na mazingira wanamoishi
    4.      
      • Ukanda wa istiwai una joto, mvua na unyevunyevu.
      • Hufanya misitu minene yenye miti mirefu.
      • Kuna mimea yakayangainayo tambaa na kukwea miti  mingine. Ukandawa savanna una joto na mvua kiasi. Sehemu nyingi ni vichaka na nyasi zisizo hitaji mvua.
    5. Upepo una faida – husukuma mawingu yanayoleta mvua.
      Hasara – upepo ukizidihudhuru mimea na wanyama.
    6.      
      1. Viungo vya kupumua.
      2. Kuvutahewa.
      3. Ukanda ulio katika sehemu ya kati ya dunia.
  2.    
    1.    
      1. Katika kisiwa cha migingo watu wanaishi pamoja katika vijiji.
      2. walivianzisha ili kuondoa dhuluma na dhiki.
      3. Wanaishi kwa jasho lao.
      4. Ushirikiano ndio msingi wa maendeleo/wote wanajitahidi kuleta maendeleo.
      5. Watu wote ni kama ndugu/wanaishi kwa umoja/hakuna ubaguzi.
      6. Wanapenda kazi zao za kilimo/hakuna anayepiga zohali/niaibu kulazad amu. (2x1=2)
    2.    
      1. viongozi na hata wazee wa vijiji hawaingilii sana vijiji hivi.
      2. huhakikisha kuwepo kwa chakula bora.
      3. Huhakikisha kuwepo kwa maji safi.
      4. huendeleza afya ya watu.
      5. Hutoa huduma kwa akina mama.
      6. Msalaba mwekundu na Mabwana Afya husaidia.
      7. Watawala wanatilia kwa watu wazima kuimarisha uvuvi. (7x1=7)
  3.      
    1. Kipasuo - /p/, /b/, /t/, /d/, /j/, /k/, /g/
      Kipasuo kwamizo - /ch/
      Kitambaz - /l/
      Kimandende - /r/Taja ½ Mfano ½
    2. Ni mkazo ambao huwekwa kwenye silabi Fulani ya neno hilo ili iweze kuleta maana yake halisi.
    3. Babu ametengeneze wakiti kizuri na mjukuu wake.
      Babu – kitondo
      Kiti – kipozi (2x1=2)
    4.    
      • Kishazi ni sehemu ya sentensi iliyonakiarifana hubeba maana kamili au isiyo kamilifu.
      • Kiraini maneno aghalabu mawili au Zaidi yanayowekwa pamojana hutekeleza jukumu sawa. (hufanyakazipamoja) kwenye sentensi.
    5. Huku ukitolea mifano mwafaka, fafanua majukumu yoyote manne ya viambishiawali. (alama 2)
      Nafsi
      Wakati/njeo/hali
      Urejeshi
      Ukanushaji
      Ngeli
      Mtendwa (4 x ½ = 2)
    6. ibada
    7. Ukiona vyaelea vimeundwa
      Usipoona vyaelea havijaundwa.
    8. Nyambua vitenzi vifuatavyo katikaka uli zilizo kwenye mabano. (alama 2)
      1. Cha (kutendwa)
        chiwa
      2. Kosa (kutendesha)
        kosesha
    9. Tunga sentensi moja kuonyesha matumizi mawili ya kiambishi –ji- (1x2= 2)
      Kiambishi cha ngeli/jina
      Kiambishi kirejeshi/nafsi/mtendwa
      Kuunda nomino zenye maana ya kazi yamazoea mnenaji.
    10. JI/MA
      JI/ME
      ϴ/ME
      1. Kihusishi cha ulinganisho
        Kuliko, zaidi
      2. Kihisishi cha hasira
        Kefule!, Ebo!, Po!, akh!, aka!
    11. Alifikakishaakaondoka
    12. Ondoka hapa.
      Ondokeni hapa!
    13. Mtoto amefunga mlango wa nyumba yao.
      Vijitoto vimefunga vilango vya vijumba vyao.
    14. Tamima hakutuzwa siku hiyo.
      Tamima atakuwa ametuzwa siku hiyo.
    15. Sufuria iliyoinjikwa mekoni ni chafu.
      Sufuria iliyoepuliwa mekoni ni safi.
    16. Mwalimu alinifoke anitoke hapo mara moja.
      “Toka hapa mara moja!” Mwalimu alinifokea.
    17.      
      • mnyama mdogo wa majini.
      • Kipande cha ukuni kilichochomwa.
      • Hutumika kuonyesha muda mrefu.
      • Pendeza.
  4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Ni uamuzi wakuchagua lugha moja au moja wapoyala haja za lugha ili kuifanyia marekebisho yakimatamshi, kisarufi, kimaana na kimaandishi ili itumike katika shughuli rasmi.
    2.  
      1. Malengo
        • Kusanifisha maandishi ni kuhakikisha mtindo mmoja unazingatiwa.
        • Kuchapisha vitabu.
        • Kuwahimiza na kuwasaidia wandishiwa Kiswahili.
        • Kuidhinisha vitabu vya kiada na ziada vinavyohitaji kakufundisha shuleni.
        • Kuwapasha waandishi habari zozote zile kuhusu njia tofauti au mitindo ya kusomeshea katika kila nchi. (zozote 4x1=4)
      2. Mafanikio
        • Vitabu vingi vya sarufi na hadithi vilichapishwa mf. Modern Kiswahili grama.
        • Tafsiri ilifanywa na vitabu kuchapishwa kwa kiwashili mf. Kisima chenye hazina.
        • Kamusi tatu zilichapishwa.
        • Vitabu vya kufunzwa Kiswahili viliidhinishwa. (zozote 4x1=4)
          Adhibu,makosa sita ya hijai x ½ = 3
          Makosa ya sarufi sita x ½ = 3
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Momaliche Joint Pre Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest