Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Asumbi Girls Highschool Pre-Mock Exams May-June 2022

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  1. Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  2. Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
  3. Jibu maswali yote.
  4. Majibu yote yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
  5. Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

KWA MATUMIZI YA MTAHINI

SWALI

UPEO

ALAMA

1

15

 

2

15

 

3

40

 

4

10

 

JUMLA

80

 


QUESTIONS

  1. UFAHAMU : (Alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali.
    Nchi nyingi duniani zimetia sahihi mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto. Haki hizi ni pamoja na uhai, lishe bora inayotosha na makazi bora yaliyo salama. Hali kadhalika, kila mtoto ana haki ya kupata elimu. Elimu inastahili kutolewa bure, iwe inafaa na inayopatikana kwa urahisi. Isitoshe , mtoto hastahili kupigwa, kudunishwa, wala kubaguliwa kwa namna yoyote ile: iwe kitabaka, kirangi, kijinsia au vinginevyo.Mtoto hapaswi kufanya kazi za kitumwa, nzito na za kushurutishwa. Vile vile , mtoto anastahili kushirikishwa katika kufanya maamuzi yanayoweza kumwathiri maishani. Pia mtoto ana haki ya kupata huduma za afya, mahitaji maalum na habari kuhusu masuala mbalimbali. Pamoja na hayo anastahili kupendwa na kuheshimiwa kimawazo na kihisia.
    Haki za watoto zinatakiwa kulindwa na kila mwanajamii, serikali na wazazi wakiwa katika mstari wa mbele. Hii ndiyo sababu serikali za mataifa mengi zimeshirikisha haki hizi katika katiba na sheria za nchi husika.Yeyote anayezikiuka anapasa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria .Walakini , haki hizi bado zinakiukwa. Watoto wengi kote duniani bado wananyimwa haki zao. Kuna watoto ambao hawajawahi hata kupata kibanda cha kuweka ubavu. Wengi wa hawa wamejipata wakiselela kwenye mitaa na hata majaa ya mji na vijiji ambako hulazimika kupitisha usiku hata katika majira ya kipupwe na masika! Wengine hawapati chakula: licha ya kuwa wanatakiwa kupata chakula chenye lishe bora. Kwao kutarajia mlo awamu tatu kwa siku ni njozi: kwani hata awamu moja ni adimu kupata! La kusitikisha ni kwamba wale wanaotarajiwa kuwa vigogo wa kuzilinda haki hizi ndio wanaoongoza katika kupalilia ukiukaji wazo. Kila siku tunasikia na kushuhudia visa vya watoto kupigwa, kushinikizwa kufanya kazi za sulubu kipunda, kunyanyaswa kinjinsia, kuishi katika mazingira hatari na hata kuuawa. Baadhi ya wanaohusika na vitendo hivi hasi huwa wazazi au jamaa wa karibu kama vile mjomba, shangazi au wahudumu wa nyumbani.
    Madhila yanayowapata watoto hayatokei tu katika mazingira ya nyumbani. Mateso huvuka mipaka na kufikia ngazi ya kimataifa. Watoto wengi katika mataifa yenye fujo na ghasia hutekwa na kutumikishwa vitani. Linalokata maini ni kwamba baadhi ya viongozi katika mataifa haya hawafanyi lolote kuwanusuru. Lao huwa kuwatazama watoto wanaotakiwa kuwalinda wakigeuzwa kuwa mababe wa kuua na kuuana.Watoto hawa huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili. Pia hulazimika kuvaa mabuti ya kijeshi ambayo huwa nanga kwao kubeba, licha ya bunduki zinazokaribia kuwazidi uzani.
    Mojawapo ya mambo ambayo viongozi nchini humu walilenga shabaha kuyafikia baada ya kijinyakulia uhuru ni elimu kwa wote. Hata hivyo, hii imekuwa kama ndoto isiyotabirika katika baadhi ya janibu. Ni kweli kwamba sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi nchini humu inaendelea kutekelezwa. Hata hivyo, asilimia ya watoto na hata watu wazima wasiojua kusoma na kuandika ingali kubwa. Jukwaa la vijiji nchini humu na hata katika mataifa mengine ya ulimwengu wa tatu limesheheni idadi kubwa ya watoto wasioenda shuleni. Kichocheo kikuu cha hali hii ni kwamba wazazi na walezi wamejipata katika lindi la ufukara uliokithiri. Hata wanapojitahidi kujinyanyua na kujikuna wapatapo kuyakidhi mahitaji ya kielimu ya wanao, wao hujipata wakitapatapa katika kinamasi hicho hicho cha ulitima. Matokeo ni kwamba watoto wa matajiri wanaendelea kuelimika huku wa maskini wakibakia kwenye kiza cha ujinga. Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kama kwamba ni waota ndoto za mchana.
    Hali ilivyo sasa hivi inadai kuwa mimi na wewe ttufanye hima tuungane mikono na kutafuta suluhisho la kudumu kuhusu utekelezaji wa haki za watoto. Twapaswa kuhimiza serikali zetu kufanya kila ziwezavyo kuhakikisha kuwa watoto wote wako shuleni. Nasi tushirikiane kutoa huduma kwa watoto na kukomesha dhuluma , mateso na dhiki kwao. Haitoshi kupeleka miswada bungeni kuhusu haki za watoto na kuipitisha kuwa sheria. Twastahili kubadilisha misimamo yetu kuhusu haki hizi na kuzilinda kwa dhati.
    1. Huku ukitoa mifano minne, eleza hali ya kinyume inayojitokeza katika aya ya pili.  (alama 4)
    2. Eleza namna hali ya usalama inavyoathiri utekelezaji wa haki za watoto kwa mujibu wa kifungu. (alama 3)
    3. Kwa kurejelea aya ya nne , onyesha mchango wa serikali katika kuwajibikia haki za watoto. (alama 3)
    4. “Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu. (alama 2)
    5. Eleza maana ya msamiati ufuatayo kama ulivyotumika katika taarifa. (alama 3)
      1. Vigogo
      2. Huwa nanga kwao
      3. Kujikuna wajipatapo
  2. MUHTASARI (Alama 15)

    Jamii ya leo inatawaliwa na kuendeshwa na kanuni ya maarifa. Inawezekana kusema kuwa uchumi wa jamii za leo na zijazo utategemea maarifa zaidi kuliko utakavyotegemea wenzo wowote mwingine. Utambuzi wa uwezo mkubwa wa maarifa katika maisha ya binadamu ndio msingi wa watu kusema ‘maarifa ni nguvu.’

    Maarifa huelezwa kwa tamathali hii kutokana na uwezo wa: kuyadhibiti,kuyaendesha,kuyatawala na kuyaongoza maisha ya binadamu popote pale walipo. Mtu ambaye ameyakosa maarifa Fulani huwa ameikosa nguvu hiyo muhimu na maisha yake huadhirika pakubwa. Kwa msingi huu, maarifa yanaweza kuangaliwa kama utajiri mkubwa ambao binadamu anaweza kuutumia kwa faida yake au kwa faida ya wanajamii wenzake. Ukweli huu ndio unaoelezwana methali ya Kiswahili: ‘Elimu ni mali.’ Elimu ni chimbuko la maarifa muhimu maishani.

    Msingi wa utajiri na maendeleo ya binadamu popote alipo basi ni maarifa. Je, maarifa kwa upande wake yana sifa gani? Maarifa yenyewe hayana upizani. Maarifa uliyo nayo huweza kuwa na watuwengine wengi pasiwe na upizani baina yenu kwa kuwa kila mmoja ana maarifa sawa.kila mmoja ana uhuru wa kuyatumia maarifa hayo kama chanzo cha kuyazalisha maarifa mengine. Utumiaji wa maarifa yenyewe hauyamalizi maarifa hayo. Maarifa hayawezi kugusika ingawa mtu anaweza kuyanyumbua maarifa yenyewe kwa kuyatumia kwa namna tofauti.

    Maarifa huingiliana na maarifa mengine. Maarifa aliyo nayo mtu mmoja huweza kuhusishwa na maarifa aliyo nayo mtu mwingine ili kuvyaza au kuzuka na maarifa tofauti. Maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa namna ambavyo mtu hawezi kufanya bidhaa nyingine ile. Kwa mfano, ni muhali mtu kulalamika kuwa hawezi kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa sababu ana mzigo mzito wa maarifa kichwani

    Sifa nyingine muhimu ya maarifa ni kuwa yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya ishara au mitindo mingine ya kidhahania. Ikiwa unataka kukihamisha chombo Fulani kutoka sehemu moja hadi nyingine, lazima uwazie ukubwa wake, uzito wake na labda hata umbali wa panapohusika. Maarifa huweza kubadilishwa au kugeuzwa na kuwa ishara ambazo huyafanya kuwasilishwa kwa njia nyepesi kuliko kwa mfano ikiwa mtu atayawasilisha katika muundo wa, kwa mfano kitabu.

    Maarifa yana sifa ya uhusianaji. Kipengele Fulani cha maarifa huwa na maana kinapowekwa sambamba au kugotanishwa na kipengele kingine cha maarifa. Huo huwa muktadha mzuri wa kueleweka au kuwa na maana. Kwa mfano , neno ‘mwerevu ‘huweza kuwa na maana kwa kuweka katika muktadha wa ‘mjinga’, ‘mjanja’, ‘hodari’, na kadhalika.
    Maarifa huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo sana. Suala hili linaeleweka kwa njia nyepesi tunapoangalia maarifa katika muktadha wa teknologia. Data zinazowahusu mamilioni ya watu, ambazo zingehitaji maelfu ya maktaba na lukuki ya vitabu, huweza kuhifadhiwa kwenye kifaa kidogo kianachoweza kutiwa mfukoni.

    Maarifa hayawezi kudhibitiwa au kuzuiliwa mahali Fulani yasisambae. Maarifa huenea haraka sana. Maarifa ni kitu kinachoepuka pingu za watu wanopenda kuwadhibiti binadamu wenzao. Hata pale ambapo mfumo wa kijamii au wa kisiasa unafanya juu chini kuwadhibiti raia au watu wenyewe, ni muhali kuyadhibiti maarifa yenyewe. Inawezekana kuzidhibiti njia Fulani za ueneaji wa maarifa lakini maarifa hayo yatapata upenyu wa kusambaa. Ni kweli kuwa maarifa ni nguvu inayozishinda nguvu zote.

    1. Fupisha aya ya pili na ya tatu. (maneno 55-60) (alama 5, 1 ya utiririko)
      • Matayarisho
      • Nakala safi
    2. Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane. (maneno 100-110) (alama 10, 2 za utirriko)
      • Matayarisho
      • ..Nakala safi
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Tofautisha sauti zifuatazo. (alama 2)
      1. /t/ /s/
      2. /h/ /gh/
      3. /o/ /u/
      4. /b/ /a/
    2.                    
      1.  Mzizi ni nini? (alama 1)
      2. Toa mfano wa kitenzi chenye mzizi huru. (alama 1)
    3. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: (alama 2)
      N+RH+t+E
    4. Ainisha mofimu katika neno lifuatalo: (alama 2)
      Kiokoteni
    5. Andika katika ukubwa. (alama 1)
      Paka hawa wamemfukuza mbwa wetu.
    6. Taja matumizi mawili ya kiambishi /e/ (alama2)
    7. Andika upya ukifuata maagizo. (alama 3)
      1. Maji ambayo wanakunywa ni hatari. (Andika katika hali ya mazoea bila kutumia amba)
      2. Watu wengi walihasirika bomu lilipolipuka katika jengo hilo. (Tumia nomino badala ya vitenzi vilivyopigwa mstari.)
      3. Pombe hiyo ilimfanya kuwa kipofu. (Tumia kitenzi badala ya neno lililopigiwa mstari)
    8. Tunga sentensi ukitumia kishazi tegemezi kinachofanya kazi ya kielezi. (alama 2)
    9. Bainisha aina ya vitenzi katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
      Wao si wahalifu ingawa walikuwa msituni walipokamatwa.
    10. Tunga sentensi ukitumia nomino waya pamoja na kivumishi cha pekee cha kusisitiza. (alama 2)
    11. Andika katika usemi halisi. (alama 2)
      Hamisi alimwambia nyanya yake kuwa siku hiyo hakuwa na nafasi lakini angemtembelea siku ambayo ingefuata.
    12. Changanua kwa jedwali. (alama 2)
      Mwenye njaa hana miiko.
    13. Taja matumizi mawili ya parandesi. (alama 2)
    14. Ainisha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia jukumu / dhamira yake. (alama 1)
      Rais amepiga marufuku ukataji miti nchini.
    15. Andika katika umoja. (alama1)
      Hao wameharibu nyua zilizotengenezwa kwa mbao.
    16. Andika katika wakati uliopita hali timilifu (alama 1)
      Miti katika msitu huo inakauka.
    17. Andika upya ukitumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari. (alama 2)
      Nyanya alisomba taka na kuitia katika jaa lililo shambani.
    18. Huku ukitoa mifano mwafaka taja miundo miwili ya nomino katika ngeli ya U/I (alama 2)
    19. Tunga sentensi ukitumia na kama: (alama 2)
      1. Kihusishi
      2. Kuonyesha umilikaji
    20. Onyesha kiima, shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
      Polisi ambao walikuja juzi waliwakamata majambazi wote jana jioni.
    21. Tunga sentensi mbili kuonyesha maana mbili za neno muhali. (alama 2)
    22. Andika methali inayoafiki maelezo yafuatayo .
      Ni afadhali kupata matatizo madogo kwa sasa ili kuyaepuka mengi baadaye.

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

  1. Eleza kwa ufupi jinsi mambo yafuatayo yanavyodhibiti mitindo ya lugha
    1. Mazingira (alama 2)
    2. Mada (alama 3)
    3. Hali (alama 2)
  2. Fafanua sera tatu ambazo zimepitishwa na serikali zinazochangia kuimarika kwa lugha ya Kiswahili. (alama 3)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. UFAHAMU : (Alama 15)
    1. Huku ukitoa mifano minne, eleza hali ya kinyume inayojitokeza katika aya ya pili. (alama 4)
      • Watoto wananyimwa haki licha ya katiba kulazimu haki hizi kutimizwa
      • Mojawapo ya haki za kimsingi ni makazi. Ilihali watoto wanalala mitaani
      • Watoto hawapati chakula ilhali wanapaswa kupata lishe bora
      • Wanaotakiwa kulinda haki za watoto ndio wanaozikiuka(vigogo)
      • Wazazi na jamaa wa karibu wanashiriki katika unyanyasaji wa watoto.
        Alama 4x1=4
    2. Eleza namna hali ya usalama inavyoathiri utekelezaji wa haki za watoto kwa mujibu wa kifungu. (alama 3)
      • Watoto hutekwa na kutumikishwa vitani
      • Watoto wanageuzwa kuwa mababe wa kuua na kuuana
      • Watoto huvishwa magwanda ambayo miili yao minyonge haiwezi kuyahimili
      • Hulazimika kuvaa mabuti ya kijeshi/ kubeba bunduki nzito
        Alama 3x1=3
    3. Kwa kurejelea aya ya nne , onyesha mchango wa serikali katika kuwajibikia haki za watoto. (alama 3)
      • Serikali / viongozi walikuwa na shabaha ya elimu kwa wote
      • Serikali kubuni sera ya elimu bila malipo katika shule za msingi
      • Utekelezaji wa sera hii unaendelea
      • Kunao wanaopigania haki ya kuwa na elimu bila malipo licha ya matatizo yaliyopo ambao wanaonekana kama waota ndoto mchana
        Alama 3x1=3
    4. “Wanaong’ang’ania kuwepo kwa elimu bila malipo ni kana kwamba ni waota ndoto mchana.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea kifungu. (alama 2)
      • Asilimia ya watoto na watu wazima wasiojua kusoma ni kubwa
      • Kuwepo kwa idadi ya watoto wasioenda shuleni
      • Wazazi wapojitahidi kujinyanyua hujipata katika kinamasi cha ulitima
      • Watoto wa matajiri wanaendelea kuelimika huku wa maskini wakibakia katika kiza cha ujinga
        Alama 2x1=2
    5. Eleza maana ya msamiati ufuatayo kama ulivyotumika katika taarifa. (alama 3)
      1. Vigogo
        • wabingwa/ wenye mamlaka/ wanaopenda kuendeleza elimu ya watoto
        • viongozi / watetezi/ washika dau/ wanaopigania haki/ wakereketwa/ vinara/ walo mstari wa mbele/ watawala/ waopigania haki za watoto
          Alama 1x1=1
      2. Huwa nanga kwao
        • Mazito/ mzigo/ uzani mkubwa/ kuwa mzigo kwao Alama 1x1=1
      3. Kujikuna wajipatapo
        • Kujitahidi kadri ya uwezo wao/ kujizatiti kulingana na uwezo/ kujaribu kujinyanyua kulingana na uwezo wake
        • Lazima aweke uwezo
          Alama 1x1=1
  2. MUHTASARI (Alama 15)
    1. Fupisha aya ya pili na ya tatu. (maneno 55-60) (alama 5, 1 ya utiririko)
      Nakala safi
      1. Maarifa huyadhibiti , huyaendesha, huyatawala na kuyaongoza maisha ya binadamu
      2. Anayekosa maarifa huathirika pakubwa
      3. Maarifa ni utajiri anaotumia binadamu kujifaidisha pamoja na wanajamii/ elimu ni mali/ msingi wa utajiri na maendeleo ni maarifa
      4. Elimu ni chimbuko la maarifa
      5. Maarifa hayana upizani
      6. Kila mtu ana uhuru wa kutumia maarifa kuzalisha maarifa mengine
      7. Utumiaji wa maarifa hauyamalizi
      8. Maarifa hayagusiki Alama 8x1/2 =4
    2. Eleza sifa kuu za maarifa kama zinavyojitokeza kuanzia aya ya nne hadi aya ya nane. (maneno 100-110) (alama 10, 2 za utirriko)
      Nakala safi
      • Maarifa huingiliana na maarifa mengine/ maarifa aliyonayo mtu mmoja huweza kuhusishwa nay a mwingine
      • Maarifa yanaweza kuhamishwa/ maarifa yanaweza kuchukuliwa kutoka sehemu moja hadi nyingine
      • Maarifa yanaweza kuwasilishwa kwa njia ya ishara au mitindo mingine ya kidhahania
      • Maarifa yanaweza kugeuzwa / kubadilishwa na kuwa ishara ambazo hufanywa / huyafanya kuwasilishwa kwa njia ya nyepesi
      • Yana sifa ya uhusianaji
      • Huweza kuhifadhiwa katika nafasi ndogo sana
      • Hayawezi kudhibitiwa au kuzuiliwa yasisambae / huenea haraka
      • Huepuka pingu za watu kuwadhibiti wenzao
      • Maarifa ni nguvu inayoshinda nguvu zote
        Alama 8x1=8
  3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
    1. Tofautisha sauti zifuatazo. (alama 2)
      1. /t/ /s/
        • /t/ kipasuo /s/ kikwamizo
      2. /h/ /gh/
        • /h/ hutamkiwa koromeo /gh/ kaakaa laini
      3. /o/ /u/
        • /o/ irabu ya wastani /u/ irabu ya juu
      4. /b/ /a/
        • /b/ konsonanti /a/ irabu
          Alama 4x ½ =2
    2.                                  
      1. Mzizi ni nini? (alama 1)
        • Sehemu ya neno inayobeba maana kuu na ambayo haibadiliki
          Alama 1x1=1
      2. Toa mfano wa kitenzi chenye mzizi huru. (alama 1)
        • Hini , subiri , samehe n.k alama 1x1=1
    3. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao: (alama 2)
      N+RH+t+E
      • Mtoto wa Juma yumo chumbani
        N RH t E alama 4x1/2 =2
    4. Ainisha mofimu katika neno lifuatalo: (alama 2)
      • Kiokoteni Ki- okot- e- ni
      • Ngeli mzizi himizo wingi alama 4x ½=2
    5. Andika katika ukubwa. (alama 1)
      • Paka hawa wamemfukuza mbwa wetu.
      • Majipaka / mapaka haya yamelifukuza jibwa letu
        Alama 1x1=1
    6. Taja matumizi mawili ya kiambishi /e/ (alama2)
      • Kauli somea, chomea, ombea
      • Rai/ himizo kasomeni ,mpikie, niambie
      • Kiambishi cha uundaji wa nomino mpambe, mshinde,
        Alama 2x1=2
    7. Andika upya ukifuata maagizo. (alama 3)
      1. Maji ambayo wanakunywa ni hatari. (Andika katika hali ya mazoea bila kutumia amba)
        • Maji wayanywayo ni hatari
          Alama 1x1=1
      2. Watu wengi walihasirika bomu lilipolipuka katika jengo hilo. (Tumia nomino badala ya vitenzi vilivyopigwa mstari.)
        • Watu wengi walipata hasara kulipotokea mlipuko wa bomu katika jingo hilo
          Alama 1x1=1
      3. Pombe hiyo ilimfanya kuwa kipofu. (Tumia kitenzi badala ya neno lililopigiwa mstari)
        • Pombe hiyo ilimpofusha. Alama 1x1=1
    8. Tunga sentensi ukitumia kishazi tegemezi kinachofanya kazi ya kielezi. (alama 2)
      Mfano ;
      • Wezi walitoroka walipowaona askari.
        Alama 2x1=2
    9. Bainisha aina ya vitenzi katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
      Wao si wahalifu ingawa walikuwa msituni walipokamatwa.
      • Wao si wahalifu ingawa – t- kipungufu
      • Walikuwa msituni – t – kikamilifu
      • Walipokamatwa –halisi
        Alama 3x1=3
    10. Tunga sentensi ukitumia nomino waya pamoja na kivumishi cha pekee cha kusisitiza. (alama 2)
      Mfano;
      • Waya wenyewe ndio uliotumiwa kufungia vitu hivyo
        Alama 2x1=2
    11. Andika katika usemi halisi. (alama 2)
      Hamisi alimwambia nyanya yake kuwa siku hiyo hakuwa na nafasi lakini angemtembelea siku ambayo ingefuata.
      • Sina nafasi leo. Nitakutembelea kesho.” Hamisi akamwambia nyanya yake.
        Alama 1/3 x6=2
    12. Changanua kwa jedwali. (alama 2)
      Mwenye njaa hana miiko

                                                   S

       KN

       KT

      W

      N

      t

      N

      Mwenye

      njaa

      hana

      miiko

      Alama 4x1/2 =2
    13. Taja matumizi mawili ya parandesi. (alama 2)
      • Hutumiwa kutoa maelezo zaidi
      • Hutumiwa katika maandishi ya kitamthi /Kufungia ufafanuzi
      • Kufungia herufi ama nambari
        Alama 2x1=2
    14. Ainisha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia jukumu / dhamira yake. (alama 1)
      Rais amepiga marufuku ukataji miti nchini.
      • Sentensi ya taarifa
        Alama 1x1=1
    15. Andika katika umoja. (alama1)
      Hao wameharibu nyua zilizotengenezwa kwa mbao.
      • Huyo ameharibu ua uliotengenezwa kwa ubao Alama 1x1=1
    16. Andika katika wakati uliopita hali timilifu. (alama1)
      Miti katika msitu huo inakauka
      • Miti katika msitu huo ilikuwa imekauka. (alama 1x1=1)
    17. Andika upya ukitumia visawe vya maneno yaliyopigiwa mstari. (alama 2)
      Nyanya alisomba taka na kuitia katika jaa lililo shambani.
      • Bibi aliokota/ alizoa taka na kuitia katika jalala lililo kondeni
        (alama 4x ½ =2 )
    18. Huku ukitoa mifano mwafaka taja miundo miwili ya nomino katika ngeli ya U/I (alama 2)
      • Mwamvuli- miavuli ( mw-mi)
      • Mti-miti (m-mi)
      • Muwa-miwa (mu-mi) alama 2x1=2
    19. Tunga sentensi ukitumia na kama: (alama 2)
      1. Kihusishi Alishambuliwa na wezi. alama 1x1=1
      2. Kuonyesha umilikaji –Yeye ana mali nyingi. (alama 1x1=1
    20. Onyesha kiima, shamirisho na chagizo katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
      • Polisi ambao walikuja juzi waliwakamata majambazi wote jana jioni.
      • Polisi ambao walikuja juzi-kiima
      • Majambazi / majambazi wote –shamirisho
      • Jana jioni-chagizo alama 3x1=3
    21. Eleza maana mbili za neno muhali. (alama 2)
      • Kutowezekana kwa jambo
      • Ghasia/ fujo (sharti atunge sentensi mbili) (alama 2x1=2)
    22. Andika methali inayoafiki maelezo yafuatayo:
      Ni afadhali kupata matatizo madogo kwa sasa ili kuyaepuka mengi baadaye
      • Heri nusu shari kuliko shari kamili
      • Heri ya mrama kuliko ya kuzama
      • Heri kuwa kibichi kuliko kuungua (alama 1x1=1) 

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

  1. Eleza kwa ufupi jinsi mambo yafuatayo yanavyodhibiti mitindo ya lugha
    1.  Mazingira (alama 2)
      • Mazingira hudhibiti ishara zinazotumika.
      • Mazingira huathiri toni/ kiimbo
      • Mzungumzaji huchota msamiati kutoka anakozungumzia
      • Mazingira hudhibiti urasmi wa lugha
        (alama 2x1=2)
    2. Madhumuni (alama 3)
      • Mada huathiri uteuzi wa msamiati
      • Mada hudhibiti toni inayotumika
      • Usanifu wa lugha hutegemea kule kunakozungumziwa
        (alama 3x1=3)
      • Hali (alama 2)
    3. Hali ya mtu huathiri toni au kiimbo k.m. mtu mwenye huzuni hutumia toni ya chini
      • Muundo wa sentensi huathiriwa na hali ya mtu
      • Hali ya mtu yaweza kuathiri usanifu wa lugha.
        (alama 2x1=2)
  2. Fafanua sera tatu ambazo zimepitishwa na serikali zinazochangia kuimarika kwa lugha ya Kiswahili. (alama 3)
    • Kiswahili kufanywa lugha rasmi
    • Kiswahili kuwa lugha ya taifa
    • Kiswahili kuwa somo la lazima shuleni
    • Kiswahili kutumiwa bungeni kama lugha rasmi
    • Kiswahili kutumiwa katika machapisho ya serikali
      (alama 3x1=3
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Asumbi Girls Highschool Pre-Mock Exams May-June 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest