MASWALI
- LAZIMA
Wewe ni kiranja mkuu wa shule ya Nyota. Umealikwa katika hafla ya kustaafu kwa Mwalimu wako; mlezi wa kidato chako. Andika wasifu utakaotoa kuhusu mwalimu huyu. (alama 20) - Magari ya matatu yameleta faida nyingi hapa nchini kuliko hasara. Jadili. (alama 20)
- Tunga kisa kinachodhihirisha maana ya mehtali ifuatayo: (alama 20)
Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. - Tunga kisa kitakachomalizika kwa maneno yafuatayo: (alama 20)
Sikutarajia hayo kutoka kwa mwandani wangu. Niliamua kuufungua ukurasa mpya wa maisha yangu.

MWONGOZO WA INSHA
- LAZIMA
Sura ya wasifu- Kichwa – kitaje wasifu ni wa nani kwa mfano, Wasifu wa Mwalimu wangu mlezi wa kidato au utaje jina, wasifu wa Mwalimu Juma na kadhalika.
- Sehemu ya mwili
- Tambulisha msifiwa kwa majina yote.
- Mwaka wa kuzaliwa, umri wake.
- Mahali pa kuzaliwa.
- Wazazi wake, familia yake n.k.
- Maelezo haya ya kimsingi yawe katika aya moja.
- Masomo yake.
- Shule ya chekechea, msingi na upili.
- Chuo kikuu (iwapo alienda)
- Ndoa yake.
- Kazi na tajiriba ya kazi.
- Mchango wake katika jamii.
- Ushirika au uanachama.
- Hitimisho
Aya ya mwisho ndiyo huhitimisha wasifu.
Mwandishi/mtahini aeleze umaarufu wa anayeandikiwa wasifu na sababu za mtu huyo, kuhitaji utambulisho au sifa alizopewa.
Tanbihi- Mtahiniwa arejelee nafsi ya tatu (umoja) kama vile Darwesh alizaliwa mnamo….
- Hutaja tu sifa chanya za mrejelewa.
- Huweze kuandikiwa aliye hai au aliyekufa.
- Mtu huyu lazima awe ametoa mchango fulani wa kupigiwa mfano.
- Ajaze urefu wa maneno 400.
- Sarufi bora izingatiwe.
- Atakayeandika wasifu kazi au tawasifu aondolewe alama 4S (sura)
- SWALI LA PILI
Mjadala/mdahalo
Arejelee sehemu mbili za swali.
Faida- Usafiri wa haraka.
- Nauli yake ni nafuu ikilinganishwa na ndege.
- Husaidia kubeba mizigo.
- Ni nyingi hivyo basi rahisi kupatikana.
Hasara. - Ajali nyingi hutokea na kusababisha majereha na mauti.
- Madereva na makanga wenye matusi.
- Abiria kurundikana pamoja ni chanzo cha kusambaza magonjwa kama vile korona, homa kali, kikohozi n.k.
- Kuongeza nauli ovyo ovyo.
- Maadam ni nyingi husababisha misongamano hususan katika miji mikubwa.
(Ongeza hoja nyingine)
Tanbihi
Sehemu moja iwe na hoja nyingi kuliko nyingine anaweza kutoa msimamo wake kutokana na idadi ya hoja.
- METHALI – MGAAGAA NA UPWA HALI WALI MKAVU.
- Kichwa ni methali yenyewe.
- Mtahiniwa arejelee sehemu mbili za methali, asipofanya hivyo asipate zaidi ya alama kumi.
- Atunge kisa kinacholenga maana na matumizi ya methali hii.
Maana na matumizi. - Mtu anayejishughulisha na jambo fulani lazima mwishowe atafanikiwa au ataambulia kitu/mapato/mavuno.
- Methali hii inamiza bidii ya kutenda jambo.
- Mtungo huu uwe na mvuto.
- Azingatie sarufi na hijai bora.
- Ajaza maneno mia nne.
- Atakayepinga maana atuzwe D03.
- Atakayetoa maelezo bila mtungo atakuwa amepotoka kimaudhui.
- MDOKEZO WA KUMALIZIA.
- Abuni kichwa mwafaka.
- Pawe na tukio linalomhusu yeye na rafiki (mwandani wake)
- Tukio hilo liwe baya la kumsaliti rafiki (kinyume na matarajio)
- Mhusika (Nafsi ya kwanza) aathirike na tendo la mwandani
- Tukio hilo liwatenganisha marafiki ndipo mmoja (nafsi ya kwanza) aamue kuanza maisha mapya bila msaada wa rafiki huyo msaliti.
- Amalize mtungo wake kwa maneno haya.
Hatua- Kichwa.
- Wahusika wawili – Mwandishi (mimi) na rafiki.
- Aonyehse urafiki huu na ushirikiano wao.
- Tukio (tendo la usaliti)
- Utengano.
- Mwandishi kuufungua ukurasa mpya.
Tukio hili linaweza kuwa:- Kumsengenya/kumsingizia.
- Kumshtaki kwa mkuu.
- Kumsaliti kwa watu wengine.
- Kumnyima nafasi fulani/kataa kumsaidia.
- Kumuibia mali
- Kumbaka n.k
Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Mumias West Pre Mocks 2022.
Tap Here to Download for 50/-
Get on WhatsApp for 50/-
Why download?
- ✔ To read offline at any time.
- ✔ To Print at your convenience
- ✔ Share Easily with Friends / Students
Join our whatsapp group for latest updates