Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mumias West Pre Mocks 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. UFAHAMU (ALAMA 15)
  Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
  Ilikuwa jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa kusikiliza taarifa ya habari.
  Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe kiinuamgongo. Mwezi mmoja mzima nilikuwa katika shughuli za kulipa deni hapa na kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.
  Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, waziri wa kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia la kilo tisini. Nami nilikuwa naanza kuumakinikia mradi huu.
  Baada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kulima nilitenga ekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wakati wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Machi, nilitafuta trekta la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro.
  Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazo bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani.
  Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua na kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini. Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia’. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.
  Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapitanjia waliajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siku wanaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata na kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.’
  Bila taarifa wala tahadhari, mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi. Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’ Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda si muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tuko lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu huku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.
  Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuns, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500. Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa. ‘MAHINDI GUNIA 900/=.’ Niligutuka usingizini.
  1. Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki cha habari. (alama 1)
  2. Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha pesa katika benki baada ya mradi kukamilika? (alama 2)
  3. Taja matatizo matatu yaliyotishia mradi wa msimulizi wa kukuza mahindi (alama 3)
  4. Eleza maana za methali zifuatazo kwa mujibu wa taarifa
   1. Usikate majani, mnyama hajauawa (alama 1)
   2. Muumba ndiye muumbua (alama 1)
  5. Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia.(alama 4)
  6. Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu? (alama 1)
  7. Eleza maana za;
   1. Kinuamgongo (alama 1)
   2. Manyakanga wa kilimo (alama 1)
 2. UFUPISHO(ALAMA 15)
  Soma makala yafuatayo kisha ufupishe kwa mujibu wa maswali uliyopewa.
  Idadi kubwa ya wanafunzi huingiwa na wasiwasi wakaribiapo kufanya mtihani kwa sababu mbalimbali, kubwa likiwa ni hofu kwa jinsi ambavyo watafanya katika mtihani huo. Asilani mambo hayafai kuwa hivyo. Wataalamu wa masuala ya saikolojia na wale wa elimu wanashauri kuwa mtahiniwa anafaaa kupata muda mwingi wa mapumziko wakati anapokaribia kufanya mtihani ili aweze kuituliza akili asije akapatwa na mzongo wa akili.
  Moja katika mashauri ni kuwa mtahiniwa anafaa kupata usingizi wa kutosha wakati akijiandaa na pia wakati akifanya mtihani. Hii ni kwa sababu mtihani wa mwisho si tofauti na mitihani mingine ambayo mtahiniwa amekuwa akifanya, pamoja na kuwa ni maswali ya jumla tu kutoka viwango vyote vya masomo. Hivyo basi, mtihani unapokaribia, mtahiniwa anafaa kudurusu na kufanya majaribio mbalimbali ya mtihani pamoja na kujikumbusha yale aliyofunzwa na mwalimu wake. Wale asimdunishe au kumdharau mwalimu hata kama stadi zake za kufundisha kazikumsisimua – alikupa kito cha thamani kitakachokufaa kama silaha wakati wa mtihani.
  Mtihani unapokaribia, mtahiniwa anafaa kuwa amekwisha kutambua udhaifu wake na kutia bidii kuudhibiti kupitia udurusu, mijadala na mashauriano. Kumbuka kuwa bidii haiui ila hulipa. Hivyo basi, kila unaposhirikisha bidii na ujasiri wa wako na kuimarisha uelewe wako wa somo, na hatimaye ukaboresha matokeo katika somo hilo. Vilevile, kujadili au kufafanua mada unayoielewa vyema kwa m wenzio aiyeielewa kutakuwezesha kuielewa hata Zaidi na hivyo kuimarisha uwezo wako wa kuzoa alama nyingi katika mtihani endapo swali litatoka katika mada hiyo.
  Pamoja na hayo, mtahiniwa anafaa kujihadhari na majuto ya kufanya kile ambacho hakupaswa kufanya. Anaweza kuhakikisha hili kwa kuyapitia maswali kwa makini Zaidi, na kuyatafakaria, kuyapangia na kuaandikia majibu sawasawa kasha kuyasoma tena majibu yake ili kuwa na uhakika kwamba hajapotoka.
  Ikiwezekana (kwa sababu ya tofauti za kimapato na uwezo wa wazazi au walezi) mtahhiniwa anafaa kula visuri kabla kuenda kufanya mtihani. Vilevile, anapaswa kufika katika chumba cha mtihani kwa wakati unaofaa – mapema kabla ya muda wa kuanza kwa mtihani – na ahakikishe amebeba kila kifaa atakachokihitaji katika mtihani huo.
  Ikiwa utashindwa kujibu swali Fulani, usipotezee muda mwingi. Baadala yake, enelea na swali linalofuatia kasha ulirejelee swali lile lililokutatiza baadaye ukishamaliza maswali yale mengine. Usipoteze muda kutafuta jibu ambalo huna kwa wakati huo. Juu ya yote, usidhubutu kuifanya hila katika mtihani kwa kuwa kitendo kama hicho kitasababisha matokeo yako kufutiliwa mbali, nayo bidii yako ya miaka mine itakuwa imeishia gizani, ukasalia kujuta.
  1. Tumia maneno 60 kueleza ujumbe ulio katika aya mbili za mwanzo. (alama 6)
   Nakala chafu
   Jibu
  2. Mwandishi anatoa ushauri gani kwa mtahiniwa katika aya ya tatu hadi ya mwisho? Eleza kwa maneno 100 (alama 9)
   Nakala chafu
   Jibu
 3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 40)
  1. Taja vipasuo viwili vya kaakaa laini. (alama 2)
  2. Andika sentensi ifuatayo katika umoja. Maseremala walilainisha mbao hizo wakatutengenezea meza. (alama 1)
  3. Weka shadda katika neno lifuatalo ili itoe maana mbili tofauti. (alama 2)
   walakini
  4. Tumia neno ‘vile’ katika sentensi kama; (alama 2)
   1. Kiwakilishi
   2. Kielezi
  5. Tambulisha vipashio vinne vya sarufi ya Kiswahili. (alama 2)
  6. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao. (alama 2)
   Nomino,kishazi kitegemezi,kitenzi,nomino,kivumishi
  7. Tumia kivumishi cha pekee katika sentensi kuonyesha umilikaji. (alama 1)
  8. Andika neno lenye muundo ufuatao wa silabi. (alama 2)
   KIKKKI___________KKKIKI________
  9. Weka maneno haya katika ngeli zake. (alama 2)
   1. Miwani
   2. Wema
  10. Ainisha mofimu katika neno lifuatalo. (alama 3)
   Hakuwakaribisha
  11. Andika kinyume cha sentensi ifuatayo kwa kuzingatia maneno yaliyopigiwa mstari ( alama 2)
   Punde tu alipouliza swali hilo Halima aliingia darasani
  12. Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika senensi ifuatayo. (alama 2)
   Utakapomkabidhi barua hii, nipashe habari
  13. Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
   Juma alimlimia nyanyake mzee shamba hilo kwa trekta.
  14. Yakinisha sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea. (alama 2)
   Hakuwasaidia wala hakuwakaribisha kwake.
  15. Tambua kirai kihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
   Jino la Tamma linauma mara kwa mara.
  16. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya udogo (alama 2)
   Mbuzi huyo wake ana ngozi laini
  17. Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
   “Nitamwalika mtondogoo.” Fatuma akasema.
  18. Changanua sentensi hii kwa kutumia matawi. (alama 4)
   Darasa lililojengwa limefunguliwa leo alasiri.
  19. Kanusha ; (alama 2)
   Ngoma hizo zilihifadhiwa ili ziuzwe mjini.
  20. Tunatumia simile tunapotaka mtu atupishe,___________ tunapoomba kitu kinusurike, na kefule__________ na jambo. (alama 1)
 4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
  1. Eleza maana ya lugha ya taifa. (alama 2)
  2. Eleza sababu tatu zinazofanya watu kubadili na kuchanganya ndimi. (alama 3)
  3. Eleza hatua tano ambazo zimesaidia kukuza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru nchini Kenya. (alama 5)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. UFAHAMU (ALAMA 15)
  1. Mashaka ya kilimo cha mahindi (alama 1)
  2. Shilingi elfu saba na mia tatu (200,000 – 192,700=7,300) ( alama 2 )
  3.      
   1. Tisho la korongo na vidiri kufukua mbegu.
   2. Kiangazi
   3. Mvua ya barafu
   4. Gharama kubora
    (1x3=alama3)
  4. Eleza maana za methali zifuatazo kwa mujibu wa taarifa
   1. Usikate majani, mnyama hajauawa (alama 1)
    Haikuwa vizuri kufurahia faida kabla ya kuuza mavuno.
   2. Muumba ndiye muumbua (alama 1)
    Mungu ana uwezo wa kuleta barafu na kiangazi na kustawisha mimea.
  5. Eleza mambo mawili yaliyosababisha msimulizi asipate faida alivyotarajia. (alama 4)
   1. Kiwango cha chini cha mavuno
   2. Kushuka kwa bei (2x2=4)
  6. Kwa nini msimulizi alisema maumbile ni kitu cha ajabu? (alama 1)
   Mahindi aliyodhani yameangamizwa na kiangazi yalinawili tena.
  7. Eleza maana za;
   1. Kinuamgongo (alama 1)
    Malipo ya kustaafu.
   2. Manyakanga wa kilimo (alama 1)
    Wataalamu wa kilimo.
    Makosa sita ya sarufi adhibu = 3
    Hijai adhibu = 3
 2. UFUPISHO ( ALAMA 15 )
  1.      
   1. Wanafunzi wengi huhofia jinsi ambavyo watafanya katika mtihani.
   2. Wataal;amu wanashauri kuwa mtahiniwa anafaa kupata muda mwingi wa kupumzika.
   3. Mtahiniwa anaweza kupata mzongo wa akili kwa kukosa mapumziko.
   4. Mtahiniwa apate usingizi wa kutosha wakati akifanya mtihani.
   5. Mtihani wa mwisho si tofauti na mwingine.
   6. Mtahiniwa afanye udurusu na majaribio ya mtihani mbalimbali. 6x1=6,ut=1
  2.          
   1. Awe ametambua udhaifu wake na kutia bidii kaudhibiti kupitia udurusu, mijadala na mashauriano.
   2. Aulize maswali kuhusu mada asioielewa.
   3. Ajadili na kufafanua mada anayoielewa kwa mwenzake asieilewa.
   4. Ajihadhari na majuto ya kufanya kile hakupaswa kufanya.
   5. Ayapitie maswali kwa makini saidi na kuyaafakari kuyapangia nakuyaandika majibu sawasawa.
   6. Ayasome tena majibu kuhakikisha kuwa hajapotoka.
   7. Ale vizuri kabla ya kwenda kufanya mtihani.
   8. Afike katika chumba cha mtihani kwa muda unaofaa na akiwa amebeba kila anachohitaji.
   9. Asipoteze muda mwing kwa swali linalomshinda bali alirejelee baadaye.
   10. Asifanye hila katika mtihani kwani matokeo yake yatafutiliwa mbali.
    9x1 =9,ut=1
    Makosa sita ya sarufi adhibu = alama 3
    Hijai adhibu = alama 3
 3. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA ( ALAMA 40 )
  1. Taja vipasuo viwili vya kaakaa laini. (alama 2)
   /k/
   /g/ 1X2=2
  2. Seremala alilainisha ubao huo akanitengenezea meza. (alama 1
  3. Weka shadda katika neno lifuatalo ili itoe maana mbili tofauti. (alama 2)
   walakini
   wala’kini-hata hivyo/kiunganishi
   wa’lakini-kasoro/dosari/hitilafu
  4. Kiwakilishi- vile vitanunuliwa
   Kielezi- Mwanafunzi aliimba vile alivyofunzwa (alama 2 )
   Kadiria sent. ya mwanafunzi
  5. Tambulisha vipashio viwili vya sarufi ya Kiswahili. (alama 2)
   Sauti
   Silabi
   Neno
   Sentensi
  6. Wanafunzi waliotia bidi masomoni walipata alama nzuri (alama 2)
   Kadiria sent. ya mwanafunzi
  7. Tumia kivumishi cha pekee katika sentensi kuonyesha umilikaji. (alama 1)
   • Matumizi ya enye.
   • Mwalimu mwenye gari amewasili.
  8. Tumia kihusishi kuonyesha uhusiano wa wakati na kiwango. (alama 2)
   KIKKKI-Jengwa,pendwa,kunywa n.k
   KKKIKI-Mbweha,ndwele,nywele,shwari n.k
  9. Weka maneno haya katika ngeli zake. (alama 2)
   1. Miwani
    I - I
   2. Wema
    U –U
  10. Ainisha mofimu katika neno lifuatalo. (alama 3)
   Hakuwakaribisha
   Ha – kikanushi cha nafsi
   ku – kikanushi cha wakati uliopita
   wa – watendewa
   karib – mzizi
   ish – kauli
   a – kiishio
  11. alipouliza-alipoulizwa/alipojibu/alipoginiza
   aliingia-alitoka/aliondoka( alama 2)
  12. Bainisha kishazi huru na kishazi tegemezi katika senensi ifuatayo. (alama 2)
   Utakapomkabidhi barua hii, nipashe habari
   Utakapomkabidhi barua hii – kishazi tegemezi.
   Nipashe habari – kishazi huru.
  13. Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo. (alama 3)
   nyanyake mzee– kitondo
   shamba hilo - kipozi
   trekta-ala
  14. Yakinisha sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea. (alama 2)
   Hakuwasaidia wala hakuwakaribisha kwake.
   Huwasaidia na kuwakaribisha kwake.
  15. Tambua kirai kihusishi katika sentensi ifuatayo. (alama 1)
   Jino la Tamima linauma mara kwa mara.
   La Tamima- RH
  16. Kibuzi hicho chake kina kigozi laini/ Kijibuzi hicho chake kina kijibuzi laini (alama 2)
  17. Andika katika usemi wa taarifa. (alama 2)
   “Nitamwalika mtondogoo.” Fatuma akasema.
   Fatuma alisema kwamba angemwalika siku tano baadaye.
  18. Changanua sentensi hii kwa kutumia matawi. (alama 4)
   Darasa lililojengwa limefunguliwa leo alasiri.
              S
       KN        KT
   N         S   T   E  E
  19. Kanusha (alama 2)
   Ngoma hizo hazikuhifadhiwa ili ziuzwe mjini.
   Ngoma hizo zilihifadhiwa ili zisiuzwe mjini.
   Ngoma hizo hazikuhifadhiwa ili zisiuzwe mjini.
   Ngoma hazikuhifadhiwa wala kuuzwa mjini.
  20. hamadi
   tunapoudhika/tunapokasirishwa/tunapokerwa/tunapogadhabishwa(alama1 )
   Makosa sita ya sarufi adhibu =alama 3
   Hijai adhibu =alama 3
 4. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
  1. Eleza maana ya lugha ya taifa. (alama 2)
   Ni lugha iliyoteuliwa kama kitambulisho cha utamaduni na ustaarabu wa taifa zima.
  2. Eleza sababu tatu zinazofanya watu kubadili na kuchanganya ndimi. (alama 3)
   1. Kusisitiza ujumbe.
   2. Upungufu wa msamiati wa lugha moja.
   3. Kutaka kudhihirisha uko kundi Fulani la watu.
   4. Kufahamu lugha Zaidi ya moja
   5. Kuficha ujumbe kwa kundi lingine katika mawasiliano (1x3=3)
  3. Eleza hatua tano ambazo zimesaidia kukuza lugha ya Kiswahili baada ya uhuru nchini Kenya. (alama 5)
   1. Kuwekwa kwa sera.
   2. Kuteuliwa kwa Kiswahili kama lugha ya taifa.
   3. Vyombo vya habari na mawasiliano mfano taifa leo.
   4. Shughuli za biashara.
   5. Uchapishaji wa vitabu.
   6. Shughuli za kidini.
   7. Kampeni za kisiasa zilitegemea matumizi ya Kiswahili. (1x5=5)
    Makosa nne ya sarufi adhibu alama 2
    Hijai adhibu alama 2
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Mumias West Pre Mocks 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest