Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mumias West Pre Mocks 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. SEHEMU A: FASIHI SIMULIZI (LAZIMA)
  Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.
  Umeanguka mwamba
  Jabali tuloegemea
  Lilotupa kimbilio
  Mahasidi kutishia
  Mti mkuu umegwa
  Wana wa ndege wa wapi?
  Bila shaka hangaiko
  Metukumba makinda.
  Angalikuwa pamwe na5si
  Maulana mungu wetu
  Swali hilo tungemuuliza
  Mbona kaacha mauko
  Ngome yetu kuvamia?
  Ela mwenyewe Mwenza
  Ajua hatima yetu
  Lilobaki kumwamini
  Riziki kutuangushia.
  1. Huu ni wimbo wa aina gani? Thibitisha. Alama 4
  2. Bainisha vipengele vitano vya kimtindo vilivyotumika katika wimbo huu. Alama 5
  3. Tungo za aina hii zinaendelea kupoteza umaarufu katika jamii yako. Fafanua hoja nne utakazotumia kuishawishi jamii yako kukinga dhidi ya hali hii. Alama 4
  4. Eleza sababu tatu za kukusanya habari kuhusu kipera hiki kwa kutumia mbinu ya kushiriki. Alama 3
  5. Ainisha kifungu kifuatacho cha sifo. Thibitisha kwa hoja tatu. Alama 4
   Ndimi Kiluki jogoo la kijijini
   Jogoo la kijijini liwikialo jijini
   Jogoo liloyavunja makoo ya jijini
   Makoo yote yanisifia
   Wangu ukoo ni wa wafalme
   Kilimo ndo nguzo yetu
   Kiluki nalima maekari kwa maekari
   Siku chache natumia
   Kandanda nasakata
   Asonijua Makinduni ni nani?
   Mbeleni ajitambulishe.

SEHEMU B: RIWAYA
ASSUMPTA K. MATEI: CHOZI LA HERI

Jibu swali la 2 au 3

 1. “Sikiliza bwana, mhitaji siku zote ni mtumwa, tangu lini maskini akabagua?
  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. Alama 4
  2. Eleza namna anayeambiwa maneno haya alivyoendeleza ploti ya riwaya ya Chozi la Heri. Alama 6
  3. Kwa mujibu wa riwaya hii, maneno ya msemaji ni ya kweli. Thibitisha kwa hoja kumi. Alama 10.
 2.         
  1. Changanua mtindo katika dondoo hili: alama 12
   Sisi tunataka kiongozi yeyote awe mwanamke au mwanamme, atakayeweza kulielekeza jahazi hili letu kwenye visiwa vya hazina. Tufikie kilele cha maendeleo pale tutakapoafikia malengo ya Kimaendeleo ya Kimilenia. Kiongozi ambaye ataendeleza zaidi juhudi za kukabiliana na wale maadui ambao wewe daima huniambia kuhusu: umaskini, ujinga, magonjwa, uhaba wa nafasi ya kazi na ufisadi. Je, huu sio uliokuwa muono wa waliopigania uhuru? Siyo ambayo viongozi waliochukua hatamu za uongozi kutoka kwa watu weupe waliyofanya juu chini kuyatekeleza?
  2. Mwalimu amekwezwa katika riwaya ya Chozi la Heri. Thibitisha. Alama 8.

SEHEMU C: TAMTHILIA
PAULINE KEA: KIGOGO

Jibu swali la 4 au 5

 1.      
  1. Mhini na mhiniwa njia yao ni moja. Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa mujibu wa tamthilia ya kigogo. Alama 10
  2. Fafanua vizingiti mbalimbali vinavyojitokeza katika harakati za Wanasagamoyo kuikomboa jamii yao. Alama 10
 2. Sina muda wa kupoteza tafakuri zangu kwa mambo yasiyoniruzuku…safari hii ni hatua kwa hatua.
  1. Weka dondoo hili katika muktadha wake. Alama 5
  2. Bainisha toni iliyotumika katika kauli hii. Alama 2
  3. Eleza umuhimu wa mandhari ambamo kauli hii inajitokeza. Alama 8
  4. Jadili sifa zozote tano za msemaji wa maneno haya. Alama 5

SEHEMU D: USHAIRI
Jibu swali la 6 au 7

 1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
  Wanaume ni wanyama
  Nakumbuka vyema sana, sisahau siku ile
  Nilipoitwa na nina, akanipa ya kivyele
  Mwanangu u msichana, nakuasa usikile
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Kuwa umevunja ungo, ni hali ya maumbile
  Bora uwapo na bongo, anasa uzikimbile
  Ukijitia maringo, utatungwa mimba mbele
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Ngawa waje na manoti, “Nakupenda” wakwambile
  Wakuvalie makoti, usiwaachie mbele,
  Hata wapige magoti, wambile mna kelele
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Ngono ni tendo la suna, Amina sikimbilile
  Wala miguu halina, kwamba lingekukimbile
  Muhimu kwako Amina, kwanza uthamini shule
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Kuzurura mitaani, si tabia njema ile
  Unapotoka nyumbani, fululiza hadi shule
  Si kwenda vichochoroni, kuwaona kina wale
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Uwe mwana msikizi, yano uyazingatile
  Mengine kuhusu penzi, mwanangu taonywa shule
  Kama mameyo mzazi, nimekuonya kimbele
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Wakaja kina Hamadi, mwana wa Mzee sule
  Kwangu wakapiga hodi, hata mkuu wa shule
  Ila nikajitahidi, kukwepa mitego ile
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Na kuna huyo Karisa, mwanafunzi kule shule
  Akawa hunipapasa, nami vile vile
  Mwishowe ikatupasa, tugawe tunda tule
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Nani akachovya uto, wa asali tamu vile
  Na kisha aape kuto, kula asali milele
  Kuwa ni mjamzito, wamenifukuza shule
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  Karisa yu vilevile, angali yuwaenda shule
  Na mie kitumbo mbele, ninajikuna upele
  Yameshatimia yale, niloonywa siku ile
  Si watu waone vile, wanaume ni wanyama.
  1. Eleza ujumbe wa shairi hili? alama 5
  2. Ainisha shairi hili kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo: alama 3
   1. vina
   2. vipande
   3. mishororo
  3. Onyesha umuhimu wa mbinu mbili alizotumia mshairi kutosheleza mahitaji ya kiarudhi katika shairi hili. alama 2
  4. Tambua nafsi neni katika shairi. Thibitisha alama 1
  5. Andika ubeti wa sita kwa lugha nathari. alama 4
  6. Tambua aina mbili za urudiaji zilizotumika katika shairi hili. Alama 2
  7. Eleza maana za maneno na vifungu vya maneno vifuatavyo: alama 2
   1. anasa uzikimbile
   2. wanaume ni wanyama
   3. tugawe tunda tule
 2. Soma shairi hili kisha ujibu maswali.
  Nikumbuke mwanangu,
  Kila asubuhi unapoamka,
  Kwenda kazini,
  Unapochukua sabuni ya kunukia,
  Na dodoki jororo
  Na kopo la koligeti,
  Kwenda kukoga hamamuni,
  Penye maji ya bomba,
  Yaliyochunjwa na kutakaswa,
  Mororo…
  Kumbuka nyakati zile,
  Za staftahi ya sima na mtama,
  Ndizi na nagwa,
  Kwa mchicha na kisamvu,
  Na ulipokwenda choo,
  Ulilia kwa uchungu,
  Nikumbuke,
  Unapotoka nyumbani asubuhi maridadi,
  Katika suti ya moto,
  Miwani ya pembe,
  Viatu vya Paris,
  Saa ya dhahabu,
  Unapong’oka kwenda kazini,
  Katika Volvo,
  Katika njia iliyosakafiwa.
  Kumbuka,
  Nyakati zile,
  Mimi ni mamako,
  Tulivyojidamka,
  Mara tu kwale wa kwanza,
  Alipoanza kukoroma,
  Jogoo wa kwanza hajawika,
  Mimi nikachukua mundu na panga,
  Mamako jembe na shoka,
  Tukaelekea porini,
  Kufyeka na kuchimbua,
  Na hubaki wajiandaa kwenda shule..
  Nikumbuke,
  Saa za jioni,
  Unapovalia kitanashati
  1. Thibitisha kuwa utungo huu ni shairi (alama 4)
  2. Fafanua toni ya utungo huu (alama 2)
  3. Huku ukitoa mifano, linganua kati ya mistari toshelezi na mistari mishata(alama 4)
  4. Eleza maudhui yoyote manne yanayojitokeza (alama 4)
  5. Tambua aina mbili za taswira zilizo katika ubeti wa mwisho. (alama 2)
  6. Eleza muundo wa shairi hili. (Alama 4)

SEHEMU E: HADITHI FUPI
Wah. Alifa Chokocho na Dumu Kayanda: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE

 1. Eleza umuhimu wa mazungumzo kati ya Sasa na Mbura katika kujenga hadithi ya Shibe inatumaliza. Alama 10
 2. Fafanua jinsi suala la malezi lilivyoshughulikiwa katika hadithi ya Tulipokutana Tena na Mtihani wa Maisha. Alama 10


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SEHEMU YA A

 1.            
  1.  Aina-Mbolezi
   • unahusu kifo; umeanguka mwamba
   • marehemu amesifiwa-jabali tuloegemea
   • toni ni ya huzuni-hangaiko metukumba
   • mbona kaacha mauko ngoma yetu kuvamia
   • imani ya jamii kuhusu kifo-Maulana ameacha kifo kuvamia jamii
    Kutaja aina=1
    Athibitishe kwa hoja tatu 3x1=3
    Jumla=4
  2.        
   • jazanda/istiara-umeanguka mwamba; mtu muhimu amefariki, makinda
   • inkisari-lilotupa, ajua
   • kuboronga sarufi-mahasidi kutishia, riziki kutuangushia
   • methali-mti mkuu umegwa
   • swali balagha-wana wa ndege wa wapi?
   • lahaja-ela
   • mbinu rejeshi-jabali tuloegemea za kwanza 5x1=5; atoe mifano.
  3.        
   1. Kurithisha kipera hiki kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
   2. Kukifanyia kipera hiki utafiti ili kubainisha sifa za uwasilishaji wazo na kuzihifadhi
   3. Kukihifadhi kwenye maandishi.
   4. Kukifunza shuleni
   5. Kuziimba mara kwa mara/kujifunza uimbaji wake.
   6. Kuhifadhi kwenye video ili kuhifadhi sifa za uwasilishaji kama vile suti/kidatu na miondoko.
   7. Kutafitia vyanzo vya kudidimia kwazo na kuzidhibiti.
   8. Kuandaa mashindano ya uimbaji ili kurithisha utambaji wazo kwa kizazi kingine.
   9. Kushirikisha wageni waalikwa katika ujifunzaji wa mbolezi/kujifunza kwa mitindo anuwai ili kuwafanya wanafunzi wavutiwe nazo, na kuziendeleza.
   10. Kutumia kufunzia masomo mengine na stadi nyingine kama vile kusikiliza na kuzungumza.
   11. Kuandaa vipindi vya redio au runinga na kuwaalika mafanani stadi kuimba ili kuwa vielelezo.
   12. Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wake. Za kwanza 4x1
  4.      
   1. Kwa kushiriki, mtafiti huja karibu zaidi na jamii na hupata habari za kuaminika moja kwa moja.
   2. Ni njia bora ya kupata habari kutoka kwa watu ambao hawajui kusoma na kuandika ama wale ambao huona vigumu kujieleza moja kwa moja.
   3. Ni rahisi kwa mtafiti kuuliza maswali muhimu kuhusu kipera hiki.
   4. Mtafiti anaweza kunakili/kunasa anayosikiliza au anayotazama, hivyo kuhifadhi sifa za kiimbo, toni na ishara.
   5. Mtafiti hupata taathira na hisia halisi ya yanayowasilishwa kwa vile anakabiliana ana kwa ana na watendaji na hivyo kuelewa zaidi.
   6. Mtafiti anaweza kuthibitisha yale aliyokusanya kupitia kwa hojaji na mahojiano kwa kuyahakiki.
   7. Kushiriki hukuza utangamano kati ya mtafiti na wanajamii.
    3x1=3; sahihisha za kwanza tatu.
  5. Aina- Majigambo/kivugo
   • anajiita jogoo la kijijini
   • linawikia jijini
   • liloyavunja makoo ya jijini
   • linasifiwa na makoo yote
   • koo wake ni wa wafalme
   • wao ni wakulima
   • yeye hulima maekari kwa maekari
   • hutumia siku chache kulima
   • anasakata kandanda
   • kila mtu anamfahamu
    Kutaja aina=1
    Kuthibitisha=3
 2. SEHEMU B: RIWAYA
  1.        
   1. Wasemaji ni viongozi wa Shirika la Maghala ya Nafaka.
   2. Aliyeambiwa ni Lunga.
   3. Alikuwa amepinga uuzaji wa mahindi yaliyoharibika.
   4. Mahindi yalitolewa ng’ambo
   5. Msimamo wa Lunga ulimfanya kuachishwa kazi.
   6. Walisisitiza kuwa ni lazima watu wapewe mahindi hayo licha ya kuwa yalikuwa mabovu/watu walikuwa maskini/wangekufa njaa.
    Dondoo limetolewa uk. 71
    Zozote 4x1
  2. Anayeambiwa maneno haya ni Lunga:
   1. Anaendeleza kipengele cha mgogoro ambacho ni muhimu katika kujenga ploti. Ana mgogoro na waajiri wake kuhusu mahindi/ na mkewe kuhusu umaskini wake.
   2. Barua anayoandikiwa ya kustaafishwa ni kipengele cha ploti. Anaachishwa kazi.
   3. Hotuba ya Lunga ni kipengele cha ploti. Anazungumzia suala la mazingira.
   4. Kumaskinika kwake kunabadilisha msuko wa riwaya. Mkewe anamtoroka.
   5. Kifo cha Lunga kinabadilisha msuko wa riwaya. Sauna anawaiba wanawe; Umu anaondoka nyumbani kwenda kupambana na wanawe.
   6. Ametumiwa kusawiri mabadiliko katika maisha ya binadamu.Alianza kukata miti. Wahusika wengi pia walibadilika kwa mfano Sauna.
   7. Amesababisha kuibuka kwa wahusika wengine kv Kimondo. Walisoma katika darasa moja.
   8. Amechangia katika kuendeleza ufaafu wa anwani. Mara nyingi alipata dhiki na faraja. Mkewe alipoondoka alisaidiwa na majirani kutunza wanawe.
   9. Tunafahamu usuli wa familia yake kupitia kwake-Mababu zake walihamia katika Mlima wa Simba kutoka Kaoleni.
    Zozote 3x2=6
  3. Athibitishe kuwa maskini ni mtumwa/hawezi kuchagua:
   1. Wahafidhina wanauziwa mahindi yaliyoharibika kwa kuwa walikuwa maskini/wangekufa njaa.
   2. Kuna watoto wengi ombaomba katika jamii km Hazina.
   3. Watu wanaopora mafuta na kujaribu kuokolewa na Makaa wanafia hapo lori linapolipuka.
   4. Maskini wanachukuwa mali zisizo zao. Wanapora maduka ya wenzao. Walipora maduka wa Wahindi na hata waafrika wenzao. Watu hawa wanafia katika jumba la Ridhaa.
   5. Chandachema anaishi maisha ya taabu baada ya kutoka kwa Bw. Tenge na Bi. Kimai. Analala kwenye michai.
   6. Wakimbizi katika mlima wa Mamba wanakula mizizi ya mwitu na matunda mwitu kwa mfano Ridhaa.
   7. Wakimbizi hawa wanang’ang’ania chakula cha msaada kinapotolewa.
   8. Wakimbizi wanakunywa maji machafu kutoka katika Mto wa Mamba.
   9. Dick, kando na kujiingiza katika matumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya kutokana na kutishwa na Buda, anataka kukidhi mahitaji yake ya kimsingi.
   10. Sauna anaingilia biashara mbalimbali haramu km ulanguzi wa watoto kutoka na kutomudu maisha yake.
   11. Lunga anaachishwa kazi kwa kuwa hana uwezo. Yeye ni mtegemezi asiye na haki.
   12. Pete anaishi maisha ya taabu baada ya kifo cha nyanya yake. Anatumiwa na wanaume; wanamzalisha watoto watatu.
   13. Vijana wa vyuo vikuu ni maskini; hela za ufadhili hazitoshi. Wanaingilia matumizi ya pombe haramu.
   14. Shamsi anamtegemea pakubwa mkewe Halua. Anamtegemea kwa chakula.
   15. Babake Shamsi ananyang’anywa shamba lake. Anatumikishwa katika shamba lilo hilo.
   16. Babake Shamsi pia ana anakula vijasumu vya mizizi mwitu kutokana na njaa.
    Zozote 10x1=10; Kadiria hoja nyingine.
 3.      
  1.      
   1. Tanakuzi-mwanamke/mwanamme
   2. Jazanda-kulielekeza jahazi hili letu kwenye visiwa vya hazina
   3. Uhuishaji-wale maadui
   4. Swali balagha-je, huu sio uliokuwa muono wa waliopigania uhuru?
   5. Mbinu rejeshi-waliochukua hatamu za uongozi
   6. Usimulizi wa nafsi ya kwanza-sisi tunataka
   7. Toni ya kushawishi na kushauri-kiongozi atakayeweza…
   8. Uradidi/takriri-kiongozi
    Dondoo limetolewa uk. 40
    Zozote 6x2=12
  2.      
   1. Wanadumisha amani miongoni mwa wanafunzi. Mwalimu wa Ridhaa anazungumza na wanafunzi kuhusu umuhimu wa amani shuleni. Wanafunzi walikuwa wamemchokoza Ridhaa.
   2. Wanawafunza wanafunzi maadili. Mwangeka anakumbuka maneno ya mwalimu wake wa dini kuwa wawaheshimu wazazi wao.
   3. Wanatafuta habari zaidi kuhusu hali ya wanafunzi wao. Bi. Dhahabu alipata habari kuhusu Umu kutoka kwa mwalimu msimamizi wa darasa lake.
   4. Wanawatafutia wanafunzi wao wazazi wa kupanga. Kwa mfano Mwalimu dhahabu anampa Umu wazaza-Apondi na Mwangeka.
   5. Wanawatafutia wanafunzi mahali pa kuishi/ makao. Bi. Tamasha anamtafutia Chandachema mahali pa kuishi-kwa Tenge na Kimai.
   6. Watu wema/wenye maelewano-mwalimu mkuu wa Kairu anamruhusu mama kulipa karo kidogo kidogo.
   7. Wanawakomaza wanafunzi wao wadogo akili kwa kuwafunza vizuri mambo ya kiuchumi na kisiasa kwa mfano Mwalimu Meli kwa kina Tila
   8. Wanasawiriwa kama wasomi-Fumba anajiongeza masomo na kuenda kufunza katika chuo kikuu.
   9. Wanatoa ushauri na uelekezaji kwa mfano Bw. Mwenge.
   10. Wanadhihirisha upendo kwa wanafunzi. Bi. Dhahabu anampenda Umu. Anamkumbusha arejee darasani.
   11. Wanadhihirika kama wenye bidii-Walimu wa mwangeka waliwafunza masomo ya ziada.
   12. Wanasisitiza umuhimu wa elimu katika kuboresha maisha ya wanafunzi. Mwalimu Dhahabu kwa wanafunzi wake.
    Zozote 8x1=8
    (kumkweza mtu ni kumtukuza/kumsifu/kumpa sifa chanya)
 4. SEHEMU C: TAMTHILIA
  1.        
   1. Majoka anawadhulumu Wanasagamoyo kwa kuwakosesha amani. Anatumia askari kuwapiga wanapoandamana. Mwishowe mkuu wa askari anamsaliti. Anamuunga mkono Tunu.
   2. Anamtuma Chopi kumwaangamiza Tunu. Chopi anamwamuru Ngurumo na Vijana wengine kumuua Tunu. Wanamvunja mguu. Mwanawe Majoka, Ngao Junior anapatika akiwa amefariki kutokana na Sumu ya Nyoka.
   3. Majoka anamuua Jabali ili asalie mamlakani. Wanasagamoyo, chini ya uongozi wa Tunu, wanamng’oa mamlakani.
   4. Ashua anawadharau na kujaribu kuwafukuza akina Tunu nyumbani kwake. Yanamwendea mrama watu wanapomgeuka na kuimwaga pombe yake.
   5. Majoka anaruhusu matumizi ya dawa za kulevya katika shule yake. Wanafunzi wanageuka makabeji. Hawafuzu. Mwanawe, Ngao Junior, anafariki kutokana na dawa za kulevya.
   6. Chopi anamnyanyasa Sud pamoja na Mkewe Ashua. Kifo chake kinapangwa na Majoka na Sudi.
   7. Majoka anawanyanyasa Wanasagamoyo kwa kulifunga soko la Chapakazi na kuwafurusha. Soko linafunguliwa baadaye na Tunu. Majoka anaondolewa uongozini.husda anamvamia Ashua ofisini mwa Majoka kwa madai ya kumwendea kinyume na mmewe. Baadaye Majoka anakiri kuwa hampendi Husda.
   8. Husda anamvamia Ashua ofisini. Wote wanatiwa mbaroni licha ya kwamba Husda aliachiliwa huru baada ya muda mfupi.
    Hoja 5x2; kadiria nyingine. Aonyeshe namna mtu alivyomtesa mwenzake naye pia akaishia kuteseka.
  2.      
   1. Askari wanatumiwa kuwatawanya wanapogoma na kuandamana. Wanapigwa na kuumizwa. Wengine wanauawa. Kwa mfano vijana watano.
   2. Majoka anatumia vitisho katika utawala wake. Anawatisha wanaompinga kama Tunu na Sudi.
   3. Majoka anawaua wapinzani wake kwa mfano Jabali.
   4. Anawakandamiza kiuchumi ili wazidi kumtegemea kwa mfano kufungwa kwa soko kunamfanya Ashua kwenda kumwomba chakula.
   5. Anawatumia vikaragosi kutekeleza amri zake. Vikaragosi hawa wanamshauri vibaya. Chopi anamshauri kutumia nguvu zaidi.
   6. Kukandamizwa kielimu. Anatoa elimu duni. Wanafunzi katika shule zake wanatumia dawa za kulevya. Hawazinduki ili kuipigania jamii.
   7. Watu wanatupiwa vijikaratasi wahame kwa kutomuunga mkono Majoka. Kwa mfano akina Siti.
   8. Anawahonga watu ili wamuunge mkono. Watu wake wanapitia mangweni na kuwanunulia vijana pombe.
   9. Anatoa kandarasi kwa njia ya ubaguzi ili wahusika waendelee kumpigania. Ngurumo anapewa kandarasi ili azidi kumhudumia majoka.
   10. Wizi wa kura-Majoka haamini katika demokrasia. Anatishia kuiba kura.
   11. Kukandamizwa kwa vyombo vya habari. Anasema kuwa atafunga vyombo vyote kisalie kimoja.
   12. Kuwafukuza wafadhili wa Tunu. Anaahidi kuwafukuza wafadhili wa Tunu ili Tunu ashindwe kuikomboa jamii yake.
   13. Propaganda-watu wa Majoka wanawachochea Tunu na Sudi. Wanadai kuwa wana mahusiano ya kimapenzi. Mke wa Sudi anaamini katika hii propaganda.
   14. Ushawishi mkubwa wa kiuchumi-Majoka anajiweza. Ana hela na raslimali za kutatiza ukombozo. Anataka kumpa Ashua kazi katika moja kati ya shule zake.
    10x1=10
 5.        
  1.      
   1. Maneno ya Ngurumo.
   2. Kauli mbili: Ya kwanza anamwambia Sudi; Sudi alimwambia atafakari kauli kuwa Tunu alikuwa amekuja kuogelea, sio kuvua.
   3. Kauli ya pili Ngurumo anawaambia sudi na Tunu kuwa ulevi ni safari ya hatua kwa hatua.
   4. Walikuwa Mangweni/Kwa Asiya/Kwa Mamapima/Kwa Boza.
   5. Tunu na Sudi walikataa kunywa pombe Mangweni.
    Dondoo ni la ukurasa wa 57
    Zozote 5x1=5
  2.    
   1. Toni ya dharau/kubeza-sina muda wa kupoteza/mambo yasiyoniruzuku
   2. Toni ya kushauri-safari hii ni hatua kwa hatua.
    1x2=2
  3.        
   1. Yanaendeleza maudhui ya ulevi-watu walikuwa kwenye makundi wakinywa pombe.
   2. Yanadhihirisha madhara ya pombe haramu-mtu II anaanguka.
   3. Ni katika mandhari haya ambamo Ngurumo anathibitisha kuwa ndiye aliyemvunja Tunu mkuu.
   4. Yanadhihirisha ujasiri wa Tunu. Alikutana na Ngurumo aliyemuumiza.
   5. Uhusiano na historia ya wahusika inajitokeza katika mandhari haya. Tunu na Ngurumo walisoma humu.
   6. Yanaendeleza ploti ya tamthilia. Tunu anaimbiwa wimbo.
   7. Uvunjaji wa sheria unajitokeza. Asiya alipewa kibali cha kuuza pombe na Majoka.
   8. Yanadhihirisha msimamo dhabiti wa Tunu na Sudi-hawanywi pombe.
   9. Yanaonyesha mabadiliko katika maisha ya wahisika. Sitia aliacha ulevi.
   10. Yanaonyesha mustakabali wa mgogoro kati ya Ngurumo na Majoka-hauishi.
   11. Yanaonyesha ufisadi wa Majoka na watu wake-wao huwanunulia vijana pombe haramu.
   12. Yanaibua taharuki. Tunu anawaalika katika mkutano. Si wazi ikiwa watu watahudhuria.
    Zozote 4x2=8
  4.      
   1. Msemaji ni Ngurumo.
   2. Ni mpenda starehe na anasa-anakunywa pombe kwa mama pima.
   3. Ni katili-ndiye aliyemvunja Tunu mguu.
   4. Mwenye mapuuza-anasema hana muda wa kupoteza.
   5. Mwenye kejeli-anamwambia Asiya kuwa siku hizi hatambui jina lake halisi…uk. 56
   6. Mwenye dharau-anaidharau familia ya Tunu. Anasema hawana wasifu wowote.
   7. Mjinga-anasema kuwa Sagamoyo ni pazuri tangu soko lilipofungwa ilhali watu wanaumia.
   8. Mkali/mwenye hasira-anawaamuru akina Sudi waondoke-uk 62
   9. Mpyaro-anamwambia Sudi kuwa ametia ndani ya kirinda na Tunu.
   10. Mwenye kumbukumbu nzuri-anaukumbuka wimbo wa Dauki Kabaka na kuuimba.
    Zozote 5x1=5
 6. SEHEMU D: USHAIRI
  1.      
   1. Mama alimshauri nafsi neni kuwa wanaume ni wanyama.
   2. Asiingilie anasa kwa kuwa amevunja ungo.
   3. Akijitia maringo atatungwa mimba.
   4. Hata wanaume waje na pesa, asiwakubali.
   5. Wakipiga magoti asiwakubali pia.
   6. Asifanye ngono; ni tendo la suna.
   7. Athamini elimu kwanza.
   8. Asizurure mitaani.
   9. Aende shuleni moja kwa moja akitoka shuleni.
   10. Asiende vichochoroni kuwaona wanaume.
   11. Awe msikivu, assize anayoambiwa.
   12. Atafunzwa mambo mengine kuhusu mapenzi atafunzwa.
   13. Aliwakataa kina Hamadi.
   14. Karisa alimpa ujauzito.
   15. Nafsi neni alifukuzwa shuleni.
   16. Karisa bado anasoma.
   17. Nafsi neni ni mjamzito; anajikuna upele.
    Zozote 5x1
  2.    
   1. Vina-ukara; vina vya kati havina urari; vya mwisho vina urari.
   2. Vipande; mathnawi; kila mshororo una vipande viwili.
   3. Tarbia; kila ubeti una mishororo mine.
    3x1=3
  3.      
   1. Inkisari – ngawa – ingawa
    taonywa – utaonywa
    umuhimu:kusawazisha mizani
   2. Tabdila – ukimbile – ukimbie
    usikile – usikie
    umuhimu: kuleta urari wa vina
   3. Kuboronga/kufinyanga/kubananga
   4. Ngono – ni tendo la suna, Amina sikimbilie
    Amina sikimbile ngono si tabia tendo la suna
   5. Kuzurura mitaani, si tabia njema ile
    Ile tabia ya kuzurura mitaani si njema
    Umuhimu: Kuleta mahadhi/kulipa shairi mapigo ya kimziki
    2x1=2
  4. Mama yake mshauriwa alama 1
   “Kama mamayo mzazi, nakuonya ukimbilie alama 1
  5. Uwe mwana anayesikia/msikivu wa kuzingatia yafuatayo /mambo kuhusu mapenzi utaonywa shuleni /lakini nikiwa mama yako mzazi ninakuonya kimbele ujihadhari na wanaume kwa sababu ni wanyama 4x1=4
  6.      
   1. Urudiaji wa vina-vina vya mwisho vimerudiwa(-le, ma)
   2. Urudiaji wa mishororo-lina kibwagizo; si watu waole vile, wanaume ni wanyama.
   3. Urudiaji wa maneno-neno mbele; 2:3, 3:2
  7.    
   1. Usifanye anasa/mapenzi
   2. Wanaume ni hatari/wanaweza kuharibu maisha yako
   3. Tufanye mapenzi
 7.    
  1.      
   1. lina beti
   2. kila ubeti lina mishororo ingawaje idadi inatofautiana katika kila ubeti
   3. lina mizani katika mishororo
   4. lina maneno machache
   5. lina kipande
   6. baadhi ya mishororo ina muwala
    4x1=4
  2. Fafanua toni ya utungo huu (alama 2)
   Toni ya kusihi- “nikumbuke mwanangu”
   Wosia/nasaha
   1x2=2
  3. Huku ukitoa mifano, linganua kati ya mistari toshelezi na mistari mishata
   Mistari toshelezi-mstari uliokamilika kimaana ilhali mstari mishata ni mstari usiokamilika kimaana
   Mfano wa mstari toshelezi-Nikumbuke mwangu,
   Mstari mishata-staftahi ya saa nane alasiri
   Kutofautisha=2
   Kuaja mifano=2
  4. Eleza maudhui yoyote matatu yanayojitokeza
   1. Umaskini- Mrejelewa na mamake walipitia maisha magumu hapo awali” kumbuka nyakati zile mimi ni mamako tulivyojidamka.
   2. Ukengeushi-anafurahia vitu vya kigeni-magari,saa
   3. Ajira-Anarauka asubuhi kwenda kazini
   4. Bidii-Anatia bidii kazini na kuweza kumiliki mali-volvo
    4x1=4
  5.      
   1. Lina beti sita
   2. Kila ubeti una mishororo tofauti
   3. Vina vyote si sawa.
   4. Lina mishata na mistari kifu.
   5. Mizani ni tofauti katika kila mishororo
    Zozote 4x1
 8. SEHEMU E: HADITHI FUPI
  1. Umuhimu wa Mazungumzo kati ya Sasa na Mbura katika Kujenga Hadithi ya Shibe Inatumaliza
   1. Yanaibua suala la ubadhirifu wa mali ya umma-jungu linateremshwa kwa gari la ikulu uk.39
   2. Ubinafsi na ulafi unajitokeza-wana vyao kisha pia ni wenye vyetu uk. 40
   3. Yanaonyesha namna viongozi wanavyoshiriki katika ubadhirifu wa mali ya umma. Sasa anamwambia mbura wawahi chakula/walijaza vyakula kwenye sahani zao.
   4. Yanaidhihirisha ufaafu wa anwani-Wanakula lakini hawashibi. Uk. 41
   5. Yanachimuza madhara ya kula sana-sukari, presha, saratani na kadhalika.
   6. Yanaonyesha umuhimu wa vyombo vya habari katika kukomesha hali ubadhirifu wa mali ya umma.-sasa alishtuka
   7. Yanaendeleza ploti ya hadithi-yanaibua masuala yanayoshughulikiwa katika hadithi. Swala la shibe kwa jumla.
    Zozote 5x2=10
  2. Namna Suala la Malezi Lilivyoshughulikiwa katika hadithi ya Tulipokutana Tena na Mtihani wa Maisha.
   Tulipokutana Tena
   1. Wazazi wa Bogoa wanayakwepa majukumu ya ulezi na kumpokeza Bogoa Bi. Sinai.
   2. Wazazi wa Bogoa wanashindwa kumudu mahitaji ya kumsingi kutokana na umaskini wao kv sabuni.
   3. Walezi wa watoto wanawadhulumu. Bi. Sinai anamtumikisha Bogoa; anamchoma.
   4. Walezi wanawabagua watoto; watoto wengine wanasoma ilhali Bogoa hapelekwi shuleni. Anachoma mandazi.
   5. Walezi wanawatisha watoto. Bi. Sinai anamwonya Bogoa dhidi ya kusema madhila aliyopitia mikononi mwake.
   6. Wazazi wanawadanganya watoto-Babake Bogoa anamdanganya kuwa angempeleka kwa marafiki zake ambao ni watu wazuri. Kumbe ni katili.-Bi. Sinai.
   7. Watoto wanatengwa na familia zao bila hiari yao-Bogoa analia san asana wanapotaka kumpeleka kwa marafiki zao lakini hasikizwi na wazazi. Uk. 114
   8. Baadhi ya wazazi wanawasomesha wanao. Kuna wanafunzi katika shule ambamo Bogoa aliuza mandazi.
    5x1=5

Mtihani wa Maisha

 1. Watoto wanapelekwa shuleni bila kubaguliwa. Babake Samueli anawasomesha ndugu zake wa kike. Pia Samweli anasomeshwa.
 2. Wazazi kuamini kuwa kufeli katika mtihani wa shuleni ni kufeli katika mtihani wa maisha. Kwa mfano babake Samueli anaamini alifeli mtihani. Anafaa kufa.
 3. Wazazi kuamini kuwa kusomesha mtoto wa kiume ndiko kunakoweza kuwakwamua kutoka katika lindi la umaskini. Babake Samueli anaamini kuwa kumsomesha Samweli kungemwopoa kutoka katik umaskini.
 4. Watoto kuwadanganya wazazi. Baba Samwuli haamini.
 5. Mama Samueli anamwonyesha mwanawe upendo. Hataki ajiue.
 6. Watoto wanafahamu hulka za wazazi wao. Samueli anajua mama angemwelewa ilhali baba angempiga kinyama kwa kufeli mtihani.
 7. Watoto wanashiriki katika mahusiano ya kiholela wakiwa shuleni. Samueli na Nina.
 8. Wazazi wanajaribu kila juhudi kuwasomesha watoto wao hata katika hali ya umaskini. Baba Samueli anauza takribani kila kitu kuwasomesha.

MUKHTASARI WA UTAHINI WA VITABU 2018-2021
HADITHI FUPI

MWAKA HADITHI VIPENGELE
2021  Masharti ya Kisasa( swali la 4)
 1. Muktadha(uk. 56)-4
 2. Toni ya dondoo-2
 3. Misumari ya nyuki kwa kurejelea hadithi-14
2021  Mame Bakari(swali la 5) Suala la uozo wa kijamii-10
2021  Ndoto ya Mashaka(swali la 5) Mchango wa wazazi katika maisha ya vijana-10
2020  Mwalimu Mstaafu (Swali la Lazima)
 1. Muktadha(uk. 121)-4
 2. Toni ya dondoo-2
 3. Namna Jairo Alivyokitia Kitumbua Mchanga-10
 4. Vipengele vya Kimtindo-4
2019  Nizikeni Papa Hapa Muktadha-4
Mbinu za kimtindo-2
Namna hadithi hii inavyohimiza uwajibikaji-6 
  Mapenzi ya Kifaurongo Umaskini-8
  Shogake Dada ana Ndevu Unafiki-12
Kuchanganua Mtindo-12
2018 Mkubwa
Kidege
Utabaka-12
Utabaka-8 
2018  Tumbo Lisiloshiba(swali la sita)
 1. Dondoo(uk.2)
 2. Tamathali za Usemi-alama 3
 3. Sifa za Mzee Mago-alama 5
 4. Namna Wanamadongoporomoka walivyolipukiwa na moto-alama 8


TAMTHILIA YA KIGOGO

MWAKA VIPENGELE
2021

Swali la lazima

 1.         
  1. Muktadha-alama 4, uk. 7
  2. vipengele vya kimtindo-2
  3. Sifa za Kombe-4
 2. kuzorota kwa maadili kunachangia kuzorota kwa mahusiano ya kijamii. 
2020

SWALI LA NNE

 1. Muktadha wa dondoo-4(uk. 92)
 2. Vipengele vya Kimtindo-4
 3. Umuhimu wa Asiya katika kujenga ploti na maudhui-12

SWALI LA TANO

 1. Mchango wa wasomi katika kuimarisha maisha ya Wanasagamoyo-10
 2. Umuhimu wa Mazungumzo kati ya Majoka na Daktari-10
2019

SWALI LA PILI

 1. Mbinu walizotumia Wanasagamoyo Kupigana na utawala dhalimu-10
 2. Namna mbinu rejeshi ilivyotumiwa kujenga wahusika na maudhui-10

SWALI LA TATU

 1. Dondoo-4(uk. 26)
 2. Dhima ya vipengele viwili vya Kimtindo-alama 4
 3. Sifa za Ashua-6
 4. Umuhimu wa Mandhari katika tamthilia hii-6
2018 

SWALI LA NNE

 1. Dondoo-4(uk. 5)
 2. Kinyume katika dondoo-16

SWALI LA TANO

 1. Dondoo(uk. 25)-umuhimu wa Ashua katika kujenga tamthilia-6
 2. Namna uongozi wa Majoka unavyoyazika matumaini ya Wanasagamoyo-14 


RIWAYA YA CHOZI LA HERI

MWAKA VIPENGELE
2021 Swali la Pili: nafasi ya mwanamke katika kuendeleza ukiukaji wa haki za kibinadamu-alama 20
Swali la tatu: kuchanganua mtindo katika dondoo(uk. 91) na umuhimu wa Cizarina na Tila(alama 10)
2020 SWALI LA PILI
Dondoo-4(uk. 153)
Aina za taswira-4
Vipengele vya kimtindo-4
Umuhimu wa mandhari katika kujenga riwaya kwa kurejelea kituo cha mwanzo mpya.
SWALI LA TATU
Kuchanganua mtindo-dondoo(uk. 181)-8
Mchango wa familia katika katika kuendeleza desturi za jamii(rejelea kisa cha Mwangeka, Mwangemi na Babu yao)
2019 SWALI LA LAZIMA
Dondoo-4(uk. 140)
Tamathali mbilI za usemi-2
Umuhimu wa Selume-6
Mikakati wanayotumia vijana kupambana na hali zao(rej. Chandachema na Dick)-8
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Mumias West Pre Mocks 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest