Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Bunamfan Cluster Pre Mock Exam 2022

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Jibu maswali manne pekee.
  • Swali la kwanza ni la lazima.
  • Maswali hayo mengine matatu yachaguliwe kutoka sehemu nne zilizobaki; yaani:
    Riwaya, Tamthilia, Hadithi Fupi na Fasihi Simulizi
  • Usijibu maswali mawili kutoka sehemu moja.
  • Majibu yote lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili


Maswali

SEHEMU A:
Ushairi

  1. Lazima

    Monyara
    Nakumbuka kwa dhiki Mto Monyara
    Tuliochelea kukaribia kingo zake
    Tukatulia kwanza; ukakamavu kujihamia
    Kwa kunyenyekea wingi wa yake maji
    Yaliyojiendea utadhani yamesimama.

    Ni katika mto huu
    Ambapo samaki wakubwa tulivua
    Maguo kuyatakasa japo kwa kunyemelea
    Na walevi stadi wakachelea kuuvuka
    Ulipofura na kupita kwa kiburi
    Kwa kushiba maji yake
    Yaliyofanya mawimbi madogo.

    Ni hapa ambapo marehemu nyanya
    Mkono alinishika na njia kuniongoza
    Juu ya ulalalo wa miti
    Vikapu vyetu hewani vikielea;
    Mimi nikishika changu kwa mkono mmoja
    Naye akikiachilia chake kujishikisha kichwani
    Masafa baina yetu na mtambo
    Uliokwenda kwa maji
    Tuliyapunguza kwa kila hatua tulopiga.

    Ni katika mto huu ambapo
    Samaki tuliowavua tuliwapasua na kuwasafisha
    Na hivyo kuuficha umaskini wetu
    Ulotuzuia kununua mnofu wa bucha
    Ni hapa ambapo wanawake walifika
    Mawe ya kusagia kupata
    Ni katika mto huu ambapo
    Waumini walifika kutakaswa kwa ubatizo
    Baada ya ulevi, uzinzi na kufuru nyinginezo.

    Ni hapa ambapo ilisimuliwa kuwa
    Hata wachawi walifika kufanya vitimbi vyao
    Baada ya utawala wa jua kumezwa na nguvu za giza
    Sasa Monyara nilioijua haipo tena
    Zimebaki kingo zilizokaukiana
    Kama uso wa mrembo aliyekosa mafuta
    Siku ayami.

    Mto huu ambapo pembeni mwake
    Watoto walipashwa tohara
    Maji yake yakishangilia, umekonda
    Na mbavu zake nje kutoa
    Na sasa vitoto vikembe vinazikanyaga
    Vikijiendea zao kusaga mahindi
    Juu mlimani
    Katika mtambo wa Kizungu
    Usioisha kulalamika
    Nao wanawake hawaji tena
    Kutafuta mawe ya kusagia wimbi
    Imebaki njia ya walevi warejeao nyumbani
    Nayo miti iliyosimama wima ukingoni
    Iliisha kuanguka kwa kuleweshwa na pumzi za walevi
    Wasioisha kupita hapa

    1. Onyesha umuhimu wa Mto Monyara kwa wanakijiji. (alama 4)
    2. Toa mifano ya mishata inavyojitokeza shairini. (alama 2)
    3. Eleza aina tatu za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
    4. Fafanua mtindo katika shairi hili. (alama 3)
    5. Tambua nafsi neni ya shairi hili. (alama 1)
    6. Jadili idhini ya kishairi katika shairi. (alama 3)
    7. Andika ubeti wa pili katika lugha nathari (alama 2)
    8. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)

SEHEMU YA B:
Riwaya: Chozi la Heri - Assumpta Matei

Jibu swali la 2 au 3

  1. “Wapo baadhi yetu ambao wizi unapotokea inasemekana wanashirikiana na wahalifu wenyewe na baadaye wanagawana ngawira nao!”
      1. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
      2. Jadili mtindo katika dondoo hili (alama 3)
      3. Eleza sifa za usemaji wa dondoo hili (alama 3)
    1. Ufisadi unaojadiliwa katika dondoo una madhara katika jamii ya Wahafidhina. Jadili. (alama 10)
  2.              
    1. Jadili mtindo kwenye dondoo hili. (alama 8)
      Jua linalochomoza halina ule wekundu wa jua la matlai ambao huleta haiba ya uzawa wa siku yenye matumaini. Naona wingu kubwa angani likitembea kwa kedi na madaha na kulifunika jua. Tukio hili linafuatwa na umeme, kisha mtutumo wa radi. Mawingu yaliyoshiba yakataka kutapika yanagooka, yanakaribiana, kupigana busu na kusababisha mwanguko wa matone mazito ya mvua; matone yanayoanguka kwenye ngozi laini za wanangu wakembe, Lime na Mwanaheri. Nawatazama kwa imani lakini siwezi kuwasaidia. Sina hata tambara duni la kuwafunikia. Linalobaki ni kumshuru Mungu kuwa tungali hai. Ubavuni mwangu amelala maskini mke wangu,Subira. Sijui kama inahalisi kumwita mke wangu kwani huyu siye Subira wangu wa zamani. Siye, siye, siye-e-e-e. Tazama uso wake ulivyovamiwa na majeraha, kikwi. Tazama tambo lake lililoumbuka. Amevimba na kuvimbiana kama dongo la unga ngano baada ya kutiwa hamira. Lakini yeye hana la hamira! Haya ni matokeo ya ubahaimu wa binadamu. Kwa mbali namwona Ridhaa – mwamu hasa – akitafuna kitu fulani, nadhani ni mzizimwitu. Ridhaa, kweli Ridhaa kula mzizi! Daktari mzima! Mkurugenzi mzima wa Wakfu wa Matibabu nchini! Wanasema wajuao kuwa simba akikosa nyama hula nyasi. Msafiri kafiri ati! Amekosa la maama, hili la mbwa ataliamwa!
    2.  “Huyu hapa ni Bwana Mwangemi na huyu hapa ni Bi Neema. Kama nilivyokujuza hapo awali, wamekuja kuchukukua kwenda kuishi nao kama mwana wao.”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Banaisha mtindo katika dondoo. (alama 3)
      3. Toa sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 5)

SEHEMU YA C
Tamthilia: Kigogo - Pauline Kea

Jibu swali 4 au 5

  1. Mwandishi wa tamthilia ya Kigogo amefanikiwa katika kutumia ishara ili kufanikisha maudhui. (alama 20)
  2. Mimi sili makombo kama kelbu! Nilishakunywa chai ya mke wangu nikaridhika.”
    1. Eleza mkutadha wa dondoo hili. (alama 4)
    2. Fafanua mtindo katika dondoo hili. (alama 4)
    3. Jadili vile Wanasagomoyo wamefanywa kelbu kula makombo (alama 12)

SEHEMU D
Hadithi Fupi: Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine - Chokocho Na D. Kayanda:
Jibu swali la 6 au 7

  1.        
    1. Tathmini umuhimu wa Samueli Matandiko Katika kuijenga hadithi, “Mtihani wa Maisha” (alama 10)
    2. Fafanua shibe inavyomaliza Waafrika katika hadithi ya “Shibe Inatumaliza”. (alama 10)
      “Tulipokutana Tena” - Alifa Chokocho.
  2.   
    1. ‘Jijini ni kuzuri. Kuna majumba makubwa, utapanda magari mazuri mazuri ya marafiki zetu, utakula vyakula vitamu na kupewa nguo za fahari. Utapelekwa shule kusoma na kwandika.’
      1. Jadili muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
      2. Eleza taswira zinazojitokeza katika dondoo hili kwa kutoa mifano. (alama 3)
      3. Aliyoambiwa msemewa ni kinyume cha yaliyotokea. Eleza. (alama 8)
    2. Wahusika mbalimbali katika hadithi hii wanatumia njia nyingi kukabiliana na matatizo yanayowakumba. Zijadili. (alama 5)

SEHEMU YA E
Fasihi Simulizi

  1. Malaika …..
    Nakupenda malaika x 2
    Ningekuoa mali we…..
    Ningekuoa dada…..
    Nashindwa na mali sina we…..
    Ningekuoa malaika x 2
    Pesa, zasumbua roho yangu x 2
    Nami nifanyeje, kijana mwenzio
    Nashindwa na mali sina we
    Ningekuoa malaika x 2

    1. Tambua utungo huu. (alama 2)
    2. Toa sababu za jibu lako hapo juu (alama 2)
    3. Taja shughuli ya kijamii na shughuli ya kiuchumi inayodokezwa kwenye kipera hiki. (alama 2)
    4. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa. (alama 2)
    5. Jadili vipi mwasilishji wa kipera hiki anaweza kuboresha wasilisho lake.(alama 6)
    6. Ni matatizo yapi yanayoweza kumkumbuka mkusanyaji wa kipera hiki nyanjani? (alama 6)


Mwongozo wa Kusahihisha

  1.          
    1. Onyesha umuhimu wa Mto Monyara kwa wanakijiji. (alama 4)
      1. Kuvua samaki ambao watatumiwa kama kitoweo;
      2. Nguo zilioshewa humo;
      3. Maji yake yaliendesha mtambo, kinu cha kusagia unga;
      4. Mawe ya wanawake ya kusagia waliyapata humo;
      5. Waumini walibatizwa/walitakaswa katika maji ya mto huo baada ya dhambi za ulevi na uzinzi;
      6. Wachawi waliutumia kufanya vitimbi vyao;
      7. Watoto walipashwa tohara kando yake, maji yalishangilia waliopashwa tohara
        (Hoja zozote 4x1= alama 4)
    2. Toa mifano ya mishata inavyojitokeza shairini. (alama 2)
      Mshororo usiokamilika, unakamilikia katika ule unaofuata.
      Ni katika mto huu ambapo
      Ni hapa ambapo ilisimuliwa kuwa
      (zozozte 2x1=alama2)
      Tathmini jibu la mwanafunzi
    3. Eleza aina tatu za taswira zinazojitokeza katika shairi hili. (alama 3)
      1. Taswira mwendo: kuenda ka maji, kuuvuka mto, vitoto kuenda kusaga mahindi;
      2. Taswaira mguso: Mikono ya nyanya na msimulizi kushikana.
      3. Taswira mwono: maji kusimama, vikabu kichwani na mkononi.
        (za kwanza 3x1=3)
    4. Fafanua mtindo katika shairi hili. (alama 3)
      1. Mbinu rejeshi: kumbukumbu za hali ya awali yam to Monyara;
      2. Tashihisi: mto ulipita kwa kiburi na ulishida maji yake; mto umekonda na kutoa mbavu zake nje;
      3. Taswira: msimulizi na nyanya tunawaona wakishikana mikono wakivuka mto kwa kupita juu ya ulalo wa miti;
      4. Tashibihi: maji yalijiendea utadhani yamesimama,
      5. Utohozi: bucha;
    5. Tambua nafsi neni ya shairi hili. (alama 1)
      1. Mjukuu;
      2. Msimulizi
        (Hoja1x1=1)
    6. Jadili idhini ya kishairi katika shairi. (alama 3)
      1. Inkisari: tulopiga- tuliyopiga Ulotuzuia-uliotuzuia;
      2. Kuboronga msamiati: Miundo mibaya ya sentensi, mfano, ukakamavu kujihamia- kujihami na ukakamavu, Mawe ya kusagia kupata – Kupata mawe ya kusagia
      3. Mazda: kujihamia- kujihami
      4. Utohozi: Bucha
        (zozote 3x1=alama3)
    7. Andika ubeti wa pili katika lugha nathari (alama 2)
      1. Msimulizi anaeleza kuwa walivua samaki wakubwa katika Mto Monyara kabla haujakauka. Kwa kuwa maji ya mtohuo yalikuwa mengi kutokana na kufurika, waliogopa kuoshea nguo ndani yake na hivyo wakazioshea kando. Walevi waliokunywa pombe ng’ambo ya pili waliporejea makwao, waliogopa kuuvuka kutokana na wingi wa maji yake. Mto ulipofurika ulifanya mawimbi kidogo kuonyesha maji yalikuwa ya kina kirefu.
        (Zozote 4x12)
    8. Eleza toni ya shairi hili. (alama 2)
      1. Toni ya kutamauka/kukata tamaa- Mto Monyara uliowapa wenyeji matumaini ya maisha mema sasa hauko, umekauka

  2. “Wapo baadhi yetu ambao wizi unapotokea inasemekana wanashirikiana na wahalifu wenyewe na baadaye wanagawana ngawira nao!”
    1.   
      1. Fafanua muktadha wa dondoo hili (alama 4)
        Msemaji: Rachel Apondi;
        Wasemewa: vikosi vya usalama/walinda usalama;
        Mahali: Warsha;
        Kuhusu: jukumu la vikosi vya usalama, amani na maridhiano. Alikuwa akiwasuta walinda usalama ambao wanatumia ushawishi/mamlaka yao kujitajirisha kwa njia za kifisadi.)
        (Zote 4x1=alama4)
      2. Jadili mtindo katika dondoo hili (alama 3)
        1. Kinaya: Haitarajiwi walinda usalama kushirikiana na wezi kuiba na kisha kugawana ngawira;
        2. Nidaa: wanagawana ngawira nao!
        3. Nahau/msemo:wanagawana ngawira
      3. Eleza sifa za usemaji wa dondoo hili (alama 3)
        1. Mwenye bidii: analea Sophie kwa juhudi;
        2. Msomi: Anafunza warsha;
        3. Mkarimu: anamkaribisha Umu. Aidha, anapokutana na Mwangeka kwa mara ya kwanza anamzungumzia vyema;
        4. Mwajibikaji: anaishughulikia familia vilivyo.
          (zozote 3x1)
    2. Ufisadi unaojadiliwa katika dondoo una madhara katika jamii ya Wahafidhina. Jadili. (alama 10)
      1. Unasababisha uharibifu wa mali. Majumba makubwa ya mabwanyenye akiwemo Ridhaa yaliyojengwa kwenye arhi iliyotengewa ujenzi wa barabara yanabomolewa;
      2. Baadhi ya familia zinaachwa bila makao baaa ya majumba kwenye mtaa wa Tononokeni kubomolewa ili kupanua barabara;
      3. Unapelekea viongozi wabaya pale vijana kama aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitman’ wanapohongwa kuchaguliwa ili kusaidia kuiba kura;
      4. Hupelekea umaskinishaji kwa vile mashamba madogomadogo yananyakuliwa na mabwanyenye wenye wenye mahsamba makubwa kwa mujibu wa kijana aliyevalia shati lililoandikwa ‘Hitman’;
      5. Kupanuka kwa mwanya kati ya matajiri na maskini/huzidisha utabaka kwani mabwanyenye wananyakua ardhi ya maskini na kujenga viwanda na maduka ya kibiashara huku maskini wakibaki bila ardhi, kwa mujibu wa kijana aliyevalia shati lililoandikwa’Hitman’;
      6. Inasababisha ubadhirifu wa pesa za umma kwani serikali inabuni tume za kuchunguza ufisadi na ripoti zenyewe hazionekani;
      7. Kufutwa kazi kwa watetezi wa haki,mfano Lunga na Shamsi wanafutwa kazi kwa kugoma;
      8. Unasababisha mahindi yaliyo hatari kwa usalama wa raia kuletwa nchini;
      9. Uharibifu wa mazingira/misitu-matrekta ya viongozi yanabeba shehena za mbao, makaa na mahindi kutoka kwenye msitu wa Mamba usiku wa manane;
      10. Uhamisho wa lazima-viongozi wanawahamisha wananchi kutoka kwenye msitu wa Mamba ili wapate mwanya wa kunyakua malia mbayo tayari walikuwa wamezalisha;
      11. Bei ya samaki kupanda hasa kufuatia nani kamiliki Ziwa Kuu. Huku kunawafanya wananchi kununua bidhaa hii kwa bei ghali kwa mujibu wa Kairu;
      12. Ukiritimba: ni watu wachache wanaouza samaki kutokana na bei ya samaki kupanda maradufu;
      13. Ongezeko la wizi/ukosefu wa usalama-polisi wanaposhirikiana na wezi kuiba na kisha kugawana ngawira;
      14. Kuvunjwa kwa sheria za barabarani: polisi wenye madaraka wanapoacha magari yao makuukuu barabarani kwa kutumia ushawishi wao;
      15. Huduma mbovu/duni za afya kwa vile dawa zilizopaswa kuwatibu watu hospitalini zinaibwa na kupelekwa katika maduka ya wasimamizi wa hospitali;
      16. Unywaji wa pombe haramu-watoto wa maskini wanajiingiza katika unywaji wa pombe haramu wanapokosa mikopo na ruzuku inapotolewa kwa wanaojiweza;
      17. Ulanguzi wa dawa zakulevya-wanafunzi kutoka familia maskini wanapokosa mikopo ya ruzuku, kwa vile inatolewa kwa watoto matajiri,wanajiingiza katika ulanguzi wa dawa za kulevya ili kujipurukusha na hali duni ya masomo chuoni. Buda analainisha viganja vya maofisa wa forodha ili kueneleza ubebaji fafina;
      18. Utamaushi- shamsi anapoteza matumaini anapokosa ajira kwa vile nafasi za ajira hutolewa kwa mapendeleo(kwa jamaa), kinasaba;
      19. Vifo- wanafunzi wa shahada ya uzamili wanakufa kutokana na unywaji wa dengelua wanapokosa mikopo na ruzuku inayotolewa kwa mapendeleo kwa wanafunzi wanaojiweza;
      20. Husababisha ubaguzi kwa sababu nafasi za ajira zinatolewa kwa mapendeleo kwa wanafunzi wanaojiweza. Shamsi anakosa ajira kwa sababu hii;
      21. Dhiki za kisaikolojia-Dick anatatizika kisaikolojia Buda anapotishia kumfisha kama hatalangua mihadharati;
      22. Hupandisha tamaa na ubinafsi- lunga anabadili nia yake ya kuhifadhi mazingira na kuanza kukata miti punde tu anapostaafishwa;
      23. Husababisha ulanguzi wa binaamu- Sauna na Bi Kangara wanashirikiana na wajasiriamali kulangua na kuuza watoto ughaibuni;
      24. Husababisha ufuska- Bi Kangara na Sauna wanawauza watoto wa kike katika madanguro wanakoendelezea ufuska;
      25. Husababisha adhabu hafifu kwa wavunja sheria- badala ya Fumba kuachishwa kazi anarudishwa kazini na kupewa uhamisho anapofanya mapenzi na kumtia ujauzito mwanafunzi wake, Rehema;
      26. Upofu- walevi wanaokunywa dengelua ya vijasumu wanapofuka, kulingana na Shamsi.
      27. Ulaghai/utapeli- Sauna anauza maji ya mito na madimbwi anayoyatia kwenye chupa za vibandiko vya mineral water;
      28. Watu kupoteza pesa baada ya kuuza vipande vya ardhi vilivyotengewa makaburi.
        (zozote 13x1=alama 13)
  3.         
    1. Jadili mtindo kwenye dondoo hili. (alama 8)
      1. Taswira oni:jua linalochomoza halina ule wekundu;
      2. Nahau/msemo: wanangu wakembe, majeraha kikwi;
      3. Ishara: wingu kubwa angani, umeme, mtutumo;
      4. Tashihisi: mawingu kupiga busu, mawingu kushiba;
      5. Takriri: siye, siye;
      6. Tashibihi: kuvimbiana kama donge la unga ngano;
      7. Nidaa: mzizi! Daktari mzima! Chini!
      8. Methali/mdokezo wa methali: samba akikosa nyama hula nyasi, Msafiri kafiri ati,amekosa la mama, hili la mbwa ataliamwa;
      9. Mbinu rejeshi; Kifungu chote ni usimulizi wa yaliyotokea.
        (zozote 8x1)
    2. “Huyu hapa ni Bwana Mwangemi na huyu hapa ni Bi Neema. Kama nilivyokujuza hapo awali, wamekuja kuchukukua kwenda kuishi nao kama mwana wao.”
      1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
        1. Msemaji: + Mwale;
        2. Msemewa: Mwaliko;
        3. Mahali: Kituo cha Benefactor;
        4. Kinachotokea: Anamweleza Mwaliko kuwa atapangwa na Neema na Mwangemi
          (zozote 4x1= alama 4)
      2. Banaisha mtindo katika dondoo. (alama 3)
        1. Uashiriaji/uigizaji: Huyu hapa ni Mwangemi na huyu hapa ni Neema’
        2. Tashibihi: Kuishi nao kama mwanawao;
        3. Mbinu rejeshi: kama nilivyokujuza hapo awali;
        4. Takriri: ‘Huyu hapa’ imerudiwa.
          (zozote 3x2=alama 6)
      3. Toa sifa za msemaji wa dondoo hili. (alama 5)
        Sifa za Anastacia Mwale:
        1. Mwajibikaji: atamtembelea Mwaliko mara kwa mara ajue vile anaendelea;
        2. Mkarimu: Anamkaribisha Mwangemi Neema;
        3. Mpenda utaratibu: atayarishia Mwangemi stakabahi asmi za kupanga motto huyu;
        4. Ana kumbukumbu nzuri: anakumbuka maelezo ya Mwaliko alimpatia;
        5. Mwenye mlahaka mwema: anawakaribisha kina Mwangemi.
          (zozote 5x1= alama 5)
  4. Mwandishi wa tamthilia ya Kigogo amefanikiwa katika kutumia ishara ili kufanikisha maudhui. (alama 20)
    1. Fimbo ya Kenga yenye kichwa cha nyoka ni ishara ya jinsi alivyokuwa katili kwa raia;
    2. Kitendo cha Majoka cha kuzungumza na babu yake anapozirai ni ishara kuwa wafu walikuwa wakimwita madhali ndiye aliyekuwa amewaua;
    3. Majoka kuvaa mkufu shingoni wenye kidani cha umbo la swila ni ishara ya namna Majoka alivyokua hatari kwa maisha ya raia wa jimbo la Sagamoyo.
    4. Kilio na machozi mengi ndani ya ziwa lililofunika damu ni ishara ya raia waliouliwa na Majoka wanalilia hali yao.
    5. Kutojaa kwa raia ilivyo kawaida katika mkutano wa kudumisha sherehe za uhuru pamoja na sikub ya kuzaliwa kwa Majoka ni ishara ya raia kuasi Majoka kutokana na uongozi wake dhalimu.
    6. Hali ya Majoka kujiona ndani ya ziwa lililofurika damu ni ishara ya mauaji mengi ya raia aliyokuwa akitekeleza katika uongozi wake.
    7. Damu ya Jabali anayoiona Majoka ikitiririka mikononi mwake akiwa amezirai ni ishari kuwa ndiye aliyemuua Jabali;
    8. Bastola ya Majoka (uk 38) silaha au chombo cha kuwatishia watawaliwa na watetzi wa maovu ya kiongozi yanayopendezwa.
    9. Chai ya maziwa (uk 31)kinywaji cha watu wenye mapato mazuri tabaka la juu.
    10. Chai ya mkandaa-kinywaji cha watu maskiniinaonyesha utabaka.
    11. Nyoka (uk 31) huashiria ushirikina na ukatili wa Majoka.
    12. Chombo cha safari ya angani (uk 30)huashiria uongozi au madaraka.Majoka ni mojawapo wa marubaini (babu,uk 80)yaani yeye ndiye kiongozi ambaye huwalaghai anawaongoza.
    13. Embe lililoiva kupitia kiasi (uk1)ni ishara ya kuzorota kwa uchumi wa Sagamoyo.
    14. Gari la kifahari (uk 8)Hali ya utajiri wa kupindukia wa viongozi na ubepari pia utamaduni wa kizungu.
    15. Hoteli za kifahari (uk 67) huashiria starehe ya tabaka la juu.
    16. Kinyago (uk 10) huashiria hali ya viongozi kupenda uluwa;hali ya viongozi kupenda makuu kwa kutaka majina ya watu wa mbani zao yazaidi kusifiwa milele kwa kuwa walipigania uhuru.
    17. Kiti cha fahari(uk 19)huashiria tabaka la juu kiuchumi,tabaka lenye starehe kutokana na utajiri wake.
    18. Mbuyu (uk 15) Mbuyu ni makao ya shetani kwa hivyo matumizi yake huashiria dhuluma za kiongozi.Kenya anawahutubia wahni dhini ya mbuyu.
    19. Mkufu wenye kidani cha umbo la swila (uk19)ni nembo ya uongozi wa kadhalimu ,pia isahara ya ushirikina.
    20. Ndoto ya Tunu(uk 53)ufunuo wa madhila ya wapiganaji/wanajamii wakati wa uongozi uliopita wa babake Majoka,Marara na bin Ngao.
    21. Pombe ni ishara ya utovu wa maadili ya jamii.
    22. Kukauka kwa mito na maziwa ni ishara ya kuisha kwa ushawishi wa Majoka katika Sagamoyo.
    23. Redio (uk 3)huashiria maendeleo ya kitenolojia yanayotumiwa na viongozi kujikuza wenyewe.
    24. Rununu (uk 3) ishara ya maendeleo katika uwanja wa mawasiliano.Ni kinaya kwa sababu hatuoni maendeleo haya ya kimawasiliano yakichangia kuiboresha hali ya maisha ya ,mwaananchi wa kawaida.
    25. Soko chafu kuashiria ishara ya uozo wa kimaadili wa kisiasa.
    26. Sumu ya nyoka (uk4) kuashiria dawa za kulevya na masaibu yanayotokana na masaibu ya wafanyikazi wa tabaka la chini yanayotokana na kunyanyaswa na viongozi au wajiri katili.
    27. Maziara kujaa ishara ya mauaji ya watuchini ya watu chini ya utawala wa Majoka. (zozote 10x2=alama 20)
  5. Mimi sili makombo kama kelbu! Nilishakunywa chai ya mke wangu nikaridhika.”
    1. Eleza mkutadha wa dondoo hili. (alama 4)
      1. Msemaji: Sudi;
      2. Msemewa: Boza na Kombe;
      3. Mahali: Karakana ya uchongaji katika soko la Chapakazi;
      4. Kiini: Sudi alisusia makombo ya keki iliyoletwa na Kenga kwa kuwa alijua alikokuwa keki kubwa.
        (zote 4x1=alama 4)
    2. Fafanua mtindo katika dondoo hili. (alama 4)
      1. Tashibihi: makombo ya kelbu;
      2. Nidaa: Mimi sili makombo kama kelbu!
      3. Jazanda: makombo, kelbu, chai;
      4. Mbinu rejeshi: Nilishakunywa chai ya mke wangu nikaridhika
    3. Jadili vile Wanasagomoyo wamefanywa kelbu kula makombo (alama 12)
      1. Wanasaamoyo wanafungiwa soko ambalo lilikuwa tegemeo adimu kwao;
      2. Wanasagamoyo wanapandishiwa bei ya bidhaa katika kioski ya soko;
      3. Vijana wanauawa wakati wa migomo;
      4. Wanasaga wanafungiwa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii;
      5. Wanasaga wanarushiwa vijikaratasi ili wahame Saga, mfano Siti na Kombe;
      6. Walimu na madaktari wanaongezewa mshahara na kupandishiwa kodi;
      7. Majoka ananyakua ardhi ya Wasaga na kujenga hoteli ya kifahari;
      8. Majoka anawaaawia vikaragosi wake ardhi ya Wanasaga mfano Kenga.
      9. Majoka anafungulia biashara ya ukataji miti na kuwafanya Wasaga kukosa maji kwa sababu mito na maziwa imekauka;
      10. Wanasagamoyo wanakufa na kupofuka kutokana na kubugia pombe haramu aliyoigema Asiya baada ya kupewa kibali kuigema;
      11. Majoka anawatuma wahuni kumuumiza na kumvunja muundi Tunu;
      12. Majoka anaagiza Ngurumo azikwe juu ya miili mingine akidai kimba ni kimba tu;
      13. Wanafunzi katika shule ya Majoka wanadungwa sumu ya nyoka na kuwa makabeji;
      14. Ashua anafungwa bila hatia;
      15. Wanasagamoyo wanaomfanyia kazi katika Majoka katika kampuni yake hawalipiwi bima;
      16. Majoka anawatusi Wasaga wanapokataa kwenda mkutano wake ikuluni;
      17. Majoka kuwakutanisha Ashua na Husda na kuwapiganisha katika ofisi yaumma.
      18. Mwanafunzi aonyeshe jinsi Wanasagamoyo wameteseka , wamedharauliwa, kukandamizwa au kudhalilishwa.
        (zozote 12x1=alama 12)
  6.            
    1. Tathmini umuhimu wa Samueli Matandiko Katika kuijenga hadithi, “Mtihani wa Maisha” (alama 10)
      1. Samueli anachimuza maudhui ya elimu,anaendea matokeo yake shule yakushtua;
      2. Anaendeleza maudhui ya ubabedume,kupitia kwake baba haoni umuhimu wa kumfunza;
      3. Anajenga maudhui ya ndoa au familia,wazazi wake wanampa elimu sawa na dadazake;
      4. Samueli anachimuza maudhui ya ya bidii kwenye hadithi.aliamka asubuhi na kutembea kilomita sita hadi shuleni na kurudi;
      5. Samueli anajenga sifa za wahusika wegine,mfano mama ni mwenye ukarimu,upendo;
      6. Anasuka ploti kwa kudokeza walikofumea mwajuma na hivyo kubadilisha mkondo wa usimulizi;
      7. Kupitia kwa Samueli tunaona baadi ya wanafunzi wanajihusisha na mizaha wakiwa shuleni jambo ambalo linapelekea kufuli kwao;
      8. Samueli anajihusisha na mahusiano akiwa shuleni,Nina ni mpenzi wake;
      9. Babake Samueli anawajibikia familia yake kwa kulipia Samueli na dadake karo;
      10. Sifa ya uwajibikaji imejitokeza kwa mama samueli anapompikia chakula na kumpa chajio.
        (zozote 10x1= alama 10)
    2. Fafanua shibe inavyomaliza Waafrika katika hadithi ya “Shibe Inatumaliza”. (alama 10)
      1. Magonjwa kama presha, obesity, saratani yanawakumba kutokana na uongozi mbaya;
      2. Kuuwana kwa mabomu, risasi, kunyongana;
      3. Mzee Mambo kutumia runinga ya Taifa kutangaza sherehe yake ya binafsi;
      4. Dj kupata huduma za kimsingi kama maji ilhali wananchi hawana;
      5. Dj anatumia sherehe kuchota mabilioni ya pesa pzmoja na viongozi wengine;
      6. Sasa na Mbura, ni mawaziri wawili wa wizara moja ya Mipango na Mipangilio;
      7. Mzee Mambo kupokea mshahara ilhali hafanyi kazi yoyote;
      8. Magari ya umma kubeba jamaa wa Mambo;
      9. Chakula cha sherehe kinapikiwa ikulu;
      10. Ukoloni mamboleo- mchele wa basmati;
      11. Dj kumiliki duka la dawa ambalo mtaji wake ni bohari kuu;
        (zozote 5x2=alama 10)
  7.          
    1. ‘Jijini ni kuzuri. Kuna majumba makubwa, utapanda magari mazuri mazuri ya marafiki zetu, utakula vyakula vitamu na kupewa nguo za fahari. Utapelekwa shule kusoma na kwandika.’
      1. Jadili muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
        1. Haya msemaji ni Babake Bogoa;
        2. Wanaoambiwa ni kina Sebu, Kazu,Temu, Tunu na Sakina;
        3. Wako Club Pogopogo;
        4. Bogoa anawasimulia kadhia iiliyowafika anapotolewa kwao.
          (zote 4x1=alama4)
      2. Eleza taswira zinazojitokeza katika dondoo hili kwa kutoa mifano. (alama 3)
        1. Taswira oni: majumba makubwa makubwa;
        2. Taswira mwonjo: utakula vyakula vitamu;
        3. Taswira mwendo: utapelekwa shule…
          (zozote 3x1=alama 3)
      3. Aliyoambiwa msemewa ni kinyume cha yaliyotokea. Eleza. (alama 8)
        Masaibu ya Bogoa
        1. Kula kutoka kwa vigae/sufuria wengine wakila kwa sahani;
        2. Kuchomwa kwa kijinga alipokuwa akioka maandazi akalala yakaungua;
        3. Kukatazwa asiende kwa shule kama watoto wengine;
        4. Kunyimwa ushirika na watoto wa Bi Sinai, wasicheze pamoja;
        5. Kukatazwa asiende kwa kina Sebu kucheza;
        6. Kufanyishwa kazi ngumu kama kuchanja kuni, kuteka maji, kufua;
        7. Kuchapwa sana alipochelewa kurudi;
        8. Kutishiwa kukatwa ulimi iwapo angesema kwa yeyote yaliyojiri humo nyumbani;
        9. Kunyimwa ushirika na wazazi wake walipokuja kumwona;
        10. Kulazimika kuamka mapema akiwa mtoto mdogo;
        11. Kula makoko ya vyakula au makombo.
          (zozote 8x1= alama 8)
    2. Wahusika mbalimbali katika hadithi hii wanatumia njia nyingi kukabiliana na matatizo yanayowakumba. Zijadili. (alama 5)
      1. Bogoa anapelekwa kulelewa na Bi Sinai kwa sababu ya umaskini;
      2. Bogoa kuweka siri ya kutoroka kwake hata hakumwambia rafikiye Sebu;
      3. Kuhama kwa Bi Sinai kwa Bogoa ni njia moja anakabiliana na tatizo;
      4. Bogoa kumwaga dukuduku lake kwa kuwahadithia marafiki wake yale yaliyomfika kwa Sinai;
      5. Bogoa kutia bidii katika maisha kwa sababu yeye ni sonara huko Tinya;
      6. Bogoa alioa Sakina ili amwondolee upweke huko Tinya;
      7. Kusamehe wazazi wake na mlezi wake Bi Sinai;
      8. Sebu na mkewe Tunu wanatembelea marafiki zao, Kazu na Temu ili kuongea,
        (zozote 5x1 =alama 5)
  8.   
    1. Tambua utungo huu. (alama 2)
      • Wimbo au
      • Wimbo wa mapenzi
        (Hoja 1x2=alama2)
    2. Toa sababu za jibu lako hapo juu (alama 2)
      1. Matumizi ya lugha ya mkato na ya kuvuta: mali we…
      2. Urudiaji wa vipande: ningekuoa malaika x2
      3. Uwepo wa beti
      4. Kuna kiitikio
        (Zozote 2x2=alama 4)
    3. Taja shughuli ya kijamii na shughuli ya kiuchumi inayodokezwa kwenye kipera hiki. (alama 2)
      1. Shughuli ya kijamii: kuoa/ndoa
      2. Shughuli ya kiuchumi: ulipaji mahari
        (Zote 2x1=alama 2)
    4. Tambua nafsi neni na nafsi nenewa. (alama 2)
      Nafsineni: kijana anayetaka kuoa
      Nafsinenewa: msichana anayechumbiwa.
    5. Jadili vipi mwasilishaji wa kipera hiki anaweza kuboresha wasilisho lake.(alama 6)
    6. Kupandisha na kushusha sauti;
    7. Matumizi ya viziada lugha;
    8. Uwa mfaraguzi;
    9. Kubadilisha kiimbo na toni kulingana na hali;
    10. Awe jasiri ili aweze kuimba bila aibu;atumie maleba yafaayo kuwasilisha ujumbe
      (zozote 3x2=alama 6)
    11. Ni matatizo yapi yanayoweza kumkumbuka mkusanyaji wa kipera hiki nyanjani? (alama 6)
      1. Gharama za utafiti ni ghali, mfano kununua vifaa kama tepurekoa;
      2. Kupotea au kufisidiwa vifaa vya kuhifahi data;
      3. Ukosefu wa wakati wa kutosha wa kufanyia utafiti;
      4. Vikwazo kutoka kwa watawala – kunyimwa nafasi;
      5. Matatizo ya mawasiliano na uchukuzi – magari;
      6. Matatizo ya kibinafsi mfano kushinwa kudhibiti wahojiwa;
      7. Ukosefu wa usalama, mfano kuvamiwa.
        (zozote 2x3 = alama 6)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Bunamfan Cluster Pre Mock Exam 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest