Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Serikali ya Kenya kupitia Wizara ya Elimu imeanzisha mfumo mpya wa elimu ya Umilisi. Mwandikie mhariri wa gazeti la Darubini ukitoa maoni yako kuhusu changamoto zinazotokana na mfumo huu.
 2. Utelekezaji wa mtoto wa kiume nchini ni janga kuu. Jadili
 3. Tunga kisa kitakachodhihirisha maana ya methali ifuatayo.
  ``Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe’’
 4. Anza kwa kifungu kifuatacho.
  ......Hapo ndipo iliponibainikia kuwa nilikuwa nikiogelea baharini pekee kinyume na wenzangu wote. (alama 20)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 

Swali 1
Changamoto za mfumo wa umilisi (CBC)

 1. Walimu wengi wangali wanatatizika jinsi ya kuendeleza mafunzo hayo kwa wanafunzi.
 2. Mtaala wa CBC unawahitaji wanafunzi watumie asilimia kubwa ya muda uliotengewa somo wakijifunza kwa vitendo wakiwa pamoja hivyo muda mwingi hupotezwa
 3. Changamoto nyingine ni ile ya kutathmini kazi ya kila mwanafunzi katika kila kipindi. Wakufunzi wanashindwa kutekeleza hilo kwani muda ulioratibiwa kwa somo unaonekana mfupi kuliko mafunzo yanayohitajika kukamilishwa.
 4. Masomo kama vile muziki, sanaa ya uchoraji, somo la kilimo na mengine ambayo yanatoa changamoto nyingi kwa walimu kwani hawajazoea kuyafunza.
 5. Aidha mbinu zinazopendekezwa kutumiwa na walimu ni ngeni na walimu hawana uzoefu wa kutosha.
 6. Mtaala huu ni ghali mno na unaegemea sana vifaa halisi vya kufunzia.
 7. Baaadhi ya wazazi hawajasoma. Hawana uwezo wa kuwasaidia wanao.
 8. Wazazi wanaona kama usumbufu kuambiwa wagharamie vifaa vya kufundishia kila mara.
 9. Kazi nyingi ya mtaala huu imeachiwa wazazi.
 10. Shule za mjini ambako hakuna shamba zimekabiliwa na changamoto ya ufunzaji wa somo la kilimo.
 11. Masomo ni mengi zaidi takribani kumi na matatu kwa mwanafunzi wa gredi ya nne. Kuna mzigo mkubwa sana kwa watoto hawa.
 12. Itakuwa vigumu sana kukadiria viwango vya kufuzu kutoka darasa moja hadi jingine.
 13. Katika kuanzisha mtaala huu raia hawakutayarishwa kupitia vikao vya umma.
 14. Wazazi wengi hawana vifaa kama simu zenye uwezo wa kuchukua picha katika baaadhi ya vipindi ili kuvipeperusha mtandaoni.
 15. Uchache au uhaba wa vitabu katika masomo mbalimbali.
 16. Idadi kubwa ya wanafunzi katika madarasa ni changamoto kwa walimu wanaoutekeleza mtaala huu.
 17. Kuna uhaba wa madarasa yenye mazingira au vifaa vinavyofaaa kufunzia mtaala huu. Mf.

Swali 2.
Utelekezaji wa mtoto wa kiume nchini ni janga kuu. Jadili
Baadhi ya hoja tarajiwa ni:

 • Kukosa waelekezi.
 • Kuwachwa kujikidhi pekee
 • Kutopigiwa debe kama msichaa
 • Kutwi kwa majukumu angali machanga
 • Kutowajali, hawana mashirika ya ufadhili
 • Vyama vya kupigania mvulana kutowajibika
 • Kunyimwa nafasi ya masomo mf. Gredi ya kujiunga na kozi mbalimbali hupendelea msichana. Pia baadhi ya hukashifiwa kufanya baadhi ya kozi kwa kunasibishwa na jinsia ya kike.
 • Kukosa mashirika ya utafiti kuhusu wavulana.
 • Wanaume kupewa kazi ngumu kuliko wanawake.
 • Kutojali usalama wa mtoto wa kiume. Mfano anapotumwa sokoni hakuna anayejali hata akichelewa ambayo ni kinyume na mtoto wa kike.
 • Kukosa Malezi/maelekezi ya Baba hivyo kutopata mtu wa kiume kumweleze matatizo anayokumbana nayo hasa anapobaleghe.
 • Wanaume kuambiwa wafumbike hisisa kwani machozi ya wanaume hayastahili kuonekana.

Janga

 • Anaacha masomo
 • Anaingilia dawa za kulevya na anasa
 • Anaunganana na vikundi vya ugaidi
 • Wanakosa hadhi ya mwanamume
 • Kuchangia kuporomoka kwa misingi ya kifamilia
 • Kukosa viongozi wa kesho.
 • Kusononeka kindani au kupatwa na kihoro. 

Mtahini akadirie hoja za mtahiniwa
TANBIHI

 1. Lazima aonyeshe pande mbili asipo atuzwe nusu ya alama
 2. Kuwe na kichwa au mada.
 3. Atimize maneno kati 350 – 400
 4. Kadiria hoja nyinginezo.

Swali 3
Hii ni insha ya methali

-Maana ya methali;
Mtu asiyetaka mwanawe alie huishia kulia yeye mwenyewe
-Methali hii huwanasihi wazazi wasichelee kuwaadhibu watoto wao wanapokosea ili waishie kuwa na tabia na mienendo mizuri.

 • Mtahiniwa atunge kisa ambacho kinalenga maana ya methali
 • Mtahiniwa anaweza kueleza maana ya methali-(si lazima)
 • Kisa kishughulikie pande zote mbili za methali.
 • Mtahiniwa anaweza kutumia methali nyingine zenye maana sawa kama;
  Usipoziba ufa utajenga ukuta.
 • Pande zote za methali zishughulikiwe. Anayeshughulikia upande moja asipite alama C 08/20
 • Anayekosa kulenga katika kisa chake amepotoka kimaudhui alama D 03/20

Swali la nne
Andika insha itakayomalizia kwa maneno yafuatayo:

.........Hapo ndipo iliponibainikia kuwa nilikuwa nikiogelea baharini pekee kinyume na wenzangu wote. (alama 20)

Mwongozo

 • Mtahiniwa aanze insha yake kwa maneno aliyopewa
 • Kisa chake kifungamane na mawazo ya kauli aliyopewa.
 • Kisa kidhihirishe tukio ambalo halikufahamika na mhusika.
 • Mtahiniwa atumie nafsi ya kwanza umoja
 • Tanbihi: insha ya 3 na 4 …kisa cha mwanafunzi ndicho maudhui hivyo mwalimu akitathmini kikamilifu. 

VIWANGO VYA KUKADIRIA
KIWANGO CHA D
MAKI 01 – 05

 1. Insha ya aina hii haieleweki kwa vyovyote, ama uwezo wa mtahiniwa wa kutumia lugha ni hafifu sana, hivi kwamba mtahini lazima afikirie kile anachojaribu kuandika.
 2. Mtahiniwa hana uwezo wa kutmia maneno ya Kiswahili kwa njia inayofaa.
 3. Lugha imevurugika, uakifishaji haufai na insha ina makosa ya kila aina; kisarufi, kimaendelezo, kimtindo n.k.

VIWANGO TOFAUTI VYA D.
D- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 01-02

 1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile kwa vyovyote vile. Kwa mfano, kunakili
  swali au kujitungia swali tofauti na kulijibu.
 2. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili.
 3. Insha za aina hii zifanywe uamuzi na kiongozi wa kikundi.
 4. Yule anayenakili kichwa kutoka karatasi ya maswali lakini hakushughulikia mada inayokusudiwa atakuwa amejitungia swali.

D (KIWANGO CHA WASTANI) MAKI 03

 1. Utiriko wa mawazo haupo.
 2. Insha haieleweki.
 3. Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukuzwa vilivyo.
 4. Mtahiniwa amepotoka kimaudhui.
  hakuzingatia urefu.
 5. kuna makosa mengi ya kila aina.

D+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 04 - 05

 1. Insha hii ina makosa mengi ya kila aina. Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kusema.
 2. Insha ina lugha dhaifu ya Kiswahili na haina mpangilio.
 3. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyoeleweka kikamilifu.
 4. hana uhakika wa matumizi ya lugha na hupotoka hapa na pale.
 5. mpangilio wa kazi ni dhaifu na mtahiniwa hujirudiarudia.
 6. mtahiniwa ana athari za lugha ya kwanza k.m. papa, badala ya baba, karamu badala ya kalamu n.k.

KIWANGO CHA C – MAKI 06 – 10
Kiwango hiki kina makosa yafuatayo:

 1. Mada haijakuzwa na kuendelezwa.
 2. Anawasilisha ujumbe kwa njia isiyovutia.
 3. Hana ubunifu wa kutosha.
 4. Anaakifisha sentensi vibaya.
 5. Hana mstamiati wa kuvutia wala msamiati mwafaka.
 6. Kuna makosa mengi ya sarufi, msamiati na hijai (tahajia).

VIWANGO TOFAUTI VYA C
C- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 06 – 07

 1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha mawazo yake.
 2. Hana msamiati wa kutosha wala muundo wa sentensi ufaao.
 3. Mada haijakuzwa na kuendelezwa kwa njia ifaayo.
 4.  Ana makosa mengi ya sarufi, tahajia na msamiati.

C (KIWANGO CHA WASTANI) MAKI 08

 1. Anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu.
 2. Hana ubunifu wa kutosha na dhana tofauti tofauti hazijotekzi wazi.
 3. Uakifishaji wa sentensi zake si mzuri.
 4. Amejaribu kushunghulikia mada aliyopewa.
 5. Ana makosa ya hijai, sarufi na mswamiati.

C+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 09 – 10

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe vizuri lakini kwa njia isiyo na mvuto.
 2. dhana tofauti tofauti zimeanza kujitokeza kwa njia hafifu.
 3. kuna utiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa.
 4. misemo, methali na tanakali za sauti zimetumiwa kwa njia hafifu.
 5. Anashughulikia mada aliyopewa kwa utiririko mzuri.
 6. Kuna makosa ya sarufi, msamiati na hijai lakini bado insha inaeleweka.

KIWANGO CHA B, MAKI 11 – 15

 1. Katika kiwango hiki mtahiniwa anaonyesha kuimudu lugha vilivyo.
 2. Mtahiniwa anadhihirisha kwamba anaweza kutumia lugha kwa urahisi katika kuieleza.
 3. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi.
 4. Mtahiniwa ana uwezo wa kutumia lugha kwa ufasaha kama vile kuandika sentensi kwa njia tofauti na zikaleta maana sawa.
 5. Mada huwa imekuzwa na kuendelezwa kikamilifu.

VIWANGO TOFAUTI VYA B
B- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 11 – 12

 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa kuonyesha hoja tofauti tofauti, akizingatia mada.
 2. Ana utiririko mzuri wa mawazo.
 3. Ana uwezo wa kutumia miundo tofauti tofauti ya sentensi.
 4. Makosa ni ya hapa na pale.

B (KIWANGO CHA WASTANI) MAKI 13

 1. Mtahiniwa anadhihirisha hali ya kuimudu lugha.
 2. Anawasilisha ujumbe wake waziwazi kwa mawazo yanayodhihirika.
 3. Matumizi ya lugha ya mnato yamejitokeza.
 4. Anatumia mifano michache ya msamiati mwafaka.
 5. Matumizi ya tamathali za semi yanaanza kudhihirika.
 6. Kuna makosa machache ya hapa na pale.

B+ (KIWANGO CHA JUU) MAKI 14 – 15

 1. Mawazo ya mtahiniwa yanadhihirika – kujitokeza waziwazi.
 2. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe wake kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada.
 3. Uteuzi wake wa msamiati ni mzuri – mchanganyiko wa msamiati.
 4. sarufi yake ni nzuri.
 5. Uakifishaji wake ni mzuri.
 6. Makosa yanaweza kutokea ya hapa na pale.

A KIWANGO CHA MAKI 16 – 20

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ujuzi wa lugha yenye mnato. Ana ubunifu wa mawazo yanayodhihirika na kutiririka.
 2. Ana uwezo wa kutumia tamathali za lugha ili kutoa hisia zake kwa njia bora na kwa urahisi.
 3. Umbuji wake nadhihirisha ukakamavu wake kimawazo na mpangilio mzuri na hali ya kumvutia msomaji wake.
 4. Kazi ya mtahiniwa ni nadhifu na hati nzuri.

VIWANGO TOFAUTI VYA A
A- (KIWANGO CHA CHINI) MAKI 16 - 17

 1. Mtahiniwa anadhihirisha ukomavu wa lugha.
 2. Ana utiririko mzuri wa mawazo kulingana na mada.
 3. Anapamba lugha kwa kutumia tamathali za usemi.
 4. Anazingatia matumizi mazuri ya msamiati na sarufi.
 5. Uakifishaji wake ni mzuri zaidi.
 6. Makosa machache yasiyokusudiwa.

A (KIWANGO CHA JUU) MAKI 19 – 20

 1. Mawazo yanadhihirika na anashughulikia mada aliyopewa.
 2. anatumia lugha ya mnato.
 3. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unavutia.
 4. Sarufi yake ni nzuri zaidi.
 5. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi.
 6. Anajieleza kikamilifu
 7. makosa ni ndra kupatikana.
 8. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe kulingana na mada.
 9. Anadhihirisha mawazo yake vizuri zaidi.
 10. Anajieleza kikamilifu bila shida.
 11. Anatoa hoja zilizokomaa.
 12. Msamiati wake ni wa hali ya juu.
 13. Makosa yote yasizidi matano.
KIWANGO ALAMA MAKI
A A+

A -
19 – 20
18
16 – 17 
B B+
B
B-
14 – 15
12 - 13
11 – 12 
C C+
C
C- 
09 – 10
08
06 – 07
D D+
D
D- 
04 – 05
03
01 -02 

JINSI YA KUTUZA INSHA MBALI MBALI

 1. Mtahiniwa asipozingatia sura ya insha aondolewe maki 4 (nne) baada ya kutuzwa (4 sura).
 2. Insha isiyotosheleza idadi ya maneno ataondolwea maki 2 (mbili) badala ya kutuzwa (2U).

SARUFI
Sahihisha kwa makini sana ukionyesha makosa yote yanayotokea. Makosa ya sarufi huwa katika:

 1. Kuakifisha vibaya; mifano, vikomo, vituo, alama ya kuuliza n.k.
 2. Kutumia herufi ndogo au kubwa mahali si pake.
 3. Matumizi mabaya ya ngeli na viambishi, nyakati, vihusiano, muundo mbaya wa sentensi na mnyambuliko wa vitenzi na majina.
 4. Kuacha au kuongeza neno katika sentensi kwa mfano, kwa kwa.
 5. Matumizi ya herufi kubwa.
  Tazama: Matumizi ya herufi kubwa.
  1. Mwanzo wa sentensi.
  2. Majina ya pekee.
  3. Majina ya mahali, miji, nchi n.k.
  4. Siku za juma, miezi n.k.
  5. Mashirika, masomo, vitaub n.k.
  6. Makabila, lugha n.k.
  7. Jina la Mungu.
  8. Majina ya kutambulisha k.m. majina ya mbwa,

MAKOSA YA HIJAI/TAHAJIA
Haya ni makosa ya maendelezo. Sahihisha huku ukiyaonyesha yanapotokea. Makosa ya tahajia huwa katika:

 1. Kutenganisha neno kama vile ‘aliyekuwa.’
 2. Kuunganisha maneno kama vile ‘kwasababu.’
 3. Kukata silabi vibaya kama vile ‘ngan-o.’
 4. Kuandika herufi isiyofaa katika neno kama ‘mahari ‘ badala ya ‘mahali.’
 5. Kuacha herufi katika neno kama ‘aliekuja’ badala ya ‘aliyekuja’.
 6. Kuongeza herufi isiyofaa katika neno kama piya badala ya pia..
 7. Kuacha alama inayotarajiwa kuwepo katika herufi.
 8. Kutoandika kistari cha kuunganisha neno ufikiapo pambazo au mwisho au kuandika mahali si pake.
 9. Kuacha ritifaa au kuiweka pasipofaa, ng’ombe, ng’ombe, ng’ombe.
 10. Kuandika maneno kwa kifupi km. v.v.

MTINDO
Mambo yatakayovunguzwa:

 1. Mpangilio wa kazi kiaya.
 2. Utiririko wa mawazo.
 3. Hati nzuri inayosomeka kwa urahisi.
 4. Namna anavyotumia methali, misemo, tamathali za usemi na mengineyo.
 5. Unadhifu wa kazi.
 6. Kuandika herufi vizuri, k.m Jj Pp Uu n.k.
 7. Sura ya Insha.

MSAMIATI
Jumla ya maneno yaliyotumiwa kuafikiana na mada au kichwa kilichopendekezwa.
MAUDHUI NA MSAMIATI
Baada ya kusoma mtungo utafikiria maudhui na msamiati uliomo kwa jumla.

ALAMA ZA KUSAHIHISHA
= Hupigwa chini ya sehemu ambayo kosa la sarufi
Limetokeza kwa mara ya kwanza.
- Hupigwa chini ya sehemu au neno ambako kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza tu.
∧ Hutumiwa kuonyesha kuachwa kwa neno
√ Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe.
X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hutiwa juu ya neno lenyewe.

Maelezo mafupi kuhusu tuzo la mtahini yanahitajika.
Kila ukurasa uwe na alama ya chini katikati kuonyesha
kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo.

MANENO
Maneno 8 - kurasa 1¾
Maneno 7 - kurasa 2
Maneno 6 - kurasa 2¼
Maneno 5 - kurasa 2¾
Maneno 4 - kurasa 3¾
Maneno 3 - kurasa 4½

001 – 174 – Robo
175 – 274 – Nusu
275 – 374 – Robo tatu
375 – 400 - Kamili


Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest