Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma taarifa ifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuatia.
Takwimu za tafiti za umaskini kila mara huonyesha kuwa bara la Afrika ndilo bara maskini kabisa kote duniani. Takriban wakazi kiasi cha asilimia themanini hawawezi kumudu kutumia dola moja kwa siku. Toka kaskazini hadi kusini, mashariki hadi magharibi mwa bara, makaazi ya vibanda yametamalaki.
Wakaazi wengi hulala njaa kutokana na ukosefu wa chakula. Watu wa mitaani waliovaa mararuraru wamejaa katika miji ya bara hili. Swali ni: Je, kwa nini umaskini umeliganda bara la Afrika hivi mithili ya kupe? Kwa nini bara huselelea katika lindi la uchochole?
Ili kuelewa sababu za umaskini kuganda barani Afrika, yampasa mtu ima fa ima kurejelea historia ya bara hili. Kwa kipindi cha karne nyingi, Afrika ilidhibitiwa na walowezi pamoja na mabeberu. Wanawake ambao wangelistwawisha bara hili kiuchumi walitwaliwa kimabavu na kupelekwa, huku wamefungwa minyororo, kustawisha uchumi wa mabara mengine. Afrika ikaporwa nguvu ambayo ni rasilimali kuu katika ustawishaji wa uchumi. La kusikitisha ni kuwa Afrika haikufidiwa kutokana na wizi huu. Badala yake iliongezewa mizigo mingine.
Baada ya kipindi cha biashara ya utumwa kumalizika, Afrika ilijipata katika janga jingine. Wakoloni wakliingilia bara kwa pupa. Wakaligawanya katika koloni mbalimbali miongoni mwao. Wakaingiwa na wendawazimu kuiba malighafi ya bara hili. Wakaiba mashamba, madini, miti na chochote cha maana walichokipata. Badala ya malighafi haya kutumika kunawirisha bara la Afrika, yalitwaliwa kustawisha chumi za walikotoka wakoloni. Afrika ikaachwa kuzidi kudidimia katika lindi la umaskini.
Wakoloni walipotoka barani Afrika na kuzipa dola nyingi za Afrika „uhuru‟, waliacha mkururo wa madhila. Madhila haya hayangeikubalia Afrika kujikomboa kutoka katika biwi la uchochole. Tatizo la kwanza na kubwa zaidi ni wakoloni kugawanya na kukatakata Afrika katika mataifa mengi. Mgawanyo huu ukawa haukufuata utaratibu wowote. Kwa sababu hii, watu wa nasaba moja wakawekwa katika nchi tofauti. Mathalani, watu wa nasaba ya kisomali waligawanywa na kuwekwa chini ya nchi huru ya Somali, wengine chini ya dola la Uhabeshi, huku wengine wakiwa nchini Kenya na Jibuti. Watu kama hawa hawakutaka mpango huu. Walioluwa Kenya na Uhabeshi wakachukua silaha na kupigana ili warejeshwe chini ya himaya moja ya taifa huru la Somali. Watu kama hawa wakatumia muda mwingi kupigana; muda ambao ungetumikaa kuinua Afrika kiuchumi. Mapigano haya ya wenyewe kwa wenyewe yamekithiri kote katika bara la Afrika.
Halikadhalika, mkoloni hakufanya juhudi zozote za kuanzisha viwanda ambavyo vingenyanyua uchumi wa Afrika na kuwatoa Waafrika katika biwi la ufukara. Palipokuwa na ari yoyote ya kuanzisha kiwanda, kilipoanzishwa hakukusaidia Afrika kiuchumi. Vilikuwa viwanda vya kupunguza zigo la bidhaa na kuzifanya kuwa nyepesi ili zisafirishwe kwa ajili ya viwanda vya nchi walizotoka wakoloni.
Kwa kipindi cha muda ambao mkoloni amekuwa na maingiliano na wakaazi wa Afrika, amehakikisha kuwa mwafrika amekuwa mtegemezi wake. Malighafi ya Afrika yalipelekwa kutayarishiwa viwanda vya wakoloni. Kisha mwafrika alirudishiwa zikiwa bidhaa kamili za kutumiwa. Mwafrika akaonyeshwa kuwa chochote kilichotoka kwa wakoloni ni bora zaidi ya chake alichozalisha. Hii ikawa ni mbini moja ya wakoloni kuwafukarisha Waafrika. Hata sasa, kilichotoka Ulaya, hata kama ni cha hali ya chini, huonekana bora zaidi kuliko alichozalisha Mwafrika.
Kwa upande mwingine, inadhihirika kuwa wakoloni hawajawahi kuondoka na kuwaachia Waafrika jukumu kamili la kuendesha uhuru wa kisiasa, kijamii na kiuchumi. Waliondoka kupita mlango mmoja na kurudi kwa pili. Mlango wa pili ukawa ni ukoloni kuchukua sura nyingine, sura ya ukoloni mamboleo. Kupitia ukoloni huu, wakoloni hudhibiti uchumi na maendeleo ya Afrika kupitia asasi mbili walizozianzisha, yaani Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. Ili kupata mikopo ya maendeleo, asasi hizi hutoa masharti ambayo hukwamiza badala ya kuchangia kuleta maendeleo barani Afrika.
Sasa hivi pana haja ya wana wa Afrika kufanya vikao vya dharura ili kujadiliana kuhusu suluhisho la tatizo hili sugu la umaskini barani. Lazima wawahimize Waafrika wote kujikomboa kiakili na kung‟amua kuwa maendeleo ya bara lazima yaongozwe na yadhibitiwe na Waafrika wenyewe. Wawahimize kuacha hulka za kukimbilia mataifa yaliyowafanya watumwa na kuwakalia kuondoa umaskini barani bali kuuendeleza.
Pana haja pia Waafrika kuwa miungano ya kiuchumi. Miungamo hii husaidia katika uteteaji wa soko pamoja na bei za bidhaa zao ikilinganishwa na taifa moja kuyaendeleza mambo haya. Halikadhalika, Waafrika wanapawa kutambua kile wanachotaka na kupanga mikakati ya kufikia mahitaji ya kimsingi kwa wananchi wake. Kwa mfano, uimarishaji wa mbinu msingi ambazo zitachangia kuimarisha uchumi wa mataifa wahitaji kuwa mstari wa mbele badala ya ununuzi wa magari na ndege za hadhi za kuwabebea viongozi.

  1. Ipe taarifa uliyosoma anwani mwafaka. (al. 1)
  2. Kutamalaki kwa umaskini barani Afrika kunadhihirishwa na nini. (al. 2)
  3. Onyesha jinsi ambavyo wakoloni wameendeleza umaskini barani Afrika. (al. 4)
  4. Thibitisha kwa kutoa hoja tatu, dhana ya kuwa “Waafrika wenyewe ndio wamechangia kuwepo kwa umaskini wa bara la Afrika.” (al. 3)
  5. Umaskini barani Afrika unaweza kukabiliwa vipi kwa mujibu wa makala haya? (al. 3)
  6. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa: (al. 2)
    1. Kuselelea
    2. mabeberu

MUHTASARI (ALAM 15)
Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali.
Sekta za umma humu nchini hazina kifani katika uzembe. Unapohitaji huduma za posta, umeme, maji, mawasiliano, utayarishaji wa mishara na malipo mengine, utalazimika kusubiri kwa siku, miezi na hata miaka ili upate haki yako, hata wakati mwingine ukakosa!
Wafanyakazi wa sekta hii hukosa kutimiza majukumu yao ipasavyo kutokana na ukosefu wa motisha yaani mishahara duni, uhaba wa nyenzo za kutekeleza majukumu yao na kutozingatia kazi kwa wakaguzi na viongozi wa wafanyakazi.
Minghairi ya hali hii, visa vya ufisadi ndivo sifa inayopambanua hudumu za umma. Baadhi ya wafanyakazi hupatikana ofisini na katika maeneo ya kazi kwa nadra sana kwa sababu huwa wanakimbilia kwingineko kutafuta malipo ya kujazia mishahara yao duni kujikumu kimaisha. Athari za matendo haya zimekuwa kukokota kukua kwa uchumi, ukosefu wa imani kwa hudumu za umma na utoaji wa hudumu hafifu.
Kufuatia udhaifu huu, katika siku za majuzi, sekta za kibinafsi zimetambulika kuwa muhimu sana katika utoaji wa hudumu kwa wananchi. Uchumi wa mataifa yanayopendelea sekta za kibinafsi yametambuliwa kukua kwa kasi kuliko yale yanayoandama mfumo kongwe wa serikali kutawala shughuli za uzalishaji mali.
Lakini kwa kuwa mashirika ya kibinafsi yamebainika kuwa na udhaifu wa aina yake, serikali inaposhirikiana kindakindaki na sekta hii, ustawishaji wa hali za kazi utajiri. Kwa kuwa dhamira kuu ya mashirika ya kibinafsi huwa kujizolea faida kemkem, yamekuwa yakifanyiza wafanyakazi wao kazi nyingi kupita kiasi ambayo mara nyingine huwadhuru kiafya. Japo mshahara wao ni afadhali kuliko wa sekta ya umma, baadhi ya sera huwa kandamizi na hutinga fursa za wafanyakazi kukuza majukumu yao binafsi, mengi yakiwa muhimu kwa jamii kijumla.
Ushirikiano wa serikali na mashirika ya kibinafsi, kwa hivyo, una uwezo mkubwa wa kustawisha na kupanua mawanda ya uchumi. Utakuwa dawa mujarabu kwa udhaifu wa pande zote. Sekta za kibinafsi zikijizolea faida nyingi kwa upande mmoja, sitasaidia katika kuondoa uzembe, utepetevu na mapuuza yanayotamalaki huduma za serikali kwani yatalenga uzalishaji mwingi ili kutimiza malengo yao.

  1. Eleza mawazo muhimu ya aya tatu za mwanzo kwa maneno 50 – 55. (al. 5, 1 utiririko)
    Matayarisho
    JIBU
  2. Fupisho aya tatu za mwisho bila kubandilisha maana iliyosudiwa kwa maneno 75 – 80.
    (al. 8, 1 utiririko)
    Matayarisho
    JIBU

SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA. (AL. 40)

  1. Huku ukitoa mfano,eleza maana ya kipasuo-kwamizo. (al. 2)
  2. Tofautisha kati ya;. (al. 2)
    Kimadende na kitambaza
  3. Huku ukitoa mifano,eleza majukumu mawili ya kiimbo. (al. 2)
  4. Tambulisha ngeli ya nomino „ kengewa‟. (al. 1)
  5. Tunga sentensi ya neno moja yenye viungo vifuatavyo. (al. 3)
    1. Kiambishi cha nafsi ya kwanza umoja
    2. Wakati
    3. Yambwa tendwa
    4. mzizi
    5. Kauli ya kufanyiza
    6. Kiishio
  6. Unda nomino kutokana na kitenzi „choma‟. (al. 1)
  7. Tambua mofimu mbili ambazo si mofimu huru. (al. 2) kingalingali, kipindupindu, suriama,mnuna,viwavi
  8. Akifisha sentensi zifuatazo. (al. 2)
    1. Enhe tena lulua mama akauliza.
    2. shirika la msalaba mwekundu limewahawilisha wakimbizi kutoka uhabeshi
  9. Huku ukitoa mfano mmoja mmoja fafanua miundo miwili ya ngeli ya U-ZI. (al. 4)
  10. Tumia kitenzi kifuatacho katika kauli ya kutendama kuunda sentensi. (al. 2)
    Funga
  11. Sentensi zifuatazo ni za aina gani? (al. 2)
    1. Alimkaribia kwa kutaka kumshika.
    2. Mungu hawezi kukuacha hivyo.
  12. Tambua aina za vihusishi katika sentensi ifuatayo.
    Mwangeka ameketi mkabala wa kidimbwi cha kuogelea (al. 1)
  13. Unda vivumishi kutokana na vitenzi vifuatavyo: (al. 2)
    1. Sadiki
    2. Dhulumu
  14. Toa maana mbili zinazojitokeza katika sentensi ifuatayo. (al. 2) Nilimpikia mama kuku.
  15. Eleza sifa tatu za vishazi tegemezi. (al. 3)
  16. Eleza matumizi ya „na‟ katika sentensi ifuatayo.
    Ridhaa na Mwangeka walikuwa wameketi karibu na jumba la kifahari walipoitwa na Apondi (al. 3)
  17. Eleza maana ya chagizo. (al. 1)
  18. Ondoa „o‟ rejeshi bila kubadilisha maana. (al. 1)
    Kuimba kunakoimbwa siku hizi kunafifisha maadili.
  19. Ni hisia zipi zinazodhihirika katika matumizi haya ya vihisishi. (al. 2)
    1. Huree!Timu yetu imetwaa taji katika mchuano huo..
    2. Mama wee!Hata Adela yumo kwenye disko!.
  20. Tambua aina za shamirisho katika sentensi ifuatayo. (al. 3) Rais alipelekewa watoto wake karamuni kwa gari la kifahari.

ISIMU JAMII (ALAMA 10)

  1. Eleza maana ya usanifishaji wa lugha.(al. 2)
  2. Fafanua mambo manne yaliyosaidia kueneza Kiswahili kutoka kitovu chake hadi bara na visiwani kabla ya uhuru.
    (al. 4)
  3. Toa sababu nne zinazothibitisha kuwa Kiswahili ni lugha ya Kibantu.(al. 4)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. Ipe taarifa uliyosoma anwani mwafaka. (al. 1)
    Asili ya Tatizo la Umaskini Barani Afrika
  2. Kutamalaki kwa umaskini barani Afrika kunadhihirishwa na nini. (al. 2)
    Asilimia themanini ya wakazi hawawezi kumudu kutumia dola moja kwa siku Watu wa mitaani waliovaa mararuraru wamejaa katika mitaa ya bara hili
  3. Onyesha jinsi ambavyo wakoloni wameendeleza umaskini barani Afrika. (al. 4)
    Wakoloni waliiba malighafi ya bara la Afrika kama vile mashamba,madini na miti.
    Wakoloni walipotoka,waligawa bara la Afrika katika mataifa mengi bila utaratibu wowote; migogoro kuhusu kugawanmywa kwa watu wa nasaba moja ukazuka na muda
    kupotezwa
    Wakoloni hawakujenga vibanda muhimu barani Afrika
    Wakoloni wameendeleza utegemezi
    Wakoloni wamerudi kwa sura mpya;ukoloni mamboleo
  4. Thibitisha kwa kutoa hoja tatu, dhana ya kuwa “Waafrika wenyewe ndio wamechangia kuwepo kwa umaskini wa bara la Afrika.”
    Waafrika wana mazoea ya kukimbilia mataifa yanayowafanya kuwa watumwa
    Waafrika huzama katika migogoro ya kisiasa
    Waafrika hawana miungano thabiti ya kiuchumi
    Waafrika hawana mipangilio na mikakati ya kutosheleza mahitaji ya kimsingi kwa raia wake (al. 3)
  5. Umaskini barani Afrika unaweza kukabiliwa vipi kwa mujibu wa makala haya? (al. 3)
    Waafrika wakome kutegemea waliokuwa wakoloni wao
    Waafrika waunde miungano thabiti ya kiuchumi
    Waafrika waweke mipango na mikakati ya kutosheleza mahitaji ya kimsingi kwa wananchi
  6. Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa: (al. 2)
    1. Kuselelea -kubakia
    2. mabeberu -wakoloni

MUHTASARI (ALAM 15)

  1. Eleza mawazo muhimu ya aya tatu za mwanzo kwa maneno 50 – 55. (al. 5, 1 utiririko)
    Matayarisho
    1. Sekta za umma humu nchini hazina kifani kaika uzembe
    2. Wanaotafuta huduma za kimsingi husubiri muda mrefu na huweza hata kukosa
    3. Wafanyakazi wa sekta za umma hukosa kutimiza majukumu yao ipasavyo kutokana na
      Kukosa motisha,uhaba wa nyenzo za kutekeleza majukumu yao na usimamizi hafifu kazini
    4. Huduma za umma hutambulika kwa ufisadi
    5. Ufisadi uliokithiri husababisha kukokota kwa uchumi,ukosefu wa imani kwa huduma za
      umma na huduma hafifu
      JIBU
      Sekta za umma nchini zimezembea sana.Wanaotafuta huduma muhimu kwazo Hucheleweshw sana au hata kuzikosa.Wafanyakazi hutelekeza majukumu yao kwa kukosa motisha.Hukosa nyenzo za kutekeleza majukumu yao na huathiriwa na usimamizi hafifu kazini. Ufisadi huhusishwa na huduma za umma.Hivyo,uchumi hukokoteshwa na watu kupoteza imani kw huduma hafifu za umma.(Maneno 52)
      Alama 5
      Alama 1 ya Mtiririko
  2. Fupisho aya tatu za mwisho bila kubadilisha maana iliyosudiwa kwa maneno 75 – 80. (al. 8, 1 utiririko)
    Matayarisho
    1. Sekta za kibinafsi zimetambulika kuwa muhimu zaidi katika utoaji wa huduma kwa Umma
    2. Chumi za mataifa yanayoendeleza sekta ya kibinafsi hukua haraka
    3. Dhamira kuu ya sekta ya kibinafsi ni kuzoa faida kemkem
    4. Serikali ikishirikiana na sekta ya kibinafsi hali ya kazi itastawishwa
    5. Wafanyakazi wa sekta ya kibinafsi hufanizwa kazi nyingi na huweza kudhurika kiafya
    6. Wafanyakazi wa sekta ya kibinafsi hulipwa mishahara afadhali kuliko sekta ya umma
    7. Baadhi za sera za kazi hukanadamiza wafanyakazi wa sekta ya kibinafsi
    8. Faida nyingi kwa sekta ya umma na kuimarishwa kwa huduma za umma huwezekana
      Kupitia ushirikiano wa sekta ya kibinafsi na serikali
      JIBU
      Sekta ya kibinafsi ni muhimu sana kwa kuwahudumia umma.
      Mataifa yanayopendelea sekta hii hukua haraka zaidi.Sekta hii hulenga faida kubwa.Ushirikiano kati ya sekta ya kibinafsi na serikali hustawisha utendakazi.Wafany kazi wa sekta ya kibinafsi hudhurika kiafya wanapofanyizwa kazi nyingi japo hulipwa mshahara afadhali kuliko sekta ya umma.Sera fulani za kazi hukandamiza wafanyakazi hao.Faida kubwa zaidi kwa sekta ya kibinafsi na huduma bora kwa sekta ya umma huwezekana kwa ushirikiano baina ya pande zote mbili.(Maneno 78)
      Alama ; 8
      Mtiririko ; Alama 1
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Sukellemo Joint Pre Mock Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest