Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda Pre-Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. Insha ya lazima
  Wewe ni katibu wa Tume ya kitaifa iliyoteuliwa na Waziri wa Usafiri kuchunguza vyanzo vya ajali barabarani. Andika ripoti ya uchunguzi wenu.
 2. Jadili mikakati ambayo serikali imeweka kuimarisha sekta ya viwanda nchini.
 3. Tunga kisa kinachoafiki matumizi ya methali hii; Mhini na mhiniwa njia yao moja.
 4. Niliamshwa na sauti ya dirisha likifunguliwa polepole. Nje kulivaa weusi wa kutisha...
  Endeleza kisa hiki.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Wewe ni katibu wa Tume ya kitaifa iliyoteguliwa na Waziri wa Usafiri kuchunguza vyanzo vya ajali barabarani. Andika ripoti ya uchunguzi wenu.
  SURA
  Hii ni insha ya ripoti kwa hivyo inachukuwa muundo wa ripoti rasmi.
  Kichwa
  Kirejelee ripoti, tume iliyoteuliwa na waziri wa usafiri kuhusu vyanzo vya ajali barabarani. Bila kichwa aondolewe alama 2; za anwani
  Utangulizi
  Mtahiniwa atangulize kwa kurejelea tume ya kuchunguza vyanzo vya ajali barabarani. Kipindi cha utafiti, mteuzi wa tume - Waziri wa Usafiri.
  Bila utangulizi, ondoa 4S
  Hladidu za rejea - ila sio lazima
  Mbinu za utafiti
  Mtahiniwa aeleze kwa kina kati ya mbinu zifuatazo walizozitumia kukusanya data.
  • Mahojiano
  • Hojaji
  • Utafiti wa maktabani
  • Uchunzaji
  • Kushiriki
   Bila kurejelea mbinu za kukusanya data, ondoa 4S
   Matokeo
   Baadhi ya matokeo ni kama yafuatavyo;
  • Njia/ barabara mbovu
  • Magari mabovu barabarani
  • Madereva wasiohitimu vizuri
  • Kuendesha magari kwa kasi
  • Kubeba abiria na mizigo kupita kiasi
  • Polisi fisadi
  • Watumizi wabarabara kutokuwa waangalifu/makini
  • Ulevi
  • Kutodhibiti usukani vizuri
  • Uchovu na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika
  • Matimizi mabaya ya dawa za matibabu
  • Matumizi ya dawa za kulevya
  • Mzongo wa mawazo
  • Usumbufu kutoka kwa abiria
   Tanbihi: mtahiniwa arejelee hoja saba na kueleza vizuri kwa kutumia mada ndoga ndogol aya.
   Mapendekezo
  • Wavunja sheria kuchukuliwa hatua za kisheria
  • Kuondoa plisi fisadi barabarani
  • Kukarabati barabara vizuri
  • Ukaguzi wa mara kwa mara wa magari
  • Mafunzo mazuri ya mara kwa mara ya madereva
  • Magari kuwekewa vidhibiti mwendo
  • Matumizi ya mikanda ya usalama
  • Vifaa vya kutambua madereva walevi
  • Madereva kuwa waangalifu na makini.
  • Watumizi wengine wa barabara kuwa makini na waangalifu
  • Madereva walio na mzongo wa mawazo kutoruhusiwa kuendesha magari
   Hitimisho
   Mtahiniwa atoe mhutasari au shukrani kwa mteuzi wa tume pamoja na walioshiriki katika utafiti. Akikosa hitimisho; ondoa 4S
   Hitimisho
   Sio lazima lazima anaweza kutoa funzo kama upekee wake."
   Ithibati
   Hii ndio sehemu ya mwisho Mtahiniwa aonyeshe ripoti imeandikwa na nani.
   Sahihi
   Jina
   Cheo- Katibu wa Tume ya uchunguzi wa vya vya ajali barabarani
   Bila sehemu hii-ondoa alama 45
 2. Jadili mikakati ambayo serekali imeweka kuimarisha sekta ya viwanda nchini.
  Muundo
  Hii ni insha ya kueleza au kufafanua
  Kichwa
  Kizizidi maneno sita na kilenge mada
  Bila kichwa ondoa alama 2A
  Utangulizi
  Sio lazima lakini ni upekee wa mtahiniwa.
  Mwili
  • Baadhi ya hoja ni kama zifuatazo;
  • Kuimarisha miundomsingi ya barabara
  • Kuimarisha miundomsingi ya nishati/stima/kawi
  • Kuimarisha miundomsingi ya reli
  • Kuimarisha miundomsingi ya viwanja vya ndege
  • Kuimarisha miundomsingi ya bandari
  • Kuimarisha vyuo vya kiufundi ili kutoa wataalamu
  • Kuimarisha sekta ya kilimo ili kutoa maligghafi hasa kwa viwanda vya kizaraa
  • Serikali kutoa mikopo ya riba ya chini
  • Serikali kutoa ruzuku kwa pembejeo na kwa wafanyibiashara ili kutimiza uwekezaji wan je na ndani
  • Utafiti kuhusiana na madini muhimu kama vile mafuta, dhahabu n.k
  • Kutoza ushuru wa chini ili kuwavutia wekezaji wa nje na ndani
  • Kupanua sekta ya kibinafsi
   Tanbihi: mtahiniwa azingatie hoja saba kama maudhui
   Hitimisho
   Si lazima lakini ni upekee wa mtahiniwa
 3. Tunga kisa kinachoafiki matumizi ya methali hii:
  Mhini na mhiniwa njia yao moja.
  Muundo
  Hii ni insha ya methali.
  Muundo uchukuwe sura ya methali
  Kichwa
  Kiwe methali yenyewe- Mhini na mhiniwa njia yao moja.
  Akibadilisha muundo wa methali atuzwe bakishishi. BK-01
  Insha bila kichwa aondolewe alama 45
  Utangulizi
  Si lazima lakini anaweza kutoa maana ya methali
  Mwili
  Kisa kilenge sehemu mbili ya methali. Sehemu ya mhini na sehemu ya mhiniwa
  Bila sehemu mbili, atakuwa amepungukiwa kimaudhui kwa hivyo atuzwe bakishihsi- BK01
  Mhini – mtu anayefanyia mweziwe maovu
  Mhiniwa - anayefanyiwa maovu
  Njia yao ni moja - wote hupata hasara
 4. Niliamshwa na sauti ya dirisha likifunguliwa polepole. Nje kulivaa weusi wa kutisha ...
  Endeleza kisa hiki.
  Muundo
  Hii ni insha ya ubunifu
  Mtahiniwa abuni kisa kimoja.
  Kichwa
  Kizizidi maneno sita
  Bila kichwa ondoa alama
  Utangulizi
  Utangulizi urejelee mdokezo bila kubadilisha chochote. Mwanafunzi akibadili atakuwa amejitungia swali. Atuzwe bakishishi - BK-01
  Mwili
  Kisa kilenge maana ya mdokezo;
  Kisa kitendeke nyakati za usiku
  Kiwe cha kutisha
  Mhusika ajihusishe na kisa hivyo atumie nafsi ya kwanza.
  Kisa kitendeke baada ya mhusika kuamka
  Bila mwelekeo huu, mtahini atakuwa amepotoka kimaudhui, hivyo atuzwe bakishishi-BK-01
  Hitimisho
  Irejele mwisho wa kisa
  Amepunguicira Kimaudhui

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - Maranda Pre-Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest