Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Maranda Pre-Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. UFAHAMU (Alama 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
  Mfinyanzi alifika ofisini mwake na kuangalia kwa mara nyingine ratiba yake ya siku. Vipindi vilikuwa vimefuatana kama msafara wa siafu. Wakati mwingine aliwazia kustaafu mapema. Angalau akifanya hivyo, atakuwa na uwezo wa kujiendeleza kiuchumi na kupata utuvu lakini kila alipofikiria kuwa taifa lilitegemea watu kama yeye ili kujiendeleza, alighairi nia. Uzalendo aliokuwa nao haukumruhusu kufa moyo. Ni wafinyanzi wangapi kama yeye ambao walirauka majogoo na kutembea masafa marefu ili kufika shuleni mapema? Ni wangapi ambao walijitolea kwa hali na mali kuhakikisha kuwa wanasalia shuleni baada ya saa za kazi ili kuwasaidia wanafunzi kama Sufuri? Ni wangapi waliokosa kula staftahi na chamcha kwa sababu ya udongo waliokuwa wakifinyanga? Ni wangapi ambao hata wakati mwingine familia zao hawakuziona? Ni wangapi ambao wakati mwingine walikejeliwa na wakubwa wao pamoja na wazazi? Ni wangapi ambao walikosa ubwabwa wa mwana wa kutosha? Kisa na maana, walijali kuhusu kesho. Kesho ambayo kwa kiasi fulani isingewafaa na hata ingewafaa, isingekuwa kwa kiasi kikubwa kama ambavyo ingewafaa hawa waliochezea kesho yao. Alichukua ile ratiba na kuirudisha ndani ya faili, akamimina maji gilasini, akapiga tama moja, akanyosha shingo na kufumba macho.
  Fikra zake zilianza kutembea, zikaambua nyayo, wayo mmoja baada ya mwingine na zilipofikia sehemu fulani, zilitua. Zilitua kama ndege atuavyo katika tawi la mti. Baada ya kutua, alishtukia anaanza kukariri shairi fulani ambalo alikuwa amekumbana nalo katika shughuli zake za kufanya utafiti kuhusu ushairi. Haikuwa mara ya kwanza ya Mfinyanzi kukariri shairi hili na ilikuwa ni kana kwamba fikra zake zilikuwa zinatua kwa shairi hili kila mara alipojipata akiwaza kuhusu jambo fulani.
  "Kiburi, unafaa kufikiria maisha yako upya. Uchukue darubini, uyachunguze kwa kina maisha yako ya baadaye. Usione sasa, tazama miaka ishirini baada ya sasa, utakuwa wapi? Utakuwa nani katika..."
  "Wewe! Tangu lini ukawa mtu wa kunishika sikio?"
  “Nakushika sikio kwa kuwa nahofia maisha ya wanao. Umetia nta sikioni, husikii la mwadhini wala la mteka maji msikitini. Au unadhani kuwa mali ya wazazi wako pamoja na ya wajomba wako ni yako? Jiangalie vizuri, jiangalie tena sana. Naku..." "Sikiliza na unisikilize kwa makini. I know what I need in my life. Haya ni maisha yangu, hayakuhusu hata tone na ukitaka nikukumbushe mimi ni nani, basi endelea kutia vyanda vyako katika mboni zangu. Umesahau?" Kiburi alijibu kwa hasira huku akimnyoshea kidole mwenzake aliyekuwa akionekana kuwa na hofu fulani. Ilibidi asogee kando kidogo asije akatobolewa mboni ya jicho kwa ukucha wa Kiburi.
  1. Ni mambo yepi yalimfanya Mfinyanzi kughairi nia ya kustaafu kwake. (alama 2)
  2. Ni sababu zipi zinadhihirisha wafinyanzi kama wazalendo. (alama 5)
  3. Mfinyanzi ana majukumu gani katika taifa? (alama 2)
  4. Wanaorejelewa kama udongo wana matatizo kielimu. Thibitisha. (alama 4)
  5. Eleza maana ya misamiati ifuatayo kama ilivyotumika kifunguni:
   1. Utuvu...
   2. Kunishika sikio .............
 2. UFUPISHO (Alama 15)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
  Mitihani imetumiwa siku nyingi kama kigezo cha kupima werevu wa mwanafunzi katika kutekeleza majukumu ya kiakili yenye kuhitaji stadi mbalimbali. Hii ni njia ya kuaminika na ni rahisi ambayo imetumiwa miaka mingi na watahini kukadiria uwezo wa mtu. Lakini wale wanaopinga mitihani wanasema kuwa mitihani haipimi kwa njia inayoaminika uwezo wa kiakili wa mwanafunzi, badala yake, mitihani inakadiri tu uwezo wa mwanafunzi wa kukadiria mambo kama kasuku kwa muda mfupi uliojaa vitisho na shinikizo.
  Wasioithamini mitihani pia wanadai kuwa mitihani humpa mtahiniwa wasiwasi mwingi. Hii ni
  muhimu wa mitihani imekuzwa sana miongoni mwa watahiniwa na jamii zima kwa jumla. Mitihani ndio kigezo pekee kinachokadiria kufaulu au kutofaulu Kwa mwanafunzi. Mustakabali wa mwanafunzi kuamuliwa na mtihani. Watahini hawajali Sana masuala mengine ambayo yanaweza kuhathiri jinsi mwanafunzi anavyoweza kuufanya mtihani. Kwa mfano, mtahiniwa anaweza kuwa mgonjwa, au pengine hakulala vizuri siku iliyotangulia mtihani. Haya yote ni masuala yanayoweza kumfanya mtahiniwa kutofanya vizuri katika mtihani.
  Elimu nzuri humfundisha mwanafunzi kutumia akili. Lakini mfumo wa elimu unaopendelea mitihani haufanyi hivyo. Mfumo wa aina hiyo husisitiza kufundisha yale yale yanayopatikana katika mwongozo uliotolewa tu. Mwanafunzi hapewi motisha ili kusoma kwa mapana na marefu ili kupanua akili yake. Badala yake mwanafunzi hufungiwa kwenye uwanja finyu ambamo haruhusiwi kutoka. Mwalimu naye kadhalika hana uhuru wa kumfundisha mwanafunzi kile anachofikiria kuwa muhimu katika maisha. Badala yake jukumu kubwa analoachiwa mwalimu huwa ni kumpa mwanafunzi mbinu za kukujibu maswali na kupita mtihani.
  Ingawa wanaoitetea mitihani hudai kuwamatokeo ya mitihani ni ya kuaminika kwa sababu husahihishwa na watu wasiowajua watahiniwa, lakini ni vizuri pia kukumbuka kuwa watahini ni binadamu tu. Binadamu huchoka, huhisi njaa na zaidi ya yote anaweza kufanya makosa. Licha ya hayo yote, watahini hutakiwa kusahihisha rundo kubwa la karatasi, kwa muda mfupi. Mjadala uliopo kati ya wanaopendelea mitihani na wale wasiopendelea watukumbusha kuwa kuna haja kubwa ya kuendelea kuboresha mfumo wa mitihani ili uweze kukadiria kwa yakini uwezo wa kiakili wa mtahiniwa. (alama 9)
  1. Fupisha aya ya kwanza na ya pili (maneno 60 - 65)
   Matayarisho................................
   Jibu................................ (alama 6)
  2. Fupisha aya ya tatu na ya nne. (maneno 45 - 50)
   Matayarisho................................
   Jibu................................
 3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)
  1. Dondoa sauti mwambatano zilizo kwenye maneno haya na utambue mahali kila moja hutamkwa. (alama 2)
   1. ngao ............
   2. avya ..
  2. Andika kivumishi chenye silabi za muundo ufuatao. (alama 1)
   Konsonanti + konsonanti, irabu + konsonanti + irabu ...........
  3. Tunga sentensi zifuatazo. (alama 2)
   1. Arifu ................
   2. Rai ............
  4. Andika mofimu katika maneno yafuatayo. (alama 4)
   1. Muundo ...........
   2. Aliaye .............
  5. Weka nomino parachichi katika ngeli mwafaka.
  6. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wingi.
   Ndoo aliyoivunja shambani mwake ilimkasirisha mturne. (alama 3)
  7. Onyesha aina za nomino katika sentensi ifuatayo.
   Biwi la takataka lilizua harufu iliyomkasirisha Upendo.
  8. Tunga sentensi ukitumia kiwakilishi cha 'a' unganifu chenye dhana ya aina au sampuli.
  9. Eleza tofauti kisarufi ya maneno yaliyopigiwa mistari.
   1. Duka la mwalimu limechomeka ............
   2. Duka la mwalimu limechomeka ...............
  10. Tunga sentensi kubainisha kiunganishi cha wakati.
  11. Mwalimu aliingia darasani. Somo lilianza. (Unganisha kuwa sentensi moja kwa kutumia neno 'pindi)
  12. Bainisha matumizi ya 'na katika sentensi ifuatayo.
   Nasi tutafunzwa na mwalimu yule mgeni.
  13. Tunga sentensi kuonyesha wakati ujao hali ya mazoea. (alama 2)
  14. Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya ukubwa. (alama 2)
   Mbwa wale wana midomo mikubwa inayotisha
  15. Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. Njenga alifunga mlango na kujibu maswali kwa ukakamavu.
  16. Tunga sentensi moja kutofautisha maana ya vitate sabuni na zabuni.
  17. Tumia neno "pongezi' katika sentensi kama:
   1. Nomino ........
   2. Kihisishi ..............
  18. Tunga sentensi yenye muundo ufuatao.
   KN(W+RH)+KT (t+E) (alama 2)
  19. Riwaya hiyo ilikuwa ndefu sana: Wanafunzi walisoma kwa muda mfupi.(Unganisha kuunda sentensi changamano) .........
  20. Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha matawi.
   Wadudu wengine huwasumbua wakulima
  21. Iandike upya sentensi ukianza kwa yambwa tendwa.
   Wafula alimkatia nyasi ng'ombe wale kwa upanga
 4. ISIMUJAMII (Alama 10)
  1. Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.
   MHUSIKA 1: Order! Order! Nidhamu, Mheshimiwa Fujo. Hili ni onyo dhidi ya tabia hiyo.
   MHUSIKA II: Nisamehe Bwana .........
   MHUSIKAI: Sasa ninakaribisha swali la tatu. Mheshimiwa Pekua, uliza swali lako.
   MHUSIKAIII: Ninaomba kufahamishwa ni kwa nini Waziri wa Maji ameshindwa kusambaza huduma za maji katika kijiji cha Majikame. 
   1. Bainisha sajili ya makala haya. (alama 1)
   2. Fafanua sifa za sajili hii kama zinavyobainika kifunguni. (alama 5)
  2. Bainisha sababu nne zilizopelekea kusanifisha lugha ya Kiswahili.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.      
  1. uzalendo/taifa lilimtegemea ili kuliendeleza kiuchumi
  2.    
   • kughairi nia ya kustaafu mapema
   • kurauka asubuhi na kutembea masafa marefu kufika shuleni
   • kusalia shuleni kuwasaidia wanafunzi baada ya saa za kazi
   • kukosa kula staftahi na chamcha
   • kukosa kuona familia zao
  3.    
   • kuwashauri wanafunzi
   • kuandaa kesho ya wanafunzi/kuwafunza
  4.    
   • wanachezwa kesho yao
   • walimu wanabaki shuleni kuwasaidia kina sufuri
   • kughairi ushauri kama kiburi
  5.    
   1. utulivu/pumziko
   2. kunishauri
 2.      
  1.    
   • Mtihari ni kigezo cha kupima werevu wa mwanafunzi.
   • Njia hii imetumiwa miaka mingi kukadiria mwezo wa mfu.
   • Kuna wanaopinga
   • Wanasema mtihani hupima ukadirifu wa mambo kikasuku.
   • Huwa na vitisho na shinikizo.
   • Mtihani huwapa wanafunzi wasiwasi.
   • Ndicho kigezo cha kukadiria kufaulu au kutofaulu.
   • Mustakabali wa mwanafunzi kuamuliwa na mtihani.
   • Watahiniwa hawajali mengine yanaweza kuathiri matokeo. 
  2.    
   • Elimu nzuri hufundisha mwanafunzi kutumia akili.
   • Mfumo wa kupendelea mitihani haufanyi hivyo.
   • Husisitiza yale yaliyoko kwenye mwongozo au silibasi.
   • Haupalii mwanafunzi motisha.
   • Mwalimu hana uhuru wa kufundisha, anafunza mbinu za kujibu maswali.
   • Watahini ni binadamu na uchoka.
   • Mtindo wa kukadiria wanafunzi huendelea na kuboreshwa.
    NAMNA YA KUTUZA
    ✓ Mtirirko (alama 2)
    ✓ Ondoa alama kwa kila kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza hadi makosa 10
    ✓ Ondoa alama kwa kila kosa la hijai litokeapo mara ya kwanza hadi makosa 6
    ✓ Nakala safi na iandikwe kiujazo/mfululizo
    MATUMIZI YA LUGHA - ALAMA 40
 3.      
  1.    
   1. ngao
    /ng/-hutamkwa kwenye kaakaa laini
   2. avya
    /vy/ -mdomo-meno
  2. Konsonanti + consonanti, trabu + consonanti+ Irabu
   mzuri, mrefu, mdogo, mkali
  3.    
   1. arifu
    Mtoto analia (tbu liwe taarifa)
   2. rai
    Tafadhali ntazime Icalami yalco/samahani/niwie radhtombu)
  4.    
   1. Muundo
    Mu- umoja/ngeli(U-I, umoja) -und- mzizi - o-urominishaji/liishio (2/0)
   2. Aliaye
    A-nafsi/ngeli-li- mzizi - a- kiishio/kauli tenda-ye- Icirejeshi (2/6)
  5.  
   1. Parachichi LI-YA/LI
  6. Ndoo aliyoivunja shambani mwake ilimkasirisha mtume
   Ndoo walizozivunja mashambani mwao ziliwakasirisha mitume.
  7.    
   • biwi-jamii/makundi,
   • harufu- dhahania,
  8.    
   • Kitambaa cha pamba kimeshonwa vizuri.
   • Kalamu ya wino inaandika vizuri.
   • Nyumba ya matofali inapendeza.
    Sharti apige mstari H+N
  9.    
   1. Kivumishi cha 'a' unganifu /RH (Kirai husishi XFI
   2. Kthusishi cha 'a' unganifu J
  10. Atumie 'halafu, kabla ya, baada ya'
   Mwalimu alitufunza virai halafu akaondoka.
  11.    
   • Pindi mwalimu alipoingia darasani, somo lilianza. Au
   • Somo lilianza pindi mwalimu alipoingia darasani.
  12.    
   • Ufupisho wa nafsi
   • Kihusishi cha mtenda.
  13. Mwalimu atakuwa amesoma
  14. Majibwa yale yana madomo malubwa yanayotisha. 
  15. Njenga alifungua mlango na kujibu maswali kwa wasiwasi/woga/ hofu/shauku/ shaka/kiwewe
  16. Kampuni ya leutengeneza sabuni ya kuoshea nguo ilipewa zabuni ya kusambaza leijijini.
   Tanbihi: Maana halisi ijitokeze wazi kwenye sentensi.)
  17.    
   • Pongezi zake zilipokelewa kwa haraka
   • Pongezi! Umefuzu vizuri
  18.    
   • Kile cha mwalimu kilikuwa shuleni
   • Yule wa Onyango atakuwa shuleni
   • Wale chini ya mti wanapanga njama ya kumpora
  19.    
  20.     
   1
  21. nyasi ilikatiwa ng'ombe wale
 4.    
  1.    
   1. Saliti ya bungeni
   2.    
    • Lugha ya bungeni: mheshimiwa nidhamu
    • Lugha mseto/kuchanganya ndimi:order!order!
    • Lugha ya heshima: mheshimiwa, ninaomba
    • Lugha amrishi : hili ni onyo dhidhi ya..
    • Kukatiza ndimi/kauli: nisamehe bwana..
    • Lugha dadisi: mheshimiwa pekua, uliza swali lako
    • Lugha elezi/ fafanuzi: hili ni onyo dhidhi ya tabia hiyo
  2.    
   • wingi wa lahala za kiswahili
   • haja ya kurahisha mawasilia
   • uvumbuzi wa siasa na teknolojia
   • hala ya kusawazisha tafiti katika kusulah
   • sababu ya kielimu - lugha sawazishi ya kufundishia
   • sababu za kiduni - lugha sawazishi ya mahubiri

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Maranda Pre-Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest