Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Maranda Pre-Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. Lazima
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.
    Milingoti
    Wanakwenda... wanakwenda..."
    Wanapiga hatua labda!
    Labda... labda... labda!
    Mwendo wa dhana yao!
    Wanakwenda kumbe wamesita.
    Safari ya kuwepo na kutokuwepo!
    Hatua zao kubwa: chapchap...
    Miondoko sawa na jongoo
    Wanakwenda pasi na kwenda
    Safari ya dhana... pekee
    Hatua zao kubwa na nia pia
    Nia zin'otoka ndani kuishia ndani
    Maishilio ni nafsi zao
    Wanapiga hatua kubwa
    ela wametwama!
    Kisha: kwa magondi husimama
    pasi na nguvu huja kuima
    kutaka kugusa mbingu.
    Mara mojamoja hutazama chini,
    kuchungua mbilikimo
    na kuhakikisha,
    jinsi walivyoziteka akili zao
    kuzichezea, kuzisuguasugua
    mchezo wenye manufaa kwao
    Mara nyingine hutazama chini
    kutemea mate mbilikimo
    "Rasharasha ya marashi!"
    Utawasikia wakisema;
    Na
    ajabu mbilikimo hufarijika!
    Hivyo daima huendelea kwenda
    Huku wamesimama milingoti
    Kwa nadra hutokezea kusikia
    Mmoja ameshateguka
    na kupoteza uzani
    kwa ule unene wao
    Na kisha hulalama na kulani
    eti wameangushwa na mbilikimo!
  2. "Dhamira ya nafsneni ni kukashifu tabia za nafsinenwa," Thibitisha.
  3. Changanua mtindo katika shairi hili.
  4. Chambua muundo wa shairi hili.
  5. Fafanua toni inayodhihirika katika shairi hili.
  6. Bainisha nafsineni katika shairi hili.
  7. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari.

SEHEMU B: RIWAYA
A. Matei: Chozi la Heri
Jibu swali la 2 au la 3.

  1. Jadili nafasi ya vijana katika kuiendeleza na kuiumba jamii kwa mujibu wa riwaya ya Chozi la Heri. (alama 20)
  2. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali:
    "Mawio ya leo yanaelekea kuwa na kiza kisicho cha kawaida," anajisemea kijakazi Sauna huku akijipindua kuusikiliza mlio wa king'ora unaosikika kwa mbali. Anaenda miayo na kujikokota kutoka kitandani. Maungo yake yanahisika kuwa mazito kama nanga. Anatamani kurudi kitandani alale lakini inabidi amtayarishie Bi. Kangara kiamshakinywa, ana miadi ya mapema na mzalendo mmoja jijini. Sauna anaingia jikoni na kujifunga kimori, tayari kuanza kuchoma mandazi. Mara moyo unaanza kumwenda mbio na vipapasio vya akili yake kusimama wima. Anajihisi kama anayetarajia kuanza kinyang'ayiro kikali cha upiganaji masumbwi. Kwa umbali anasikia mbisho hafifu langoni mwa jumba hili. Anatoka nje kwenda kuitikia mbisho huu. Ghafla, uso wake unakumbana ana kwa ana na polisi! Mara anasikia moyo wake ukimwambia, "Yako ya arubaini imefika," huku akijaribu kuvaa tabasamu na kuwakaribisha maafisa hawa nyumbani.
  3. Bainisha aina nne za taswira zinazojitokeza katika dondoo hili.
  4. Changanua mtindo katika dondoo hili.
  5. Jadili ujumbe unaojitokeza katika masimulizi ya wahusika wafuatao:
  6. Kaizari
  7. Chandachema

SEHEMU C: TAMTHILIA
P. Kea: Kigogo
Jibu swali la 4 au 5
"Mashujaa halisi ni wale waliouliwa msituni wakipigana. Waliwahangaisha wakoloni hata wakawatimua. Hao waliofungwa walitufaa vipi? Mtu anaweza kutoa mchango gani akiwa gerezani? Uhuru wa waliofungwa ulikuwa mikononi mwa waliokuwa vitani. Kama wangelaza damu ama kuzembea, wafungwa wangejifia huko korokoroni."

  1. Yaweke maneno haya katika muktadha wake. (alama 4)
  2. Eleza mchango wa msemewa katika kujenga ploti ya tamthilia hii. (alama 5)
  3. Onyesha jinsi mashujaa halisi walivyopigania ukombozi wa Sagamoyo. (alama 11)
  4. "Umeugonga msumari kichwani nyanya, lakini wake nao wajirudi, wameenda sana!
    Vinginevyo asasi ya ndoa imo hatarini."
  5. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  6. Eleza vipengele viwili vya kimtindo vinavyojitokeza katika dondoo. (alama 2)
  7. Kwa kurejelea tamthilia nzima, thibitisha kuwa asasi ya ndoa imo hatarini. (alama 14)

SEHEMU D: HADITHI FUPI
A. Chokocho na D. Kayanda (Wah.): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine
Jibu swali la 6 au 7

  1. Eleza namna haki za watoto zinavyokiukwa katika hadithi ya "Tulipokutana Tena" (alama 10)
  2. Huku ukitoa mifano mwafaka, eleza matumizi ya jazanda katika hadithi "Shibe Inatumaliza" (alama 10)
  3. "Huwezi kushindwa na mtihani wa shule na vilevile kushindwa na mtihani wa maisha."
  4. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4)
  5. Eleza sifa sita wa msemaji wa maneno haya. (alama 6)
  6. Kwa kurejelea hadithi nzima ya Mtihani wa Maisha, onyesha jinsi msemewa anavyoshindwa na mtihani wa maisha. (alama 10)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI

Soma maigizo yafuatayo kisha ujibu maswali
MSAKATONGE: Limekucha sasa jua, nimetoka gizani, Haki zangu nazijua, tasema nataka nini, Mzigo huu najitua, siumbuki mwako kondeni, Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea.
MWENYETONGE: Hayo unayoyanena, hapa hayatakikani,
Ni hatia kubwa sana, kabisa iso kifani,
Mambo yaso na maana, kayasikia na nani,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.
MSAKATONGE: Malipo ninayopata, sio pesa ni mapeni,
Maisha yangu ni mwata, hayaniishi madeni,
Shida zinaniambata, kwa wangu umaskini,
Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea
Nitazame mwili wangu, sinayo siha mwilini,
Haitoshi kula yangu, kwa kuwa sina mapeni,
Ni mararu nguo zangu, nachekwa kiwa njiani,
Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea.
MWENYETONGE: Uchumi ‘meharibika, kote kote duniani,
Hata huko Amerika, walia nifanye nini,
Kuache kulalamika, uchangamke kazini,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.
Utaweza kuushika, uvuvi dhiki majini?
Mararu kujifunika, si fedheha mwafulani,
Mradi wanufaika na malipo hatimani,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.
MSAKATONGE: Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani.
Silioni lenye heri, kwa nguvu za muilini,
Inaniandama shari, nyumbani hata kazini,
Vifaa naweka chini, kazi leo nagomea.
MWENYETONGE: Basi tuache hasira, isiongoze njiani,
Tuitumie busara, tuketi hizi thenini,
Bila hata ya papara, tupime kwenye mizani,
Vifaa kuweka chini, wajitosa taabani.

  1. Bainisha kipera cha maigizo kinachorejelewa. Thibitisha jibu lako kwa mifano mitatu. (alama 4)
  2. Eleza ujumbe wa maigizo uliyoyasoma hapo juu. (alama 4)
  3. Eleza shughuli tatu za kiuchumi ambazo zimejitokeza katika utungo huu. (alama 3)
  4. Wewe ni mwigizaji wa michezo jukwaani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia katika uwasilishaji wako. (alama 5)
  5. Unanuia kutumia mbinu ya kuchunza/ utazamaji kukusanya habari kuhusu miviga ya tohara. Eleza manufaa manne ya kutumia mbinu hii. (alama 4)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1.      
    1. "Dhamira ya nafsneni ni kukashifu tabia za nafsinenwa," Thibitisha. (alama 5)
      • Nafsinenwa hawajielewi - Wanakwenda kumbe wamesita. 
      • Nafsinenwa ni mabinafsi - Nia zin'otoka ndani kuishia ndani, Maishilio ni nafsi zao
      • Nafsinenwa wana pupa na kukosa utaratibu na mpangilio - Wanapiga hatua kubwa, ela wametwama!
      • Nafsinenwa ni wenye tamma - pasi na nguvu huja kuima, kutaka kugusa mbingu
      • Nafsinenwa ni walaghai na wenye mbinu hasi za kujitakia makuu - na kuhakikisha, jinsi walivyoziteka akili zao, kuzichezea, kuzisuguasugua, mchezo wenye manufaa kwao
      • Nafsinenwa ni wenye dharau - Mara nyingine hutazama chini, kutemea mate mbilikimo
      • Nafsinenwa ni wenye kulaumu na kulaani wengine wanpokumbwa na shida - Na kisha hulalama na kulani , eti wameangushwa na mbilikimo!
        Zozote 5x1 = 5
    2. Changanua mtindo katika shairi hili. (alama 5)
      • Nidaa - Wanapiga hatua labda! Labda... labda... labda! Mwendo wa dhana yao!
      • Mdokezo - Wanakwenda... wanakwenda... Safari ya dhana... pekee
      • Takriri - Labda... labda... labda! 
      • Tanakuzi - Wanakwenda kumbe wamesita, Safari ya kuwepo na kutokuwepo! 
      • Tanakali za sauti - Hatua zao kubwa: chapchap... 
      • Tashbihi - Miondoko sawa na jongoo
      • Jazanda-Nia zin'otoka ndani kuishia ndani, kutaka kugusa mbingu, kutemea mate mbilikimo 
      • Taswira - Wanakwenda... wanakwenda... kutaka kugusa mbingu. kutemea mate mbilikimo 
      • Litifati - "Rasharasha ya marashi!" 
      • Ukwelikinzani - Wanakwenda kumbe wamesita. Wanakwenda pasi na kwenda
        Zozote 5x1 = 5
    3. Chambua muundo wa shairi hili. (alama 3)
      • Shairi lina beti saba 
      • Idadi ya mizani ya kila mshororo inabadilika badilika 
      • Idadi ya mishororo katika kila ubeti inabadilika badilika 
      • Beti za zna kipande kimoja 
      • Vina vya nje vinatofautiana kutoka ubeti hadi ubeti
        zozote 3x1 = 3
    4. Fafanua toni inayodhihirika katika shairi hili. (alama 2)
      Toni ya kukashifu / kukejeli / kudhihaki - Wanakwenda kumbe wamesita. Wanakwenda pasi na kwenda
      Yoyote 1x2 (kutambua moja na kutoa ithibati moja)
    5. Bainisha nafsinenwa katika shairi hili.
      (alama 2) Wakubwa katika jamii – Mara mojamoja hutazama chini,
      1x2=2
    6. Andika ubeti wa mwisho kwa lugha nathari. (alama 3)
      Ni nadra wakubwa kupata shida ila hilo inanetoken who halalamika na kulonni kuwa shida hiyo imesababishwa na wanyonge.
  2. Nafasi ya vijana katika kuiendeleza jamii yao katika Chozi la lleri,
    1. kupinga ubaguzi wa kiukoo. Mwangcka nn Apondi wnnafunga ndon licha ya koo zao kubaidika kama ardhi na mbingu. Lucia Kiriri kukubali kuolewa katika ukoo wa Waombwe licha ya ukoo wake wa Anyamvua kukataa.
    2. Kutoa msaada kwa maskini. Apondi na Mwungeka wanawasaidia maskini wanaomiminika kwao. Umu anampa Hazina sh. 200 ili anunue mkate.
    3. Kukashifu ukiukaji wa haki za binadamu. Apondi anawaonya walinda usalama dhidi ya mauaji ya kiholela.
    4. Kubadilisha imani potovu katika jamii. Mwangeka anabadilisha imani potovu ya jamii kuwa wanajeshi ulitengewa watu wa viwango vya chini vya elimu kwa kujiunga nao licha ya kuwa na shahada ya uhandisi.
    5. Kudumisha amani. Mwangeka anaenda Mashariki ya Kati kudumisha Amani.
    6. Kuwalea watoto wahitaji. Apondi na Mwangeka wanampanga Umu kama mwanao na kugharimia masomo yake.
    7. Kusuta visa vya uhalifu. Apondi anakashifu askari wanaogawana mali ambazo zimeibwa na wahalifu.
    8. Kuacha ulanguzi wa mihadarati. Dick anaacha biashara haramu ya kulangun dawa za kulevya na kuanzisha biashara halali ya kuuza vifaa vya simu.
    9. Kujielimisha. Dick anajiunga na chuo cha ufundi anakosomea Teknolojia ya Mawasiliano ya Simu.
    10. Kutoa ajira kwa vijana. Dick anawaajiri vijana baada ya kuanzisha biashara ya kuuza vifaa vya simu.
    11. Kupalilia msamaha. Dick anawahimiza nduguze Umu na Mwaliko kumsamehea mama yao Naomi baada ya kuwatelekeza.
    12. Kuacha matumizi ya vileo. Kipangga anabadilika na kuacha kunywa kangara iliyowaua walevi wenzake sabini.
    13. Kuthamini haki za watoto. Neema anakiokota kitoto kilichotupwa kwenye taka na kukipeleka kwenye kituo cha polisi.
    14. Kusitisha ukandamizaji. Wanafunzi shuleni wanasitisha ukandamizaji wao kwa Ridhaa baada ya mwalimu kuzungumza nao.
    15. Kutetea haki za wafungwa. Tila anataka kusoma na kuwa jaji katika mahakama kuu ili asikize kesi za washukiwa waliokaa kwenye rumande.
    16. Kupigania uhifadhi wa misitu. Lunga akiwa shuleni anawasuta viongozi wanaofyeka miti na kujenga viwanda.
    17. Kufanya vibarua ili kujitegemea. Chandachema anafanya kazi ili kupata pesa za kununua sare na madaftari.
    18. Kukashifu ukoloni mamboleo. Tila anakashifu hali ya taifa la Wahafidhina kuwa watoto wa miaka hamsini na kuwategemea wageni.
    19. Kusitisha ghasia. Baada ya vijana kugundua kuwa wanatumiwa na viongozi kama vilupizi vya ghasia, wanasitisha ghasia na amani inarejea nchini mwao.
    20. Kuwa na maazimio maishani. Chandachema ana azma ya kusoma na kuwa mwanasheria au afisa mkuu wa maslahi ya kijamii.
      zozote 20x1 = 20
  3.    
    1.       
      1. Aina za taswira katika dondoo
        • Taswira oni-uso wake unakumbana ana kwa ana na polisi. 
        • Taswira hisi-maungo kuhisika yakiwa mazito kama nanga.
        • Taswira sikivu - kuusikiliza mlio wa king'ora/ mbisho langoni.
        • Taswira mwonjo - kuchoma mandazi.
        • Taswira mwendo - anatoka nje kujikokota kutoka kitandani/kumwenda mbio. 
        • Taswira mguso-mbisho kwenye lango/kujifunga kimori/ vipapasio vya akili.
          Zozote 4 x 1 = 4
      2. Andika vipengele vingine vya kimtindo vinavyojitokeza katika dondoo.
        •  Nahau - enda miayo 
        • Chuku - maungo kuhisika kuwa mazito kama nanga. 
        • Tashbihi - mazito kama nanga/ anajihisi kama anayetarajia. 
        • Tashihisi/ubaishaji/uhuishi - moyo wake ukimwambia.
        • Mdokezo wa methali yako ya arubaini imefika.
        • Usimulizi wa wakati uliopo - mara anasikia... 
        • Taashira-vipapasio vya akili kusimama ni ishara ya woga. 
        • Nidaa/siyahi -ana kwa ana na polisi. 
        • Uradidi/takriri/urudiaji - neno mara
          Zozote 6x1=6
    2. Nafasi ya wahusika wafuatao katika kuijenga riwaya
      1. Kaizari
        • Inaelezea chanzo cha ghasia inayosababisha uharibifu
        • Inaonyesha suala la utabaka: msimulizi anaonyesha kwamba hata kifoni watu hutofautiana.
        • Inasawiri hali duni katika vituo vya afya; jamaa za wagonjwa wanahitajika kununua hata sindano.
        • Inakashifu ufisadi. Vijana wanatumiwa kuiba kura.
        • Inaangaza dhiki zinazowakumba wakimbizi.
        • Inaonyesha jukumu la vijana katika ujenzi wa jamii.
        • Inaonyesha mashirika ya kidini katika maisha ya kijamii. Wakimbizi wanaletewa chakula cha msaada na mashirika haya.
          Zozote tano -5x1=5
      2. Chandachema
        • Inachimuza maudhui ya malezi. Babake Chandachema anamtelekezea kwa nyanya; hashughuliki kuchunguza namna anavyokua.
        • Inadokeza masaibu yanayomkumba Chandachema. Anapata athari za kisaikolojia kwa Tenge na Satua anamtesa.
        • Kuonyesha ukiukaji wa haki za watoto. Anashiriki ajira ya watoto. Inachimuza maudhui ya umaskini. Anakosa mahitaji ya kimsingi kama sare za shule.
        • Inachimuza uwajibikaji. Anashughulika ajira ya watoti ili kujikimu kimaisha.
        • Kukashifu upujufu wa maadili. Ni zao la uhusiano wa Mwalimu Fumba na mwanafunzi wake Rehema.
          Zozote tano -5x1 = 5
  4.    
    1. Msemaji - Sudi
      Msemewa - Ngurumo
      Mahali - Mangweni
      Kiini . Tunu na Sudi wamefika kuwaalika wote katika mkutano mkubwa utakaofanyika mbele ya lango kuu la soko la Chapakazi siku ya maadhimisho ya uhuru. Ngurumo na walevi wengine hawapendezwi na mwaliko huo.
      4x1=4
    2. Eleza mchango wa msemewa katika kujenga ploti ya tamthilia hii. (alama 5)
      • Kupitia Ngurumo tunaonyeshwa usuli wa utoaji wa kandarasi ya uokaji keki. Yeye na Asiya walimwandama Husda. 
      • Kupitia Ngurumo tunaonyeshwa mgogoro kati ya wazalendo na vibarakala. 
      • Kupitia Ngurumo tunapata wahusika wengine kama mwalimu wake wa historia na ulevi wa awali wa Siti..
      • Anafanikisha maudhui kama vile ukatili, uporomovu wa maadili na ubarakala.
      • Kupitia Ngurumo tunafichuliwa matukio fulani kama aliyemuumiza Tunu. Anaashiria mguu wa Tunu ulioumia.
      • Kupitia Ngurumo tunaonyeshwa hatima ya mgogoro baina ya viongozi na wanyonge. Anauliwa.
      • Kupitia Ngurumo tunaonyeshwa mustakabali wa Sagamoyo. Yeye na vijana wengine walevi wanaundeleza uongozi dhalimu wa Majoka.
      • Wimbo anaouimba Ngurumo ni kipengele cha ploti. Anautumia kuonyesha ubabedume wake
        5x1=5
    3. Onyesha jinsi mashujaa halisi walivyopigania ukombozi wa Sagamoyo. (alama12)
      1. Sudi anakataa kuchonga kinyago anachotaka Majoka ila kuchonga cha Tunu
      2. Sudi kumuunga Tunu katika harakati za kuwakomboa wanasagamoyo 
      3. Sudi kukataa kula keki ambayo ni makombo sababu uhuru wa kufurahia haupo 
      4. Sudi kukataa ahadi ya zawadi ikiwa atachonga kinyago sababu ni kubadhiri pesa za mkopo
      5. Tunu kusomea sharia ilia je kuwakomboa wanasagamoyo kutoka kwa dhulma za Majoka
      6. Tunu kukabiliana na Majoka afisini ili soko lifunguliwe 
      7. Tunu na sudi kuwasihi walevi kule Mangweni kuhudhuria mkutano sokoni ili wahamasishwe kuhusu umuhimu wa uhuru, kufunguliwa kwa soko, uongozi nk
      8. Ashua kutokubali kazi ya Majoka ya ualimu sababu shule hiyo inaendelea kukuza wanafunzi wasio na umuhimu wowote - makabeji
      9. Walimu na wauguzi wanagoma ili mishahara yao iongezwe na ilipwe kwa wakati
      10. Asiya kuwacha kuuza pombe ili watu wasiendelee kufa
      11. Asiya, Kingi, Kenga wanajiunga na mrengo wa Tunu ili pawepo mabadiliko
      12. Umati unamshangilia Tunu kuwa kiongozi wao husu ukimkashifu Majoka
      13. Gazeti na runinga kuangazia harakati za wazalendo za kukomboa Sagamoyo
      14. Wanasagamoyo kususia mkutano wa Majoka na kushabikia ule wa Tun
  5.    
    1. Muktadha wa dondoo
      Maneno ya Majoka Anamwambia Husda Wamo ndani ya ambulensi Baada ya Husda kumwambia Majoka kuwa wanaume wanastahili kuufikiria upya uume wao na waseme na wake zao. (4x1=4)
    2. Vipengele vya kimtindo.
      • Nidaa - wameenda sana! 
      • Nahau - umeugonga msumari kichwani 2x1 - 2
    3. Thibitisho kuwa asasi ya ndoa imo hatarini.
      1. Kushinikizwa kuoa; Majoka alilia na machozi kumwisha kwa kulazimishwa kuoa Husda.
      2. Ukosefu wa upendo; Majoka anakiri kuwa hampendi mkewe Husda.
      3. Kupenda mke wa mwingine; Majoka anampenda Ashua na kumtamani kimapenzi licha ya kuwa mkewe Sudi. 
      4. Kupiga mke - Majoka anamwambia Husda kuwa asimfanye amuumize akizomeana na Ashua na kumuuliza iwapo amemsahau; ishara ya kuwa Majoka humpiga.
      5. Kudhalilisha mke - Majoka anamdhalilisha mkewe Husda kwa kumwambia 'Shut up woman' mbele ya Ashua.
      6. Kutelekezwa kwa majukumu ya unyumba. Husda anateta kuwa mumewe Majoka haonekani nyumbani kwake.
      7. Uchochezi. Majoka anamchochea Ashua kuivunja ndoa yake kwa kumhimiza kuomba talaka mumewe.
      8. Kufunga mke. Majoka anazorotesha uhusiano wake na mkewe kwa kumfunga.
      9. Kuomba talaka. Ashua anaomba talaka mumewe Sudi kwa madai kuwa amechoka kupendwa kimaskini.
      10. Uzinifu. Mamapima anamsaliti mumewe Boza kwa kuzini na Ngurumo.
      11. Kupenda mali badala ya mume. Majoka anateta kuwa mkewe Husda anapenda mali zake na hampendi yeye.
      12. Kutoaminiana. Husda anazua fujo ofisini mwa Majoka anapomkuta mumewe na Ashua na kudhani kuwa Ashua ni kimada wake.
      13. Kutamani waume nje ya ndoa. Husda anamtazama Chopi kwa macho ya uchu na kumtamani kimapenzi.
      14. Ujane. Bi. Hashima na mkewe Ngurumo wanabaki wajane baada ya waume zao kufa.
      15. Kurithi mjane. Japo Majoka ana mkewe Husda, anataka kumrithi Bi. Hashima baada ya kifo cha mumewe.
      16. Ndoa za kupangiwa. Majoka anapanga kumwoza Tunu kwa Ngao Junior japo Tunu anakataa.
      17. Kuchelewa kuolewa. Tunu amehitimu masomo ila haolewi hadi walevi wanaimba nyimbo za kumkejeli.
        Zozote 10 x 1 =10
  6.    
    1.      
      1. Kufanyizwa kazi. Bi. Sinai anamtumia Bogoa kuchanja kuni, kufagia, kufua na kuteka maji kisimani
      2. Kuamshwa mapema. Bi. Sinai anamwamsha Bogoa alfajiri kuchoma mandazi na kuyapeleka shuleni kuyauza.
      3. Kufanyizwa biashara. Bi. Sinai anamtumia kuuza maandazi shuleni badala ya Bogoa kuwa shuleni kusoma.
      4. Kubaguliwa. Bi. Sinai anamwambia wanawe kuwa watoto wa kimaskini hawakustahiki kusoma.
      5. Kunyimwa uhuru wa kucheza na watoto wa majirani. Sinai anamzuia Dugua kucheza na watoto wa majirani ila kwa kutoroka.
      6. Kuchapwa. Bogoa anapochelewa kurudi kutoka mchezoni, Bi. Sinai anampiga vibaya.
      7. Kuzuiliwa kutangamana na wazazi. Bi. Sinai anamzuia Bogoa kutangamana na wazaziwe wanapomtembelea.
      8. Kula makombo. Bi. Sinai anamwacha Bogoa kula makombo ya watu waliyoacha baada ya kushiba.
      9. Kuwa wa mwisho kula. Bogoa ni mtoto ila ndiye anayekula wa mwisho wakati kila mtu ameshakula kwa Bi. Sinai.
      10. Kulia sufuriani. Bogoa anakula kweliye sufuria na vyungu kwa Bi. Sinai wakati kila mtu alikula sahanini.
      11. Kuchomwa. Bi. Sinai anamchoma Bogoa viganajani baada ya kusinzia na kuyaacha maandazi kuungua.
      12. Kutusiwa. Bi. Sinai anamtusi na kumsimanga Bogoa.
      13. Kutishwa. Bi. Sinai alimtisha Bogoa kuwa angemkata ulimi kama angesema chochote kuhusu madhila aliyopitia kwake.
        Zozote 10 x 1 =10
    2. Matumizi ya jazanda katika hadithi "Shibe Inatumaliza"
      1. Anwani Shibe Inatumaliza ni jazanda ya madhara ya ufisadi/ufujaji wa pesa za umma.
      2. Kupika wanapika wapikao lakini Mzee Mambo kazi yake ni kupakua. Kupika ni jazanda ya kufanya kazi na kupakua ni jazanda ya Mambo kupokea mshahara.
      3. Walaji na wanywaji kwa Mzee Mambo wanakula bila kuchunguza mpishi ni nani na hivyo vyakula vimepikwaje. Mpishi ni jazanda ya wafanyikazi; vyakula ni
        jazanda ya rasilimali zinazoporwa na viongozi fisadi. Kutochunguza ni jazanda ya jinsi viongozi fisadi wanavyopora rasilmali za umma bila kuwazia athari zake.
      4. Jungu linalopelekwa nyumbani kwa Mambo ni jazanda ya rasilmali za taifa.
      5. Tendo la Sasa na Mbura kuwahi foleni tena na tena na kupakua chakula mara tatu ni jazanda ya tamaa na ubinafsi wa viongozi.
      6. Mchele wa Mbeya ni jazanda ya bidhaa za nchi zinazopuuzwa na Waafrika.
      7. Mchele wa basmati ni jazanda ya vyakula vinavyozalishwa na vya kigeni ambavyo vinapendwa na Waafrika.
      8. Magonjwa yanayosababishwa kutokana na ulaji ni jazanda ya matokeo ya ufisadi Wimbo wa sijali lawama ni jazanda ya jinsi viongozi hupuuza wananchi na hawajali hisia zao.
      9. Waziri kivuli ni jazanda ya wafanyakazi ambao hawana majukumu maalum na hupata mshahara bila kufanya kazi.
      10. Kula bila kushiba ni jazanda ya viongozi kula bila kutosheka na kuendelea kula mali ya umma tena na tena.
      11. Mitambo ya wasapu, fesibuku na runinga ya taifa kurusha sherehe moja kwa moja ni jazanda ya jinsi vyombo vya habari huangazia mambo yasiyokuwa na maana. Zozote 10x1-10
  7.    
    1. Muktadha wa dondoo
      Maneno ya mamake Samueli.
      Akimwambia Samucli.
      Wako katika ukingo wa bwawa.
      Hii ni baada ya Samueli kutaka kujitosa majini na babake kumpa kamba ajimalize kisha mamake akatokea.
    2. Sifa za mzungumzaji
      Mzungumzaji ni mamake Samueli.
      1. Mwenye busara. Anamweleza Samueli kuwa Mungu hamkoseshi mja wake yote.
      2. Mwenye utu. Anapompata Samueli akitaka kujiua, anamshika mkono mwanawe bila kumhukumu wala kumwadhibu.
      3. Mwajibikaji. Yeye huandalia familia yake lishe.
      4. Mshauri mwema. Anamshauri Samueli kuwa mustakabali wa familia nzima unategemea mafanikio ya Samueli ilia atie bidi masomoni.
      5. Mwenye matumaini. Ana matumaini kuwa Samueli ataikwamua familia hiyo kutoka kwenye ulitima akifanikiwa masomoni.
      6. Mlezi mwema. Licha ya babake Samueli kumpa Samueli kamba ajimalize, anamshika mwanao Samueli mkono na kumweleza waende nyumbani watafute suluhu. Za kwanza 6x1= 6
    3. Jinsi Samuli anavyoshindwa na Mtihani wa Maisha.
      1. Anashindwa kujidhibiti kimawazo akiwa katika foleni. Amejawa wasiwasi na ana mtafaruku wa hisia ikiwa amepita au amefeli.
      2. Anamsimanga mwalimu mkuu na kumwita hambe. Hivyo anafeli mtihani wa maisha kwa kutoheshimu wakubwa wake.
      3. Anashindwa kujasirika na kukubali matokeo yake hadharini na badala yake anajitoma katika faragha ya msalani ili ajionee matokeo yake ya mtihani.
      4. Alishindwa kukubali udhaifu wake masomoni alipokuwa mwanafunzi.
      5. Anajishaua kuwa yeye si mjinga na kuwa alijua mito yote Afrika.
      6. Anashindwa kukubali kufeli kwake na kuamua kumhadan babake kuwa mwalimu mkuu hajampa matokeo kwa vile hakumaliza kulipa karo.
      7. Anashindwa kujidhibiti kihisia anapopapia mapenzi akiwa angali mwanafunzi. Alikuwa na kipenzi chake Nina. Anatamauka maishani na kuwazia kujiua kwa kujitosa majini.
      8. Anashindwa kudhibiti kihoro na dhiki za kisaikolojia zinazomwandama baada ya kupokea matokeo yake.
      9. Anakosa kuwa na mlahaka mwema na wanafunzi wenzake. Anawasimanga na kuwaita chakumbimoi wenye tabia za kumbikumbi.
      10. Akiwa mwanafunzi alikuwa na mahoka na alibandikwa lakabu 'rasta'. Hii inaonyesha alivyoshindwa kuhimili mazingira na ulimwengu wa shule na masomo.
      11. Anashindwa na mtihani wa maisha anapofananisha kufeli mtihani wa shule na kufeli maishani. Kulingana naye, baada ya kufeli mtihani wa shule, kuishi hakuna maana tena.
      12. Anashindwa kuwaambia wanafunzi wenzake kuhusu matokeo yake.
      13. Anamhadaa Nina kuwa alikuwa bingwa masomoni.
      14. Anawazia kubadilisha alama zake katika cheti chake.
      15. Anashindwa kuelewa mambo darasani.
        Zozote 10 x 1 = 10
  8.    
    1. Bainisha lipera cha maigizo kinachorejelewa. Thibitisha jibu lako kwa mifano mitatu. (alama 4)
      Ngonjera
      • Kujibizana kwa wahusika wawili 
      • Wahusika kupingana mwanzoni. 
      • Wahusika hufikia uafikiano kufikia mwisho. 
      • Mhusika mmoja huzua jambo na mwingine hujibu. 
      • Huendelezwa kwa njia ya ushairi.
        Kipera = 1. Ithibati 3x1 =3
    2. Eleza ujumbe wa maigizo uliyoyasoma hapo juu. (alama 4)
      • Mwajiriwa amezinduka, anazifahamu haki zake na kuzitetea. 
      • Mwajiri anaghairi kusikiliza malalamishi ya mwajiriwa - unayoyanena, hapa hayatakikani
      • Mwajiriwa anapata mshahara duni ambao unaendelea kuyaza umaskini wake.
      • Uchumi umeharibika kote kote duniani 
      • Kugomea kzi ni kujitosa taabani - mahitaji utayakosa. 
      • Njia mojawapo ya waajiriwa kupigania haki zao ni kugoma / kususia kazi. 
      • Mwajiriwa anapitia dhuluma kiwandani - Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani. 
      • Mwajiriwa ni mvumilivu - Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani. 
      • Basi tuache hasira, isiongoze njiani,
      • Mwajiri na mwajiriwawawache na watumie busara, kusuluhisha tofauti zao bila papara.
        4x1 =4
    3. Eleza shughuli tatu za kiuchumi ambazo zimejitokeza katika utungo huu. (alama 3)
      • Kilimo-siumbuki mwako kondeni, 
      • Uvuvi - Utaweza kuushika, uvuvi dhiki majini?
      • Viwanda - Kwa miaka na dahari, natumika kiwandani.
        3x1 =3
    4. Wewe ni mwigizaji wa michezo jukwaani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia katika uwasilishaji wako kifungu. (alama 5) 
      1. Kuzungumza moja kwa moja na hadhira - mjukuu wangu sijui kama umewahi kuwazia
      2. Kujenga taswira zinazoweza kutambulika na hadhira. - kutetemeka kama kondoo/shikwa na mtapo 
      3. Kushirikisha hadhira kwa kuuliza maswali - ungekuwa Msakatonge ungefanya nini? 
      4. Matumizi ya lugha sahili
      5. Taharuki / lugha inayojenga taharuki.
      6. Kujivika maleba yanayooana na kinachoigizwa ili kutia uhai maigizo.
      7. Matayarisho kabambe kabla ya maigizo.
      8. Lugha yenye ufundi wa juu kama vile picha, mafumbo na tamathali za usemi
      9. Matumizi ya ishara na viziada lugha
      10. Udramatishaji kwa kucheza na kadhalika
        Za kwanza 5x1 = 5
    5. Unanuia kutumia tabinu ya kuchunza / utazamaji kukusanya habari kuhusu miviga ya tohara. Eieza manufaa manne ya kutumia mbinu hii. (alama 4)
      1. Kupata habari za kuiegemewa na kuaminika.
      2. Ni rahisi kuzek ai kama vile kwa vinasa sauti, video na kadhalika.
      3. Ni njia bora kwa wasiojua kusoma na kuandika
      4. Kuweza kupata sifa za uwasilishaji kama vile. toni/kiimbo, ishara na kadhalika.
      5. Kuweza kupatsie Salisi za uwasilishaji.
        Za kwanza 4x1 =4
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - Maranda Pre-Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest