Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 2

Share via Whatsapp

Maswali

Maagizo

  • Andika insha mbili. Insha ya kwanza ni ya lazima.
  • Kisha chagua insha nyingine moja kati ya hizo tatu zilizobakia.
  • Kila insha isipungue maneno 400.
  • Kila insha ina alama 20.
  • Kila insha lazima iandikwe kwa lugha ya Kiswahili.

 

  1. Wewe ni mhariri mkuu wa Gazeti la Mwangaza, andika tahariri kuhusu namna tatizo la ukosefu wa nafasi za ajira miongoni mwa vijana linavyoweza kukabiliwa.
  2. Serikali za ugatuzi zina faida nyingi kuliko hasara . Jadili
  3. Andika insha inayooana na methali kutangulia si kufika
  4. Andika insha itakayoanza kwa maneno haya:
    Milipuko mikubwa ilisikika pu! Pu! Puu! Kisha niliwaona watu wakikimbia kuelekea pande zote…

Mwongozo wa Kusahihisha

  1. MAJIBU
    Hii ni tahariri ambapo muundo lazima uzingatie yafuatayo
    1. Jina la gazeti – Mwangaza
    2. Tarehe km Oktoba 23, 2021
    3. Kichwa – Utatuzi wa Ukosefu wa Ajira
    4. Utangulizi – ataje maelezo yakimsingi kuhusu ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana
    5. Mwili – hapa ndipo maudhui kuhusu mapendekezo ya kubuni nafasi za ajira zitolewe
    6. Hitimisho – maoni matarajio.
    7. Anwani/Ya barua pepe, Jina la mhariri .

      Baadhi ya hoja
      • Mja mmoja asiruhusiwe kushikilia zaidi ya wadhifa mmoja/zaidi ya kazi moja.
      • Wageni wowote wale wasipewe vibali ‘vya kuajiriwa nchini mwetu.
      • Viwanda zaidi vianzishwe hususa katika sehemu za mashambani na vile vilivyofungwa vifufuliwe
      • Hali ya usalama iimaarishwe ili wageni wanaotaka kuwekeza nchini na katika kaunti zetu wafanye hivyo bila hofu ya kupoteza mali yao.
      • Mtu yeyote aliyetimiza umri wa kustaafu (miaka 60) asipewe kandarasi ya kuendelea na ajira ilhali vijana hawana kazi.
      • Nchi yetu isiagize baadhi ya vifaa kutoka ng’ambo badala ya kuvizalisha nchini mfano mchele,viberiti,fanicha n.k.
      • Watu waelimishwe kuhusu umuhimu wa kujiajiri
  2. Serikali ya ugatuzi ina faida nyingi kuliko hasara. Jadili.
    • Hii ni insha ya mjadala.
      Faida za serikali.
    • Ajira itakuwa na usawa.
    • Raslimali kutumiwa na wananchi wenyewe.
    • Miundo msingi kuboreshrwa.
    • Utawala kuwa karibu na wananchi.
    • Maendeleo kusawazishwa sehemu zote nchini.
    • Kuleta huduma muhimu karibu na watu.
    • Kuzidisha uwajibikajji wa watawala.
    • Kupanua uwakilishi wa watu.
    • Kushirikisha jinsia zote uongozini.
      Hasara za serikali ya ugatuzi.
    • Kodi itaongezeka hasa katika majimbo maskini.
    • Gharama ya maisha itapanda –watawala watakuwa wengi.
    • Kuleta tofauti za kimaendeleo.
    • Hasira kikabila zitakuzwa.
    • Mvutano baina ya serikali kuu na ugatuzi.
    • Mapendeleo katika kutoa ajira.
    • Huenda watu wasiohitimu kupata kazi katika maeneo Fulani huku waliohitimu wa kikosa kuajiriwa kwingineko.

      TANBIHI.
    • Mtahiniwa azingatie pande zote mbili
    • Akiegemea upande mmoja tu asipate zaidi ya alama 10
  3. kutangulia si kufika. Hili ni swali la methali
    • Mtahiniwa si lazima aeleze maana ya methali .
    • Mtahiniwa aanze na kisa moja kwa moja .
    • Dhana ya kutangulia ieleweke vizuri katika kisa chake.
    • Aonyeshe sehemu hizo mbili.
      1. Kutangulia kwa maana ya mafanikio maishani –utajiri, elimu na nyanja zingine za maisha.
      2. Si kufika
        Utajiri kuisha na wengine kuibuka matajiri au kupitwa na wengine katika uwanja wa maisha.
        1. Mwanafunzi achukue msimamo yaani kuunga mkono methali kwani kila methali ni ukweli usiopingika.
        2. Mwanafunze aepuke msamiati wa paukwa pakawa ambacho ni kipengele cha fasihi simulizi.
  4. Ni sharti mtahiniwa aanze kwa maneno aliyopewa.
    Anatakiwa kuanza kwa maneno yale bila ya kubadilisha wala kuyapunguza.
    Kisa chake kiwa cha kuvutia na aonyeshe ni matukio yapi yaliyosababisha milipuko ile, kulikuwa na majeruhi na watu walitoroka kwenda wapi? Ni nini kilichotokea baada ya hapo? 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 1 Questions and Answers - KCSE 2022 Mock Exams Set 2.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?