Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Maranda High Pre Mock Exams 2023

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote
  1. Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Mbuga ya Ziwa Nakuru, sasa limesafishwa katika mojawapo ya juhudi za kukabiliana na maji taka yanayoingia mbugani. Wasimamizi wa mbuga walitumia huduma za vijana wasiokuwa na ajita kutoka mitaa ya Bondeni, Kivumbini, Lake view Freearea na Flamingo kusafisha mito inayobeba uchafu huo.

    Vibarua walizoa jumla ya tani 1.5, na baadaye tani 4.2 idadi inayofikisha zaidi ya tani 6.0 kwa siku mbili mfululizo.Hili linaashiria jinsi kina cha uchafuzi wa mazingira kwenye ziwa Nakuru umeshamiri,na baadhi ya wafanyikazi wanaona litajwe kuwa janga la kitaifa linalokodolea macho mbuga nyingi humu nchini.

    Shughuli hiyo ilivutia hisia mseto huku maswali mengi kuliko majibu yakiibuka, endapo KWS ina bajeti ya kung'arisha mbuga za wanyama.

    Akizungumza na Taifa Leo,mwangalizi wa utalii kutoka ya wanyama ya Ziwa Nakuru Bw Sirman Kioko,alisema maji taka yamekuwa yakiingia  kwenye mbuga kutokana na miundo msingi duni.Aliongezea kuwa maisha ya wanyama hasa simba, nyati, vifaru, chui, viboko na flamingo yalikuwa hatarini kwa sababu ya maji taka yalikuwa yamebadili mkondo na kupenyeza kwenye mbuga.

    Miaka mitano iliyopita mbuga ya Nakuru ikuwa na idadi kubwa ya ndege aina ya heroe, lakini sasa wamebakia 200 tu. Hali hii itazidi kuwa mbaya,endapo idara husika haitaweka mikakati ya kutafuta suluhu la kudumu kwa wanyama pori wanaozidi kuangamia. Aidha uchafuzi katika ziwa Nakuru umefanya ndege kuhamia ziwa Bogoria ambapo inaaminika angalau chakula ni tele. "Tunakubali kuwa gharama ya kusafisha mbuga ni kubwa, lakini pia tunaomba umma kupunguza matumizi ya mifuko ya plastiki inayoziba njia za maji,"alisema.

    Pia aliongezea kuwa ni jukumu la mbuga kusafisha mazingira ya wanyama,lakini baraza la mji wa Nakuru pia lina nafasi kubwa ya kuhakikisha makazi ya watu ni safi,kwa kuzoa taka ipasavyo. Anaona kuna utepetevu mkubwa kutoka kwa usimamizi wa mazingira NEMA,wanaostahili kuweka sheria kali za kukabiliana na wale wanaoharibu mazingira.

    Aliongezea kuwa baraza la kusimamia huduma za wanyama pori (KWS),halina bajeti ya kusafisha mbuga na ndio sababu waliwaajiri vibarua saba kuendesha shughuli hiyo ya siku tatu. Uchafuzi wa mito inayoingia ziwa Nakuru hutokea msimu wa mvua ambapo maji hufurika na kusomba taka kutoka kwenye makazi ya watu.

    Wanyama wanaovutia watalii kama vile Nyati hupata maradhi wanapokunywa maji chafu, yaliyochanganyika na mifuko ya plastiki. Licha ya KWS kumiliki kituo cha kufanyia utafiti aina ya maradhi mbalimbali yanayokabili wanyama bado hawajafanikiwa kwa asilimia kubwa kuyazuia.

    Hili linajiri siku moja tu baada ya wakazi wa mtaa wa Bondeni kuandamana barabarani wakilalamikia,ongezeko la kiwango cha takataka kwenye makazi ya watu.
    (Imenukuliwa kutoka kwa Gazeti la Taifa Leo)

    Maswali
    1. Ipe taarifa hii kichwa mwafaka.  (alama 1)
    2. Eleza sababu zinazofanya Ziwa Nakuru kuchafuka.  (alama 2)
    3. Ni nini madhara ya kuchafuliwa Ziwa Nakuru?(alama 4)
    4. Eleza vizingiti vinavyofanya ziwa hili kuendelea kuchafuliwa.   (alama 2)
    5. Toa mapendekezo yanayoweza kusaidia kumaliza uchafuzi wa Ziwa Nakuru kulingana na taarifa hii. (alama4)
    6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika taarifa. (alama 2)
      1. Kupenyeza
      2. Utepetevu
  2. MUHTASARI
    Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.


    Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili na maarifa fuvu tele ili kuratibu shughuli na mambo; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhifadhi viumbe wengine kwa njia mbalimbali na jumla jamala; hichi ndicho kiumbe kilichopewa idhini maalum ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama Hawa anbaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe.

    Kwa sababu ya bongo alizonazo, binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake na ithibati zipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari; amefika mwezini; amevumbua mangala; amevumbua uyoka; amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni za kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu.

    Chambacho wavyele akili nyingi huondoa maarifa. Binadamu amekuwa dubwana linalojenga kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole. Rabana ndiye msanii asiye mfanowe kwani aliisawiri dunia kwa kila lililo jema kwa siku sita mtawalia na kumpa binadamu mazingira murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri; akamwambia binadamu, "Haya, twende kazi !"

    Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji-taka ovyo hadi mitoni, maziwani na baharini na matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya majini kama samaki ambavyo ni urithi aliyopewa na muumba. Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili Maisha bila maji safi. Maji yote sasa yametiwa sum na binadamu kwa sababu ya 'maendeleo yake. Joshi kutoka katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyesha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta mdhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa 'tsunami' bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima. Vimbunga navyo vimetokea kwa wingi. Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi?

    Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni Imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongo wa kuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote.Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe.

    Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba, mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengi kuangamia kwa sababu ya ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemchemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia Kamba motoni. itambidi aanze kujenga kwa matofali ya barafu.

    MASWALI
    1. Jadili jinsi binadamu ana veza kutumia uwezo wake vizuri.   (alama 6)
      Matayarisho 
      Jibu
  3. SARUFI
    1. Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/ . (alama 2)
    2. Andika neno lenye vipengele vinavyofuata vya kikanushi, ngeli , wakati, kitendwa, mzizi na kiishio.  (alama 2)
    3. Tumia kitenzi kishirikishi kipungufu bila kupoteza maana ya sentensi hii. (alama 2)
      Mwanafunzi mmoja angali analala bwenini
    4. Andika sentensi katika wakati usiodhihirika ukitumia nomino moja ya jamii. (alama 2)
    5. Tungia sentensi moia ukitumia neno ziara na maziara ili kubainisha maana zao.   (alama 2)
    6. Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii.  (alama 2)
      Wanakujua huku.
    7. Ainisha sentensi zifuatazo kimuundo.   (alama 2)
      1. Mimi sijaelewa kamwe somo hili.
      2. Watoto ambao walipotea juzi wamepatikana leo asubuhi.
    8. Andika sentensi inayofuata katika usemi halisi ukianza na kihisishi cha dharau. (alama 3
      Mzee Anandwa alishangaa na kusema kuwa kijana huyo alikuwa amekuwa kaida kama Kirongwe.
    9. Bainisha tofauti na usawa kati ya mofimu na viambishi  (alama 2)
    10. Ainisha vishazi katika sentensi.
      Endapo atanialika, nitamtembelea. (alama 2)
    11. Tambua kiima, aina za shamirisho na chagizo katika sentensi hii. (alama 3)
      Kimemletea taabu sana.
      Kiima
      Shamirisho: 
      Chagizo:
    12. Andika umoja wa sentensi inayofuata katika hali yakinifu. (alama 2)
      Kina mama wasingefika mapema fuoni, wasingewahi mashua.
    13. Tumia kivumishi cha a- unganifu katika sentensi ili kuleta dhana ya sifa. (alama 2)
    14. Tumia O rejeshi tamati. Mwanafunzi ambaye hufanikiwa ni yule ambaye hudurusu kwa makini.  (alama 2)
    15. Bainisha matumizi ya 'KI' katika sentensi hii. (alama 2)
      Seremala akiwasili leo atakuwa akitengeneza kiti cha kitoto chake.
    16. Pambanua kwa michoro ya mstari sentensi inayofuata.
      Ikiwa atawasili mapema, atafungua mkutano
    17. Onyesha na ueleze matumizi ya viwakilishi vifuatavyo. (alama 2)
      Kibainishi
      Mkwaju 
    18. Tofautisha matumizi ya 'Ngali' katika tungo hizi.   (alama 2)
      Mama angali mlimani
      Otiende angalisoma kwa bidi angaliishi maisha mema.
    19. Mkwezi hupanda miti _________________ hufanya kazi maktabani, mpanzi _________________ huendesha gari la moshi na mpagazi _____________________  (alama 2)
  4. ISIMUJAMII    (ALAMA 10)
    ... Bwana Spika, ninaomba kufahamishwa kwa nini Waziri wa Biashara ameshindwa kuchuka hatua kukomesha uuzaji wa vileo hatari kwa watoto wa shule.
    1.  
      1. Kwa kutolea mfano taja sajili iliyodokezwa hapo juu.  (alama 2)
      2. Fafanua sifa zozote nane za sajili inayorejelewa na maneno haya   (alama 8)

MARKING SCHEME

  1.  
    1. Ipe taarifa hii kichwa mwafaka.  (alama 1)
      • MAZINGIRA...
      • MBUGA ZA WADHAMA
    2. Eleza sababu zinazofanya Ziwa Nakuru kuchafuka.    (alama 2)
      • Miundo Misingi duni.
      • Matumizi ya mifuko ya plastiki inayoziba njia za maji
      • Ukosefu wa bajeti ya kusafisha mbuga za wanyama
      • Utepetevu kutoka kwa wasimamizi wa mazingira NEMA
      • Kutokuwajibika kwa wafanyikazi, kuhakikisha makazi ya wanyama ni safi.
    3. Ni nini madhara ya kuchafuliwa kwa Ziwa Nakuru?  (alama 4)
      • Maisha ya wanyama kuwa hatarini na hata kufariki
      • Ndege kuhamia ziwa Bogoria kutafuta chakula 
      • Idadi kubwa ya ndege kudidimia, kupungua
      • Wanyama pori  kuzidi kuangamia.
      • Wanyama wanaovutia watali K.V Nyati hupata Maradhi pindi wanapokunywa maji chafu
    4.  Eleza vizingiti vinavyofanya ziwa hili kuendelea kuchafuliwa   (alama 2)
      • Misimu ya mvua ambapo maji hufurika na kusomba taka kutoka kwenye makazi ya watu.
      • Utepetevu mkubwa kutoka kwa usimazizi wa mazingira.
      • Matumizi ya mifuko ya plastiki inayoziba
      • Kuweka mikakati Imara ya kushughulikia mafuriko
    5. Toa mapendekezo yanayoweza kusaidia kumaliza uchafuzi wa Ziwa Nakuru kulingana na taarifa hii. (alama4)
      • Usimamizi wa Mazingira NEMA, kuweka sheria kali kukabiliana na wale wanachafua mazingira.
      • Kuifahamisha umma kutotupa mifuko ya plastiki ovyo na athari za mifuko hio.
      • Kuhakikisha makazi ya watu ni safi, kwa kuzoa taka.
    6. Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika taarifa (alama 2)
      1. Kupenyeza - kuingia kwa lazima
      2. Utepetevu - uvivu
  2. MUHTASARI
    1. Jadili jinsi binadamu anaweza kutumia uwezo wake vizuri.  (alama 6)
      Matayarisho
      1. Kuratiba shughuli na mambo.
      2. kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala.
      3. Kufaidi viumbe wengine kwa njia mbalimbali.
      4. Kuzaana na kujaza dunia.
      5. Kutumia teknolojia kwa manufaa yake.
      6. Viwanda ya binadamu vinatiririsha maji-taka maziwani na baharini na kusababisha vifo vya viumbe vya majini.
      7. Moshi kutoka viwandani limeḥasiri ukanda wa ozoni ambao umeleta jua kali linalosababisha joto kali.
      8. Mvua ya asidi inayonyesha katika sehemu nyingi inaleta madhara makubwa.
      9. Bahari ilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu,
      10. Vimbunga navyo vimetokea kwa wingi.
      11. Viwango vya miyeyuko na maji yatazidi kwa sababu ya joto.
      12. Maradhi na ufukura zimehamia kwa binadamu kwa sababu ya idadi yao kuongezeka.
      13. Binadamu amefyeka misitu hivyo basi kuwafurusha wanyama kwa kukosa chakula na kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira
      14. Chemichemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi.
  3. SARUFI
    1. /a/ hutamkwa kati ya ulimi ilhali /e/ hutamkwa mbele ya ulimi
    2. hazikumpita (kadiria)
    3. Mwanafunzi mmoja yu bwenini (kadiria)
    4. Umati wa watu waelekea shuleni (kadiria)
    5. Katika ziara yao walienda kwenye ziara (kadiria)
    6.  
      • Wanakujua eneo hili (kadiria).
      • Mahali kusikodhihirika
    7.  
      1. Sahili
      2. Changamano
    8. zii! Aka! Ebo! Ng'o! Wapi! Poko! Ebo! Kijana huyu ni kaidi kama Kirongwe Mzee Anandwa alisema. (Asipoanza na kihisishi cha dharau atuzwe 0)
    9. Usawa - zote huwa na maana kisarufi
      Tofauti - katika viambishi, mzizi si sehemu ya viambishi ilhali katika mofimu, mzizi ni sehemu ya mofimu.
    10. Kishazi huru - nitamtembelea
      Kishazi tegemezi - endapo atanialika
    11. kiima - taabu sana
      Shamirisho - m-
      Chaagizo - sana
    12. Mama angefika mapema fuoni, angewahi mashua.
    13. Mtu wa hasira amefika hapa.
    14. Mwanafunzi afanikiwaye ni yule adurusaye kwa makini
    15.  Seramal aki(i)wasili leo atakuwa aki(ii)tengeneza ki(iii)ti cha ki(iv)toto chake.
      1. ki - masharti
      2. ki - hali ya kuendelea
      3. ki - kipatanishi cha ngeli
      4. ki - udogo
    16. S - KN(T) + KT ( T + N)
    17.  
      1. Kibainishi
        • Kudondoshwa kwa herufi - N'shakuja
        • Shadda - 'meza
        • Nazali - ng'ombe
        • Ufupisho - 'mefika
        • Kuandika miaka  1'13
      2. Mkwaju
        • Tarehe 5/6/2021
        • Kuandika akiswami 2/3 
        • kuonyesha au/ama
        • Kumbukumbu KUMB. 1/2
    18.  
      1. Kitenso bado kinaendelea
      2. Masharti/ hakuna uwezekano.
    19. Mkwezi hupanda miti ____mkutubi____ hufanya kazi maktabani, mpanzi ___hupanda mbegu, kandawali__ huendesha gari la moshi na mpagazi ___hubeba mizigo_____ 
  4.  
    1.  
      1. Sajili ya bungeni - Bwana spika
      2.  
        1. Utohozi - spika
        2. Lugha amrishi hutumika hasa na spika
        3. Lugha ya heshima na adabu hutumika k.m Aomba
        4. Sentensi ndefundefu ili kuelezea mambo kikamilifu
        5. Wakati mwingine kuna kukatizana kauli.
        6. Lugha ni ya kimdahalo
        7. Huzingatia mtindo wa kuhutubu
        8. Kuna kuchanganya ndimi ili kujieleza vizuri
        9. Matumizi ya ishara lugha/ viziada lugha.
        10. Hutaja vifungo mbalimbali vya sheria
        11. Lugha fafanuzi/ elezi - kutoa maelezo ya kina
        12. Msamiati maalum k.v mswada
        13. Urudiaji wa kauli fulani
        14. Mtindo maalum wa kuanzisha na kuendeleza mazungumzo
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 2 Questions and Answers - Maranda High Pre Mock Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?