Kiswahili Form 1 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote. Majibu yako yaandikwe katika nafasi zilizoachwa wazi katika kijitabu hiki cha maswali.


MASWALI

SEHEMU YA A: INSHA

Andika insha itakayoanza kwa:

Tuliamka asubuhi ya majogoo tayari kwa safari tuliyoingojea kwa siku nyingi…

SEHEMU YA B : UFAHAMU B 

Mavazi Rekebisheni
Vazi jema kivaliwa, huongeza heshima,
Staha mtu kapewa, pote endapo daima,
Mavazi duni si sawa, kina dada ninasema,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Longi kwa nyuma kushika, na mapajani kubana,
Chupi zilipowafika, dhahiri kuonekana,
Bure munaaibikia,na kujishusha maana,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Kifuani kujikaza, maziwa yaning’inie,
Kitu gani munawaza, hamna habari nyie,
Ni ashiki mwasambaza, sikizeni niwambie,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Msichana ni hatia, magotini kufichuka,
Hivyo basi kuvalia,rinda lisoyafunika,
Huenda zusha hisia, maovu yakawafika,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Kuwa wazi kinenani, hupendeza Baniani,
Kwao mila ya zamani, si kujitakia shani,
Weusi twatafutani, kuiga za Ulayani,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Sitakosa kuzitaja, skati mnazovaa,
Zaisha kwa mapaja,kikiri kuchuchumaa,
Iko wazi nyonga moja, mkato ulivyokaa,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Wazi nitawasomea, nguo hizi nguo gani ?
Dada zetu mwakosea, kuzivaa hadharani,
Ndizo hizo huchochea, usherati mitaani,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Nguo chini zishusheni, mwilini mzipanue,
Heri kuingia deni, za heshima mnunue,
Kuigiza za kigeni, ni utumwa mtambue
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

Beti tisa namaliza, kalamu naweka chini,
Iwapo wajiuliza, nakereketwa ni nini ?
Ni staha nahimiza, sio wake kuhaini,
Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

  1. Shairi hili ni la aina gani? ( alama 1)
  2. Shairi hili lina beti ngapi? ( alama 1 )
  3. Eleza vina vya ubeti wa kwanza . ( alama 1 )
  4. Shairi hili lina kibwagizo au kimalizio? Kwa nini ? ( alama 1 )
  5. Taja tatu nne za mavazi ambazo msanii ana kashifu. ( alama 3)
  6. Kwa kuzingatia maudhui ya shairi hili , fafanua methali : ( alama 2 )
    Chema chajiuza, kibaya chajitembeza.
  7. Eleza umbo la shairi. ( alama 4 )
  8. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi. ( alama 3)
    1. staha
    2. ashiki
    3. twatafutani

SEHEMU C: MATUMIZI YA LUGHA

  1. Toa tatu mbili za irabu i (al3)
  2. Taja sauti mbili ambazo ni vipasuo vya ufizi (al2)
  3. Eleza maana ya silabi kwa kutolea mfano (al2)
  4. Maneno yafuatayo yana silabi ngapi? (Al2)
    1. Maktaba
    2. Mwanafunzi
  5. Unda neno moja lenye sauti mwambatano (al1)
  6. Andika sentensi zifuatazo bila ya kutumia kirejeshi amba---- (al2)
    Fulana ambayo imefumwa ni nyekundu
  7. Tunga sentensi mbili kudhihirisha tofauti kati ya: (al4)
    1. Tata
    2. Dada
  8. Taja vipashio vine vya lugha. (al4)
  9. Andika sentensi hii katika ukubwa wingi (al2)
    Mtu mrefu alianguka pu!
  10. Bainisha maneno katika sentensi ifuatayo. (al3)
    Mzazi ataenda mjini.
  11. Ainisha viambishi katika sentensi. (al2)
    Nilikimbia
  12. Toa matumizi mawili ya mkwaju (/). (al2)
  13. Weka maneno yafuatayo katika ngeli zao. (al 3)
    1. Mbuyu
    2. Kifaru
    3. Chai
  14. Sahihisha sentensi ifuatazo. (al1)
    Huko ndimo alimopatikana.
  15. Geuza sentensi ifuatayo iwe katika wakati ujao. ( al1)
    Mimi ninapenda mtoto mtiifu
  16. Andika wingi wa: (al2)
    Mtoto ataenda shuleni.
  17. Kanusha (al1)
    Nitaruka kamba.
  18. Panga maneno haya ili kupata sentensi sahihi
    Mbegu mkulima nyingi amepanda. ( al 2)


SEHEMU D: ISIMU JAMII. 

  1. Eleza maana ya sajili ya lugha. [alama 2]
  2. Taja mambo manne yanayosababisha kuibuka kwa sajili tofauti. [alama 4]
  3. Huko ukitoa mifano eleza sifa nne za sajili ya sokoni. (alama 4)

SEHEMU YA E: FASIHI

  1. Fafanua aina mbili za fasihi (alama 2)
  2. Eleza sifa nne za mtambaji bora ( alama 4)
  3. Eleza aina mbili za ngano ( alama 2)
  4. Taja sifa tatu za fasihi simulizi (alama 4 )
  5. Fafanua aina tatu ya wahusika katika fasihi simulizi. ( alama 3)


MWONGOZO KUSAHIHISHA

SEHEMU A: INSHA 

  • Lazima mtahiniwa aanze kwa mdokezo
  • Mawazo katika kisa cha mtahiniwa lazima yalingane na mdokezo
  • Azingatie nafsi na wakati
  • Insha iwe na kichwa

SEHEMU B: UFAHAMU

  1. Shairi hili ni la arudhi aina ya tarbia ( alama 2 )
  2. Shairi hili lina beti tisa ( alama 1 )
  3. Eleza vina vya beti za kwanza mbili. ( alama 2 )
    • Ubeti 1
      Wa,ma,
      Wa,ma,
      Wa,ma
      Ni,di.
    • Ubeti 2
      Ka, na,
      Ka, na,
      Ka, na,
      Ni, di.
  4. Shairi hili lina kibwagizo . Kwa sababu mshororo wa mwiisho unarudiwarudiwa kutoka ubeti hadi ubetiau kimalizio ( alama 2 )
  5. Taja aina nne za mavazi ambazo msanii ana kashifu. ( alama 4)
    • Long`i zinazobana
    • Long`I zinazoonyesha chupi
    • Nguo fupi isiyofunika magoti
    • Nguo wazi kitovuni.
    • Skati fupi zinazobana zenye mikato ya ajabu
    • Nguo zinazoacha maziwa nje
  6. Chema chajiuza, kibaya chajitembeza. ( alama 2 )
    • Msichana mrembo sio lazima avae mavazi ya kumkosesha heshima ili aonekane na apendeze. Uzuri wake utaonekana hata akivaa nguo za heshima
  7. Umbo la shairi. ( alama 4 )
    • Lina beti tisa
    • mishororo minne kwa kila ubeti
    • lina mizani nane katika ukwapi na nane katika utao
    • lina vipande viwili ukwapi na utao
    • lina vina vya ndani na nje
  8. maana ya maneno kama yalivyotumika katika shairi. ( alama )
    1. staha- heshima
    2. ashiki-tamaa
    3. twatafutani- tunatafuta nini

SEHEMU C: MATUMIZI YA LUGHA

  1. sifa tatu za irabu i (al3)
    • irabu ya mbele
    • irabu ya juu
    • mdomo umetandazwa
  2. vipasuo vya ufizi (al2)
    • /t/,/d/
  3. Silabi ni pigo moja la tamshi (al1)
  4. (Al2)
    1. Maktaba - tatu
    2. Mwanafunzi - nne
  5. neno moja lenye sauti mwambatano (al1)
    • Mbwa, jangwa, ngoma
  6. Fulana iliyofumwa ni nyekundu
  7. Hakiki sentensi
    • Tata- sio rahisi kueleweka    -fujo
    • Dada –ndugu wa kike
  8. vipashio vine vya lugha. (al2)
    • sauti
    • silabi
    • neno
    • sentensi
  9. majitu marefu yalianguka pu! (al2)
  10. Mzazi ataenda mjini.
       N          T          E
  11. viambishi katika sentensi. (al2)
    Nilikimbia
    • Ni- nafsi
    • li-wakati
    • kimbi.-mzizi
    • a-kiishio
  12. matumizi mawili ya mkwaju (/).
    • kuonyesha maana ya neno au
    • kutenga shilingi na senti
    • kuandika tarehe (al2)
  13. ngeli za. (al 3)
    1. Mbuyu U-I
    2. Kifaru A-WA, KI-VI
    3. Chai I-I,I-ZI
  14. (al1)
    • Huko ndiko alikopatikana.
    • Hapo ndipo alipopatikana
    • Humo ndimo alimopatikana
  15. Mimi nitapenda mtoto mtiifu(a 1)
  16. Andika wingi wa: (al2)
    Mtoto ataenda shuleni.
    • Watoto wataenda shuleni
  17. Kanusha (al1)
    Nitaruka kamba.
    • Sitaruka kamba
  18. Panga maneno kupata senetensi sahihi (al2)
    Mbegu mkulima nyingi amepanda. 
    • Mkulima amepanda mbegu nyingi

SEHEMU D:ISIMUJAMII. 

  1. maana ya sajili ya lugha. [alama 2]
    • Ni mitindo mbalimbali ya matumizi ya lugha ile moja
  2. Taja mambo manne yanayosababisha kuibuka kwa sajili tofauti. [alama 4]
    • muktadha
    • mada
    • uhusiano
    • jinsia
    • umri
    • lengo
    • hali
  3. sifa nne za sajili ya sokoni. (alama 4)
    • msamiati maalum wa kibiashara-pesa, bei, ghali,
    • lugha huwa changamfu nay a kupendeza.
    • lugha huwa ya kushawishi wanunuzi.
    • Utohozi hutumiwa.kastoma
    • Kuna kuchanganya ndimi- vyenyewe ni fresh
    • Kuna kuhamisha ndimi. Fair prices
    • Huwa na mzaha mwingi- mali ya kuongeza furaha na mapenzi nyumbani
    • Huwa na sarufi legevu

SEHEMU YA E: FASIHI

  1. aina mbili za fasihi (alama 2)
    • Fasihi simulizi ni fasihi inayowasilishwa kwa njia yam domo.
    • Fasihi andishi ni inayowasilishwa kwa maandishi.
  2. Sifa nne za mtambaji bora ( alama 4)
    • kuwa na ubunifu wa juu
    • kuijua hadhira yake na mahitaji yake
    • kuielewa na kuimudu lugha ya hadhira yake.
    • kuyaelewa mazingira ya hadhira yake ili kutoa mifano mwafaka.
    • kuwa jasiri wa kuweza kuzungumza hadhira
    • kuujua utamadani wa hadhira yake ili kuepuka miiko.
    • kuwa mcheshi
  3. aina mbili za ngano ( alama 2)
    • Ngano za wanyama
    • Ngano za mtanziko
    • Ngano za mashujaa
    • Ngano za mazimwi
    • Ngano za kiayari
  4. sifa tatu za fasihi simulizi (alama 4 )
    • Huwa ina utendaji
    • Huwa ni hai
    • Lazima iwe na mtendaji
    • Huwa na mahali maalum pa kutendea
    • Ni mali ya jamii
    • Huwa na wakati maalum ya kuwasilishia
  5. aina tatu ya wahusika katika fasihi simulizi. ( alama 3)
    • Wahusika wanyama
    • Wahusika binadamu
    • Wahusika vitu
    • Wahusika mazimwi
    • Fanani hadhira
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Form 1 Questions and Answers - Term 3 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest