Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 1 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KIDATO CHA 1
MTIHANI WA KATI YA MUHULA
MUHULA WA 1

MAAGIZO

 • Jibu maswali yote
 1. UFAHAMU
  Soma taarifa ifuatayo kasha ujibu maswali.

  Historia ya katiba

  Katiba ni utaratibu wa sheria unaoweka mpango wa jamii kuendesha mambo.Ni muhimu kila raia ajue katiba ya nchi yake. Katiba yaweza kuwa imeandikwa au haikuandikwa. Katika jamii za jadi, katiba ilihifadhiwa na kupokezwa kwa mdomo. Mtindo wa kuandika katiba ulianza nchini Marekani mwaka 1787. Ingawa katiba hii imefanyiwa mabadiliko hapa na pale,bado ni ileile. Kenya ilipowekwa chini ya himaya ya Uingereza mwaka 1895, ilianza kutumia katiba ya Uingereza. Baada ya masetla wa kikoloni kujikita, Kenya kuwa koloni. Hii ililazimu pawe na katiba nyingine mwaka 1920. Waafrika waliupinga mfumo huu kwa sababu haukuwahusisha kikamilifu kwenye masuala ya uongozi. Utetezi wa wanasiasa uliilazimisha serikali ya Uingereza kuitisha makongamano mbalimbali kama vile lile la Devonshire na mengine ili kurekebisha katiba. Waafrika hawakuridhika. Wakaendelea kudai katiba mwafaka. Harakati hizi zilileta kuitishwa kwa kongamano la katiba la Lancaster. Lengo lilikuwa kuandika katiba itakayotumiwa nchini hadi leo. Kati ya wajumbe walioenda Uingereza kuandika katiba mwaka 1962 ni pamoja na Tom Mboya, Jean Marie Seroney, Julius Kiano, Jomo Kenyatta, Masinde Muliro, Oginga Odinga, Ronald Ngala, Daniel Arap Moi na James Gichuru. Wengine ni Martin Shikuku, Dennis Akumu, Taita Towett, Abdilahi Nassir, Jeremiah Nyaga na John Keen.

  Katiba ni kitovu cha taifa. Baina ya mambo inayotekeleza ni kuweka utaratibu na kanuni za utawala, kwa mfano, utawala wa kimikoa na serikali za wilaya. Pamoja na haya, katiba hufafanua vyombo vikuu vya serikali ,mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda. Vyombo hivi ni bunge, mahakama, urais, jeshi n.k. Hali kadhalika, katiba hupambanua haki za raia.

  Hii hudumisha demokrasia na huwawezesha wananchi kupata uhuru na haki za kimsingi. Katiba hukinga haki za kila raia, hasa kutokana na udhalimu wa wengi au wenye uwezo mkubwa. Zaidi ya yote, katiba huimarisha asasi za umma ili kudumisha uwajibikaji.

  Katiba huhalalishwa na watawaliwa. Hii hutokea wanaposhirikishwa katika uandishi wake. Kuanzia miaka ya themanini, raia walianza kudai katiba igeuzwe. Mwamko wa kutaka mageuzi ulianza kwa harakati za kubadilisha mfumo wa kisiasa kutoka ule wa chama kimoja hadi ule wa demokrasia ya vyama vingi. Haja ya mfumo mpya wa kisiasa ulilenga kuwashirikisha wananchi katika utawala na kuondoa uimla.

  Harakati zilitia fora miaka ya tisini. Mambo yaliyochochea hali hii ni mengi. Kwanza, katiba iliyokuwa imeandikwa na watu wachache ilikuwa imefanyiwa marekebisho mengi. Marekebisho haya yalimpa rais mamlaka mengi juu ya serikali kuu na vyombo tofauti vya serikali. Pili, viongozi na watu wenye uwezo na utajiri walipuuza katiba. Raia walihisi wanadhulumiwa. Walipinga hali ya wachache waliomzunguka rais kunufaika huku umma ukitengwa. Tatu, kutokana na uongozi uliokuweko wakati huo, wanawake, watoto na walemavu walidhulumiwa na kukosa uwakilishi ufaao.Hatimaye, pakawa na ongezeko la uharibifu wa mazingira, ufisadi na unyakuzi wa mali ya umma kama vile ardhi.

  Waliopigania katiba mpya walikuwa na haja ya katiba ambayo uandikaji wake ungewahusisha Wakenya wote. Mwanzoni, serikali ilipinga wito wa mabadiliko. Lakini mnamo mwaka 2001 iliunda Tume ya Marekebisho ya Katiba ili kutekeleza mahitaji ya wananchi. Tume hii iliwahamasisha na kuwashawishi raia kutoa maoni. Tume iliandaa vikao katika maeneo ya ubunge 210 ambapo wananchi walitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya katiba waliyotaka.

  Katika mapendekezo hayo raia walisisitiza mambo kadhaa. Jambo la kwanza ni utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi na maafisa wa umma .Jambo lingine ni kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na walemavu. Raia walidai kanuni za usawa na ulinganifu. Aidha walitilia mkazo mahitaji ya msingi kama chakula, afya nzuri, makao, elimu, usalama, uchumi, na kadhalika. Msingi wa mapendekezo hayo yote ni kuwepo na amani ya kitaifa, umoja na uadilifu ili kulinda maslahi ya wananchi wote na taifa.

  Maswali :
  1. Eleza kilichosababisha kongamano la katiba la Lancaster (alama3)
  2. Taja mambo matatu yaliyotiliwa mkazo na raia katika maoni yao kuhusu katiba. (alama3)
  3. Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu wa taarifa. (alama3)
  4. Eleza maan aya neno hili kama ilivyotumiwa katika taarifa (Al 1)
   1. Hamasisha
 2. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Kamilisha mchoro ufuatao (Al 3)
   kiwahili ulimi irabu jibu

  2.    
   1. Tofautisha kati y asauti ghuna na sauti sighuna . (Al 2)
   2. Eleza tofauti kati ya sauti hizi (Al 2)
    1. /ny/ na /gh/
    2. /l/ /r/
  3.    
   1. Sauti mwambatano ni nini? (Al 1)
   2. Huku ukionyesha, andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo (Al 2)
    1. KI (Konsonanti, irabu)
    2. KKKI ( consonanti, konnsonanti,konsonanti, irabu)
  4. Onyesha utakapoweka shadda katika maneno haya. (Al 3)
   1. Atatutembelea
   2. oevu
   3. Kiswahili
  5. Tunga sentensi zenya miundo hii (Al 2)
   1. N + V + T + N
   2. T + E + E
  6. Taja sifa tano za lugha. (Al 5)

MAJIBU

 1.      
  1. Eleza kilichosababisha kongamano la katiba la Lancaster (alama3)
   • Waafrika hawakua wamehusushwa katika katiba ya mwaka wa 1920.
   • Waafrika walitaka kuhusika katika masuala ya uongozi.
   • Utetezi wa wanasiasa ulilazimu serikali ya uingereza kuitisha kongamano.
  2. Taja mambo matatu yaliyotiliwa-mkazo na raia katika maoni yao kuhusu katiba. (alama3)
   • Utawala mwema na uwajibikaji wa viongozi.
   • Kulinda haki za binadamu zikiwemo za wanawake, watoto na walemavu.
   • Kanuni za usawa na ulinganifu
  3. Eleza umuhimu wa katiba kwa mujibu wataarifa. (alama3)
   • kuweka utaratibu na kanuni za utawala mf utawala wa kimikoa.
   • Hufafanua vyombo vikuu vya serikali, mamlaka yavyo na mipaka yavyo ya kutenda.
   • Hupambanua haki za raia.

   • Tia watu hamu ya kufanya jambo
 2. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Kamilisha mchoro ufuatao (Al 3)
   kiwahili ulimi irabu
  2.    
   1. Tofautisha kati ya sauti ghuna na sauti sighuna . (Al 2)
    • Sauti ghuna ni sauti ambazo husababisha mtetemeko/ mtikisiko/mrindimo wa nyusi – sauti wakati wa utamkaji ilhali sauti sighuna ni sauti ambazo hazisababishi mtetemeko/ mrindimo wa nyusi sauti wakati wa utamkaji
   2. Eleza tofauti kati ya sauti hizi (Al 2)
    • /ny/ na /gh/
    • /ny/ - ni nazali/vipua/ving’ong’o
    •  hutamkwa kwenye kaakaa gumu
    • /gh/ - Vikwamizo
    • hutamkwa kwenye kaakaa laini
    • /l/ /r/
    • /l/ - ni kitambaza
    • /r/ - ni kimadende
  3.    
   1. Sauti mwambatano ni nini? (Al 1)
    • sauti mwambatano ni sauti ambazo j=hujumuisha konsonanti mbili au zaidi kabla ya irabu kasha kutamkwa kama silabi moja.
   2. Huku ukionyesha, andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo (Al 2)
    • KI (Konsonanti, irabu)
    • KKKI ( consonanti, konnsonanti,konsonanti, irabu)
    • Tathamini jibu la mwanafunzi
    • Tathamini jibu la mwanafunzi
  4. Onyesha utakapoweka shadda katika maneno haya. (Al 3)
   • Atatutembe’lea
   • O’evu
   • Kiswa’hili
  5.      
   1. Taja vipashio vya lugha (Al 2)
    • Sauti
    • Silabi
    • Neno
    • Sentensi (1/2 mk each)
   2. Tunga sentensi zenya miundo hii (Al 2)
    • N + V + T + N
    • Tathamini jibu la mwanafunzi
    • T + E + E
    • Tathamini jibu la mwanafunzi
  6. Taja sifa tano za lugha. (Al 5)
   • Hakuna lugha iliyobora kuliko/kushinda zingine. Lugha zote ni sawa.
   • Kila lugha ina sauti zake zilizo tofauti na nyingine.
   • Lugha hubadilika kutegemea mazingira , aina ya tukio, wakati n awatumizi wa lugha hiyo.
   • Lugha ina uwezo wa kukua.
   • Lugha hufa, kwa msamiati wake kupotea.

 


Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 1 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest