Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 1 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA
MUHULA WA KWANZA, 2021
KIDATO CHA KWANZA

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote
  1. INSHA
    Andika barua kwa mwalimu mkuu ukiomba msamaha kwa kutofaulu katika mjarabu wa kwanza.

  2. UFAHAMU: (ALAMA 15)
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.

    Gogo
    Umezuka moto kweli, misitu yateketea,
    Wachanji wameduwili, hakuna pa kukimbia,
    Zimewakwama akili, mashoka yanaungua,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Kwa kweli kila mahali, halaiki yaumia,
    Si Kenya si Shelisheli, mamia yaangamia,
    Shikeni yangu kauli, msije kujijutia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Ijapokuwa kalili, muda wa kuhadithia,
    Yapimeni kwa ratili, haya ninayowambia,
    Sijegeuka shubili, tamu mnayodhania,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Moto huno ni kukuli, hauchomi kuchagua,
    Hauna jaji wakili, kwamba utajitetea,
    Huchoma kiwiliwili, pingiti likasalia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    We mchanji kaa tuli, boresha yako tabia,
    Kugwenya lile na hili, magongo kujsombea,
    Twaja tujipige wali, siku ya kukufukia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Ili wepuke muhali, usije kujililia,
    Gogo ulo na kibali, chanja ulilozowea,
    Usiyachanje mawili, zani utajibwagia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Maswali:
    1. Shari hili ni la aina gani? (ala 2)
    2. Eleza vina vya shairi hili. (ala 2)
    3.    
      1. Eleza maana ya mizani? (ala 1)
      2. Shairi hili lina mizani ngapi katika ubeti wa tatu mshororo wa kwanza?(ala 1)
    4. Taja kibwagizo cha shairi hili . (ala 1)
    5. Taja nchi mbili zilizotajwa katika shairi. (ala 1)
    6. Mshairi ametumia uhuru wa kishairi. Eleza huku ukitolea mifano kila maelezo. (ala 4)
    7. Eleza maana ya msamiati ufuatao: (ala 1)
      1. Pingiti –
      2. Zani –
    8. Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi. (ala 1)

  3. SARUFI: ALAMA 25
    1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au sighuna. (ala 1)
      1. /s/
      2. /z
    2. Eleza maana ya shadda. (ala 1)
    3. Tia shadda kwenye maneno yafuatayo ili kuleta maana iliyo katika mabano.
      Ala (kifaa)
      Ala (mshangao)
      Barabara (njia kuu)
      Barabara (sawasawa) (ala 2)
    4. Toa mifano miwili ya aina za kamusi. (ala 1)
    5. Tunga sentensi moja ili kutofautisha maana ya maneno yafuatayo pafu and bafu. (ala 1)
    6. Taja vipashio vya lugha. (ala 2
    7. Andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo;
      KKKI
      II (ala 1)
    8. Bainisha maneno katika sentensi zifuatazo.
      Kitabu kimeanguka chini ya meza. (ala 2)
    9. Taja na ueleze aina mbili za viambishi. (ala 2)
    10. Jaza viambishi vinavyofaa katika nafasi.
      1. Mitikiti _____liyopandwa juzi ____ mimea. (ala 1)
    11. Ainisha viambishi katika sentensi ifuatayo: (ala 3)
      Walitupongeza.
    12. Taja sifa mbili za lugha. (ala 2)
    13. Onyesha matumizi ya alama zifuatazo za uafikishaji. (ala 2)
      1. Mshazari
      2. Koloni –
    14. Yaweke maneno yafuatayo katika ngeli mwafaka: (ala 2)
      1. Sukari
      2. Chuma –
    15. Onyesha matumizi mawili ya kiimbo. (ala 2)

  4. ISIMU JAMII: (ALAMA 10)
    1. Eleza kaida za lugha. (ala 4)
    2. Taja sifa za sajili ya shuleni. (ala 6)

MAAKIZO

  1. UFAHAMU: (ALAMA 15)
    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.

    Gogo
    Umezuka moto kweli, misitu yateketea,
    Wachanji wameduwili, hakuna pa kukimbia,
    Zimewakwama akili, mashoka yanaungua,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Kwa kweli kila mahali, halaiki yaumia,
    Si Kenya si Shelisheli, mamia yaangamia,
    Shikeni yangu kauli, msije kujijutia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Ijapokuwa kalili, muda wa kuhadithia,
    Yapimeni kwa ratili, haya ninayowambia,
    Sijegeuka shubili, tamu mnayodhania,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Moto huno ni kukuli, hauchomi kuchagua,
    Hauna jaji wakili, kwamba utajitetea,
    Huchoma kiwiliwili, pingiti likasalia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    We mchanji kaa tuli, boresha yako tabia,
    Kugwenya lile na hili, magongo kujsombea,
    Twaja tujipige wali, siku ya kukufukia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Ili wepuke muhali, usije kujililia,
    Gogo ulo na kibali, chanja ulilozowea,
    Usiyachanje mawili, zani utajibwagia,
    Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.

    Maswali:

    1. Shari hili ni la aina gani? (ala 2)
      • Tarbia – lina mishororo mine katika kila ubeti.

    2. Eleza vina vya shairi hili. (ala 2)
      • _________ li ________a
        ________ li _______ a
        ________ li _______ a
        ________ to _______ ni
    3.    
      1. Eleza maana ya mizani? (ala 1)
        • Mizani ni silabi katika kila mshororo.

      2. Shairi hili lina mizani ngapi katika ubeti wa tatu mshororo wa kwanza?(ala 1)
        • Mizani kumi na sita (160 – (8a, 8b)

    4. Taja kibwagizo cha shairi hili . (ala 1)
      • Kibwagizo ‘Gogo linawaka moto, wachanji tahadharini.’

    5. Taja nchi mbili zilizotajwa katika shairi. (ala 1)
      • Nchi mbili – Kenya, Shelisheli.

    6. Mshairi ametumia uhuru wa kishairi. Eleza huku ukitolea mifano kila maelezo. (ala 4)
      • Uhuru wa mshairi:
      • Kuboronga sarufi – ubeti 5 mshororo wa kwanza ‘boresha yako tabia’ badala ya boresha tabia yako.
      • Inkisari sijegeuka badala ya isijegeuka.

    7. Eleza maana ya msamiati ufuatao: (ala 1)
      1. Pingiti – sehemu ya mwili iliyo kati ya viungo viwili.
      2. Zani – kitendo kinachoweza kuleta hasara, balaa janga.

    8. Eleza ujumbe unaowasilishwa na mshairi. (ala 1)
      • Mshairi anawaonya wanadamu dhidi ya tama ina kutotosheka. Anawatahadharisha na ugonjwa hatari unaochoma kuwili.

  2. SARUFI: ALAMA 25
    1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au sighuna. (ala 1)
      1. /s/- si ghuna
      2. /z/ - ghuna

    2. Eleza maana ya shadda. (ala 1)
      • Shadda ni  mkazo unaowekwa katika neno ili kuleta maana iliyokusudiwa.

    3. Tia shadda kwenye maneno yafuatayo ili kuleta maana iliyo katika mabano.
      Ala (kifaa) -  ‘Ala
      Ala (mshangao)- A’la!
      Barabara (njia kuu) - Bara’bara
      Barabara (sawasawa) - Ba’rabara (ala 2)

    4. Toa mifano miwili ya aina za kamusi. (ala 1)
      • Kamusi ya methali
      • Kamusi ya semi

    5. Tunga sentensi moja ili kutofautisha maana ya maneno yafuatayo pafu and bafu. (ala 1)
      • Pafu – Kiungo cha mwili
      • Bafu – chumba cha kuogea

    6. Taja vipashio vya lugha. (ala 2)
      • Sauti /m/
      • Silabi ma
      • Neno mama

    7. Andika maneno yenye miundo ya silabi ifuatayo;
      KKKI - Mbwa, mbweha.
      II - oa, au
      (ala 1)
    8. Bainisha maneno katika sentensi zifuatazo.
      Kitabu kimeanguka chini ya meza. (ala 2)
      N              T            H           N
    9. Taja na ueleze aina mbili za viambishi. (ala 2)
      • Viambishi awali
      • Viambishi tamati.
    10. Jaza viambishi vinavyofaa katika nafasi.
      1. Mitikiti _____liyopandwa juzi ____ mimea. (ala 1)
        • Mitikiti iliyopandwa juzi imemea.

    11. Ainisha viambishi katika sentensi ifuatayo: (ala 3)
      Walitupongeza.
      • Wa – li – tu – pongez – a
        Nafsi  wakati  tendwa   mzizi   kiishio/tamati

    12. Taja sifa mbili za lugha. (ala 2)
      • Hakuna lugha bora kuliko nyingine.
      • Lugha hufa.
      • Lugha hukua.

    13. Onyesha matumizi ya alama zifuatazo za uafikishaji. (ala 2)
      1. Mshazari
        • Kuandika tarehe ,
        • Kuonyesha au/ama
        • Kutenga shilingi na senti.

      2. Koloni –
        • Kuorodhesha
        • Kutenga saa na dakika.
        • Kutenga msemaji na maneno yake katika mazungumzo.

          (mwanafunzi atoe mifano)

    14. Yaweke maneno yafuatayo katika ngeli mwafaka: (ala 2)
      1. Sukari- I – I
      2. Chuma – KI – VI
    15. Onyesha matumizi mawili ya kiimbo. (ala 2)
      • Kuonyesha kauli, swali?, mshangao/hisia!

  3. ISIMU JAMII: (ALAMA 10)
    1. Eleza kaida za lugha. (ala 4)
      • Umri
      • Wahusika
      • Tabaka
      • Wakati 
      • Elimu
      • Uhusiano
      • Mahali
        (mwanafunzi aeleze.)

    2. Taja sifa za sajili ya shuleni. (ala 6)
      • Lugha ya heshima
      • Lugha ya upole na Adabu ya mwanafunzi
      • Msamiati maalum na unaoana na mazingira
      • Kuzingatia sarufi.
        (zozote 3, ala 2) 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 1 2021.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest