Kiswahili Questions And Answers - Form 1 Term 2 Opener 2021

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU(Alama 15)

                                               Ajira ya watoto
    Kingi alizaliwa vuruni kijiji kilichosifika kwa ukarimu wa wanakijiji wake.Ingawa walikuwa karimu,Wavuruni wengi walikosa elimu.Fauka ya hayo,walininginia katika umaskini uliokithiri.Hivyo,wengi waliselea katika kazi za kijungu jiko.Watot wa umri wa kwenda shule walikosa elimu na kuzurura mitaani.Udhaifu huu ulimpa faida Mwakisu,tajiri mmoja aliyemiliki shamba kubwa.Aliwaajiri watoto hao.

    Mwakisu alikuwa mkwasi alietononoka si haba.Kama ni senti ,alikuwa nazo.Kilichotia doa jina lake ni kiburi. Mbali na kiburi hicho,yeye hakujaliwa moyo wa huruma na utu.
    Hakubarikiwa kuwa mwema . Maadili hutuongoza kila mara kuwa ‘wema hauozi’.

    Kwa Mwakisu,wema ulioza na kuvunda .Utu uling’oka katika bawaba za moyo wake na ukawa msamiati aliouchukia.Aliwatumikisha watoto wa wenzake huku wake wakisoma shule.Tabia yake hiyo ndiyo iliyowafanya Wavuruni kumtoa katika orodha yao ya watu wema.

    Mwakisu alistaajabisha!Hakutaka kununua kununua mashine zozote za kufanya kazi shambani ingawa alikuwa nao uwezo. Alistahabu kuajiri watoto wadogo na kuwadhulumu.Mkwasi huyu alifurahia kuona vitoto vikimenyana na kazi shambani kwake tangu mawio hadi machweo na hatimaye kuwapa ujira mdogo.

    Siku moja Kingi alimtaka radhi, “Bosi naomba uniongezee chochote ,kwani tuna shida nyumbani.” Mwasiku alimkodolea macho huku mdomo ukimcheza.Hapo alimchomolea mwajiriwa wake tusi kubwa kutoka kwenye hazina yake isiyopungua.Tusi ambalo lilimtaabisha Kingi kulisahau.Lilikaririwa akilini mwake kwa sonono. Tangu siku hiyo Kingi akaona kuwa kuajiriwa na Mwakisu ni kufadhiliwa u chini.

    Kiburi cha mwakisu kilidhihirika kila mara .Kila alipomwona motto akilia kwa uchovu au maumivu , ungemsikia akimfokea ,”Chapa kazi!Unalilia nani hapa?Kama humudu kazi rudi kwa mamako ukanyonye.”

    Kazi nyingi zilikuwa ngumu na hazikuwastahili watoto wenye umri mdogo.Si kipupwe, si kaskazi,si vuli,si kiangazi ,si kusi:kazi ziliongezeka na kuwaumiza watoto.Kingi,kwa mfano,alitakikana akame ng’ombe kumi na abebe maziwa hadi kwenye tangi kubwa .Kisha angewakatia mg’ombe nyasi na kuwasafisha . Hatimaye angehitajika kuzoa samadi.

    Msimu wa kipupwe uliwadia.Baridi ikawatafuna watoto hao waliokosa mavazi bora.Kingin aliugua. Watoto wengi wakapatwa na maradhi.Wawili wakaaga dunia.Wazazi walipoona maisha ya watoto wao yamo hatarini,wakaandamana hadi kwa Mwakisu.tajiri huyo aliwajia kwa meno ya juu,’msiniitie kibuhuti. Mimi niliwaajiri watoto,sio watoto na wazazi wao”.Wazazi wakatanabahi kuwa , ‘Pa shoka hapaingii kisu’.Waliandamana hadi kwa chifu.Chifu alipoyaona yamempita kimo,akafululiza hadi kituo cha polisi.

    Mwakisu akakamatwa , akashtakiwa na kuhukumiwa . Alipatikana na makosa ya kuwaajiri watoto wenye unri mdogo na kusababisha vifo vya wawili hao.

    Serikali ikatoa amri kwa wazazi kupeleka watoto wao shuleni. Ikatoa pia misaada ya kuendeleza elimu;elimu ya bure kwa shule za msingi. Kingi akasoma hadi kuhitimu chuo kikuu. Akawa daktari.
    Alfajiri moja mahabusu waliletwa hospitali kuu ya mkoa kwa matibabu. Kingi akampa huduma mzee aliyejawa mvi na kukoboka meno. Alipomtazama kwa makini akamkumbuka.
    Mwakisu akabahatisha,”sura yako….ni kama Kingi…”Kingi akamjibu,”Mimi ndiye Kingi.”Wakakondoleana macho,huku machozi yakimtiririka Mwakisu.

    Maswali
    1. Toa kichwa kingine kwa habari hii. (alama 1)
    2. Taja matatizo mawili yaliyowakabili wanakijiji cha Vuruni. (alama 2)
    3. Ni mambo gani yaliyowafanya wanakijiji kumtoa Mwasiku katika orodha yao? (alama 2)
    4. Taja kazi alizofanya Kingi. (alama 3)
    5. Mwasiku alishtakiwa kwa makosa gani? (alama 1)
    6. Eleza maana ya semi hizi. (alama 3)
      1. Kazi ya kijungu jiko.
      2. Tononoka si haba.
      3. Kodolea macho.
    7. Toa maana ya methali hizi: (alama 2)
      1. Wema hauozi.
      2. Pa shoka hapaingii kisu.
    8. Toa maana ya msamiati huu kama ulivyoptumiwa katika makala: (alama 1)
      1. Fauka ya
      2. Alistahabu
  2. MATUMIZI YA LUGHA(alama 40)
    1. Taja na utofautishe aina mbili kuu za sauti za lugha ya Kiswahili (alama 2)
      Kutaja
      Tofauti
    2. Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu. (alama 5)
      F1 Kiswa Q2b T2 opener 2021
    3. Eleza maana ya
      1. Shadda
      2. Kiimbo (alama 2)
      3. Weka shadda neno barabara (alama 2)
        Kuonyesha maana ya shwari na baraste
        Shwari ______________________ Baraste_______________
    4. Taja vipashio vinne vijenzi vya lugha ya Kiswahili. (alama 4)
    5. Tenga silabi na uainishe katika neno (alama 2)
      Muhtasari
    6. Sahihisha sentensi hizi
      1. Mtoto amerara usingizi mnono.
      2. Papu yangu ni mzee kiazi. (alama 3)
    7. Tofautisha sauti . (alama 2)
      /r/ na /l/
    8. Eleza sifa tatu za Kamusi ya lugha ya Kiswahili. (alama 3)
    9. Kamilisha methali. (alama 2)
      Mgagaa na upwa ______________
    10. Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi. (alama 5)
      1. Mwalimu anaandika .
      2. Mwalimu anaandika ubaoni.
    11. Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa. (alama 4)
      Mofimu _______________
      Viambishi_______________
    12. Andika visawe vya viwakifishi hivi. (alama 4)
      1. Nukta-
      2. Koma –
      3. Mkwaju-
      4. Mtajo-


MARKING SCHEME

  1. UFAHAMU(Alama 15)
    1. Toa kichwa kingine kwa habari hii. (alama 1)
      Anwani mf.
      • Udhalimu wa mwakisu.
      • Shida za wanakijiji wa vuruni.
      • Tajiri mwakisu.√ 1×
    2. Taja matatizo mawili yaliyowakabili wanakijiji cha Vuruni. (alama 2)
      1. Walikuwa maskini.
      2. Waliikosa elimu.
      3. Watoto wao walizuru mitaani.
      4. Walikosewa heshima na mwakisu.
      5. Aliwadhulumu wanakijiji.
    3. Ni mambo gani yaliyowafanya wanakijiji kumtoa Mwasiku katika orodha yao? (alama 2)
      1. Mwakisu alikosa utu,huruma na alijaa kiburi.
      2. Mwakisu aliwaumikisha watoto
    4. Taja kazi alizofanya Kingi. (alama 3)
      1. Kuwa kama ng’ombe kumi kila siku.√1×3
      2. Kubeba maziwa hayo hadi kwenye tangi kubwa.
      3. Kuwataftia ng’ombe nyasi.
      4. Kuwasafisha ng’ombe.
      5. Kuzoa samadi.
    5. Mwakisu alishtakiwa kwa makosa gani? (alama 1)
      • Aliwaajiri wtoto wenye umri mdogo na kusababisha vifo vya wawili wao.
    6. Eleza maana ya semi hizi. (alama 3)
      1. Kazi ya kijungu jiko.
        • Kazi ya malipo haba mno.
      2. Tononoka si haba.
        • Kuwa tajiri sana.
      3. Kodolea macho.
        • Tazama kwa mshangao
    7. Toa maana ya methali hizi:
      1. Wema hauozi.
        • Matendo mema daima hudumu√1×2
      2. Pa shoka hapaingii kisu.
        • Kutafta mbinu au njia bora ya kutatua tatizo
    8. Toa maana ya msamiati huu kama ulivyotumiwa katika makala:
      1. Fauka ya
        • Zaidi ya/juu ya hayo √ ½
      2. Alistahabu
  2. MATUMIZI YA LUGHA(alama 40)
    1. Taja na utofautishe aina mbili kuu za sauti za lugha ya Kiswahili (alama 2)
      Kutaja
      Irabu na Konsonanti 1×1
      Tofauti
      Irabu hutamkwa kwa ulaini ilhali konsonanti hazina ulaini.
    2. Onyesha matamshi ya vokali ukitumia mchoro huu wa pembe tatu
      F1 Kiswa ans2b T2 opener 2021
      Tan irabu zote zionyeshwe sawasawa  1×5√
    3. Eleza maana ya
      1. Shadda
        • Mkazo fulani katika silabi fulani za neno.√ 1×2
      2. Kiimbo
        • Kupanda na kushuka kwa sauti. (alama 2)
      3. Weka shadda neno barabara
        Kuonyesha maana ya shwari na baraste
        Shwari - Ba’rabara     Baraste  -Bara’bara    (alama 2)
    4. Taja vipashio vinne vijenzi vya lugha ya Kiswahili. (alama 4)
      • Sauti-Silabi-Neno-Sentensi
    5. Tenga silabi na uainishe katika neno(alama 2)
      Muhtasari
      Muh-ta-sa-ri
      KIK- KI- KI-KI
    6. Sahihisha sentensi hizi
      1. Mtoto amerara usingizi mnono.
        • Mtoto amelala usingizi mnono. 6× ½
      2. Papu yangu ni msee kiazi. (alama 3)
        • Babu yangu ni mzee kiasi.
    7. Tofautisha sauti (alama 2)
      /r/ na /l/
      • /r/-Kimadende 1×1
      • /l/-Kitambaza
    8. Eleza sifa tatu za Kamusi ya lugha ya Kiswahili. (alama 3)
      1. Maneno yamepangwa Kialfabeti
      2. Maana ya maneno
      3. Matumizi katika sentensi
      4. Aina ya maneno
      5. Visawe
      6. Huwa na michoro ya kufafanua zaidi.
      7. Ngeli ya neno.
      8. Alama nyingi hutumika  Mf. alama wimbi (2)
      9. Vifupisho hutumika mf. KI-kielezi, k.m-kwa mfano,kama vile(kv) n.k-na kadhalika
    9. Kamilisha methali. (alama 2)
      Mgagaa na upwa hali wali mkavu.
    10. Bainisha aina za maneno katika sentensi hizi. (alama 5)
      1. Mwalimu anaandika .
            N            T
      2. Mwalimu anaandika ubaoni.
            N           T              E            √1×5
    11. Ainisha mofimu na viambishi katika neno Aliyesomewa. (alama 4)
      Mofimu                 Viambishi
      A-nafsi                  Aliye-Awali
      li-wakati                ewa-Tamati
      ye-o-rejeshi
      som-mzizi
      ew-kauli
      a-kiishio/ kitamatishi
    12. Andika visawe vya viwakifishi. (alama 4)
      1. Nukta-kitone/kikomo.
      2. Koma –mkato/kipumuo/kituo.
      3. Mkwaju-mshazari.
      4. Mtajo-alama nuklishi/za semi.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions And Answers - Form 1 Term 2 Opener 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest