Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KIDATO CHA 1
MTIHANI WA KATI YA MUHULA

MAAGIZO:

  • Jibu maswali yote
  • Insha isipungue maneno 300

 

  1. UFAHAMU (ALAMA 15)

    Elimu

    Ni dhahiri kabisa kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo.Elimu ya ujuzi na maarifa humfaidi mtu kwa kila njia-kiuchumi, kisayansi, katika utafiti wa aina tofautitofauti na kwa kuinafidhi jamii kwa jumla.Bila elimu, maendeleo hayawezi kupatikana kamwe; kuyataraji ni kama kutumaini kupata kitu kwenye ombwe tupu.

    Binadamu si kibonge au kidude kinachoweza kukaa bila chakula, mawasiliano na uhusiano kati yake na mazingira.Bila elimu, matatizo chungu nzima yatamkumba mwanadamu.Mifano ya matatizo haya ni kama vile ukosefu wa vyakula, hali duni ya mawasiliano, mmomonyoko wa udongo na hali nyingine za kuhuzunisha na kuaibisha.Maliasili yaweza kutumika tu iwapo pana ujuzi.

    Mito, misitu na madini ni vitu ambavyo vinaweza kurahisisha mno maisha ya wananchi vikitumiwa kwa ujuzi.Kwa mujibu wa ukweli huu, kujua kusoma na kuandika, ambacho ndicho kiini cha elimu, ni jambo la lazima katika Maisha. Elimu hurahisisha mawasiliano.Uwezo wa kupashana habari hutegemea ujuzi.Mawasiliano ni ya njia nyingi tofauti kama vile simu, barua, telegramu na njia nyingine.Nchi isiyo na mawasiliano bora ni kama jangwa lisilopitika.Kwa vile kila habari hugeuza hali Fulani ya Maisha, bila ujuzi wa kusoma na kuandika, mawasiliano hayawezekani.

    Maandishi mengi huwa na uzito wa maana na mtu yeyote asiyejua kusoma na kuelewa hawezi kunufaika kupitia kwa maandishi ilhali ajuaye atasoma, aelewe na kutimiza wajibu wake wa ujenzi wa taifa.Wahenga walisema, fumbato mfumbie mjinga, mwerevu huling’amua, kwani mwenye macho haambiwi tazama.Ni wazi kwamba mwenye ujuzi wa kusoma na kuandika ndiye atakayeelewa mawazo ya wenzake yaliyoandikwa na kuyatumia katika harakati za ujenzi wa taifa.

    Shuleni, wanafunzi hufunzwa kusoma na kuandika kusudi waweze kuchambua maandishi tofauti ili wawe na uwezo wa kujitegemea wenyewe kimaarifa.Kwa kuchambua maandishi tofauti, wanafunzi huelewa yale yafaayo na yasiyofaa katika jamii kwa kutumia mifano mizuri au mibaya ya wahusika katika kazi za kisanaa.Kwa njia hii, wanafunzi hupima kila hali kwa makini-yaani huwaza na kuwazua kabla ya kukata shauri kutenda lililo bora na la kuleta maendeleo.

    Katika ulimwengu wa biashara, kujua kusoma na kuandika ni jambo muhimu kwa vile mfanyi biashara ni lazima achemshe bongo ili kazi yake isidhoofike na mwishowe aangamie kifedha.Ni lazima biashara itunzwe isije ikadidimia na ufukara ukaingia.Ufanisi katika biashara zifanywazo na watu binafsi huchangia ufanisi katika nchi kwa jumla, kwa maana haba na haba hujaza kibaba.

    Kupitia kwa utafiti katika nyanja tofauti, wanasayansi huwahudumia wananchi kwa njia nyingi madhubuti. Bila ujuzi wa kusoma na kuandika, watafiti, marubani, manahodha, madaktari na wahandisi na wenye taaluma nyingine hawawezi kupatikana.Kila mjuzi huwa na jukumu lake katika kuchangia maendeleo nchini; ni lazima mhandisi arekebishe mitambo, daktari atibu watu, nahodha aongoze chombo na mwalimu afundishe.Wote wanahitaji elimu.

    Kwa mujibu wa hali hizi zote, ni Dhahiri kuwa ujuzi wa kusoma na kuandika ni jambo la lazima iwapo vikwazo katika ujenzi wa taifa vitaondolewa ili tupige hatua kubwa kimaendeleo.

    Maswali
    1. Je, elimu ina faida gani kwa mtu? Alama 2
    2. Taja aina nne za shida zinazoweza kumkumba mtu kutokana na ukosefu wa elimu. Alama 4
    3. Ni nini hasa kiini cha elimu? Alama 2
    4. Eleza maana kamili ya mawasiliano na utaje mifano minne. Alama 3
    5. Mwandishi anamaanisha nini anapotumia methali ‘fumbsto mfumbie mjinga, mwerevu huling’amua’? alama 2
    6. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika kifungu. Alama 2
      Madini
      Ombwe

  2. MATUMIZI YA LUGHA ALAMA 35
    1. Sauti hizi hutamkiwa wapi? Alama 2
      /w/
      /d/
    2. Tofautisha kati ya irabu na konsonanti. Alama 4
    3. Taja vikundi saba vya konsonanti kwa kutolea mfano ukizingatia hali ya mtetemeko katika nyuzi za sauti. Alama 7
    4. Kwa kupigia mstari, onyesha viambishi awali na tamati katika neno lifuatalo. Alama 2
      Anakochezea
    5. Taja vipashio vya lugha. Alama 2
    6. Eleza maana ya: Alama 4
      1. Shadda
      2. Kiimbo
    7. Unda neno lenye muundo ufuatao. Alama 2
      KKIKKI
    8. Weka shadda mahali pafaapo. Alama 1
      1. Marudio 
      2. Karatasi 
    9. Eleza maaana ya maneno yafuatayo: alama 3
      1. Kimbishi
      2. Kihisishi
      3. Kiwakilish
    10. Sahihisha. Alama 2
      nelson mandela, aliyekuwa rais wa afrika kusini, alifanya mashauri na mobutu sesseseko wa zaire.
    11. Geuza sentensi ifuatayo iwe katika wakati ujao. Alama 2
      Mpwa wangu anafua nguo zake.
    12. Andika kinyume cha sentensi ifuatayo. Alama 2
      Mama anapika ilhali dada anaanika nguo.
    13. Andika katika wingi alama 2
      Baba anachimba kisima.

  3. ISIMU JAMII (ALAMA 10)
    1. Eleza majukumu yoyote matano ya lugha alama 10
      Kiswahili Kidato 1
  4. FASIHI SIMULIZI ALAMA 20
    1. Eleza dhima ya fasihi katika jamii. alama 10
    2. Onyesha tofauti kati ya fasihi andishi na fasihi simulizi alama 10

INSHA
Mwandikie mzazi wako barua ukimweleza jinsi maisha yalivyo katika shule ya upili.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Mid Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest