Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Term 2 Opener Exams 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. INSHA (ALAMA 20)
  Mwandikie rafiki yako barua ukimwambia kuhusu maisha yalivyo katika shule ya upili.
 2. UFAHAMU (ALAMA 10)
  Soma kifungu kisha ujibu maswali yanayofuata. 
  NDOTO YANGU
     Kila mara huwa ninawaza na kuwazua juu ua maisha yangu ya usoni.  Fikra zangu hupaa mithili ya chombo kutafuta jawabu la kitendawili cha maisha yangu ya baadaye.  
      Azma niliyo nayo maishani ni ndoto.  Ni ndoto ya muda mrefu mfano wa kiu inayosumbua nafsi yangu.  Ndoto hiyo ni ile ya kuwa mkulima.
       Zaraa ni kazi yenye mvito mkubwa kwangu. Nimwonapo mkulima amejipinda, jembe mkononi, mgongo kauachilia jua limchome litakavyo, misuli imemtutumka na macho kayakaza kwa kwa ari, moyo wangu huchanuka kwa furaha mfano wa ua la alfajiri. Furaha yangu ni nimwone mkulima mwenye himaya ya shamba kubwa lenye mashine na matrekta huku wafanyakazi wakijizatiti kulihudumia.
       Ninastahabu kuwa mkulima kwani tajiri wangu atakuwa Maulana kuliko kuajiriwa na mwanadamu mwenzangu.  Mkulima anapotayarisha shamba lake huwa anaweka matumaini yake kwa Rabuka.  Kuchipuka na kutoa kwa mbegu alizozifukia hutegemea mapenzi ya muumba wake.  Vilevile, mifugo wake huongezeka kutokana na baraka za Mola, kinyume cha kazi ambayo ambayo ujira unatokana na kulipwa na tajiri-binadamu.
       Furaha yangu kama mkulima ni kusimama juu ya kichuguu ili nishibishe macho yangu kwa mandhari yenye kuvutai. Mandhari ya ardhi  miti na mimea iliyofunika na kutanda kama vile zulia la kijani. Nione pia mifugo wengi wakijilia majani na nyasi bila hofu.  Sauti zao zikisikika zikipokezana kana kwamba wanatoa shukrani kwa Muumba wao.
      Nitaridhika nionapo vijulanga wenye afya kutokana na lishe bora wakicheza na kurukaruka. Watoto wenye nyuso zinazobashiri matumaini maishani.  Vilevile, ni furaha iliyoje kuona wananchi wanaopata lishe bora ya kuwapa nguvu na afya kwa minajili ya kujenga taifa lao! 
      Kama mkulima nitachukua jukumu la kuwahamasisha wananchi kutilia maanani umuhimu wa kuhifadhi udongo ya njaana kutunza vyanzo vya maji kwa kutokata miti kiholela.
       Nataraji kuwa mkulima ili nijiunge na wakulima wenzangu nchini, kwa lengo la kuikinga jamii yetu dhidi ya njaa.  Nchi isiyo na chakula cha kutosha cha kuwalisha raia wake huwa na matatizo.  Tatizo mojawapo  ni kulazimika kuagiza chakula kutoka nchi zingine.  Hii huleta hali ya utegemezi na matumizi ya juu ya fedha za nchi.
        Ndoto yangu ni kuona watu wakipata ajira kutokana na kilimo.  Waama ajira mashambani au katika viwanda huhitaji malighafi kutoka kwenye sekta ya zaraa.  Nitaridhika mno nionapo wafanyakazi nitakaowaajiri wakiimarisha maisha yao.  
       Wanafunzi wenzangu hushangaa kuona vile ninavyopenda zaraa.  Wao hawajui nia yangu.  Nia hiyo ni ile ya kuitimiza ndoto yangu, kwani safari ya kesho hufungwa leo.
  MASWALI
  1. Andika kichwa kingine cha taarifa hii. (ala 2)
  2. Eleza sababu za mwandishi kutaka kuwa mkulima. (ala 3)
  3. Ni vipi tajiri wa  mkulima ni Maulana. (ala 3) 
  4. Umuhimu wa lishe bora ni upi ? (ala 2)
  5. Taja aina za kilimo zilizoelezwa katika habari. (ala 2)
  6. Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (ala 3)
   1. Azma 
   2. Ajira
   3. Vijulanga
 3. MATUMIZI YA LUGHA (ALAMA 30)
  1. Taja aina mbili kuu za sauti. (ala 2)
  2. Ni nini jina jingine la irabu ? (ala 1)
  3. Taja irabu mbili za kati. (ala 2)
  4. Toa mifano mitatu ya konsonanti za ufizi/ masine. (ala 3)
  5. Ni nini maana ya sauti za nazali ? (ala 2) 
  6. Orodhesha ala tatu tuli za kutamkia. (ala 3)
  7. Elezea maana ya silabi. (ala 2)
  8. Unda maneno mawili yenye sauti mwambatano . (ala 2)
  9. Shadda/ mkazo ni nini ? (ala 2)
  10. Taja vipashio vinne vya lugha. (ala 4)
  11. Taja aina mbili za maneno katika sentensi. (ala 2)
  12. Tunga sentensi yenye muundo huu. (ala 2)
   N + V + T + E
  13. Toa mfano mmoja wa kamusi. (ala 1)
  14. Taja aina moja ya maktaba. (ala 1)
  15. Kamilisha methali hii. (ala 2)
   Mgaagaa na upwa                                                             .
 4. ISIMU JAMII (ALAMA 5)
  1. Eleza maana ya lugha. (ala 1)
  2. Taja sifa mbili za lugha. (ala 2)
  3. Orodhesha dhima (umuhimu) mbili za lugha. (ala 2)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.             
  1. Mapenzi yangu kwa kilimo/kilimo ni uti wa mgongo
  2.      
   • Ni kazi yenye mvuto mkubwa kwake - kuimarisha lishe bora
   • Tajiri wake atakuwa ni Mola/Mungu kuliko kuajiriwa
   • Kilimo hujenga maandhari yenye kuvutia
  3. Mkulima huweka matuamini yake kwa Rabuka baada ya kupanda mimea yake
  4. Huwapa watu nguvu na afya kwa minajili ya kujenga taifa lao
  5.        
   • Kilimo cha kupanda mimea
   • Kilimo cha kufuga wanyama/mifugo
  6.      
   1. nia, lengo, sababu
   2. kazi
   3. watoto, wana
 2.      
  1.        
   • Irabu
   • Konsonanti
  2. Vokali/Voweli
  3. /e/ , /o/, /a/
  4. /d/, /t/, /z/, /s/, /n/, /r/, /l/
  5. Nisauti ambayo wakati wa kutamka huwa nyingi hutokea pwani
  6.        
   • meno
   • ufizi
   • kaakaa gumu
   • kaakaa laini
   • koo/koromeo/komeo/umio/kidakatonge
   • pua
  7. Hii ni sauti inayotakwa bila ya hewa kubanwa/ kufungiwa na ala za kutamkia
  8.           
   1. mbao, mbwa, mbata, mbili
   2. mbavu, mbiun, mbona, mboga
  9. ni kutilia mkazo silabi fulani katika neno ili kuleta maana iliyokusudiwa
  10.        
   • sauti
   • silabi
   • neno
   • sentensi
  11.        
   • nomino
   • kitenzi
   • kivumilishi
   • kiwakilishi
   • kielezi
   • kiunganishi
   • kihusishi
  12. Mwanafunzi mwerevu amefaulu sana(mtahini ahakiki sentensi ya mtahiniwa)
  13.            
   • kamusi ya kiswahili sanifu
   • kamusi ya methali
   • kamusi ya semi na nahau
   • kamusi ya isimu
   • kamusi ya sayansi
  14.      
   • ya kibinafsi
   • ya nyumabi
   • ya darasa
   • ya shule
   • ya kitaifa
   • maktaba inayosafiri
  15. hali wali mkavu
 3.        
  1. Ni mfumo wa sauti nasibu zinazopangwa kwa utaratibu fulani ili kutumika katika mawasiliano ya jamii fulani
  2.        
   1. lugha huzaliwa
   2. lugha hukua
   3. lugha yaweza kufa
   4. lugha hubadilika kutungwa na mazingira
   5. hakuna lugha bora kuliko nyingine
   6. kila lugha na sauti zake
   7. kila lugha ina wazungumzaji wake
  3.        
   • huwezesha mawasiliano
   • hukuza umoja wa jamii/taifa
   • hutambulisha jamii
   • huwezesha kupitisha hisia na mawazo ya watu
   • hujenga mahusiano baina ya watu

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 Term 2 Opener Exams 2022.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest