Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Examinations 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1. SEHEMU YA A: USHAIRI
    (SWALI LA LAZIMA)
    Soma shairi hili kisha ujibu maswali yafuatayo. 
    Nikumbuke mwanangu, 
    Kila asubuhi unapoamka 
    Kwenda kazini, 
    Unapochukua sabuni ya kunukia, 
    Na dodoki jororo. 

    Na kopo la koligeti,
    Kwenda kukoga hamumuni,
    Penye maji ya bomba, 
    Yaliyochujwa na kutakaswa, 
    Mororo… 

    Kumbuka nyakati zile, 
    Za staftahi ya sima na mtama, 
    Ndizi na nagwa, 
    Kwa mchicha na kisamvu, 
    Na ulipokwenda choo,
    Ulilia kwa uchungu 

    Nikumbuke,
    Unapotoka nyumbani asubuhi maridadi, 
    Katika suti ya moto,
    Miwani ya pembe, 
    Viatu vya Parisi, 
    Saa ya dhahabu, 
    Unapong’oka kwenda kazini, 
    Katika Volvo, 
    Katika njia iliyosakafiwa 

    Kumbuka, 
    Nyakati zile,
    Mimi na mamako, 
    Tulinyojidamka, 
    Mara tu kwale wa kwanza,
    Alipoanza kukoroma, 
    Jogoo wa kwanza hajawika, 
    Mimi nikachukua mundu na panga, 
    Mamako jembe na shoka,
    Tukaelekea porini, 
    Kufyeka na kuchimbua 

    Nahubaki wajiandaa kwenda shule… 
    Nikumbuke, 
    Saa za jioni, 
    Unapovalia kitanashati. 
    1. Thibitisha kuwa utungo huu ni shairi (alama 2) 
    2. Fafanua toni ya utungo huu. (alama 1) 
    3. Huku ukitoa mifano,linganua kati ya mistari toshelezi na mistari mishata. (alama 4) 
    4. Eleza maudhui yoyote matatu yanayojitokeza kwenye shairi. (alama 3)
    5. Kwa kutoa mifano tambua aina nne za taswira. (alama 4)
    6. Eleza mbinu za kimtindo zilizotumika katika shairi hili kando na taswira. (alama 4) 
    7. Tambua nafsi neni katika shairi hili na udhibitishe. (alama 2)

SEHEMU B: RIWAYA
Assumpta K. Matei - CHOZI LA HERI
Jibu swali la 2 au 3

  1. “Sijui kama kijana umesoma ile nadharia ya “deconstruction”. Ni muhimu pia ujue kwamba , ikiwa unataka kujiokoa au kuzoea hali mbaya inayokukabili, ni muhimu kujiingiza katika hali yenyewe, ukaikabili vilivyo ili uache kuiogopa , au iache kukuathiri vibaya.’’
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili ( alama 4)
    2. Tambua mbinu ya lugha iliyotumika kwenye dondoo. ( alama 1)
    3. Eleza sifa nne za msemewa wa dondoo hili. ( alama 4)
    4. Kwa kutolea mifano mwafaka riwayani, jadili nadharia ya ‘Deconstruction’ (alama 11)
      au
  2. Tathmini umuhimu wa usimulizi wa Pete katika kuijenga Riwaya Chozi la Heri.
    ( alama 20)

SEHEMU YA C : TAMTHILIA 
P. Kea - KIGOGO
Jibu swali la 4 au 5 

  1. Huku ukitoa mifano mwafaka, fafanua mbinu zinazotumiwa na utawala wa Majoka kuendeleza udhalimu katika jimbo la Sagamoyo. ( alama 20)
    au
  2. “… binadamu ni mavumbi na mavumbini aatarejea kwa maana, kwa tamaa mtu amependa kula kuku huku nduguze wakila kama kuku. Na katika uchu huo huo amependa kukifikia kilele cha ufanisi kwa kukanyaga migongo ya wenziwe. Hatajali kufanya  ujahili uwao ule, hata kupora wafu, almradi tu aweze kulifikia dhamirio lake.’’
    1. Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 4) 
    2. Eleza aina mbili za taswira zinazojitokeza katika dondoo. ( alama 4)
    3. Tambua mbinu nyingine mbili za kimtindo katika dondoo hili. (alama 2)
    4. Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. ( alama 10)

SEHEMU YA D: HADITHI FUPI-TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE 

  1. “Kwanza nilimwogopa sana…kwa sababu kila siku alinitishia…” 
    1. Fafanua muktadha wa dondoo. (alama 4) 
    2. Eleza sifa zozote nne za msemaji . (alama 4) 
    3. Ni sababu zipi zilichangia msemaji kujikuta katika mikono ya mrejelewa? (alama 4)
    4. Jadili masaibu wanayopitia watoto huku ukirejelea hadithi hii (alama 8)
      au
      S. Omar: Shibe Inatumaliza
  2.    
    1. Jadili matumizi ya kinaya  katika hadithi ya “ Shibe inatumaliza’’ (alama 10)
    2. “Tunakula tu. Vyetu na vya wenzetu… Na watakozaliwa miaka hamsini ijayo.”
      Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kutoa hoja kumi. (alama 10)

SEHEMU YA E: FASIHI SIMULIZI

  1. Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Malaika nakupenda Malaika
    Malaika nakupenda Malaika
    Nami nifanyeje?
    Kijana mwenzio 
    Nashindwa na mali sina we!
    Ningekuoa Malaika

    Pesa zasumbua moyo wangu
    Pesa zasumbua moyo wangu
    Nami nifanyeje?
    Kijana mwenzio 
    Nashindwa na mali sina wee
    Ningekuoa Malaika
    1. Tambua utungo huu. (alama 1)
    2. Thibitisha jibu la (a) . (alama 2)
    3. Tambua nafsineni katika utungo huu. (alama 1)
    4. Eleza toni inayojitokeza katika utungo huu. (alama 2)
    5. Umealikwa kuwasilisha utungo huu mbele ya wanafunzi wa shule yako.Taja mambo sita utakayozingatia ili kufanikisha uwasilishaji huu. (alama 6)
    6. Tambua na uthibitishe shughuli mbili za kijamii zinazojitokeza katika utungo. (alama 2)
    7. Taja mbinu mbili za kimtindo zilizotumika katika utungo. (alama 2)
    8. Eleza dhima ya utungo wa aina hii katika jamii. (alama 4)


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. SEHEMU A: USHAIRI 
    1. Umegawika katika beti 
      Kila ubeti una mishororo ingawa idadi inatofautiana katika kila ubeti (2 x 1= 2) 
    2.      
      1. Toni ya kusihi-nikumbuke mwanangu 
      2. Kushauri /wasia/nasaha-nikumbuke (1 x 1 =1) 
    3. Mistari toshelezi ni mistari iliyokamilika kimaana ilhali mistari mishata ni mistari mishata  isiyokamilika kimaana. 
      Mifano;mstari toshelezi-Nikumbuke mwanangu  mstari mshata-staftahi ya saa nane alasiri 
      (kulinganua, alama 2, mifano 2 x 2=4) 
    4. Umaskini-Wazazi wa mnenewa walikuwa wakiishi maisha ya uchochole huku wakifanya  kazi ya ukulima. 
      Mapenzi ya wazazi kwa watoto-wazazi wanawajibika kwa kuhakikisha kwamba wanalisha na kusomesha watoto wao. 
      Kazi/ajira-baba anamwambia mwanaye kwamba amkumbuke anapoenda kazini. 
      Elimu-nahubaki wakijiandaa kwenda shule (zozote 3 x 1 = 3) 
    5.        
      • Taswira mnuso mf. Sabuni ya kunukia
      • Taswira hisi mf ulilikia kwa uchungu
      • Taswira sikivu mf. Jogoo wa kwanza hajawika
      • Tawsira mwendo mf. Tukaelekea porini n.k
        (4x 1 = 4) 
    6. mbinu rejeshi/kisengere nyuma Kumbuka nyakati zile
      • utohozi Parisi  koligeti-
      • Mdokezo mf. Mororo... 
      • Chuku mf maji yaliyochujwa na kutakaswa
      • Takriri mf. Nikumbuke 
      • Usambamba mf. Unapotoka, unapochukua, unapong’oka ( 1x4 =4)
    7. nafsi neni – mzazi wa kiume – (mimi na mamako)
      (kutaja 1 ithibati 1)
  2. SEHEMU B: RIWAYA 
    Assumppta K. Matei - CHOZI LA HERI
    1.      
      1. msemaji ni Ridhaa
      2. msemewa ni mwangeka
      3. pale nyumbani mwa Ridhaa/gofu/ganjo/kiunzi
      4. mwangeka alipomtazama baba / Ridhaa kana kwamba anataka kuhakikishiwa jambo/ ridhaa anapokataa kuyaondoa majivuya familia yake iliyoteketea. 
    2. kuchangaya ndimi – deconstruction 
    3. sifa za mwangeka 
      • mwenye utu
      • mshauri bora
      • mlezi mwema
      • amewajibika
      • mwenye upendo
      • mdadisi
      • mwenye majuto
      • mwenye bidii
      • mwenye mawazo mapevu
      • mwenye msimamo imara
      • mzalendo
      • kumbukizi
      • mbunifu
      • mkakamavu/jasiri
      • mvumilivu
      • karimu
      • mtiifu
      • mwenye mzaha/mcheshi/
      • msomi
      • mnyenyekevu 
    4.        
      • ridhaa anakataa kushirikiana na majirani kuyachimba “mass grave” na kuyazika majivu ya familia yake.
      • Mwangeka anamshawishi Ridhaa akibomoe bkiunzi kile cha chumba lakini babake anakataa na kushikilia ndilo kaburi la ukumbusho wa familia yake. 
      • Ridhaa siku za mwanzoni pale kambini hakuweza kuitumia misala ya sandarusi lakini baadaye ilimbidi kujizoazoa na kuyatumia. 
      • Kaizari walipokuwa msituni na aila yake iliwabidi bkukata miti na kuvijenga vijijumba vilivyoezekwa kwa nyasi na kukandikwa udongo baada ya kufukuzwa makwao. 
      • Wakimbizi wakiwemo Ridhaa na Kaizari walipata changamoto ya maji safi ya kunywa lakini kiu ilipobisha hodi iliwabidi wanywe maji yale. 
      • Selume alipokosa glavu na vifaa vingine hopitalini ilimbidi kuvinunua ili awazalishe wajawazito.
      • Umu alipowakosa ndugu zake ilimbidiaanze kuwatafuta na kuelekea hadi kituo cha polisi.
      • Umu ilimbidi aelekeee mjini karaha kuanza maisha mapya /kutafuta usaidizi baada ya kuachwa peke yake.
      • Chandachema alikuwa analala kwingi ikiwemo kwenye michai iliyo na baridi ili aendele na masomo yake. Alifanya hivyo hadi akafuzu katika mtihani.
      • Waziri mstaafu pale kambini alilazimika kuishi maisha ya ukimbizi hata akasaidia katika ugawaji wa chakula. 
      • Dick alipoiingizwa katika biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya alilazimika kufanya kuzisafirisha hadi ughaibu baada ya kutishwa na Buda.
      • Zohali alipoona kuwa pale nyumbani hatakikani baada ya kupata mimba anatorokea mjini anakoanza maisha ya kuzururazurura mtaani.
      • Pete alilazimika kufanya kazi mbalimbali jijini baada ya fungona baadaye nyangumi kumfukuza. Alifanya kazi duni ili kuwakimu wanawe. 
      • Sauna anapobakwa na babake mlezi anaondoka kwao na kuungana na Bi kangara anapohusishwa na biashara ya ulanguzi wa watoto.
      • Mwangemi na Neema wanapokosa mtoto, inawabidi kumchukua mwaliko kama mtoto wao wa kupanga. 
      • Bi. Mwekevu alipojitosa siasani akijua kwamba jamii ina  taasubi dhidi ya wanawake.
      • Lunga anapokataa wananchi kuuziwa mahindi yaliyoharibika na shirika la Maghala na Nafaka akijua ataingia matatani.
      • Ridhaa anapobomolewa na kuchomewa majumba yake, anaendelea na ujenzi hadi anapojenga nyumba mpya ktika mtaa wa Afueni. 
      • Licha ya Mwangeka kumptoteza mkewe Lily na Mwanawe Becky anaamua kumuoa Apondi na kuanza maisha upya.
      • Naomi anaamua kumwacha mumewe na wanawe anaposhindwa kuyavumilia maisha mapya na kuamua kuenda kupambana na ulimwengu , huenda atasaidia familia yake .
      • Viongozi wanaposhindwa kuwajengea wakazi wa mtaa wa somber misala, inawabidi kutumia sandarusi kama misala.
      • Tuama anapashwa tohara baada ya shinikizo kutoka kwa wasichana wenzake na hamwambii babake mzee maarifa. 
  3.               
    • Kuonyesjha shida zinazokumba ndoa k.m Pete na babake
    • Kukashifu uavyaji mimba km. Pete kumeza vidonge
    • Kuchimuza maudhui ya umaskini km. Pete hana sodo
    • Kuendeleza maudhui ya utamaushi km. anaamua kunywa sumu ya panya afe
    • Kuonyesha maudhui ya mapuuza km. nyanyake pete anawarai wajomba kutomwoza Pete kwa Fungo lakini wanampuuza.
    • Kujenga maudhui ya utu km. anamlea pete baada ya kukanwa na babake mzazi
    • Kuendeleza maudhui ya elimu. Pete alikuwa darasa la saba akiozwa kwa fungo
    • Kukashifu ndoa za lazima km. 
    • Kudokeza athari za tohara ya wasicjhana km. 
    • Kuendeleza maudhui ya uwajibikaji km. nynyake anapinga tendo la kumwoza pete
    • Kubainisha changamoto zinzokumba ndoa ya mitara
    • Kukashifu ubaguzi wa kijinsiia km. pete anakatizwa masomo ili nduguze wasome
    • Kuchimuza maudhui ya utegemezikm Pete anategemea wanaume kukilisha kitoto
    • Kuendeleza maudhui ya usaliti
    • Kuomnyesha madhara ya ulevi – mlevi mmoja anambaka pete
    • Kuendeleza maudhui ya mabadiliko – pete anataka kubadilisha ,ustakabali na kuamua kutoishi
    • Kukashifu ukiukaji wa hakli za wafanyakazi
    • Kuonyesha ukiukaji wa haki za watoto
    • Anajenga sifa za wahusika 
    • Ukatili wa mamake pete unabainika anapomwoza pete akiwa darasa la saba
    • Kuendeleza ploti ya Riwaya. 
  4. SEHEMU YA C : TAMTHILIA
    P. Kea – KIGOGO
    • 4. 
    • Propaganda 
    • Kuwafukarisha raia
    • Kuwajaza raia hofu
    • Vitisho
    • Mauaaji
    • Matumizi ya seli
    • Matumizi ya polisi
    • Hongo/vishawishi
    • Kufunga runinga ya mzalendo
    • Kufuta watu kazi – Kingi
    • Udanganyifu/hila/.ujanj
    • Kuwafitinisha wanaharakati
    • Matumizi ya pombe
    • Kuharamisha maandamano
    • Kuwazawidi viobaraka
    • Kuwaangamiza wanaharakati
    • Kuzilipa familia ambazo amedhulumu – ngurumo
    • Kuwafurusha asiowataka jimboni – vikaratasi
    • Kuhonga wanaharakati kwa kazi
    • Kufukuza wafadhili wa wana harakati
    • Matumizi ya mshauri mkuu
    • Ndoa – Ngao junior
    • Matumizi ya wahumi
    • Kuurithisha uongozi kwa mwanawe
    • Hotuba kwenye vyombo vya habari
    • Kuwapa maskini chakula 
      (zozote 20x1)
  5.      
    1.        
      1. msemaji ni Babu
      2. msemewa ni majoka
      3. katika chumba cha wagonjwa
      4. kuhusu maovu ya majoka (4x1)
    2.      
      1. taswira muonjo – wakila kama kuku
      2. taswira mguso – kukangaga migongo ya wenziwe ( 2x 2)
    3.      
      1. Tashbihi – wakila kama kuku
      2. msemo – kukanyaga migongo ya wenziwe
      3. jazanda – kukanyaga migongo ya wenziwe ( kunyanyasa)
      4. takriri – kuku / mavumbi n.k
    4.      
      • usaliti katika ndoa – majoka hampendi husda uk.76
      • nafasi ya mwanamke – wasioweza kutegemewa uk.76
      • ukosefu wa uwajibikaji wa uongozi – hajashika usukani uk 80
      • wanasagamoyo wamezinduka – wanalilia damu yake uk79
      • mgogoro wa kinafsi – kilio kikubwa ndani kwa ndani –uk 75
      • kudokeza hatari inayongojea majoka – mikono yangu imefungwa kwa minyororo uk 73
      • kuchimuza matokeo ya awali – kuuawa kwa jabali  uk73
      • kuonyesha sifa za wahusika – tama ya husda uk 
      • sagamoyo haipigi hatua kimaendeleo – uk 81 .
      • mgongano kati ya utawala wa Babu na ule wa Majoka – kutikisa na kuubadilisha mkondo uk8 ( zozote 5x 2 = 10)
  6. SEHEMU D: TUMBO LISILOSHIBA NA HADITHI NYINGINE 
    1. haya ni maneno ya Bogoa akimjibu Sebu katika Club Pogopogo. 
      Sebu alitaka kujua kwa nini Bogoa hakumweleza matatizo yake kwa Bi. Sinai kama kunyimwa nafasi ya kuwaona wazazi wake na kulishwa makombo. (4 x 1 = 4) 
    2. sifa za Bogoa 
      1. Msiri;anaficha siri ya kuchomeka viganja, anatororka kisiri kutoka kwa Bi Sinai. 
      2. Mvumilivu;anavumilia mateso ya Bi Sinai hadi kubalaghe 
      3. Mwenye mapenzi;anampenda Sebu sana ndiposa anamwambia siri zake 
      4. Mwenye bidii; anajibidiisha kujifunza usonara na anaifanya kwa bidii 
      5. Karimu;anawanunulia kina Sebu vinywaji katika Club Pogopogo 
        (Za kwanza 4 x 1 =4)
    3. sababu zilizomchangia Bogoa kujikuta mikononi mwa Bi. Sinai 
      1. asubuhi moja babake alimwamsha mapema na kumtayarisha kisha babake akamwambia waende mjini amuache kwa marafiki zake/mrejelewa 
      2. babake alimshawishi kuwa jijini ni kuzuri na angekula vizuri na angeenda shuleni kusoma na kuandika . 
      3. babake alimshikia mkwaju na kutishia kumchapa iwapo angekataa kwenda kwa mrejelewa 
      4. umaskini wa wazazi wake uliwapelekea kumpeleka kulelewa kwa mrejelewa 
      5. mjini angepata maisha bora zaidi ya kitajiri 
        (zozote 4 x 1 = 4) 
    4. masaibu ya watoto 
      1. kutelekezwa wazazi wake bogoa wanayatelekeza majukumu yao ya malezi na kumpeleka kwa Bi Sinai
      2. kunyimwa usingizi wa kutosha annamshwa mapema kuchoma mandazi na kuyapeleka shuleni kuyauza
      3. kunyimwa uhuru wa kucheza na watoto wa jirani
      4. kunyimwa nafasi ya kusoma – Badala ya kupelekwa shuleni na Bi Sinai anamtumia kuchoma mandazi na kuyauza.
      5. kupigwa sana Bogoa anapoenda kucheza na kuchelewa kurudi Bi Sinai anamtafuta na kumpiga vibaya
      6. Kutishwa ; Bogoa anatishwa kukatwa ulimi akitoa siri ya nyumba ya Bi Sinai
      7. Kunyimwa nafasi ya kutangamana na wazazi wao . Bi Sinai anamzuia Bogoa kupatana na wazazi wake wanapomtembelea ili asipate nafasi ya kusimulia madhila anayopitia.
      8. Kubaguliwa Bi Sinai anawaambia wanawe kuwa watoto wa kimaskini  wanastahili kutumwa na hawastahili kwenda shuleni
      9. kutengwa na watoto wenzao Bogoa anateganishwa na wanuna wake anapopelekwa kwa Bi Sinai
      10. kulishwa makombo Bogoa anakula makombo ya watu waliokula na kushiba
      11. maoni yao kutosikilizwa ; babake Bogoa alimtishia kwa mkwaju 
      12. Kulia sufuriani Bogoa anakula kwenye sufuria na vyungu wakati kila mtu alikulia sahanini 
      13. Kufanyizwa kazi. Bi Sinai anamtumikisha Bogoa kuchanja kuni, kufagia, kuteka maji, kufua ilhali ni kitoto cha miaka mitano tu
        (zozote 8 x 1 =8)
  7.        
    1.      
      • Ni saa sita kamili na jua limewaka ila  sasa Mbura wamejikunyata
      • Mzee mambo ana vyeo anavyopata mishahara kupitia kuavyo ila hajui maana yavyo umuhimu wavyo wala majukumu yavyo.
      • Katika taifa la Mzee Mambo kinachoangaliwa Zaidi ni kwenda kazini wala si kufanya kazi.
      • Mzee Mambo hafanyi kazi ilhali ndiye anayepokea mshahara mkubwa kuliko wale wanaofanya kazi kama Sasa na Mbura.
      • Ni kinaya serikali kufuja mali ya umma. Kugharamia sherehe za mtu binafsi(Mzee Mambo)ambaye anaifisidi serikali iyo hiyo kwa kulipwa mshahara bila kufanya kazi.
      • Sasa na Mbura walikuwa wamepakua chakula mara mbili na kukila lakini wanapopakuwa mara ya tatu mwandishi anasema kuwa huo ndio wakati walipoanza kula.
      • Sasa na Mbura wanafanya kazi kwa kujituma na kujitutumua ila kazi yenyewe ni ya ukwe isiyo na malipo.
      • Mwandishi anasema kuwa Sasa na Mbura hawana wasichofanya lakini hawana wafanyacho.
      • Ni kinaya kwa mzee Mambo kufisidi serikali na kujiliwaza kwa neno lake Mola kuwa Mungu humpa amtakaye bila ya kiwango maalum ilhali ameliibia taifa lake.
      • DJ anamfanyia kazi mzee mambo lakini analipwa mshahara na serikali badala ya kulipwa na mzee Mambo.
      • DJ mwenye pesa halipi huduma za maji, umeme na matibabu ilhali raia maskini wanalipia huduma hizo. (zozte 10x1=10)
    2.      
      1. Mzee Mambo kupakua mshahara licha ya kuwa waziri kivuli.
      2. Kuandaliwa kwa sherehe isiyo na umuhimu wowote – kwa sababu mmoja ameota jino na mwingine anajiunga na nasri skuli
      3. Magari ya serikali kutumiwa katika sherehe ya kibinafsi
      4. Waliohudhuria sherehe kula vyakula vingi bila kujali lawama
      5. Unyakuzi wa dawa za umma – DJ anamiliki duka ambalo mtaji wake ni bohari kuu ya dawa za serikali
      6. DJ na wenzake kuchota mabilioni ya pesa kwa sherehe
      7. Mawaziri wawili kufanya kazi katika wizara moja – Sasa na Mbura
      8. DJ kupata huduma za umeme bila malipo licha ya kuwa na pesa.
      9. Sasa na Mbura kuibia serikali muda wa kufanya kazi kwa kwenda kuhudhuria sherehe nyumbani mwa Mambo.
      10. Mzee Mambo anatumia mabilioni ya serikali kugharamia sherehe nyumbani kwake.
      11. Mzee Mambo anatumia magari ya serikali kusomba maji, kubeba jamaa zake kuelekea kwenye sherehe nyumbani kwake.
      12. Mzee Mambo anatumia runinga ya taifa kupeperusha sherehe  ya kibinafsi ilhali anastahili kupeperusha maswala ya kitaifa.
        (za kwanza 10x1=10)
  8.      
    1. Tambua utungo huu
      alama 1
      Wimbo wa mapenzi
    2. Thibitisha jibu la (a) . alama 2
      Anasema anampenda Malaika
      Anasema angemuoa Malaika
    3. Tambua nafsineni katika utungo huu. Alama 1
      mvulana
    4. Eleza toni inayojitokeza katika utungo huu. Alama 2
      kubembeleza/ kushawishi
    5. Umealikwa kuwasilisha utungo huu mbele ya wanafunzi wa shule yako.Taja mambo sita utakayozingatia ili kufanikisha uwasilishaji huu. Alama 6
      1. awe jasiri -aweze kuimba wimbo mbele ya watu bila uoga
      2. mbunifu-auimbe wimbo huu kwa njia ya kuvutia ili aondoe ukinaifu /mbinyo
      3. atumie ishara za uso , za mwili na miondoka ambayo ianaoana na wimbo wake.
      4. Awe mjuzi wa lugha  ya jamii husika
      5. Aielewe hadhira yake
      6. Avae maleba  yanayooana na wimbo anaoimba
      7. Abadilishe toni na kiimbo kulingana na wimbo wake.
      8. Ashirikishe hadhira kwa kuuliza maswali ya balagha ili kuondoa uchovu.
      9. Mfaraguzi-awe na uwezo wa kubadilisha wimbo wake papo hapo.
      10. Awe na sauti inayosikia na hadhira yake. 
    6. Tambua shughuli mbili za kijamii zinazojitokeza katika utungo. (Alama 2)
      ndoa – ningekuoa 
      kulipa mahari – nashindwa na mali sina
      (kutaja ½ mfano ½ )
    7. Taja tamathali mbiliza usemi zilizotumika katika utungo.alama 2
      sitiari-malaika
      swali la balagha-Nami nifanyeje?
      Takriri – malaika / nashindwa na mali sina 
      Nidaa – nashindwa na mali sina wee!
    8. Eleza sababu nne utakazowahimiza wanafunzi wenzako wadumishe utungo huu katika   jamii.alama 4
      1. Kitambulisho cha jamii
      2. Huburudisha
      3. Huliwaza
      4. Huhifadhi utamaduni
      5. Hurithisha elimu ya jamii
      6. Hukuza lugha
      7. Hukuza ubunifu
      8. Huadilisha
      9. Huhifadhi hisoria ya jamii
      10. Hupumbaza
        (Zozote nne =4)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Paper 3 Questions and Answers - MECS Cluster Joint Mock Examinations 2022.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?