Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 1 Exams 2023

Share via Whatsapp

Kiswahili Insha

Mwandikie rafikiyo mliyesoma naye barua ukimwelezea mambo mbalimbali kuhusu shule yako mpya ya upili   (Alama 20)

USHAIRI

Ukimwi vielelezo, vyake vinoendeleza,
Mtu hasa ni wa mwanzo, Yule asojituliza,
Hupata maambukizo, wengine kuwarukiza,
Hiyo njia mojawapo, inosambaza ukimwi.

Damu nayo huchangiya, pasi na kuichunguza,
Tenye vidudu vibaya, mwengine kumuongeza,
Kuona wasaidiya, kumbe wamuangamiza,
Na hilo ni mojawapo, lisambazalo ukimwi

Shidano kutochemsha, hata nahilo laweza,
Ukimwi kusababisha, kwengine kuufikiza,
Kuona wasalimisha, na huku wadidimiza,
Hiyo ni njia, yatatu, kutapakaza ukimwi.

Tuwe nayo tahadhari, hayana kujikimbiza,
Ni ugonjwa wa tahari, waganga wanaeleza,
Tuufate ushauri, ule wa kujituliza,
Hii ndio njia bora, kujikinga na ukimwi

 1. Toa kichwa mwafaka acha ushairi huu (Al 2)
 2. Shairi hili ni la aina gani? Eleza sababu. (Al2)
 3.  Eleza vina vya ubeti wa pili. (Al2)
 4. Andika mizani ya ubetu wa tatu mshororo wa pili. (Al2)
 5. Ni mambo yepi yanayosambaza ugonjwa wa ukimwi kulingana na ushairi huu. (Al2)

MATUMIZI YA LUGHA

 1.  
  1. Tofautisha kati ya irabu n akonsonanti. (Al 2 )
  2. Taja kipasuo hafifu cha mdomo (Al 1)
  3. Tofautisha kati ya konsonanti (r) na (l) (Al 2 )
 2. Tunga sentensi zenye miundo hii (Al 4)
  1. I + N + T + E
  2. N + V + T + E + E
 3. Eleza dhima tatu za lugha (Al 3)
  1. Bainisha viambishi awali na viambishi tamati katika sentensi zifuatazo. (Al 2)
   1. Analima
   2. Wanacheza
  2. Kiambishi ni nini? (Al 1)
 4. Taja matumizi ya alama hii ya kuakifisha (:) kwa kutoa mifano katiak sentensi (Al 3)
 5. Ukitaka kupata maana ya maneno yafuatayo kwenye kamusi utatazama neno gani? (Al 2)
  1. Alimkibilia
  2. Kilivunjika
 6. Taja aina tatu za maktaba (Al 3)
  1.  Je, Kiimbo ni nini? (AL 1)
  2. Onyesha matumizi matatu ya kiimbo. (Al 3 )
 7.  
  1. Ngeli ni nini? (Al 1)
  2. Maneno haya yako katika ngeli zipi? (Al 2)
   1.  Mbuyu
   2. Chetezo

ISIMU JAMII


  1. Eleza maana ya maneno yafuatayo. (Al 2 )’
   1. Isimu jamii
   2. Sajili
  2. Taja kaida tatu za lugha. (Al 3)
 1. Soma makala yafuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata.
  Mhusika A: Karibu kastoma nikuuzie. Hujambo?
  Mhusiak B: Salama ndugu. Naomba uniuzie.
  Mhusika A: Chagua, kila kitu kipo. Bei nafuu, bei ya kuelewana, vitu fresh.
  Mhusika B: Debe moja la viazi vitamu wauzaje?
  1. Tambua sajili hii. (al 1)
  2. Eleza sifa nne za sajili uliyoitambua. (Al 4 )


MWONGOZO

 1. Toa kichwa mweafak acha ushairi huu (Al 2)
  • ukimwi, Ugonjwa wa ukimwi
 2. Shairi hili ni la aina gani? Eleza sababu. (Al2)
  • Tambia – lina mishororo mine katika kila ubeti
 3. Eleza vina vy aubeti wa pili. (Al2)
  • Ya, Za
  • Ya, za
  • Ya, za
  • Po, mwi
 4. Andika mizani ya ubetu wa tatu mshororo wa pili. (Al 2)
  • U – ki – mwi - ku – sa - ba – bi – sha, kwe – ngi – ne ku – u – fi – ki – za
 5. Ni mambo yepi yanayosambaza ugonjwa wa ukimwi kulingana na ushairi huu. (Al2)
  • Kutotulia n akuambukiza wengine (rukiza )
  • Kusaidian akwa damu iliyo n avirusi
  • Kutumia shidano
 6.  .
  1. Tofautisha kati ya irabu n akonsonanti. (Al 2 )
   • Irabu hutamkwa kwa ulaini bila hewa kuzuiliwa na ala za kutamkia.
   • Konsonanti zinapotamkwa hewa hubwan / huzuiliwa na sehemu mbili za kutamkia
  2. Taja kipasuo hafifu cha mdomo (Al 1)
   • Kipasuo hafifu cha mdomo /P/
  3. Tofautish akati ya akonsonati (r) na (l) (Al 2 )
   • /r/ - ni kimadende, ulimi (Ncha ) hupigapiga ufizi
   • /l/ - kitambaza, ncha ya ulimi hugusa ufisi mara moja
 7. Tunga sentensi zenye miundo hii (Al 4)
  1. I + N + T + E
   • Lo! Mama ameanguka sokoni.
  2. N + V + T + E + E
   • Mtoto mdogo anasoma vizuri sana
 8. Eleza dhima tatu za lugha (Al 3)
  • Mawasiliano
  • Chombo cha kujieleza na kutoa mawazo yetu
  • Hujenga uhusiano baina ya watu
  • Kitambulisho cha
 9.  
  1. Bainisha viambishi awali na viambishi tamati katika sentensi zifuatazo. (Al 2)
   • KISFM1QN5Analima
  2. Kiambishi ni nini? (Al 1)
   • Sehemu ndogo ya neno iliyo na maana kisarufi
 10. Taja matumizi ya alama hii ya kuakifisha (:) kwa kutoa mifano katiak sentensi (Al 3)
  • Huashiria orodha - Alinunua : maziwa, mkate na sukari
  • Kutenganisha tarakimu
  • Hutenganisha sa na dakika
  • Hutenganisha maadishi na tamthilia
 11. Ukitaka kupata maana ya maneno yafuatayo kwenye kamusi utatazama neno gani? (Al2)
  1. Alimkibilia – kimbia
  2. Kilivunjika – vunja
 12. Taja aina tatu za maktaba (Al 3)
  • Maktaba ya kibinafsi
  • Maktaba ya nyumbani
  • Maktaba ya darasa
  • Maktaba ya shuleni
  • Matkaba ya kitaifa
 13.  
  1. Je, KIimbo ni nini? (AL 1)
   • Ni upandaji na ushukaji wa sauti
  2. Onyesha matumizi matatu ya kiimbo. (Al 3 )
   • Kuuliza swali – ameenda?
   • Kuonyesha kauli – Ameenda.
   • Mshangao – Ameenda!
 14.  
  1. Ngeli ni nini? (Al 1)
   • Ni mgawanyiko wa nomino katiak makundi
  2. Maneno haya yako katika ngeli zipi? (Al 2)
   1. Mbuyu – u - i
   2. Chetezo – ki - vi
 15.  
  1. Eleza maana ya maneno yafuatayo. (Al 2 )’
   1. Isimu jamii
    • Ni matumizi ya lugh akatika jamii sayansi inayochunguza uhusiano kati ya lugha na jamii.
   2.  Sajili
    • Matumizi ya lugha katika muktadha Fulani.
  2. Taja kaida tatu za lugha. (Al 3)
   • Wahusika
   • Uhusiano
   • Mahali
   • Jinsia
   • Tabaka
   • Elimu
   • Umri
 16. Soma makal yafuatayo kasha ujibu maswali yanayofuata.
  Mhusika A: Karibu kastoma nikuuzie. Hujambo?
  Mhusiak B: Salama ndugu. Naomba uniuzie.
  Mhusika A: Chagua, kila kitu kipo. Bei nafuu, bei ya kuelewana, vitu fresh.
  Mhusika B: Debe moja la viazi vitamu wauzaje?
  1. Tambua sajili hii. (al 1)
   • Sajili ya sokoni
  2. Eleza sifa nne za sajili uliyoitambua. (Al 4 )
   • Msamiati maalum – kastoma, fresh
   • Utohozi hutumiwa, kastom a, fresh
   • Lugha ya kushawishi wanunuzi
   • Lugha ya kuchanganya ndimi
   • Lugha huwa na mzaha
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 1 End Term 1 Exams 2023.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest