Print this page

KISWAHILI - Form 2 End of Term 1 2019 Examinations

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.

    Ponografia ni tendo, maandishi, picha au michoro inaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa ajili ya kuchochea ashiki ya kuifanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana kupitia sinema, magazeti, vitabu, muziki, televisheni, tovuti na kanda za kunasia picha na sauti.
    Ponografia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii ni kwa sababu imeenea kote ulimwenguni mithili ya moto mbugani wakati wa kiangazi. Kuenea kwake kumechangiwa na mambo kdha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi ukiwa umetokana na kuimarika kwa vyombo vya teknologia ya habari na mawasiliano. Hata hivyo, kazi hii hubuniwa au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi lingine ni lile la wanaochukia ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Kwa mfano, baadhi ya wanamuziki hutumia ponografia kuvutia wateja na hivyo kuzidisha mauzo yao.
    Kushamiri kwa wimbi na uonyeshaji wa ponografia kuna athari kubwa kwa jamii hasa watoto.Ingawa watu wengine hudai picha hizi haziwathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wale wanaotazama picha za ngono hupata matatizo. Lazima ieleweke kwamba kinachoonekana kwa jicho au kusikika kwa sikio huathiri fikira au hisia. Picha za matusi zinachangia kwa kiasi kukubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia mambo muhimu kama vile masomo, watu huanza kutafakari mambo machafu.
    Vijana wengi ni kama bendera, huyaiga wanayoyaona na kuyasikia. Hili ni tatizo linalowafanya kuacha mkondo wa maadili. Hivyo basi wengi hushawishiwa kuingilia shughuli za ngono mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni ukahaba, utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya ya darasani na mimba zisizotarajiwa. Vijana wengi huacha shule kabisa huku wengine wakiambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo yanaweza kuwaletea mauti.
    Yasemekana kuwa akili za binadamu hunasa zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha na hivyo basi matusi haya yaweza kudumishwa katika kumbukumbu zao. Tabia mbaya kama vile ushoga, ubasha na usagaji huwa matokeo yake na hata matokeo ya vijana hugeuka wanapoanza kuiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao. Hali kadhalika, lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono huibuka. Yote haya yanakinzana na desturi za mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kuchapo. Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama vile unywaji pombe na matumizi ya vileo ambavyo huchochea uchu wa ngono na kuibua tabia za kinyama.
    Kuendelea kuzitazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu, huondoa makali kiasi kwamba hata katika uzima mtu hupoteza mhemko na kugeuzwa kuwa mtegemezi wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mjini na vijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na malezi haya yasiyo na kizuizi.
    Kuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi, watu kuwajibika kwa kuwalinda na kuwahimiza vijana kuhusu maovu haya na wale wenye midahilishi, video na sinema kutowaruhusu vijana kutazama uchafu huu kunaweza kuwa maana ya kuyakinga au hata kuyaepuka madhara ya ponografia. Ni sharti pia sheria izuie na kupiga marufuku utengenezaji na ueneaji wa upungufu huu. Bila shaka, sheria na hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi ya waivunjao. Hali kadhalika, wazazi wasijipweteke tu bali wawaelekeze watoto wao ipasavyo na kila mtu alitekeleze jukumu lake.

    MASWALI
    1. Yape makala uliyosoma anwani mwafaka       (al 1)
    2. Toa sababu za kusambaa kwa uchafu unaozungumziwa katika taarifa. (al 2)
    3. “Bendera hufuata upepo” Thibitisha ukweli wa kauli hii   kulingana na makala (al 1)
    4. Ponografia huchangia madhara mengi hasa miongoni mwa vijana. Taja manne.(al 4)
    5. Ni hatua zipi zinazofaa kuchukuliwa dhidi ya aina ya uozo unaozungumziwa na mwandishi?  (al4)
    6. Fafanua msamiati huu kimuktadha.
      1. Uchu
      2. Wasijipweteke
      3. Kuwa butu
  2. MATUMIZI YA LUGHA (AL 55)
    1.  
      1. Sauti ni nini katika lugha (al 1)
      2. Taja sifa mbili bainifu za /m/    (al 2
    2. Kwa kutoa mifano, eleza dhana hizi: (al 2)
      1. Silabi wazi
      2. Silabi funge
    3. Ainisha mofimu katika neno : (al 3)
      Anatupikia
    4. Bainisha aina za nomino zilizotumika katika sentensi ifuatayo.
      Juma alimpa mtoto yule maji ya Baraka      (al 4)
    5.  
      1. Andika kwa wingi:
        Ile ya kujengea haijaletwa (al 2)
      2. Andika kwa umoja
        Mishale yao ilifungwa kwa manyoya mengi meusi   (al 2)
    6. Andika katika ukubwa wingi
      Njia hii inafaa zaidi kuliko ile (al 2)
    7. Yakinisha:
      1. Sikusikia kuwa alichapwa wala kuumizwa (al 2)
      2. Asingefika mapema asingemsaidia       (al 2)
    8. Taja ngeli za nomino zifuatazo    (al 3)
      1. Maziwa
      2. Chai
      3. Kinyongo
    9. Tofautisha maana katika sentensi zifuatazo:
      1. Chakula chote kinapendeza
      2. Chakula chochote kinapendeza
    10. Tumia neno “alasiri” katika sentensi kama: (al 2)
      1. Nomino
      2. Kielezi
    11. Kirai ni nini? (al 2)
    12. Wachezaji walikula chakula chote.
      Anza: Chakula
    13. Tambua aina ya maneno :
      1. Ng’ombe mweusi atachinjwa leo      (al 2)
      2. Kwa kutoa mifano, eleza maneo mawili ya Ritifaa
    14. Eleza maana ya: (al 2)
      1. Ala tuli
      2. Ala sogezi
    15. Bainisha matumizi ya kiambishi ‘ni’ katika sentensi hizi:-
      1. Alikula shuleni
      2. Ni mchezo huo    (al 2)
    16. Andika sentensi zifuatazo ukizingatia maagizo uliyopewa katika mabano. (al 2)
      1. Magari yote yalitiwa vidhibiti mwendo (Mazoea)
      2. Alichora na akatuzwa (hali timilifu)
    17.  Kamilisha methali zifuatazo (al 2)
      1. Zimwi likujualo……………………………………………..
      2. ……………………………..……..…… Hafikilii mbingu
    18. Toa maana mbili ya sentensi hii:-
      Babu alinipigia mpira                                           (al 2)
    19. Eleza maana ya misemo hii (al 2)
      1. Valia miwani
      2. Kula kadhongo
    20. Huku ukitoa mifano, eleza maana ya viambishi awali na viambishi tamati. (al 4)
  3. ISIMU JAMII        (AL 12)

    Soma kifungu kifuatacho kasha ujibu maswali.

    Jane:                Hallo John
    John:                Hallo Jane
    Jane:                Uko wapi
    John:                Niko kazini
    Jane:                Umelost hivi kwa nini?
    John:                Kazi mob tu na…….
    Jane:                Tukutane wapi............lini?
    John:                Hallo…..hallo
    1. Tambulisha muktadha wa mazungumzo haya. (al 2)
    2. Taja sifa zozote nne zinazotambulisha mazungumzo haya.(al 8)
  4. FASIHI SIMULIZI     (AL 20)
    1. Eleza sifa za hadithi.    (al 5)
    2. Taja sifa tano za mtambaji bora.  (al 5)
    3. Eleza umuhimu wa vitanza-ndimi .    (al 5)
    4. Eleza kikamilifu umuhimu was fasihi simulizi katika jamii. (al 5)
Join our whatsapp group for latest updates

Download KISWAHILI - Form 2 End of Term 1 2019 Examinations.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Read 7449 times

Related items

Get on WhatsApp Download as PDF