Kiswahili Form 2 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021

Share via Whatsapp

Kiswahili Form 2 End Term 2 Exams 2021 with Marking Schemes

  1. SEHEMU A; INSHA ALAMA 20

    Andika ratiba ya siku ya wazazi shuleni

  2. SEHEMU YA B: UFAHAMU: (ALAMA 15)

    Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayo.

    MAVAZI REKEBISHENI

    Vazi njema kivaliwa, huongezeka heshima,
    Staha mtu kapewa, poteendapo daima,
    Mavazi duni si sawa, kina dada ninasema,
    Mavazi rekebisheni usherati umezidi.

    Longi kwa nyuma kushika, na mapajani kubana,
    Chupi zilipowafika, dhahiri kuonekana,
    Bure munaaibika, na kujishusha maana,
    Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

    Kifua nikujikaza, maziwa ya ning’inie,
    Kitu gani munawaza, hamna bahari nyie,
    Ni ashiki mwasambaza, sikizeni niwambie,
    Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

    Msichana ni hatia, magotini kufichuka,
    Hivyo basi kuvalia, rinda lisoyafunika,
    Huenda zusha hisia, maovu yakawafika,
    Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

    Sitakosa kuzitaja, skati mnazovaa,
    Zaisha kwa mapaja, kikiri kuchuchumaa,
    Iko wazi nyonga moja, mkato ulivyokaa,
    Mavazi rekebisheni, usherati lumezidi.

    Wazi nitawasomea, nguo hizi nguo gani?
    Dada zetumwakosea, kuzivaa hadharani,
    Ndizo hizo huchochea, usherati mitaani,
    Mavazi rekebisheni, usherati umezidi.

    Nguo chini zishusheni, mwilini mzipanue,
    Heri kuingia deni, za heshima mnunue,
    Kuigiza za kigeni, ni utumwamtambue,
    Mavazi rekebisheni, usheratiumezidi.

    Betiti sana maliza, kalamunaweka chini,
    Iwapo wajiuliza, nakereketwa ni nini?
    Ni stahanahimiza, sio wake kuhaini,
    Mavazi rekebisheni, usheratiumezidi.

    MASWALI YA USHAIRI
    1. Shairi hili ni la aina gani?      (alama 2)
    2. Eleza vina vya beti za kwanza mbili  (alama 2)
    3. Toa kibwagizo cha shairi hili kisha ufafanue maana yake.    (alama 2)
    4. Eleza maana ya misamiati hii kama ilivyotumika katika ushairi.      (alama 4)
      Staha –
      Dhahiri –
      Shani –
      Duni –
    5. Shairi hili liko katika bahari zipi? (alama 2)
    6. Uhuru wa mshairiunadhihirikavipi katika shairi hili? ( Alama 3)

  3. MATUMIZI YA LUGHA (AL 30)
    1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au si ghuna. (al 1)
      /Z/
      /K/
    2. Eleza maana ya kiimbo. (al 1)
    3. Eleza maana ya shadda. (al 1)
    4. Eleza maana ya mofimu.(al 2)
    5. Andika kwa wingi sentensi hizi. (Al.2)
      1. Goti la mtoto liliumia.
      2. Ukwato wa ngamia ni mpana.
    6. Bainisha nomino hizi ni za aina gani. (al.2)
      1. Sukari.
      2. Mapenzi.
    7. Tumia vivumishi vya sifa katika mabano kukamilisha sentensi zifuatazo. (al 2)
      1. Mtoto Yule ni ______________________ (nene)
      2. Bei ya meli ni _____________________ mno (ghali)
    8. Jaza pengo kwa kiulizi sahihi kisha uandike sentensi kwa wingi (al 2)
      Ni mpishi ________________ aliyepika.

    9. Fafanua maana ya misemo ifuatayo. (al2)
      1. Kula mate.
    10. Andika katika wingi. ( al 2)
      1. Jiji hili litapanuka upesi.
      2. Jizee lililokosa adabu limekaripiwa.
    11. Geuza sentensi zifuatazo katika hali ya usemi halisi. (al 2)
      1. Ruheni alishauriwa na kasisi aache tabia mbaya.
      2. Mwalimu alimwambia premji afanye bidii katika masomo yake.
    12. Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeshana. (al 2)
      1. Penda .
      2. Endesha.
    13. Tambua kikundi nomino (KN) na kikundi tenzi (KT) katika sentensi zifuatazo. (al 2)
      1. Anatembea kwa madaa kama tausi.
    14. Kanusha sentensi zifuatazo. (Al) 2
      1. Mimi nilicheza.
      2. Wewe huchora.
    15. Kamilisha methali zifuatazo ?(al 1)
      1. Cha kuvunda. _____
    16. Andika kinyume cha maneno yafuatayo. (al 2)
      1. Tandika ______________
      2. Umba _____________
    17. Pambanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mstari. (al 2)
      Naimba huku nafanya kazi. _____________________________

ISIMU JAMII( ALAMA 5)

Eleza sifa za lugha ya hotelini

FASIHI SIMULIZI ( al 10)

  1. Taja aina nne za hadithi.
  2. Eleza umuhimu wa hadithi.

Mwongozo wa kusahihisha

  1. SEHEMU A; INSHA ALAMA 20
  2. SEHEMU YA A: UFAHAMU: (ALAMA 15)

    MASWALI YA USHAIRI
    1. Shairi hili ni la aina gani?        (alama 2)
      Tarbia
    2. Eleza vina vya beti za kwanza mbili   (alama 2)
      Ubeti 1
      wa , ma

      wa, ma
      wa , ma
      ni , di

      ubeti 2
      ka, na

      ka, na
      ka,na
      ni, di

    3. Toa kibwagizo cha shairi hili kisha ufafanue maana yake.    (alama 2)
      Mavazi rekebisheni , usherati umezidi
      Maelezo, watu wavae nguo za heshima ili kupunguza usherati
    4. Eleza maana ya misamiati hii kama ilivyotumika katika ushairi.      (alama 4)
      Staha – heshima
      Dhahiri – wazi
      Shani – shangaza
      Duni – siokuwa na thamani
    5. Shairi hili liko katika bahari zipi? (alama 2)
      Mathnawi – vipande viwili
      Ukaraguni- vina vinabadilika badilika
    6. Uhuru wa mshairi unadhihirika vipi katika shairi hili? ( Alama 3)
      Kuboronga sarufi
      Inkisari- kivalia
      Utohozi - longi
  3. MATUMIZI YA LUGHA.(AL 30)
    1. Pambanua sauti hizi kama ni ghuna au si ghuna. (al 1)
      /Z/ - Ghuna
      /K/ - si ghuna
    2. Eleza maana ya kiimbo. (al 1)
      Ni mkazo
    3. Eleza maana ya shadda. (al 1)
      Ni upandaji na ushukaji wa sauti unaofanyika wakati mtu anapozungumza
    4. Eleza maana ya mofimu.(al 2)
      Ni ile sehemu ndogo ya neno inayowasilisha maana
    5. Andika kwa wingi sentensi hizi. (Al.2)
      1. Goti la mtoto liliumia.
        Magoti ya watoto yaliumia
      2. Ukwato wa ngamia ni mpana.
        Kwato za ngamia ni pana.
    6. Bainisha nomino hizi ni za aina gani. (al.2)
      1. Sukari.- wingi
      2. Mapenzi – dhahania
    7. Tumia vivumishi vya sifa katika mabano kukamilisha sentensi zifuatazo. (al 2)
      1. Mtoto Yule ni ______________________ (nene)
        mnene
      2. Bei ya meli ni _____________________ mno (ghali)
        ghali
    8. Jaza pengo kwa kiulizi sahihi kisha uandike sentensi kwa wingi (al 1)
      Ni mpishi ________________ aliyepika.
      Yupi
    9. Fafanua maana ya msemo ifuatayo. (al2)
      Kula mate.- kosa riziki
    10. Andika katika wingi. ( al 2)
      1. Jiji hili litapanuka upesi.
        Majiji haya yatapanuka upesi
      2. Jizee lililokosa adabu limekaripiwa.
        Majizee yaliyokosa adabu yamekaripiwa.
    11. Geuza sentensi zifuatazo katika hali ya usemi halisi. (al 2)
      1. Ruheni alishauliwa na kasisi aache tabia mbaya.
        “Ruheni, wacha tabia mbaya.” Kasisi alimushauri
      2. Mwalimu alimwabia premji afanye bidii katika masomo yake. (al 2)  “ Premji, fanya bidii katika masomo yako.” Mwalimu alimwabia.
    12. Andika vitenzi vifuatavyo katika hali ya kutendeshana. (al 2)
      1. Penda .
        pendezana
      2. Endesha.
        Endeshana
    13. Tambua kikundi nomino (KN) na kikundi tenzi (KT) katika sentensi zifuatazo. (al 1)
      1. Anatembea kwa madaha kama tausi.
        Kundi tenzi
    14. Kanusha sentensi zifuatazo. (al 2)
      1. Mimi nilicheza.
        Mimi sikucheza
      2. Wewe huchora.
        Wewe huchori
    15. Kamilisha methali ifuatayo ?(al 1)
      1. Cha kuvunda. __hakina ubani
    16. Andika kinyume cha maneno yafuatayo. (al 2)
      1. Tandika – tandua
      2. Umba – umbua
    17. Pambanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mstari. (al 2)
      Naimba huku nafanya kazi.
      S – S1+U+S2.
      S1 – KN +KT.
      KN + Ø.
      KT- T.
      T – naimba.
      U – huku.
      S2 – KN + KT.
      KN – Ø
      KT – T+N .
      T – nafanya.
      N – kazi .
  4. ISIMU JAMII (al 5)
    1. Eleza sifa za lugha ya hotelini .
      1. Kuna kutaja bei.
      2. Matumizi ya lugha ya heshima.
      3. Huwa na sentensi fupi fupi.
      4. Huwa na msamiati maalum kama vile, chakula, chai, soda nk.
      5. Wakati mwingini huashiria amrisho.
  5. FASIHI SIMULIZI (al 10)
    1. Taja aina nne za hadithi.
      1. Hekaya
      2. Hurafa
      3. Visasili
      4. Visaviini
      5. Mighani
    2. Eleza umuhimu wa hadithi.
      1. Huielekeza jamii
      2. Huridhisha elimu ya jamii
      3. Hukuza uwezo wa kukubuka
      4. Huhalalisha baadhi ya desturi za jamii
      5. Huonya
      6. Hushauri
      7. Huhifadhi na kuendeleza historia ya jamii
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Form 2 Questions and Answers - End Term 2 Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest