Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 3 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI


KIDATO CHA PILI


MUHULA WA TATU,

 1. INSHA
  Wanafunzi wa shule yenu walienda safari mji wa karibu (wewe ukiwemo).Eleza jinsi safari ilivyokuwa (alama 20)
 2. UFAHAMU
  SOMA TAARIFA IFUATAYO KISHA UJIBU MASWALI YANAYOFUATA

  Wanasayansi wengi wameshindwa kuelewa ni kwanini watu huvuta sigara kwa kuwa moshi wa sigara huathiri wavutaji wa sigara na watu walio karibu nao na pengine huleta ugonjwa wa moyo. Wavutaji hupatwa na kikohozi cha daima kisicho sikia dawa, maisha hupata limewatatiza binadamu kwa karne nyingi zilizopita na kuwacha rundo la maswali kuhusu uvutaji sigara.

  Sigara au sigareti ni kitu cha uraibu wa kuvuta, kinachotengenezwa kwa majani ya tumbako yaliyokaushwa. Husokotwa katika karatasi maalum.Tumbako pia huvutwa kwenye kiko, hunuswa na hutafunwa.Tumbako inayosagwa na kunuswa au kubwiwa huitwa ugoro.

  Hapana shaka wavutaji sigara huharibu afya yao. Wataalamu wa sayansi na madaktari wamefanya uchunguzi na wamethibitisha maradhi mfano wa pumu kutokana na moshi wa sigara unaowakereta koo. Kuna pia wanaosema kwamba uvutaji sigara unasababisha saratani ya mapafu.Watu wengi hufa kwa ugonjwa wa ghafla kwa sababu ya sumu ya moshi wa sigara ambao hutunguza na kuyatoboatoboa mapafu.

  Baadhi ya wavuta sigara hutupa vipande vya sigara ovyo bila kuzimwa na hivyo husababisha hasara kubwa kama vile uchomaji wa misitu, nyumba na nguo na wakati mwingine husababisha hata vifo. Uvutaji sigara umefika kiwango cha kusikitisha, utaona vijana, yaani wasichana na wavulana wadogo sana, wakivuta sigara mbele ya watu wazima bila kujali hii ni aibu kubwa sana.

  Tabia hii inatokana na mifano wanayoiona kutoka kwa wazazi wao au watu wengine. Si ajabu kumsikia mzazi akimtuma mwanawe akamununulie pakiti ya sigara au kopo la tumbako.Wazazi kama hao huwafanya watoto wavute sigara ili nao wajione kama ni watu wazima.

  Sababu nyingine ya kuvuta sigara ni kutaka kujionyesha ati wana nakidi na kwao, au umaarufu. Hivyo basi sigara hazifai kupatiwa matangazo yenye kuvutia kwa vijana.

  Aina nyingine ya uaraibuni uvutaji bangi. Bangi ni aina ya mimea fulani unaolevya na kupumbuza akili yanapotafunwa au kuvutwa. Wavuta bangi kwa hakika hupatwa na baa nyingi mwilini. Hukonda na huvaringika akili usijue wanalofanya. Wataalamu husema bangi ikiingia akilini, huharibu kitivo cha fikira mpaka mtu huwa kama mwenda wazimu.

  Ni muhimu wazazi na walimu wa wakataze na wawakanye watoto wasishiriki katika tabia hizi mbaya.  MASWALI
  1.  Ipe taaarifa uliyosoma kichwa mwafaka. (al 1)
  2. Taja madhara ya sigara katika afya zetu. (ala 2)
  3. Sababu zipi hufanya watu kuvuta sigara? (ala 2)
  4. Taja jukumu la wazazi na walimu dhidi ya uvutaji sigara.(ala 1)
  5. Hasara gani zinazopatikana katika mazingira yetu kutokana na uvutaji sigara (al 2)
  6. Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari hii (ala 3)
   1. Uraibu
   2. Nakidi
   3. Bwiwa
 3. LUGHA
  1. .
   1. Taja mifano ya nusu-irabu (ala 2)
   2. Kwanini huitwa nusu-irabu
  2. Toa majukumu manne ya kiimbo (ala 2)
  3. .
   1. Mofimu ni nini? (al 1)
   2. Bainisha matumizi ya mofimu katika neno hili:
    hajanifurahisha (al 3)
  4. Yakinisha sentensi hii (al 1)
   Sijawahi kumsalimia wala kumkaribia
  5. Pambanua sentensi hii kwa njia ya mistari. (al 2)
   Mama alinijia shuleni na kunipa uji mtamu.
  6. Andika sentensi hii katika udogo- wingi (ala 2)
   Ng’ombe huyu ana pembe ndefu kuliko swara.
  7. Andika sentensi hii kwa wingi ( ala 2)
   Ua wake una ua zuri na kubwa.
  8. Andika kinyume cha: (al 2)
   Siku ya kuhama mjini umefika.
  9. Tambua viwakilishi katika sentensi hizi
   1. uleni wake.(ala 1)
   2. Kingi ni kipi?(ala1)
  10. Tunga sentensi iliyo na kihisishi cha dharau (al 1)
  11. Tunga sentensi na vihisishi hivi (ala 1)
   1. hohehahe!
   2. Ebo!
  12. Eleza maana ya nahau zilizopigwa mistari (ala 2)
   1. Juma alimlilia ngoa mtoto wa watu
   2. Tangu mtoto apotee amekuwa kiguu na njia
 4. FASIHI SIMULIZI (ALA 5)
  1. Eleza maana ya maigizo (ala 2)
  2. Taja vipera vitatu vya maiigizo (al 3)
 5. ISIMU JAMII
  1. Eleza maana ya Isimujamii (ala 1)
  2. Sajili ni nini? (ala 1)

MAJIBU

 1. INSHA
 2. UFAHAMU
  1. Ipe taaarifa uliyosoma kichwa mwafaka. (al 1)
   Uvutaji sigara
  2. Taja madhara ya sigara katika afya zetu. (ala 2)
   -Huunguza na kutobo amapafu
   -Husababisha saratani ya mapafu
   -Hupata maradhi ya pumu
   -Kufa kwa ugonjwa wa ghafla.
  3. Sababu zipi hufanya watu kuvuta sigara. (ala 2)
   - Kujiona wana nakidi ya pesa
   - Watoto huiga mifano ya wazazi wao.
   - Hutokana na matangazo ya kuvutia
  4. Taja jukumu la wazazi na walimu dhidi ya uvutaji sigara wa vijana (ala 1)
   - Wazazi na walimu wa wakanye vijana kuvuta sigara
  5. Hasara gani zinazopatikana katika mazingira yetu kutokana na uvutaji sigara (al 2)
   - Misitu huchomeka, nyumba na nguo
  6. Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari hii (ala 3)
   1. Uraibu- uzoefu, kupenda sana
   2. Nakidi- pesa taslimu
   3. Bwiwa- bugia, mumunya
 3. LUGHA.
  1. .
   1. Taja mifano ya nusu-irabu (ala 2)
    /Y/ na /W/
   2. Kwanini huitwa nusu-irabu
    - Huitwa nusu irabu kwa kuwa zinatamkika kwa urahisi na muundoni (W- ua) (y ia)
  2. Toa majukumu manne ya kiimbo (ala 2)
   - Huulizia swali- Unanijua?
   - Huwa kauli – Unanijua
   - Mshangao - Unanijua!
   - Hutoa amri- Toka
  3. .
   1. Mofimu ni nini? (al 1)
    - ni kipashio/ sehemu ndogo zaidi ya lugha yenye maana
   2. Bainisha matumizi ya mofimu katika neno hili.
    hajanifurahisha (al 3)
    -Ha- kikanusho, ja – kikanushi cha – me,- ni – kirejeshi cha mtendwa,furah- mzizi , ish- kutendesha, a –kiishio.
  4. Yakinisha sentensi hii (al 1)
   -Sijawahi kumsalimia wala kumkaribia
   -Nimewahi kumsalimia na kumkaribia
  5. Pambanua sentensi hii kwa njia ya mistari. (al 2)
   Mama alinijia shuleni na kunipa uji mtamu.
   N + T + E + N + T + N + V
  6. Andika sentensi hii katika udogo- wingi (ala 2)
   Ng’ombe huyu anapembe ndefu kuliko swara.
   Vigombe hivi vina vipembe virefu kuliko viswara
  7. Andika sentensi hii kwa wingi ( ala 2)
   Ua wake una ua zuri na kubwa.
   - Nyua zake zina maua mazuri na makubwa
  8. Andika kinyume cha: (al 2)
   Siku ya kuhama mjini umefika.
   - Siku ya kuhamia mjini imefika
  9. Tambua viwakilishi katika sentensi hizi
   1. ule ni wake.
    - Ule na wake, (ala 1)
   2. Kingi ni upi?
    - kingi na kipi (ala1)
  10. Tunga sentensi iliyo na kihisishi cha dharau (al 1)
   - Mwalimu ahakiki kazi ya mwanafunzi ebu! Ng’ou, Ny’oo, Potea! Po!
  11. Tunga sentensi na vihisishi hivi (ala 1)
   1. hohehahe!
    (Ovyoovyo)
   2. Ebo! - (dharau)
  12. Eleza maana ya nahau zilizopigwa mistari (ala 2)
   1. Juma alimlilia ngoa mtoto wa watu
    Litangoa – onea wivu
   2. Tangu mtoto apotee amekuwa kiguu na njia
    Anatembea tu hatulii
 4. FASIHI SIMULIZI (ALA 5)
  1. Eleza maana ya maigizo (ala 2)
   Maigizo- ni utanzu wa fasihi simulizi unaohusu kuigiza vitendo vya watu wengine na nia ya kufurahisha hadhira.
  2. Taja vipera vitatu vya maiigizo (al 3)
   - Vipera vya maigizo;
   1. mchezo jukwaani
   2. Vichekesho
   3. Majigambo
   4. michezo ya watoto
 5. ISIMU JAMII
  1. Eleza maana ya Isimujamii (ala 1)
   - Ni sayansi inayochunguza uhusiano uliopo kati ya lughana jamii.
  2. Sajili ni nini? (ala 1)
   - Ni matumizi ya lugha katika muktadha Fulani.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 End Term 3 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest