Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 1 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp
 1. UFAHAMU (Alama10)
  Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
  Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa msururu wa migomo na maandamano ya raia. Fujo za karibuni kabisa ni zile zinazoshuhudiwa katika miji mikubwa za wachuuzi na wafanyibiashara wakipinga hatua za serikali za kaunti kuwatoza ushuru takribani kwa kila huduma na bidhaa ikiwemo wanyama, kuku na ndege. La kuhuzunisha zaidi katika baadhi ya majimbo imeripotiwa kuwa raia wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti.

  Wanasiasa wameonekana kuwa na wakati mgumu kutetea mfumo huu mpya wa ugatuzi huku baadhi wakisema kwamba matatizo yanayoshuhudiwa kwa sasa yametokana na ugeni wa mfumo huo. Wengine wameinyoshea kidole serikali ya kitaifa kwamba ndiyo inayosambaratisha muundo huu. Wengine wanahoji kuwa bado ni mapema na kwamba kunahitajika muda mrefu ili kufaulu.

  Ni wazi kwamba kumekosekana nidhamu bora ya kusimamia maisha ya raia nchini Kenya. Matatizo yanayokumba raia kwa sasa ni dalili kuwa mfumo wa serikali ya ugatuzi umeongezea chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu. Swali ni je, hadi lini nidhamu ya kusimamia raia itakuwa ni suala la majaribio na makosa?

  Hatua ya kuwarundikizia raia ushuru mkubwa ni kitendo cha unyonyaji na cha dhuluma kinachofaa kupingwa. La kufahamishiwa hapa ni kwamba ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serikali zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi wa kibepari ikiwemo Kenya. Asilimia 90 ya mapato ya serikali za kibepari huegemea ushuru. Kwa hivyo hatua ya serikali za kaunti katika kuwanyonya raia kwa kuwalipisha ushuru si ajabu bali ni thibitisho kuwa jamii ya Kenya inaongozwa na nidhamu ya kiuchumi ya ubepari mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji. Ukweli unabakia kuwa ndani ya serikali za kibepari raia ndio hubebeshwa mzigo wa ushuru unaoishia matumboni mwa viongozi!

  Miito ya mabadiliko ya katiba na ya miundo mipya ya kiutawala si lolote ila ni moja tu ya hatua za mfumo wa kibepari kujipa muda wakuishi na kuziba aibu zake za kushindwa kusimamia maisha ya watu. Kufeli huku kwa mfumo huu kunashuhudiwa hadi kwenye nchi kubwa za kibepari kama Marekani na Uingereza hivyo nazo zimekumbwa tele na maandamano na fujo za raia wakilalamikia hali ngumu ya maisha.

  Maswali
  1. Yape makala haya anwani mwafaka. (alama 1)
  2. Eleza mtazamo wa wanasiasa kuhusu utepetevu wa mfumo huu. (alama 3)
  3. Migomo ni zao la matatizo yaliyogatuliwa kutoka kuu. Toa sababu nyingine zinazosababisha migomo katika serikali za ugatuzi (alama 3)
  4. Thibitisha jinsi mfumo wa ugatuzi umeongeza chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu (alama 2)
  5. Eleza maana ya neno lifuatalo (alama 1)
   Ugatuzi
 2. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Tofautisha kati ya mofimu huru na mofimu funge. (Alama 2)
  2. Ainisha mofimu hizi. (Alama 2)
   1. Mende
   2. Mpwa
  3. Ainisha viambishi katika neno lifuatalo. (Alama 2)
   Anayemtembelea
  4. Tunga sentensi moja ili kutofautisha maana. (Alama 2)
   1. Baba
   2. Papa
  5. Tumia neno safi kama nomino kutungia sentensi. (Alam 2)
  6. Tumia kivumishi kiashiria cha mbali kidogo pamoja na ngeli ya I- ZI katika sentensi sahihi. (Alama 2)
  7. Kanusha katika ukubwa wingi. (Alama 2)
   Mtoto alikuwa amelia.

   ISIMU JAMII
  8. Taja sifa tano za sajili ya hotelini. (Alama 5)


Marking Scheme

 1. UFAHAMU
  1. Changamoto za Ugatuzi/Matatizo ya ugatuzi/Ugatuzi( alama 1x1 = 01)
  2.  
   • Ugatuzi ni mfumo geni (Alama 3x1=03)
   • Serikali kuu kutowajibika
   • Kudai kuwa mfumo huu unahitaji mda zaidi
  3.  
   • Hali mbaya ya muundo msingi (alama 3x1= 03)
   • Viongozi kuenda za ufisadi
   • Ukosefu wa usawa katika ugavi wa rasilimali
   • Viongozi kupuuza mchango wa wananchi
  4.  
   • Raia kulazimishwa kulipa ili kuona maiti za jamaa zao katika fuo (alama 2x1=02)
   • Raia kurundikiziwa mzigo wa kulipa ushuru mkubwa
   • Ushuruunaolipwanawananchihauwasaidiiwananchi la huishiamifukonimwaviongozi
  5.  
   • Ugavi wa mamlaka na raslimali kutoka serikali kuu hadi mashinani (alama 2x1 =02)
 2. MATUMIZI YA LUGHA
  1. Mofimu huru ni zile ambazo hubeba maana hata bila kuambatanishwa na viambishi vyovyote, ilihali mofimu funge ni zile hupatikana katika nomino, viwakilishi na vivumishi ( mofimu hizi hazimbatanishwi na viambishi vyovyote. (Alama 1X2 )
  2.  
   1. Mende – Mofimu huru
   2. Mpwa – Mofimu tegemezi. (Alama 2)
  3. A – Kiambishi cha ngeli pia nafsi ya tatu umoja
   na – Liambishi cha wakati uliopo
   ye – Kirejeshi
   m – Mtendwa
   tembe – Mzizi
   le – kauli
   a – kiishio
  4.  
   1. Baba
   2. Papa (Mwalimu akadirie kazi ya mwanafunzi)
  5. (Mwalimu akadirie kazi ya mwanafunzi)
  6. Majitoto hayakuwa yamelia.

   ISIMU JAMII
  7. Sifa za hotelini
   • Huwa na msamiati maalum kama vile; bei, chenji,chai, soda.
   • lugha inayotumika si sanifu
   • Kuna kuchanganya ndimi
   • Huwa na kauli fupi fupi
   • Lugha ya kushawishi huenda ikatumika

 


Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 1 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


Join our whatsapp group for latest updates
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

 • easyelimu app
 • Telegram
 • facebook page
 • twitter page
 • Pinterest