Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 1 Mid Term Exams

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KIDATO CHA PILI
MTIHANI WA KATI WA MUHULA
MUHULA WA KWANZA
SAA 2½

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote katika mtihani huu.

SEHEMU A
INSHA (ALAMA 20)

  1. Andika insha itakayomalizika kwa maneno haya: “……. siku hiyo nilirudi nyumbani nikiwa nimesikitika na kujawa na majonzi tele. Nilikuwa sijawahi kuona ajali mbaya kama hiyo”

SEHEMU B
UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.

Ukandaji

Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka dahari? Watu wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.

Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.

Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.

Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo mbalimbali mwilini.

Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa chembechembe za sumu mwilini.

Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo. Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi hayapendekezwi.

Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu. Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.

Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji. Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha mikononi.

Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana maradhi ya ngozi.

MASWALI

  1. Ukandaji ni nini? (alama 1)
  2. Eleza manufaa matatu ya ukandaji. (Alama 3)
  3. Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani? (alama 2)
  4. Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini? (alama 2)
  5. Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi. (alama 2)
  6. Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika: (5 alama)
  7. ufunguzi
  8. auni
  9. maradufu
  10. maji vuguvugu
  11. shinikizo la damu

SEHEMU C
UFUPISHO
Soma taarifa hii kasha ujibu maswali

Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe kumwadhibu kwa makosa aliyofanya bali iwe kumtibu na kujaribu kumrekebisha tabia yake ili awe raia mwema.

Zamani wahalifu waliadhibiwa kwa mujibu wa makosa waliyoyafanya. Mhalifu aliyefanya makosa madogo madogo alifungwa lakini mtu aliyeua naye aliuawa. Sasa wataalamu wanatuambia kuwa mhalifu akiadhibiwa anapokuwa kifunguno,basi akitoka hurejea tena kufanya uhalifu. Madhumuni ya kumtia jela iwe si kumwadhibu bali kumfunza tabia njema. Wanatuambia kuwa makosa afanyayo mhalifu yanatokana na matatizo ya jamii kwa jumla,nayo ni matatizo kama ya umaskini, msongamano wa watu,kosa afanyalo mhalifu si kosa lake pekee bali ni kosa la jamii nzima.

Jitu lilizoea kuua halioni kitu kumpiga mtarimbo au rungu la kichwa na kumyang’anya kila alicho nacho. Siku hizi,jitu kama hili baadhi ya wataalamu husema lisiuawe lifungwe maisha tu. Lakini ‘kifungo cha maisha’ ni kama tunavyokijua. Muuaji hufungwa pengine miaka kumi tu kisha husamehewa muda uliobaki. Hapo tena huwa huru ama kuifichua mali aliyoiiba na kuistarehea raha mustarehe au kurejea tena kufanya uhalifu.

Haya ni kinyume kabisa na mambo yaliyokuwa zamani. Aliyeua aliuawa kwa hivyo watu waliogopa kuua. Raia na pia askari waliokuwa wakiwasaka wahalifu walinusurika vifo kwani wahalifu wengine walichukua silaha za hatari kama bastola na bunduki.

Sasa wale wahalifu wabaya sana – mijizi, minyang’anyi na wauaji ndio wanaotukuzwa. Magazeti huwashawishi makatili hawa na kuwapa mapesa chungu nzima waeleze maisha yao ya kikatili. Magazeti haya sasa ndiyo yanayopata wasomaji wengi. Pia wachapishaji vitabu vya hadithi zinazohusikia na uhalifu, biashara zao zinazidi kustawi. Kadhalika sinema zinazoonyesha picha za ukatili; wizi na mauji hujaa watazamaji wanaoshangilia uhalifu ufanywao.

Wahalifu kwa upande mmoja wanatukuzwa na masinema vitabu na magazeti na kwa upande mwingine “haki” zao zinapiganiwa na baadhi ya wataalamu. Watu wanaowalaani wahalifu ni wale waliohasirika tu na kuteswa na wahalifu . Baadhi yao hata kulaani hawawezi kwa sababu wameshauawa,hawana tena kauli.

MASWALI

  1. Fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu kwa maneno 50.
    Matayarisha
    Nakala safi (alama 6/mtiririko 2)
  2. Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno kati ya 45-50
    Matayarisho
    Nakala safi (alama 6/Mtiririko 1)

SEHEMU D
MATUMIZI YA LUGHA: (ALAMA 40)

  1. Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /d/ (ala 1)
  2. Eleza tofauti kati ya:
    1. Mofimu huru
    2. Mofimu tegemezi (ala 2)
  3. Ainisha viambishi katika sentensi hii.
    1. Mlipewa (ala 2)
  4. Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii.
    1. Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa. (ala 2)
  5. Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo
    1. Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika.
    2. Wageni watatumbuizwa na bengi ya kayamba Afrika.
  6. Bainisha vitenzi halisi kwa kuvipigia mstari
    1. Nyanchama hakufika mkutanoni
    2. Horukut amerudi kutoka masoni (ala 2)
  7. Eleza maana ya misemo ifuatayo.
    1. kupiga domo
    2. kupiga kijembe (ala 2)
  8. Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya.
    1. shuka
    2. suka (ala 2)
    3. Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo.
  9.      
    1. Anayetaka chakula kitamu ni nani?
    2. Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio. (ala 2)
  10. Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi
    Mtoto mbaya aliadhibiwa (ala 1)
  11. Yakinisha sentensi ifuatayo katika umoja.
    Nyuzi zisingekatika zisingepotea (ala 2)
  12. Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.
    1. Nafsi viambata
    2. Visisitizi
  13. Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti.
    Ritifaa (ala 4)
  14. Andika katika udogo na wingi
    Njusi aliyekuwa na jicho moja alianguka mtoni (ala 2)
  15. Taja visawe vya maneno yafuatayo.
    1. Damu
    2. Mjinga
  16. Andika sentensi hii katika ukubwa
    1. Huyo nyoka alikatwa mkia na mvulana yule (ala 2)
  17. Tumia kitenzi jina na kivumishi kutunga sentensi (ala 2)
  18. Nyambua
    Filisisha (tenda) (ala 1)
  19. Sahihisha:
    Kwenye nilisomea ni bali (ala 1)
  20. Tumia herufi mwafaka kuainisha maneno katika sentensi hii.
    Ingawa anataka kucheza karata,ni mlevi (ala 3)

SEHEMU E.
ISIMU – JAMII
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa.
                 Mtakula nini?
Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali. Fanya haraka.
Mteja 2: Mhudumu,hebu leta madodo na chemsha mbili. Pia niletee maji ya machungwa.
Mhudumu: Sawa. Baada ya dakika moja utapata yote uliyoagiza.
Mteja 1: (Akila) Wewe-Please bring me drinking water. Yawe baridi tafadhali.
Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani. Glasi ndio hii pia,karibu.
Mteja 2: Nina haraka mzee. Wapi tooth pick?
Mhudumu: Hizo hapo ,mezani karibu na maji.
Mteja 1: (Akiita) Mhudumu,naomba uniletee ugali saucer tafadhali.
Mhudumu: Naam.
Mteja 2: (Akisimama) Nimeshiba. Hizi hapa pesa
             Niletee change haraka niondoke.

MASWALI

  1. Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya? (ala 2)
  2. Taja sifa zozote tano za sajili hii (ala 5)
  3. Dondoa msamiati unaotambulisha sajili hii (ala 3)

MAAKIZO

SEHEMU A
INSHA (ALAMA 20)

  1. Andika insha itakayomalizika kwa maneno haya: “……. siku hiyo nilirudi nyumbani nikiwa nimesikitika na kujawa na majonzi tele. Nilikuwa sijawahi kuona ajali mbaya kama hiyo”
    • Mdokezo aliopewa na anjaribu kuwaza na kuona utaingiliana na hadithi ya aina gani,kwani mdokezo huo ndio kiini cha inshaAtumie lugha fasaha ambayo inamvutia msomaji wa insha yake.
    • Azingatie kanuni zote za uandishi wa insha kama alama za uwakifishi,sarufi bora,upangaji mzuri wa aya n.k.
    • Asiyehitimisha kwa hilo dondoo atukuwa amejitungia swali.
    • Atakayeongezea maneno yasiyozidi matano ataondolewa maki (02 kimalizio)

SEHEMU B
UFAHAMU (ALAMA 15)
Soma taarifa hii kisha ujibu maswali ifuatayo.

Ukandaji

Je,unajua kuwa ukandaji wa mwili umetumika kama njia mojawapo ya matibabu toka dahari? Watu wanaofahamika kutumia ukandaji kimatibabu toka jadi ni Wahindi,Wachina,Wagiriki,Warumi na Waafrika.

Ukandaji unajulikana kuwa na manufaa makubwa kimatibabu. Mathalani,ukandaji hufungua vitundu vya ngozi. Ufunguzi huu huondoa sumu mwilini kupitia kwa utoaji jasho. Pili,ukandaji hupunguza mkazo wa misuli. Misuli ikiwa na mkazo zaidi kwa muda mrefu huleta urundikaji wa asidi. Ukandaji huondoa asidi hii,huufanya mwili kuwa mlegevu,humletea mtu uchangamfu na kuondoa uchovu.

Halikadhalika,ukandaji huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi. Hali hii huhakikisha kuwa virutubishi vya mwili huweza kufikia viungo vyote vya mwili. Hili nalo huchangia kuzidisha uwezo wa mwili kujikinga na maradhi. Hewa safi ya oksijeni huweza pia kusambaa kote mwilini kupitia kwa uimarishaji wa mzunguko wa damu. Aidha,ukandaji wa taratibu na polepole hupunguza mkazo wa neva na kuziliwaza ukandaji wa kasi huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wake.

Ukandaji unaweza kufanyiwa kiungo chochote mwili ni. Ukandaji huu huweza kuwa na matokeo mbalimbali mwilini.

Mathalani,ukandaji wa njia ya chakula mwilini,hasa tumbo na utumbo,huimarisha usagaji wa chakula na kuchangia uondoaji wa uchafu na sumu mwilini. Nao ukandaji wa njia ya mkonjo hustawisha uondoaji wa chembechembe za sumu mwilini.

Kwa kawaida,viganja vya mikono hutumika katika ukandaji. Viungo hivi vinapaswa kuwa na wororo. Wororo huu hupatikana kwa kutumia mafuta. Mafuta ambayo ni bora zaidi kwa shughuli za ukandaji ni ya ufuta au simsim. Matumizi ya kitu chochote kama ungaunga kinachoweza kuziba vitundu vya ngozi hayapendekezwi.

Ukandaji wapaswa kutekelezwa kwa njia ifuatayo. Mtu aanzie mikono na miguu. Kisha aingie kukanda kifua,tumbo,mgongo na makalio. Hatimaye,akande uso na kichwa. Mtu anaweza kutumia kitambaa kukandia mgongo. Ni bora kutumia viganja vya mikono kukandia. Kwa njia hii,manufaa huwa maradufu. Kwanza,tutanufaika na ukandaji na wakati huo huo tutakuwa tukifanya mazoezi ya viungo. Wasioweza kujikanda,wanaweza kuomba msaada. Ni muhimu ukandaji ufuatiwe na kuoga kwa maji vuguvugu.

Kwa walio na tatizo la shinikizo au mpumuko wa damu wanaweza kubadilisha utaratibu wa ukandaji. Waanzie kichwani,kisha waelekee usoni,kifuani,tumboni,mgongoni,makalioni,miguuni na kuhitimisha mikononi.

Hata hivyo,ukandaji haupaswi kufanywa wakati mtu anaugua maradhi yoyote. Wanawake wajawazito nao wanatakiwa kuepuka ukandaji wa tumbo. Halikadhalika,ukandaji wa tumbo hauruhusiwi wakati mtu anaendesha,ana vidonda vya tumbo au uvimbe tumboni. Hatimaye,ukandaji haupendekezwi iwapo mtu ana maradhi ya ngozi.

MASWALI

  1. Ukandaji ni nini? (alama 1)
    • Ni shughuli ya kusugua na kubinyabinya viungo vya mwili kwa mikono au mashine.

  2. Eleza manufaa matatu ya ukandaji. (Alama 3)
    • Hufungua vitundu vya ngozi,jambo ambalo husaidia kuondoa sumu mwilini kupitia kwa utokaji jasho.
    • Kupunguza mikazo ya misuli. Mikazo ya misuli mwilini kwa muda mrefu huleta ulundikaji wa asidi mwilini; jambo ambalo ni hatari.
    • Huimarisha mzunguko wa damu mwilini kwa wepesi.
    • Hii hurahisisha virutubishi vya mwili kufika sehemu zote mwilini
    • Huondoa uchovu na kuleta uchangamfu mwilini.
    • Ukandaji huchangamsha neva na kuimarisha utendaji kazi wa neva hizo. (hoja zozote tatu,kila moja alama 1)

  3. Ukandaji unatakiwa kutekelezwa kwa njia gani? (alama 2)
    • Ukandaji unatakiwa kufanywa kwa kutumia mafuta,hasa ya ufuta au simsim kisha mtu aanzie mikononi na miguuni,aingie kifuani,tumboni,mgongoni na makalioni.  Hatimaye,aingie usoni na kumalizia kichwani,iwapo anayehusika ana tatizo la shinikizo la damu,utaratibu auazie kichwani kisha aelekee usoni,kifuani,tumboni na kumalizia mgongoni. (alama 2 iwapo utaratibu mmojawapo umekamilishwa)

  4. Ukandaji unatakiwa kutekelezwa na nani na kwa nini? (alama 2)
    • Unatakiwa kufanywa na mtu mwenyewe.  Hii ni kwa kuwa atakuwa akijikanda vizuri na pia atakuwa akifanya mazoezi ya kunyoosha viungo.

  5. Onyesha ni lini ukandaji haupendekezwi. (alama 2)
    • Wakati mtu anaugua maradhi yoyote.
    • wakati mwanamke ni mjamzito
    • wakati mtu anaendesha,asikande tumbo au akiwa na vidonda vya tumbo
    • wakati mtu ana maradhi yoyote ya ngozi(hoja zozote 2,kila hoja alama 1)

  6. Eleza maneno yafuatayo kama yalivyotumika: (5 alama)
    1. ufunguzi - kufungua
    2. auni - kusaidia,msaada
    3. maradufu - Mara  mbili
    4. maji vuguvugu - Maji yasiyo baridi wala moto sana
    5. shinikizo la damu - Mpumuko wa damu au moyo kupiga sana kwa kasi isiyokuwa ya kawaida

SEHEMU C
UFUPISHO
Soma taarifa hii kasha ujibu maswali

Kuna wataalamu siku hizi wanaosema kuwa jela si pahala pa adhabu bali pa matibabu. Yaani madhumuni ya kumtia mhalifu jela isiwe kumwadhibu kwa makosa aliyofanya bali iwe kumtibu na kujaribu kumrekebisha tabia yake ili awe raia mwema.

Zamani wahalifu waliadhibiwa kwa mujibu wa makosa waliyoyafanya. Mhalifu aliyefanya makosa madogo madogo alifungwa lakini mtu aliyeua naye aliuawa. Sasa wataalamu wanatuambia kuwa mhalifu akiadhibiwa anapokuwa kifunguno,basi akitoka hurejea tena kufanya uhalifu. Madhumuni ya kumtia jela iwe si kumwadhibu bali kumfunza tabia njema. Wanatuambia kuwa makosa afanyayo mhalifu yanatokana na matatizo ya jamii kwa jumla,nayo ni matatizo kama ya umaskini, msongamano wa watu,kosa afanyalo mhalifu si kosa lake pekee bali ni kosa la jamii nzima.

Jitu lilizoea kuua halioni kitu kumpiga mtarimbo au rungu la kichwa na kumyang’anya kila alicho nacho. Siku hizi,jitu kama hili baadhi ya wataalamu husema lisiuawe lifungwe maisha tu. Lakini ‘kifungo cha maisha’ ni kama tunavyokijua. Muuaji hufungwa pengine miaka kumi tu kisha husamehewa muda uliobaki. Hapo tena huwa huru ama kuifichua mali aliyoiiba na kuistarehea raha mustarehe au kurejea tena kufanya uhalifu.

Haya ni kinyume kabisa na mambo yaliyokuwa zamani. Aliyeua aliuawa kwa hivyo watu waliogopa kuua. Raia na pia askari waliokuwa wakiwasaka wahalifu walinusurika vifo kwani wahalifu wengine walichukua silaha za hatari kama bastola na bunduki.

Sasa wale wahalifu wabaya sana – mijizi, minyang’anyi na wauaji ndio wanaotukuzwa. Magazeti huwashawishi makatili hawa na kuwapa mapesa chungu nzima waeleze maisha yao ya kikatili. Magazeti haya sasa ndiyo yanayopata wasomaji wengi. Pia wachapishaji vitabu vya hadithi zinazohusikia na uhalifu, biashara zao zinazidi kustawi. Kadhalika sinema zinazoonyesha picha za ukatili; wizi na mauji hujaa watazamaji wanaoshangilia uhalifu ufanywao.

Wahalifu kwa upande mmoja wanatukuzwa na masinema vitabu na magazeti na kwa upande mwingine “haki” zao zinapiganiwa na baadhi ya wataalamu. Watu wanaowalaani wahalifu ni wale waliohasirika tu na kuteswa na wahalifu . Baadhi yao hata kulaani hawawezi kwa sababu wameshauawa,hawana tena kauli.

MASWALI

  1. Fupisha aya ya kwanza hadi ya tatu kwa maneno 50.
    Matayarisha
    Nakala safi (alama 6/mtiririko 2)
    • Jela si mahali pa adhabu bali pa matibabu
    • zamani wahalifu waliadhibiwa kwa makosa waliyofanya
    • Sasa wataalamu wasema aliyeadhibiwa
    • Kifungoni,akitoka hurejea tena kufanya uhalifu
    • Madhumuni ya kuvutia jela iwe si kumwadhibu bali kumfunza tabia njema
    • Makosa afanyayo mhalifu yanatokana na matatizo ya jamii
    • Kosa afanyalo mhalifu si kosa lake pekee bali ni kosa la jamii

  2. Fupisha aya mbili za mwisho kwa maneno kati ya 45-50
    Matayarisho
    Nakala safi (alama 6/Mtiririko 1)
    • Sasa wale wahalifu wabaya sana ndio wanaotukuzwa
    • Magazeti huwashawishi makatili na kuwapa pesa waeleze maisha yao
    • Magazeti haya yanapata wasomaji wengi
    • Wachapishaji vitatu vya hadithi za uhalifu,biashara zao zinastawi.
    • Sinema zinazoonyesha uhalifu hujaa watazamaji
    • Wahalifu kwa upande mmoja wanatukuzwa na upande mwingine haki zao kupiganiwa
    • Wahalifu wanalaaniwa na waliohasirika na kuteswa
    • Wengine hawawezi kulaani kwa sababu wameuawa

SEHEMU D
MATUMIZI YA LUGHA: (ALAMA 40)

  1. Eleza tofauti kati ya sauti /z/ na /d/ (ala 1)
    • /z/ - kikwamizo
    • /d/ kipasuo

  2. Eleza tofauti kati ya:
    1. Mofimu huru - ni zile ambazo hubeba maana hata bila kuambatanishwa na viambishi vyovyote.
    2. Mofimu tegemezi (ala 2) - ni zile ambazo haziwezi kujisimamia

  3. Ainisha viambishi katika sentensi hii.
    1. Mlipewa (ala 2)
      • M – kiambishi awali cha nafsi(pili – umoja)
      • li – kambishi awali cha wakati uliopita
      • p – mzizi
      • ew – kiishio

  4. Onyesha kundi nomino na kundi tenzi katika sentensi hii.
    1. Nyayo za wanyama hao zimeonekana hapa. (ala 2)
       KN                                 KT

  5. Onyesha nomino za jamii katika sentensi zifuatazo
    1. Chuki baina ya jamii lazima ikomeshwe barani Afrika.
      • jamii

    2. Wageni watatumbuizwa na bendi ya kayamba Afrika.
      • bendi ya kayamba afrika

  6. Bainisha vitenzi halisi kwa kuvipigia mstari
    1. Nyanchama hakufika mkutanoni
      • Hakufika

    2. Horukut amerudi kutoka masoni (ala 2)
      • Amerudi

  7. Eleza maana ya misemo ifuatayo.
    1. kupiga domo
      kuzungumza kupitisha wakati

    2. kupiga kijembe (ala 2)
      Kusema kwa mafumbo

  8. Tunga sentensi mbili kuonyesha tofauti kati ya maneno haya.
    1. shuka - enda chini kutoka juu ya kitu/pungua thamani
    2. suka (ala 2) - kutengeneza nywele/Tikisa kitu

  9. Onyesha vivumishi vya sifa katika sentensi zifuatazo.     
    1. Anayetaka chakula kitamu ni nani?
      kitamu

    2. Kiatu kirefu kimeng’oka kikanyagio. (ala 2)
      kirefu

  10. Geuza neno lililopigwa mstari kuwa kiwakilishi
    Mtoto mbaya aliadhibiwa (ala 1)
    Mbaya aliadhibiwa

  11. Yakinisha sentensi ifuatayo katika umoja.
    Nyuzi zisingekatika zisingepotea (ala 2)
    • Uzi usingekatika usingepotea
  12. Tunga sentensi ukitumia viwakilishi vifuatavyo.
    1. Nafsi viambata - Alicheza
    2. Visisitizi - Yuyu huyu ametuzwa.

  13. Tumia kiwakifishi kifuatacho kubainisha matumizi yake katika sentensi ili kutoa maana mbili tofauti.
    Ritifaa (ala 4)
    • Hutumiwa kuonyesha tarakimu imeachwa. Mf 19’
    • kuandika sauti za ving’ong’o mf ng’ombe, ng’ara
    • kupunguza mizani katika ushairi mf n’shafika

  14. Andika katika udogo na wingi
    Njusi aliyekuwa na jicho moja alianguka mtoni (ala 2)
    • Vijijusi/vijusi vilivyokuwa na vijisho vilianguka vijitoni
  15. Taja visawe vya maneno yafuatayo.
    1. Damu - Ngeu
    2. Mjinga - mpumbavu,zuzu,baradhuli,renge,bunga

  16. Andika sentensi hii katika ukubwa
    1. Huyo nyoka alikatwa mkia na mvulana yule (ala 2)
      • Hilo joka lilikatwa jikia/kia na vulana /jivulana lile
  17. Tumia kitenzi jina na kivumishi kutunga sentensi (ala 2)
    • Mf wa sentensi:Kuimba kwetu kuliwavutia
  18. Nyambua
    Filisisha (tenda) (ala 1)
    • filisi

  19. Sahihisha:
    Kwenye nilisomea ni bali (ala 1)
    • Nilikosomea ni mbali

  20. Tumia herufi mwafaka kuainisha maneno katika sentensi hii.
    Ingawa anataka kucheza karata,ni mlevi (ala 3)
    • Ingawa anataka kucheza karata ni mlevi

SEHEMU E.
ISIMU – JAMII
Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Mhudumu: Mnakaribishwa. Menyu hii hapa.
                 Mtakula nini?
Mteja 1: Naomba uniletee mix na ugali. Fanya haraka.
Mteja 2: Mhudumu,hebu leta madodo na chemsha mbili. Pia niletee maji ya machungwa.
Mhudumu: Sawa. Baada ya dakika moja utapata yote uliyoagiza.
Mteja 1: (Akila) Wewe-Please bring me drinking water. Yawe baridi tafadhali.
Mhudumu: Ndiyo haya hapa mezani. Glasi ndio hii pia,karibu.
Mteja 2: Nina haraka mzee. Wapi tooth pick?
Mhudumu: Hizo hapo ,mezani karibu na maji.
Mteja 1: (Akiita) Mhudumu,naomba uniletee ugali saucer tafadhali.
Mhudumu: Naam.
Mteja 2: (Akisimama) Nimeshiba. Hizi hapa pesa
             Niletee change haraka niondoke.

MASWALI

  1. Ni sajili gani inayohusishwa katika mazungumzo haya? (ala 2)
    • Sajili ya hotelini

  2. Taja sifa zozote tano za sajili hii (ala 5)
    • Matumizi ya lugha ya ucheshi na utani
    • Matumizi ya lugha sio lazima yazingatie kanuni za lugha sanifu ama ile isiyofuata kaida za lugha
    • Matumizi ya msamiati maalumu
    • Lugha ya hotelini inaweza kuchanganya ndimi
    • Ni lugha shawishi na rahishi kueleweka
    • Wakati mwingine kuna matumizi ya chuku
    • Ni lugha ya kupumbaza na kufurahisha kwa kuwa inanuiwa kuvutia.

  3. Dondoa msamiati unaotambulisha sajili hii (ala 3)
    • menyu
    • Mix na ugali
    • Madodo na chemsha mbili
    • Tooth pick 
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 1 Mid Term Exams.

Tap Here to Download for 50/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students

Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest