Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 2 Opener Exams 2021

Share via Whatsapp

KISWAHILI
KIDATO CHA PILI
MTIHANI WA MWANZO WA MUHULA
MUHULA WA PILI

MAAGIZO

  • Jibu maswali yote

 

  1. INSHA – ALAMA 20
    “Wewe ni mwalimu mkuu wa shule yako. Andika hotuba utakayoitoa siku ya wazazi shuleni mwako.”

  2. UFAHAMU
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali uliyoulizwa. (ala 15)

    Mateso ya wanawakiwa ni suala la kijamii linalofaa kutazamwa kwa darubini kali. Hata hivyo wanoathirika zaidi ni watoto ambao bado wako katika umri unaohitaji kulelewa na kupewa mahitaji ya msingi kama mavazi, malazi, elimu na mengine anuwai. Hali ya kuachwa na wazazi imekuwa ikizikumba jamii tangu enzi za mababu na kila itokeapo, wanajamii huipokea kwa mitazamo tofautitofauti, hivyo kuwafanya wanawakiwa kuathirika sana.

    Baadhi ya jamii zina imani za kijadi pamwe na mila zilizochakaa zinazozifanya kuamini kuwa baadhi ya vifo hutokana na laana. Wengine huchukulia kuwa mwendazake ameondolewa na ulogi. Imani kama hizi huifanya jamii kuwatia watoto waliochwa katika mkumbo ule ule, hivyo kuwaangalia kwa macho yasiyo ya kawaida. Hii husababisha dhana gande. Hali hii husababisha kuwachukulia watoto kama wanaotoka katika kizazi kilicholaaniwa. Jamii basi hukosa kuwapa watoto hawa stahiki yao. Hata wanapojitahidi kuiwania nafasi yao, waliowazunguka huwavunja mioyo. Jitihada zao huishia kuwa si chochote kwa kuwa jamii inawatazama kama waliolaaniwa.

    Punde baada ya mzazi mmoja au wote wawili waendapo wasikorudi, inatarajiwa kwamba aliyeachiwa mtoto awe mzazi wake, mwanafamilia au jirani awajibike na kumtunza mwanamkiwa. Kunao kadha wa kadha wanaowajibika – nina wavulia kofia. Hata hivyo wengi hutelekeza jukumu hii walilopewa na Muumba. Si ajabu basi kuona kuwa idadi ya watoto wanaozurura mitaani inazidi kuongezeka kila uchao. Ukichunguza utakuta kuwa wengi wa watoto hawa ni waliopotelewa na wazazi wao. Inakera zaidi kugundua kuwa baadhi ya watoto hawa wana mzazi mmoja. Kwamba mke au mume wa mtu ameaga, au iwe kwamba mzazi mmoja alimza mtoto na kumwachia mwenzake mzigo wa ulezi, aliyeachiwa na jukumu la kumpa mwanawe mahitaji ya msingi. Machoni pa jalali, kila anayeupuuza wajibu huu ana hukumu yake siku ya kiama!

    Ni haki ya kila mtoto kupata elimu. Katika katiba ya Kenya mathalan, elimu ya msingi, yaani kuanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne ni ya lazima. Tangu hapo hata hivyo, jamii zimekuwa zikiwanyima wanawakiwa wengi elimu. Kwamba kunao wachache wanaowaelimisha baadhi ya wanawakiwa ni kweli. Hata hivyo, wengine hukosa hata wa kuwapeleka katika shule ya chekechea, hivyo kuishia kutojua hata kuandika majina yao. Mfikirie mtu katika karne ya 21 asiyejua kusoma wala kuandika! Nani ajuaye, huenda huyo mwanamkiwa asiyepelekwa shuleni ndiye angalikuwa profesa, daktari, mwalimu, rubani au msomi mtajika na mtaalamu wa uwanja muhimu katika jamii!

    Kila mtoto ana haki ya kulelewa hadi kufikia utu uzima kabla ya kupewa majukumu mazito. Katika katiba ya Kenya, utu uzima, ulio umri wa kuanza kufanya kazi huanzia miaka 18. Wanaohakikisha watoto hawa wametimiza utu uzima kabla ya kufanyizwa gange ngumu wanafaa pongezi. Hata hivyo wanawakiwa wamekuwa wakitumiwa na wengi kama punda wa huduma. Wanaaila wengine huwachukua wanawakiwa kwa machozi mengi wazazi wao waagapo na kuapa kuwahifadhi na kuwatunza wana wale wa ndugu zao, kumbe ni machozi ya simba kumlilia swara! Hata kabla ya mwili wa mzazi mhusika kuliwa na viwavi, mateso kwa mtoto yule huanza, akawa ndiye afanyaye kazi zote ngumu. Utakuta watoto wao wamekaa kama sultan bin jerehe huku mwanamkiwa yule akiwapikia, kuwafulia nguo, kudeki, karibu hata wa waoshe miili! Kazi kama zile za shokoa huwa za sulubu na aghalabu husindikizwa kwa matusi yasiyoandikika.

    Baadhi ya waja walionyimwa huruma huwahadaa wanawakiwa na kuwapeleka ng’ambo wakitumia vyambo, kuwa wakifika kule watapata kazi za kifahari. Maskini wale huishia kushikwa shokoa, wakawa watumwa katika nyumba za waajiri wao, bila namna ya kujinasua. Wengine huishia kutumiwa kama watumwa wa ‘Kimapenzi’ katika madanguro, miili yao ikawa ya kuuziwa makahaba waroho wasiojali utu. Kujinasua kule huwa sawa na kujitahidi kuokoa ukuni uliokwishageuka jivu, maadamu wanawakiwa aghalabu hukosa watu wenye mioyo ya huruma ya kuwashughulikia. Wengi huitumia methali ‘ mwana wa ndugu kirugu mjukuu mwanangwa’ kuwapuuzilia mbali wanawakiwa ambao hukimbiliwa tu wabinafsi hawa wanapofaidika wenyewe.

    Maswali

    1. Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka. (ala.1)
    2. Eleza dhana ya ‘Mwanamkiwa. (ala. 1)
    3. Ni kategoria gani ya wanawakiwa inayosumbuka sana? (ala. 2)
    4. Taja mambo mawili ambayo baadhi ya imani na mila za jadi huchukulia kuwa chanzo cha uanaukiwa. (ala.1)
    5. Eleza kwa kifupi hali ya elimu ya wanawakiwa. (ala.2)
    6. Taja mateso mawili ambayo wanawakiwa wanaoahidiwa kulepekwa ng’ambo hukumbana nayo. (ala.2)
    7. Eleza unafiki wa baadhi ya watu wa jamii ya wanawakiwa. (ala.3)
    8. Eleza maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika makala. (ala.3)
      1. Inakela
      2. Waja
      3. Kujinasua

  3. UFUPISHO
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali uliyoulizwa

    Wanawake wanaoishi katika maeneo ya mashambani katika nchi zinazoendelea ni baadhi ya watu waliotopea na kubobea kwenye umaskini mkubwa na wanaoathiriwa na matatizo kwa kiwango kikubwa ulimwenguni. Jumla ya idadi ya wanawake hawa wanaoishi chini ya kiwango cha chini cha umaskini inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 600. Hii ni idadi kubwa hasa ikikumbukwa kuwa ni asilimia kubwa ya wanawake wanaoishi kwenye maeneo haya.

    Ulimwengu umeshuhudia ongezeko la idadi ya watu au dadiwakazi; kuwako kwa matatizo ya kiuchumi ulimwenguni; mitafaruku na vita vya kikabila, majanga ya kiasilia kama mafuriko ya maji, ukame au milipuko ya volkeno katika maeneo yanayoathiriwa nayo. Sababu nyingine ni uharibifu na ushukaji wa hali ya kimazingira, mabadiliko ya desturi au thamani za kitamaduni; kusambaratika kwa familia au misingi ya familia; utengano na hasa wakati wa shida pamoja na uhamaji wa wanaume na kuwaachia jukumu kubwa. Aidha kuna kuongezeka kwa hali ya wanawake kuwa wazazi pekee na hivyo kuongeza idadi ya miji inayoongozwa na wanawake na kukosekana kwa mikakati bora au ifaayo ya kupambana na maisha.

    Wanawake wanaoishi mashambani wanaathrika vibaya sana. Kwanza, kama masikini wanaishi katika mazingira makali. Pili, kama wanawake wanakabiliana na mapendeleo ya kisera na kitamaduni ambayo yanaudharau na kuupuuza mchango wao katika maendeleo. Tatu, kama viongozi wa miji (hasa wale wanaolea na kuzitunza jamaa zao peke yao) wanalazimika kupambana na uongozi wa miji pamoja uzalishaji. Aghalabu hawapati usaidizi au auni yoyote katika majukumu kama haya: wanalazimika kupambana nayo peke yao. Katika hali zote tatu zilizotangulia, wanawake hawapati nafasi zifaazo kushiriki katika maamuzi ya masuala yanayowahusu. Masuala mengi yanaamuliwa na wanaume bila ya kuwahusisha.

    Licha ya dhiki yao kubwa, wanawake hawa wanachangia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa njia tatu kuu. Mchango huu unaonekana katika kiwango cha jamii na taifa, kiwango cha mji na kupitia kwa kizazi kijacho. Katika kiwango cha kijamii na kitaifa, wanawake hawa ni chanzo cha nguvukazi. Nguvukazi hii inatokana na wao wenyewe pamojo na kizazi chao. Pia ni msingi muhimu wa uwekaji rasilmali na kuhifadhi; aghalabu wana uwezo bora wa kutunza chochote walicho nacho kuliko wanaume. Katika kiwango cha mji, wanawake wa mashambani wanahakikisha kuwako kwa chakula, na njia za kukitayarisha chakula hicho. Katika kiwango cha vizazi, wanawake hawa wanakuwa kiungo kikubwa kati ya kizazi kijacho na vizazi vya kesho. Hawa ndio wanaowatunza, kuwalea na kuwaelimisha watoto na kuhakikisha kuwa pana muungano kati ya vizazi vya jamii.

    Maswali
    1. Ni sababu zipi zinazosababisha umaskini wa wanawake wa shambani? (Maneno 50 -55)
      Matayarisho
      Jibu
    2. Eleza jinsi wanawake wa mashambani wanavyoathirika vibaya( maneno 40 – 45)
      Matayarisho
      Jibu

  4. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA. (ala. 40)
    1. Eleza sifa mbili za sauti|k|. (ala.2)
    2. Andika mfano mmoja wa neno lenye muundo ufuatao: (ala.1)
      IKII
    3. Sentensi ambatano ni ipi? (ala. 2)
    4. Unda sentensi yenye muundo ufuatao. (ala.2)
      W+V+T+E
    5. Onyesha viwakilishi (w) katika sentensi ifuatayo na ueleze ni vya aina gani. (ala. 2)
      Wote walipewa kile kizuri.
    6. Yakinisha sentensi ifuatayo. (ala. 1)
      Hakula akashiba.
    7. Kanusha sentensi ifuatayo. (ala.2)
      Ningeenda kwake leo angenipa mawaidha.
    8. Eleza dhana zinazojitokeza katika maneno yaliyopigiwa mstari. (ala.3)
      1. Mtoto mwenyewe alianguka mle
      2. Mtoto mwenye tabia nzuri ni Yule.
    9. Tunga sentensi kuonyesha vielezi vifuatavyo. (ala.3)
      1. Kielezi cha wakati
      2. Kielezi cha mahali
      3. Kielezi cha namna/jinsi
    10. Andika katika msemo halisi. (ala. 2)
      Rafiki yetu alitujulisha kuwa tungeondoka siku iliyofuatia kuelekea Afrika kusini.
    11. Unda nomino kutokana na maneneo yafuatayo. (ala. 3)
      Neno Nomino
      Fikiri   
      -la  
      kubwa  
    12. Tunga sentensi moja moja kuonyesha aina zifuatazo za nomino. (ala. 2)
      1. Nomino kitenzi – jina
      2. Nomino dhahani
    13. Onyesha vivumishi (v) kwa kupigia mstari na ueleze ni vya aina gani. (ala.2)
      Waziri wa kawi anaishi katika nyumba kubwa
    14. Tumia alama ya ritifaa katika sentensi kuonyesha matumizi mawili tofauti. (ala. 2)
    15. Bainisha viambishii katika neno lifuatalo. (ala.3)
      Waliotutenga
    16. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa. (ala.6)
      Kitenzi tendesha tendeshea
      Piga    
      -la    
      -nywa    
    17. Mahali palipotayarishwa pamejaa wageni kutoka mbali. ( Anza kwa: wageni…) ( al.2)

  5. ISIMU – JAMII
    Mtu X : wauza how much?
    Mtu Y: Hamsini kastoma.
    Mtu X: Kumbe ni expesive hivyo?
    Mtu Y: Nitakupunguzia. Toa arobaini.
    Mtu X: Haya. Nipatie change.
    1. Hii ni sajili gani? (ala.1)
    2. Eleza sifa tano za sajili hii. (ala5)
    3. Taja athari mbili hasi za lugha ya ‘Sheng’ (ala.2)
    4. Kwa nini vijana hutumia lugha ya ‘Sheng’ Eleza sababu mbili. (ala.2)

MAAKIZO

  1. INSHA
  2. UFAHAMU
    1. Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka. (ala.1)
      • Wanawakiwa/ Mateso ya wanawakiwa 1x1 = 1mks
    2. Eleza dhana ya ‘Mwanamkiwa. (ala. 1)
      • Ni Yule yaliyefiwa na mzazi mmoja au wote wawili
    3. Ni kategoria gani ya wanawakiwa inayosumbuka sana? (ala. 2)
      • Ni watoto wanahitaji kulelewa na kupewa matakwa ya kimsingi kama chakula, mavazi, malazi elimu n.k 1x 2 = 2
    4. Taja mambo mawili ambayo baadhi ya imani na mila za jadi huchukulia kuwa chanzo cha uanaukiwa. (ala.1)
      • Laana 2x 1 = 2
      • Urogi
    5. Eleza kwa kifupi hali ya elimu ya wanawakiwa. (ala.2)
      • Baadhi ya walioachiwa wanawakiwa huwaelimisha
      • Wengine huwanyima hata elimu hivyo baadhi yao kutojua kusoma na kuandika.
    6. Taja mateso mawili ambayo wanawakiwa wanaoahidiwa kulepekwa ng’ambo hukumbana nayo. (ala.2)
      • Kushikwa shokoa
      • Kutumiwa kama vyombo vya kuuza madanguroni 2x 1= 2mks)
    7. Eleza unafiki wa baadhi ya watu wa jamii ya wanawakiwa. (ala.3)
      • Kujitia wana huruma mzazi afapo.
      • Kuishia kuwatesa wanawakiwa
      • Huwapeleka ng’ambo wanakoteswa 3x1 = 3mks)
    8. Eleza maana za maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika makala. (ala.3)
      • Inakela – Sumbua
      • Fanya jambo la karaha au kuleta uchukivu
      • Waja – wanadamu/watu/adinasi/insi

  3. UFUPISHO
    1. Ni sababu zipi zinazosababisha umaskini wa wanawake wa shambani? (Maneno 5-55)
      Jibu
      • Mazingira magumu
      • Wanabaguliwa na sera nautamaduni
      • Wanakumbana na matatizo kama viongozi wa miji
      •  Hawapati usaidizi
      •  Hawana nafasi ya kushiriki katika maamuzi
        Alam 5
        Mtiri 2
    2. Eleza jinsi wanawake wa mashambani wanavyoathirika vibaya( maneno 40 – 45)
      Jibu
      • Umaskini unaotokana na ongezeko la watu
      • Matatizo ya kiuchumi ulimwenguni
      • Majanga ya kiasilia
      • Uharibifu wa mazingira
      • Kuvunjika kwa familia
      • Ukosefu wa mikakati ya kupambana na hali alama 6 mtiririko 2

  4. SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA. (ala. 40)
    1. Eleza sifa mbili za sauti|k|. (ala.2)
      • Ni kipasuo
      • Ni sauti si ghuna
    2. Andika mfano mmoja wa neno lenye muundo ufuatao: (ala.1)
      IKII
      • Okoa
      • Itia
      • Elea
      • Ozea
    3. Sentensi ambatano ni ipi? (ala. 2)
      • Ni sentensi iliyoundwa kutokana na sentensi mbili sahili au zaidi zilizounganishwa kwa viunganishi
    4. Unda sentensi yenye muundo ufuatao. (ala.2)
      • W+V+T+E
      • Yule mzuri amepita sana
    5. Onyesha viwakilishi (w) katika sentensi ifuatayo na ueleze ni vya aina gani. (ala.2)
      Wote walipewa kile kizuri.
      • wote – w- cha pekee
      • Kile – w ( kionyeshi/ kiashiria)
    6. Yakinisha sentensi ifuatayo. (ala. 1)
      Hakula akashiba.
      • Alikula akashiba
    7. Kanusha sentensi ifuatayo. (ala.2)
      • Ningeenda kwake leo angenipa mawaidha.
      • Nisingeenda kwake leo asingenipa mawaidha.
    8. Eleza dhana zinazojitokeza katika maneno yaliyopigiwa mstari. (ala.3)
      • Mtoto mwenye tabia nzuri ni Yule.
        Mwenye – dhana ya ‘kuwa na’ ‘ kumiliki’
      • Mtoto mwenyewe alianguka mle
        Mwenye – dhana ya ‘kuwa na,’ ‘kumiliki’
        Mle – dhana ya mahali ndani
        Mle – dhana ya kiashiria cha umbali
    9. Tunga sentensi kuonyesha vielezi vifuatavyo. (ala.3)
      • Kielezi cha wakati
        Tulienda nyumbani jana
      • Kielezi cha mahali
        Kamau alienda nje
      • Kielezi cha namna/jinsi
        Waliandika insha vizuri
    10. Andika katika msemo halisi. (ala. 2)
      Rafiki yetu alitujulisha kuwa tungeondoka siku iliyofuatia kuelekea Afrika kusini.
      • “Mtaondoka kesho kuelekea Afrika kusini.” Rafiki yetu alitujulisha.
    11. Unda nomino kutokana na maneneo yafuatayo. (ala. 3)
      Neno Nomino
      Neno Nomino
      Fikiri  fikira
      -la chakula
      kubwa ukubwa 
    12. Tunga sentensi moja moja kuonyesha aina zifuatazo za nomino. (ala. 2)
      • Nomino kitenzi – jina
        Kucheka huko kunaudhi.
      • Nomino dhahania
        Ukali wake ulimfanya aogopwe
    13. Onyesha vivumishi (v) kwa kupigia mstari na ueleze ni vya aina gani. (ala.2)
      Waziri wa kawi anaishi katika nyumba kubwa.
      • V ‘wa’ cha a- unganifu
        V ‘kubwa’ cha sifa
    14. Tumia alama ya ritifaa katika sentensi kuonyesha matumizi mawili tofauti. (ala. 2)
      • Ng’ombe atachinjwa
      • Tutapika s’s’ hivi.
      • Taralamu iliyoachwa km mwaka wa is.
    15. Bainisha viambishi katika neno lifuatalo. (ala.3)
      Waliotutenga
      • wa – nafsi
      • li – wakati
      • o – kirejeshi
      • tu – watendwa
      • teng - Mzizi wa kitenzi
      • a - kiishio
    16. Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli ulizopewa. (ala.6)
      Kitenzi tendesha tendeshea
      Piga pigisha pigishia
      -la lisha lishia
      -nywa nywesha  nyweshea
    17. Mahali palipotayarishwa pamejaa wageni kutoka mbali. ( Anza kwa: wageni…)al.2)
      • Wageni kutoka mbali wamejaa mahali palipotayarishwa

  5. ISIMU – JAMII
    1. Hii ni sajili gani? (ala.1)
      • sokoni
    2. Eleza sifa tano za sajili hii. (ala5)
      • Ni lugha isiyo rasmi
      • Lugha ya kuchanganya ndimi
      • Ina – matumizi ya utohozi
      • Huwa ni lugha ya mazungumzo ya kitamthilia
      • Ina ushawishi mwingi
      • Msamiati maalum unaohusiana na biashara mf. ngapi, expensive, kastoma
    3. Taja athari mbili hasi za lugha ya ‘Sheng’ (ala.2)
      • Kushindwa kuzungumza lugha sanifu hasa katika mazingira rasmi.
      • Huchangia makosa ya kisarufi
      • Ni vigumu kujifunza lugha sanifu
      • Wazungumzaji huenda wasielewane.
    4. Kwa nini vijana hutumia lugha ya ‘Sheng’ Eleza sababu mbili. (ala.2)
      • Kutaka kuwa ni siri katika mazungumzo
      • Kutaka kujitambulisha na kundi fulani
      • Kurahisisha mazungumzo yao
      • Kuhisi kuwa ni mabingwa katika kubuni msamiati mpya.
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Form 2 Term 2 Opener Exams 2021.


Tap Here to Download for 50/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


Get on WhatsApp Download as PDF
.
Subscribe now

access all the content at an affordable rate
or
Buy any individual paper or notes as a pdf via MPESA
and get it sent to you via WhatsApp

 

What does our community say about us?

Join our community on:

  • easyelimu app
  • Telegram
  • facebook page
  • twitter page
  • Pinterest